Kutoka 15:1-27, Kutoka 16:1-36 NEN

Kutoka 15:1-27

Wimbo Wa Mose Na Miriamu

15:1 Hes 21:17; Amu 5:3; 2Sam 22:1; 1Nya 16:9; Ay 36:24; Za 59:16; 105:2; Ufu 15:3; Za 13:6; 21:13; 27:6; 61:8; 104:33; 106:12; Isa 12:5-6; 42:10; 44:23; Kum 11:4; Za 76:6; Yer 51:21; Kut 14:27; Yn 2:11Ndipo Mose na Waisraeli wakamwimbia Bwana wimbo huu:

“Nitamwimbia Bwana,

kwa kuwa ametukuzwa sana.

Farasi na mpanda farasi

amewatosa baharini.

15:2 Za 18:1; 59:17; Mwa 45:7; Kut 14:13; Za 18:2, 46; 25:5; 62:2; 118:14; Isa 12:2; 33:2; Yn 2:9; Hab 3:18; Mwa 28:21; Kum 10:21; 2Sam 22:47; Za 22:3; 34:3; 35:27; 99:5; 103:19; 107:32; 108:5; 118:28; 145:11; 148:14; Isa 24:15; Yer 17:14; Dan 4:37Bwana ni nguvu zangu na wimbo wangu;

amekuwa wokovu wangu.

Yeye ni Mungu wangu, nami nitamsifu,

Mungu wa baba yangu, nami nitamtukuza.

15:3 Kut 14:14; 3:15; Ufu 19:11Bwana ni shujaa wa vita;

Bwana ndilo jina lake.

15:4 Kut 14:6-7; Yer 51:21Magari ya vita ya Farao na jeshi lake

amewatosa baharini.

Maafisa wa Farao walio bora sana

wamezamishwa katika Bahari ya Shamu.

15:5 Kut 14:28; Neh 9:11Maji yenye kina yamewafunika,

wamezama mpaka vilindini kama jiwe.

15:6 Za 16:11; 17:7; 21:8; 63:8; 74:11; 77:10; 89:13; 118:15; 138:7; Kut 3:20; Ay 40:14; Hes 24:8; 1Sam 2:10; Za 2:9“Mkono wako wa kuume, Ee Bwana

ulitukuka kwa uweza.

Mkono wako wa kuume, Ee Bwana,

ukamponda adui.

15:7 Kum 33:26; Za 150:2; 2:5; 78:49-50; Yer 12:13; 25:38; Kut 24:17; Kum 4:24; 9:3; Za 18:8; 59:13; Ebr 12:29Katika ukuu wa utukufu wako,

ukawaangusha chini wale waliokupinga.

Uliachia hasira yako kali,

ikawateketeza kama kapi.

15:8 Kut 14:21; Za 18:15; Yos 3:13; Za 78:13; Isa 43:16; Kut 14:22; Za 46:2Kwa pumzi ya pua zako

maji yalijilundika.

Mawimbi ya maji yakasimama imara kama ukuta,

vilindi vikagandamana ndani ya moyo wa bahari.

15:9 Kut 14:5-9; Kum 28:45; Za 7:5; Mao 1:3; Amu 5:30; Isa 9:3; 53:12; Lk 11:22“Adui alijivuna,

‘Nitawafuatia, nitawapata.

Nitagawanya nyara;

nitajishibisha kwa wao.

Nitafuta upanga wangu

na mkono wangu utawaangamiza.’

15:10 Neh 9:11; Za 32:6; Ay 4:9; 15:30; Isa 11:4; 30:33; 40:7; Za 29:3Lakini ulipuliza kwa pumzi yako,

bahari ikawafunika.

Wakazama kama risasi

kwenye maji makuu.

15:11 Kut 8:10; Za 77:13; 99:3; 110:3; 4:2; 26:8; Isa 46:5; 35:2; 40:5; Law 19:2; 1Sam 2:2; 1Nya 16:29; Isa 6:3; Ufu 4:8; Kut 3:20“Ni nani miongoni mwa miungu aliye kama wewe, Ee Bwana?

Ni nani kama Wewe:

uliyetukuka katika utakatifu,

utishaye katika utukufu,

ukitenda maajabu?

15:12 Kut 7:5; Hes 16:32; 26:10; Kum 11:6; Za 106:17Uliunyoosha mkono wako wa kuume

na nchi ikawameza.

15:13 Neh 9:12; Za 77:20; Kut 6:6; Ay 33:28; Za 71:23; 106:10; Isa 1:27; 41:14; 43:14; 44:22-24; 51:10; 63:9; Tit 2:14; Za 68:16; 76:2; 78:54“Katika upendo wako usiokoma utawaongoza

watu uliowakomboa.

Katika nguvu zako utawaongoza

mpaka makao yako matakatifu.

15:14 Kut 23:27; Kum 2:25; Yos 2:9; 9:24; 1Sam 4:7; Es 8:17; Za 48:6; 96:9; 99:1; 114:7; Eze 38:20; Isa 13:8; Za 83:7Mataifa watasikia na kutetemeka,

uchungu utawakamata watu wa Ufilisti.

15:15 Mwa 36:15; Kum 2:4; Hes 22:3; Za 114:7; Yos 2:9, 24Wakuu wa Edomu wataogopa,

viongozi wa Moabu watatetemeka kwa hofu,

watu wa Kanaani watayeyuka,

15:16 Mwa 35:5; 1Sam 25:37; Za 74:2; 2Pet 2:1-2; Kum 2:4; Yos 2:9vitisho na hofu vitawaangukia.

Kwa nguvu ya mkono wako

watatulia kama jiwe,

mpaka watu wako waishe kupita, Ee Bwana,

mpaka watu uliowanunua wapite.

15:17 Kut 23:20; 32:34; 33:12; 2Sam 7:10; Za 44:2; 80:8; Isa 5:2; 60:21; Yer 2:21; 11:17; 24:6; Amo 9:15; Kum 33:19; Za 2:6; 3:4; 78:54-68; 133:3; Dan 9:16; Yoe 2:1; Oba 1:16; Sef 3:11; Za 132:13-14; 78:69; 114:2Utawaingiza na kuwapandikiza

juu ya mlima wa urithi wako:

hapo mahali, Ee Bwana, ulipopafanya kuwa makao yako,

mahali patakatifu, Ee Bwana, ulipopajenga kwa mikono yako.

15:18 Mwa 21:33; Za 9:7; 29:10; 55:19; 66:7; 80:1; 102:12; 145:13; Mao 5:19Bwana atatawala

milele na milele.”

15:19 Kut 14:28; 14:22Farasi wa Farao, magari yake ya vita na wapanda farasi wake walipoingia baharini, Bwana aliyarudisha maji ya bahari yakawafunika, lakini wana wa Israeli walipita baharini mahali pakavu. 15:20 Kut 2:4; Hes 12:1; 20:1; 26:59; 1Nya 4:17; 6:3; Amu 4:4; 2Fal 22:14; 2Nya 34:22; Neh 6:14; Isa 8:3; Eze 13:17; Mwa 31:27; 1Sam 18:6; Za 81:2; Isa 30:32; Mwa 4:21; Amu 11:34; 21:21; 2Sam 6:8-16; Za 30:11; 149:3; Wim 6:13; Yer 31:4, 13Kisha Miriamu yule nabii mke, ndugu yake Aroni, akachukua matari mkononi mwake na wanawake wote wakamfuata na matari yao wakicheza. 15:21 1Sam 18:17; Amo 2:15; Hag 2:22; Kut 14:27; 15:1Miriamu akawaimbia:

“Mwimbieni Bwana,

kwa maana ametukuka sana.

Farasi na mpanda farasi

amewatosa baharini.”

Maji Ya Mara Na Elimu

15:22 Za 78:52; Mwa 16:7; Kut 17:1-3; Hes 20:2-5; 33:14; Za 107:5Kisha Mose akawaongoza Israeli kutoka Bahari ya Shamu na kuingia katika Jangwa la Shuri. Kwa siku tatu walisafiri jangwani bila kupata maji. 15:23 Hes 33:8; Rut 1:20Walipofika Mara, hawakuweza kunywa maji yake kwa sababu yalikuwa machungu. (Ndiyo sababu mahali hapo panaitwa Mara15:23 Mara maana yake ni Chungu.) 15:24 Kut 14:12; 16:2; Hes 14:2; Yos 9:18; Za 78:18, 42; 106:13, 25; Eze 16:43; Mt 6:31Kwa hiyo watu wakamnungʼunikia Mose, wakisema, “Tunywe nini?”

15:25 Kut 14:10; 2Fal 2:21; 4:41; Amu 3:4; Ay 23:10; Za 81:7; Isa 48:10Ndipo Mose akamlilia Bwana, naye Bwana akamwonyesha kipande cha mti. Akakitupa ndani ya maji, nayo maji yakawa matamu.

Huko Bwana akawapa amri na sheria na huko akawajaribu. 15:26 Kut 32:22; Kum 11:13; 15:5; Yer 11:6; Kut 19:5-6; 20:2-7; Kum 7:12, 15; 28:27, 58; 32:39; 1Sam 5:6; Za 30:2; 41:3-4; 103:3; Kut 23:25-26; 2Fal 20:5; Za 25:11; 107:20; Yer 30:17; Hos 11:3Mungu akasema, “Kama mkisikiliza kwa bidii sauti ya Bwana Mungu wenu na kuyafanya yaliyo sawa machoni pake, kama mkiyatii maagizo yake na kuzishika amri zake zote, sitaleta juu yenu ugonjwa wowote niliowaletea Wamisri, kwa kuwa Mimi ndimi Bwana, niwaponyaye.”

15:27 Hes 33:9Kisha wakafika Elimu, mahali palipokuwa na chemchemi kumi na mbili, na miti sabini ya mitende, wakapiga kambi huko karibu na maji.

Read More of Kutoka 15

Kutoka 16:1-36

Mana Na Kware

16:1 Kut 17:1; Hes 33:11-12; Kut 6:6; 12:1-2Jumuiya yote ya Kiisraeli ikaondoka Elimu, wakafika Jangwa la Sini, lililokuwa kati ya Elimu na Sinai, siku ya kumi na tano ya mwezi wa pili baada ya kutoka Misri. 16:2 Kut 15:24; 14:11; 1Kor 10:10Huko jangwani hiyo jumuiya yote wakawanungʼunikia Mose na Aroni. 16:3 Kut 17:3; Hes 14:2; 20:3; 11:4, 34; Kum 12:20; Za 78:18; 106:14; Yer 44:12; Mwa 47:15Waisraeli wakawaambia, “Laiti tungelikufa kwa mkono wa Bwana huko Misri! Huko tuliketi tukizunguka masufuria ya nyama na tukala vyakula tulivyovitaka, lakini ninyi mmetuleta huku jangwani ili mpate kuua mkutano huu wote kwa njaa.”

16:4 Dan 8:3; Neh 9:15; Za 78:24; 105:40; Yn 6:31; Mwa 22:1Kisha Bwana akamwambia Mose, “Nitanyesha mikate kutoka mbinguni kwa ajili yenu. Watu watatoka kila siku na kukusanya kitakachowatosha kwa siku ile, kwa njia hii, nitawajaribu nione kama watafuata maelekezo yangu. 16:5 Law 25:21Siku ya sita watatayarisha kile waletacho ndani, nacho kitakuwa mara mbili kuliko ya kile walichokusanya kila siku.”

16:6 Kut 6:6Kwa hiyo Mose na Aroni wakawaambia Waisraeli wote, “Jioni mtajua kwamba Bwana ndiye aliwatoa Misri, 16:7 Kut 24:16; 29:43; 33:18-22; 40:34; Law 9:6; Hes 16:19; Kum 5:24; 1Fal 8:11; Za 63:2; Isa 6:3; 35:2; 40:5; 44:23; 66:18; Eze 1:28; 10:4; 43:5; Hab 2:14; Hag 2:7; Yn 11:40; Hes 11:1; 17:5; 16:11kisha asubuhi mtauona utukufu wa Bwana, kwa sababu amesikia manungʼuniko yenu dhidi yake. Sisi ni nani hata mtunungʼunikie?” 16:8 Hes 23:21; Kum 33:5; Amu 8:23; 1Sam 8:17; 12:12; Mt 10:40; Rum 13:2; 1The 4:8Pia Mose akasema, “Mtajua kuwa alikuwa Bwana wakati atakapowapa nyama mle ifikapo jioni na mikate yote mtakayohitaji asubuhi kwa sababu amesikia manungʼuniko yenu dhidi yake. Sisi ni nani? Hamnungʼuniki dhidi yetu, bali dhidi ya Bwana.”

Kisha Mose akamwambia Aroni, “Iambie jumuiya yote ya Waisraeli kwamba, ‘Mje mbele zake Bwana, kwa maana amesikia manungʼuniko yenu.’ ”

16:10 Yn 11:2; Kut 13:21; 40:34-35; 1Fal 8:10; 2Nya 7:1; Eze 10:4Aroni alipokuwa akizungumza na jumuiya yote ya Waisraeli, wakatazama kuelekea jangwani, na huko wakaona utukufu wa Bwana ukitokeza katika wingu.

Bwana akamwambia Mose, 16:12 Kut 6:2; 16:7; 20:2“Nimesikia manungʼuniko ya Waisraeli. Waambie, ‘Jioni mtakula nyama, na asubuhi mtashiba mikate. Ndipo mtajua ya kwamba Mimi ndimi Bwana Mungu wenu.’ ”

16:13 Hes 11:31; Za 78:27-28; 105:40; 106:15; Hes 11:9Jioni ile kware wakaja wakaifunika kambi na asubuhi kulikuwa na tabaka la umande kuzunguka kambi. 16:14 Hes 11:7-9; Kum 8:3, 16; Za 105:40Wakati umande ulipoondoka, vipande vidogo vidogo kama theluji vilionekana juu ya uso wa jangwa. 16:15 Kum 8:16; Neh 9:20; Yn 6:31Waisraeli walipoona, wakaambiana, “Hiki ni nini?” Kwa kuwa hawakujua kilikuwa kitu gani.

Mose akawaambia, “Huu ndio mkate ambao Bwana amewapa mle. Hivi ndivyo Bwana alivyoamuru: ‘Kila mmoja akusanye kiasi anachohitaji. Chukueni pishi16:16 Pishi ni kipimo cha ujazo, kwa Kiebrania ni omeri, ambacho ni sawa na kilo mbili. moja kwa kila mtu mliye naye katika hema yenu.’ ”

Waisraeli wakafanya kama walivyoambiwa, baadhi yao wakakusanya zaidi, wengine pungufu. 16:18 2Kor 8:15Nao walipopima katika pishi, yule aliyekusanya zaidi hakuwa na ziada, wala aliyekusanya kidogo hakupungukiwa. Kila mmoja alikusanya kiasi alichohitaji.

16:19 Kut 12:10; 23:18Kisha Mose akawaambia, “Mtu yeyote asibakize chochote mpaka asubuhi.”

16:20 Kut 32:31Hata hivyo, wengine hawakuzingatia aliyosema Mose, wakahifadhi kiasi fulani mpaka asubuhi, lakini kile alichohifadhi kikajaa mabuu na kuanza kunuka. Kwa hiyo Mose akawakasirikia.

Kila asubuhi, kila mmoja alikusanya kiasi alichohitaji na jua lilipokuwa kali, iliyeyuka. 16:22 Kut 34:31Siku ya sita, wakakusanya mara mbili, kiasi cha pishi mbili kwa kila mtu, nao viongozi wa jumuiya wakaja kumwarifu Mose. 16:23 Mwa 2:3; Kut 20:8; Kum 5:13-14Mose akawaambia, “Hivi ndivyo alivyoagiza Bwana: ‘Kesho itakuwa siku ya mapumziko, Sabato takatifu kwa Bwana. Kwa hiyo okeni kile mnachotaka kuoka na mchemshe kile mnachotaka kuchemsha. Hifadhini chochote kinachobaki na mkiweke mpaka asubuhi.’ ”

Kwa hiyo wakavihifadhi mpaka asubuhi, kama Mose alivyoagiza, na havikunuka wala kuwa na mabuu. Mose akawaambia, “Kuleni leo, kwa sababu leo ni Sabato kwa Bwana. Hamtapata chochote juu ya nchi leo. 16:26 Kut 20:9-10Kwa siku sita mtakusanya, lakini siku ya saba, yaani Sabato, hakutakuwepo chochote.”

Hata hivyo, baadhi ya watu wakatoka kwenda kukusanya siku ya saba, lakini hawakupata chochote. 16:28 Yos 9:14; Za 78:10; 106:13; 107:11; Yer 32:23; 2Fal 17:14Ndipo Bwana akamwambia Mose, “Je, mtaacha kushika maagizo na maelekezo yangu mpaka lini? Fahamuni kuwa Bwana amewapa ninyi Sabato, ndiyo sababu katika siku ya sita amewapa mikate ya siku mbili. Kila mmoja inampasa kukaa pale alipo katika siku ya saba. Hata mmoja haruhusiwi kutoka.” Kwa hiyo watu wakapumzika siku ya saba.

Watu wa Israeli wakaita ile mikate mana16:31 Mana maana yake ni mkate kutoka mbinguni. Ilikuwa myeupe kama mbegu za mtama na ladha yake ilikuwa kama mkate mwembamba uliotengenezwa kwa asali. Mose akasema, “Hivi ndivyo alivyoagiza Bwana: ‘Chukueni pishi ya mana na kuhifadhi kwa ajili ya vizazi vijavyo ili vione mikate niliyowapa mle jangwani nilipowatoa katika nchi ya Misri.’ ”

16:33 Ebr 9:4; Ufu 2:17Kwa hiyo Mose akamwambia Aroni, “Chukua gudulia na uweke pishi moja ya mana ndani yake. Kisha uweke mbele za Bwana ili kihifadhiwe kwa ajili ya vizazi vijavyo.”

16:34 Kut 25:16, 21-22; 27:21; 31:18; 40:20; Law 16:13; Hes 1:50; 7:89; 10:11; 17:4; Kum 2:10; 1Fal 8:9; 2Nya 5:10Kama Bwana alivyomwagiza Mose, hatimaye Aroni alikuja kuihifadhi ndani ya Sanduku la Ushuhuda. 16:35 Yn 6:31, 49; Hes 14:33; 33:38; Kum 1:3; 2:7; 8:2-4; Yos 5:6; Amu 3:11; Neh 9:21; Za 95:10; Amu 5:25; Yos 5:12Waisraeli wakala mana kwa miaka arobaini, mpaka walipofika katika nchi iliyokaliwa na watu; walikula mana hadi walipofika mpakani mwa Kanaani.

16:36 Law 5:11; 6:20; Hes 5:15; 15:4; 28:5(Pishi moja ni sehemu ya kumi ya kipimo cha efa.16:36 Efa moja ni sawa na kilo 22.)

Read More of Kutoka 16