Kutoka 23:1-33, Kutoka 24:1-18 NEN

Kutoka 23:1-33

Sheria Za Haki Na Rehema

23:1 Mwa 36:7; Mt 19:18; Lk 3:14; Kut 20:16; Kum 5:20; 19:16-21; Za 27:12; 35:11; Mit 19:5; Mdo 6:11“Usieneze habari za uongo. Usimsaidie mtu mwovu kwa kuwa shahidi mwenye nia ya kudhuru wengine.

23:2 Law 19:15, 33; Kum 1:17; 27:19; 1Sam 8:3; Kum 24:17; 16:19; Ay 31:34“Usifuate umati wa watu katika kutenda mabaya. Unapotoa ushahidi kwenye mashtaka, usipotoshe haki ukijumuika na umati wa watu, 23:3 Rum 12:20; Law 6:2-3; 19:11; Kum 22:1-2nawe usimpendelee mtu maskini katika mashtaka yake.

“Kama ukikutana na maksai au punda wa adui yako anapotea, hakikisha umemrudisha kwake. 23:5 Kum 22:4Ukiona punda wa mtu anayekuchukia ameanguka na mzigo wake, usimwache hapo alipoangukia; hakikisha kuwa umemsaidia.

23:6 Kum 23:16; Mit 22:22“Usiwanyime haki watu wako walio maskini katika mashtaka yao. 23:7 Kut 20:16; Efe 4:24-25; Mt 27:4; Mwa 18:23; Kut 34:7; Kum 19:18; 25:1Ujiepushe na mashtaka ya uongo, wala usimuue mtu asiye na hatia au mtu mwaminifu, kwa maana sitamhesabia hana hatia yeye aliye na hatia.

23:8 Kut 18:21; Law 9:15; Kum 10:17; 27:25; Ay 15:34; 36:18; Za 26:10; Mit 6:35; 15:27; 17:8; Isa 1:23; 5:23; Mik 3:11; 7:3“Usipokee rushwa, kwa kuwa rushwa hupofusha wale waonao, na kupinda maneno ya wenye haki.

23:9 Kut 22:21; Law 19:33-34; Eze 22:7“Usimwonee mgeni; ninyi wenyewe mnajua jinsi mgeni anavyojisikia, kwa sababu mlikuwa wageni Misri.

Sheria Za Sabato

“Kwa muda wa miaka sita mtapanda mashamba yenu na kuvuna mazao, 23:11 Law 25:1-7; Neh 10:31lakini katika mwaka wa saba usiilime ardhi wala kuitumia, ili watu walio maskini miongoni mwenu waweze kupata chakula kutoka kwenye hayo mashamba, nao wanyama pori wapate chakula kwa yale mabaki watakayobakiza. Utafanya hivyo katika shamba lako la mizabibu na la mizeituni.

23:12 Kut 20:9; Lk 13:14; Mwa 2:2-3“Kwa siku sita fanya kazi zako, lakini siku ya saba usifanye kazi, ili maksai wako na punda wako wapate kupumzika, naye mtumwa aliyezaliwa nyumbani mwako, pamoja na mgeni, wapate kustarehe.

23:13 Kum 4:9, 23; 1Tim 4:16; Kum 12:3; Yos 23:7; Za 16:4; Zek 13:2; Kum 18:20; Hos 2:17“Uzingatie kutenda kila kitu nilichokuambia. Usiombe kwa majina ya miungu mingine, wala usiyaruhusu kusikika kinywani mwako.

Sikukuu Tatu Za Mwaka

(Kutoka 34:18-26; Kumbukumbu 16:1-17)

23:14 Kut 12:14; 34:23-24; Kum 16:16; 1Fal 9:25; 2Nya 8:13; Eze 46:9“Mara tatu kwa mwaka utanifanyia sikukuu.

23:15 Kut 12:17; Mt 26:17; Lk 22:1; Mdo 12:3; Kut 12:2; 22:29“Utaadhimisha Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu; kwa siku saba utakula mikate isiyotiwa chachu kama nilivyokuagiza. Fanya jambo hili kwa wakati uliopangwa katika mwezi wa Abibu, ndio mwezi wa nne, kwa sababu katika mwezi huo ulitoka Misri.

“Mtu yeyote asije mbele yangu mikono mitupu.

23:16 Law 23:15-21; Hes 28:26; Kum 16:9; 2Nya 8:13; Kut 22:29; 34:22; Law 23:34, 42; Kum 16:16; 31:10; Ezr 3:4; Neh 8:14; Zek 14:16; Yer 40:10; Kum 16:13“Utaadhimisha Sikukuu ya Mavuno kwa malimbuko ya mazao yako uliyopanda katika shamba lako.

“Utaadhimisha Sikukuu ya Kukusanya mavuno mwishoni mwa mwaka, unapokusanya mavuno yako toka shambani.

“Mara tatu kwa mwaka wanaume wote watakuja mbele za Bwana Mwenyezi.

23:18 Kut 34:25; Law 2:11; Kut 12:8“Msitoe damu ya dhabihu kwangu pamoja na kitu chochote kilicho na chachu.

“Mafuta ya mnyama wa sadaka ya sikukuu yangu yasibakizwe mpaka asubuhi.

“Utaleta malimbuko bora ya ardhi yako katika nyumba ya Bwana Mungu wako.

“Usimchemshe mwana-mbuzi katika maziwa ya mama yake.

Malaika Wa Mungu Kuandaa Njia

23:20 Mwa 16:7; Kut 15:17; 32:34“Tazama, ninamtuma malaika akutangulie mbele yako akulinde njiani na kukuleta mpaka mahali nilipoandaa. 23:21 Kum 18:19; Yer 13:15; Kum 29:20; 2Fal 24:4; Mao 1:17; Hes 17:10; Kum 9:7; 31:27; Yos 24:19; Za 25:7; 78:8, 40; 106:33; 107; 11; 1Yn 5:16; Kut 3:15Mtamtii na kusikiliza kile anachokisema. Usiasi dhidi yake; hatakusamehe uasi wako, kwa maana Jina langu limo ndani yake. 23:22 Kut 15:26; Mwa 12:3; Isa 41:11; Yer 30:20Kama ukitii kweli kweli kile asemacho na kufanya yote nisemayo, nitakuwa adui wa adui zako, na nitawapinga wale wakupingao. 23:23 Hes 13:29; 21:21; Yos 3:10; 24:8-10; 24:8-11; Ezr 9:1Malaika wangu atatangulia mbele yako na kukuleta katika nchi ya Waamori, Wahiti, Waperizi, Wakanaani, Wahivi na Wayebusi, nami nitawafutilia mbali. 23:24 Kut 20:5; Law 18:3; 20:23; Kum 9:4; 12:30-31; Yer 10:2; Kut 34:13; Hes 33:52; Kum 7:5; 12:3; Amu 2:2; 2Fal 18:4; 23:14; Kum 16:22; 1Fal 14:23; 3:2; 10:26; 17:20; 2Nya 14:2-3; Isa 27:9Usiisujudie miungu yao, au kuiabudu, wala kufuata desturi yao. Utayabomoa kabisa na kuvunjavunja mawe yao ya ibada vipande vipande. 23:25 Mt 4:10; Law 26:3-13; Kum 7:12-15; 28:1-14; Kut 15:26Utamwabudu Bwana Mungu wako, na baraka zake zitakuwa juu ya vyakula vyako na maji yako. Nami nitaondoa maradhi miongoni mwako, 23:26 Law 26:3-4; Kum 7:14; 28:4; Mal 3:11; Mwa 15:15; Kum 4:1, 40; 21:12na hakuna atakayeharibu mimba wala atakayekuwa tasa katika nchi yako. Nami nitakupa maisha makamilifu.

23:27 Mwa 35:5; Kut 15:14; 14:24; Kum 7:23; 2Sam 22:41; Za 18:40; 21:12“Nitapeleka utisho wangu mbele yako na kufadhaisha kila taifa utakalolifikia. Nitafanya adui zako wote wakupe kisogo na kukimbia. 23:28 Kum 7:20; Yos 24:12; Kut 33:2; 34:11, 24; Hes 13:29; Kum 4:38; 11:23; 18:12; Yos 3:10; 24:11; Za 78:55Nitatanguliza manyigu mbele yako kuwafukuza Wahivi, Wakanaani na Wahiti waondoke njiani mwako. 23:29 Kum 7:22Lakini sitawafukuza kwa mara moja, kwa sababu nchi itabaki ukiwa na wanyama pori watakuwa wengi mno kwako. 23:30 Yos 23:5Nitawafukuza kidogo kidogo mbele yako, mpaka uwe umeongezeka kiasi cha kutosha kuimiliki nchi.

23:31 Mwa 2:14; Kum 34:2; Ezr 4:20; Kum 7:24; 9:3; Yos 21:44; 24:12-18; Za 80:8“Nitaweka mipaka ya nchi yako kuanzia Bahari ya Shamu hadi Bahari ya Wafilisti, na kuanzia jangwani hadi Mto Frati. Nitawatia watu wanaoishi katika nchi hizo mikononi mwako, nawe utawafukuza watoke mbele yako. 23:32 Mwa 26:28; Kut 34:12; Kum 7:2; Yos 9:7; Amu 2:2; 1Sam 11:1; 1Fal 15:19; 20:34; Eze 17:13Usifanye agano lolote nao wala na miungu yao. 23:33 Kut 10:7; Za 106:36Usiwaache waishi katika nchi yako, la sivyo watakusababisha utende dhambi dhidi yangu, kwa sababu ibada ya miungu yao hakika itakuwa mtego kwako.”

Read More of Kutoka 23

Kutoka 24:1-18

Agano Lathibitishwa

24:1 Kut 19:24; 6:23; Hes 11:16; Law 10:1-2Kisha Mungu akamwambia Mose, “Njooni huku juu kwa Bwana, wewe na Aroni, Nadabu na Abihu, pamoja na wazee sabini wa Israeli. Mniabudu kwa mbali, 24:2 Hes 12:6-8lakini Mose peke yake ndiye atakayemkaribia Bwana; wengine wasije karibu. Nao watu wasije wakapanda pamoja naye.”

24:3 Kut 21:1; Gal 3:19; Kut 19:8; Yos 24:24; Kum 5:27Mose alipokwenda na kuwaambia watu maneno yote na sheria zote za Bwana, wakaitikia kwa sauti moja, “Kila kitu alichosema Bwana tutakifanya.” 24:4 Kut 17:14; Mwa 8:20; 28:18; Kum 31:9; 27:2Ndipo Mose akaandika kila kitu Bwana alichokuwa amesema.

Akaamka kesho yake asubuhi na mapema na kujenga madhabahu chini ya mlima na kusimamisha nguzo kumi na mbili za mawe kuwakilisha makabila kumi na mawili ya Israeli. 24:5 Law 1:3; Mwa 31:54Kisha akawatuma vijana wanaume wa Kiisraeli, nao wakatoa sadaka za kuteketezwa na dhabihu za mafahali wachanga kuwa sadaka za amani kwa Bwana. 24:6 Kut 14:15; 32:31; Za 99:6; Ebr 9:18; Law 1:11; 3:2, 8; 5:9; Mt 26:28Mose akachukua nusu ya damu ya wale wanyama na kuiweka kwenye mabakuli na nusu nyingine akainyunyiza juu ya madhabahu. 24:7 2Fal 23:2, 21; Ebr 9:19; Kut 19:8; Yer 40:3; 42:6, 21; 43:2Kisha akachukua kile Kitabu cha Agano na kuwasomea watu. Nao wakajibu, “Tutafanya kila kitu alichosema Bwana, nasi tutatii.”

24:8 Ebr 9:19; 1Pet 1:2; Law 26:3; Kum 5:2-3; Yos 24:25; 2Fal 11:17; Yer 11:4-8; 31:32; 34:13; Zek 9:11; Mt 26:28; Lk 22:20; Ebr 9:20Ndipo Mose akachukua ile damu, akawanyunyizia wale watu, akasema, “Hii ni damu ya agano ambalo Bwana amelifanya nanyi kufuatana na maneno haya yote.”

Mose na Aroni, Nadabu na Abihu, pamoja na wazee sabini wa Israeli wakapanda mlimani, 24:10 Mwa 16:13; Hes 12:6; Isa 6:1; Eze 8:3; 40:2; Yn 1:18; Ay 28:16; Isa 54:11; Ufu 4:3nao wakamwona Mungu wa Israeli. Chini ya miguu yake kulikuwa na kitu kama sakafu ya mawe ya yakuti samawi, iliyo safi kama anga angavu. 24:11 Kut 3:6; 19:2; Eze 44:3; Mt 26:29; Mwa 32:30Lakini Mungu hakuinua mkono wake dhidi ya hawa viongozi wa Waisraeli; walimwona Mungu, nao wakala na kunywa.

24:12 Kut 31:18; 32:15-16; 34:1, 28, 29; Kum 4:13; 5:22; 8:3; 9:9-11; 2Kor 3:12Bwana akamwambia Mose, “Panda uje kwangu huku mlimani na ukae hapa, nami nitakupa vibao vya mawe, vyenye sheria na amri ambazo nimeziandika ziwe mwongozo wao.”

24:13 Kut 17:9; 3:1Basi Mose akaondoka na Yoshua mtumishi wake, naye Mose akapanda juu kwenye mlima wa Mungu. 24:14 Kut 17:10; 18:16Mose akawaambia wazee wa Israeli, “Tungojeni hapa mpaka tutakapowarudia. Aroni na Huri wako pamoja nanyi, na kila aliye na neno aweza kuwaendea wao.”

24:15 Kut 19:9; Mt 17:5Mose alipopanda juu mlimani, wingu liliufunika huo mlima, 24:16 Kut 16:7; Law 9:23; Hes 14:10; 1Sam 4:21-22; Eze 8:4; 11:22; Kut 19:11; Za 99:7nao utukufu wa Bwana ukatua juu ya Mlima Sinai. Kwa muda wa siku sita wingu lilifunika mlima, na siku ya saba Bwana akamwita Mose kutoka katikati ya lile wingu. 24:17 Kut 15:7; 19:18; Ebr 12:18, 29Kwa Waisraeli utukufu wa Bwana ulionekana kama moto uteketezao juu ya mlima. 24:18 1Fal 19:8; Mwa 7:4; Mt 4:2; Kut 34:28; Kum 9:9Kisha Mose akaingia ndani ya lile wingu alivyokuwa akipanda mlimani. Naye akakaa huko mlimani kwa muda wa siku arobaini, usiku na mchana.

Read More of Kutoka 24