Kutoka 1:1-22, Kutoka 2:1-25, Kutoka 3:1-22 NEN

Kutoka 1:1-22

Waisraeli Waonewa

1:1 Mwa 46:8Haya ndiyo majina ya wana wa Israeli ambao walikwenda Misri na Yakobo, kila mmoja akiwa pamoja na jamaa yake: Reubeni, Simeoni, Lawi na Yuda; Isakari, Zabuloni na Benyamini; 1:4 Mwa 35:22-26; Hes 1:20-43Dani na Naftali, Gadi na Asheri. 1:5 Mwa 46:26Wazao wote wa Yakobo walikuwa watu sabini; Yosefu alikuwa tayari yuko Misri.

1:6 Mwa 50:26; Mdo 7:15Basi Yosefu na kaka zake wote na kizazi kile chote walikufa, 1:7 Mwa 12:2; Kum 7:13; Eze 16:7lakini Waisraeli walikuwa wamezaana na kuongezeka sana, idadi yao ikawa kubwa mno, kwa hiyo wakaijaza nchi.

1:8 Yer 43:11; 46:2Kisha mfalme mpya ambaye hakufahamu habari za Yosefu akatawala Misri. 1:9 Mwa 26:16Akawaambia watu wake, “Tazameni, Waisraeli wamekuwa wengi mno kwa idadi kutuliko sisi. 1:10 Mwa 15:13; Kut 3:7; 18:11; Za 64:2; 71:10; 83:3; 105:24-25; Isa 53:3; Mdo 7:17-19Njooni, ni lazima tuwashughulikie kwa uangalifu, la sivyo watazidi kuwa wengi zaidi, na ikiwa patatokea vita, watajiunga na adui zetu kupigana dhidi yetu na kuondoka katika nchi hii.”

1:11 Kut 3:7; 5:4, 10-14; 6:6-7; 2:11; Mwa 15:13; 47:11; Yos 9:27; Isa 60:10; 1Fal 9:19, 21; 1Nya 22:2; 2Nya 8:4Basi Wamisri wakaweka wasimamizi wa kuwasimamia na kuwatesa Waisraeli kwa kazi ngumu, nao wakajenga miji ya Pithomu na Ramesesi ya kuweka akiba ya Farao. Lakini walivyozidi kuteswa ndivyo walivyozidi kuongezeka na kuenea katika nchi; Wamisri wakawaogopa Waisraeli, 1:13 Mwa 15:13-14; Kut 5:21; 16:3; Law 25:43-53; Kum 4:20; 26:6; 1Fal 8:15; Za 129:1; Isa 30:6; 48:10; Yer 11:4kwa hiyo wakawatumikisha kwa ukatili. 1:14 Kum 26:6; Ezr 9:9; Isa 14:3; Mwa 11:3; Kut 2:23; 3:9; Hes 20:15; Mdo 7:19; 1Sam 10:11; 2Sam 13:4Wakafanya maisha ya Waisraeli kuwa machungu kwa kufanya kazi ngumu ya kutengeneza lami na kufyatua matofali, na kazi zote za mashambani; katika kazi zao zote ngumu, Wamisri waliwatumia Waisraeli kwa ukatili.

1:15 Mwa 35:17Mfalme wa Misri akawaambia wakunga wa Kimisri waliowazalisha wanawake wa Kiebrania, ambao majina yao ni Shifra na Pua, “Mtakapowazalisha wanawake wa Kiebrania, chunguzeni wanapojifungua. Ikiwa ni mtoto wa kiume, muueni, lakini ikiwa ni msichana, mwacheni aishi.” 1:17 Mit 16:6; 1Sam 22:17; Dan 3:16-18; Mdo 4:18-20; 5:29Lakini hao wakunga walimcha Mungu na hawakufanya kile mfalme wa Misri alichowaambia kufanya, bali wakawaacha watoto wa kiume waishi. Ndipo mfalme wa Misri akawaita hao wakunga, akawauliza, “Kwa nini mmefanya hivi? Mbona mmeacha watoto wa kiume waishi?”

1:19 Law 19:11; Yos 2:4-6; 1Sam 19:14; 2Sam 17:20Wakunga wakamjibu Farao, “Wanawake wa Kiebrania ni tofauti na wanawake wa Kimisri; wao wana nguvu, nao hujifungua watoto kabla wakunga hawajafika.”

1:20 Mit 11:18; 22:8; Mhu 8:12; Isa 3:10; Ebr 6:10Kwa hiyo Mungu akawatendea mema wakunga hao. Waisraeli wakaongezeka na kuendelea kuwa wengi zaidi. 1:21 1Sam 2:35; 2Sam 7:11, 27-29; 1Fal 11:38; 14:10Kwa vile hao wakunga walimcha Mungu, Mungu akawajalia kuwa na jamaa zao wenyewe.

1:22 Mwa 41:1; Mdo 7:19Kisha Farao akatoa agizo hili kwa watu wake wote: “Kila mtoto wa kiume atakayezaliwa kwa Waebrania lazima atupwe katika Mto Naili, bali kila mtoto wa kike aachwe aishi.”

Read More of Kutoka 1

Kutoka 2:1-25

Kuzaliwa Kwa Mose

2:1 Mwa 29:34; Kut 6:20; Hes 26:29Basi mtu mmoja wa nyumba ya Lawi akaoa mwanamke Mlawi, 2:2 Mwa 39:6; Ebr 11:23naye mwanamke huyo akapata mimba, akazaa mtoto wa kiume. Alipoona mtoto huyo ni mzuri, akamficha kwa miezi mitatu. 2:3 Isa 18:2; Mwa 6:14; 41:2; Ay 8:11; Mdo 7:21Lakini alipoona hawezi kumficha zaidi, akamtengenezea kisafina cha mafunjo, akakipaka lami. Kisha akamweka huyo mtoto ndani yake, akakificha katikati ya matete kando ya ukingo wa Mto Naili. 2:4 Kut 15:20Dada ya huyo mtoto akasimama mbali ili kuona kitakachompata mtoto.

2:5 Kut 7:15; 8:20Ndipo binti Farao akateremka mtoni Naili kuoga, nao wahudumu wake wakawa wanatembea ukingoni mwa mto. Binti mfalme akaona kisafina katikati ya manyasi, akamtuma mmoja wa watumwa wake wa kike kukichukua. Alifungua kisafina akaona mtoto ndani yake. Mtoto alikuwa akilia, akamhurumia. Akasema, “Huyu ni mmoja wa watoto wa Kiebrania.”

Ndipo dada wa huyo mtoto akamuuliza binti Farao, “Je, niende nikakutafutie mmoja wa wanawake wa Kiebrania akulelee huyu mtoto?”

Binti Farao akamjibu, “Ndiyo, nenda.” Yule msichana akaenda akamleta mama wa mtoto. Binti Farao akamwambia, “Mchukue huyu mtoto unisaidie kumlea, nami nitakulipa.” Basi yule mwanamke akamchukua mtoto na kumlea. 2:10 1Sam 1:20; 2Sam 22:17Mtoto alipokua, akampeleka kwa binti Farao, naye akawa mwanawe. Akamwita jina lake Mose akisema, “Nilimtoa kwenye maji.”

Mose Akimbilia Midiani

2:11 Mdo 7:23; Ebr 11:24-26; Kut 1:11Siku moja, baada ya Mose kukua, akaondoka kwenda walikokuwa watu wake, na akachunguza jinsi walivyokuwa wakifanya kazi ngumu. Akamwona Mmisri akimpiga Mwebrania, mmojawapo wa watu wake. Mose akatazama huku na huko asione mtu yeyote, akamuua yule Mmisri, akamficha mchangani. 2:13 Mdo 7:26Kesho yake akatoka, akaona Waebrania wawili wakipigana. Akamuuliza yule aliyekosa, “Mbona unampiga Mwebrania mwenzako?”

2:14 Mwa 13:8; Mdo 7:27Yule mtu akamjibu, “Ni nani aliyekufanya mtawala na mwamuzi juu yetu? Je, unataka kuniua kama ulivyomuua yule Mmisri?” Ndipo Mose akaogopa na kuwaza, “Jambo lile nililofanya lazima limefahamika.”

2:15 Kut 4:19; Ebr 11:27; Mwa 31:21Farao aliposikia jambo hili, alijaribu kumuua Mose, lakini Mose akamkimbia Farao na kwenda kuishi katika nchi ya Midiani, akaketi kando ya kisima. 2:16 Kut 3:1; 18:1; Mwa 24:11Kuhani wa Midiani alikuwa na binti saba, nao wakaja kisimani ili kuchota maji na kujaza hori kwa ajili ya kunyweshea mifugo ya baba yao. 2:17 1Sam 30:8; Za 31:2; Mwa 29:10Baadhi ya wachungaji wakaja wakawafukuza hao wasichana. Ndipo Mose akainuka, akawasaidia na kunywesha mifugo yao.

2:18 Kut 3:1; 4:18; 18:5-12; Hes 10:29Hao wasichana waliporudi nyumbani kwa Reueli baba yao, akawauliza, “Imekuwaje leo mmerudi mapema hivyo?”

Wakamjibu, “Mmisri mmoja alituokoa kutoka mikononi mwa wachungaji. Pia mtu huyo alituchotea maji na kunywesha mifugo.”

2:20 Mwa 18:2-5Akawauliza binti zake, “Yuko wapi? Mbona mmemwacha? Mkaribisheni ale chakula.”

2:21 Kut 4:25; 18:2; Hes 12:1Mose akakubali kukaa kwa huyo mtu, ambaye alimpa Mose binti yake aliyeitwa Sipora amwoe. 2:22 Amu 18:30; Mwa 23:4; Ebr 11:13Sipora alizaa mtoto wa kiume, naye Mose akamwita Gershomu, akisema, “Nimekuwa mgeni katika nchi ya kigeni.”

2:23 Mdo 7:30; Kut 4:19; 1:14; 3:7-9; 6:5; Hes 20:15-16; Kum 26:7; Yak 5:4; Amu 2:18; 1Sam 12:8; Za 5:2; 18:6; 39:12; 81:7Baada ya muda mrefu, mfalme wa Misri akafa. Waisraeli wakalia kwa huzuni katika utumwa wao, walilia na kilio chao cha kutaka msaada kwa ajili ya utumwa kikamfikia Mungu. 2:24 Mwa 8:1; 9:15; 15:15; 17:4; 22:16-18; 26:3; 28:13-15; Kut 32:13; 2Fal 13:23; Za 105:10, 42; Yer 14:21Mungu akasikia kilio chao cha huzuni, akakumbuka Agano alilofanya na Abrahamu pamoja na Isaki na Yakobo. 2:25 Kut 3:7; 4:31; Lk 1:25Kwa hiyo Mungu akawaangalia Waisraeli na kuwahurumia.

Read More of Kutoka 2

Kutoka 3:1-22

Mose Na Kichaka Kinachowaka Moto

3:1 Kut 2:16, 18; 17:6; 19:1-11; 33:6; 4:27; 18:5; 24:133:1 Kum 1:2-6; 4:10, 11-15; 5:2; 1Fal 19:8; Amu 1:16; Mal 4:4Basi Mose alikuwa anachunga mifugo ya Yethro mkwewe, kuhani wa Midiani. Mose akapeleka mifugo mbali nyuma ya jangwa, naye akafika Horebu, mlima wa Mungu. 3:2 Mwa 16:7; Kut 2:2-6; 19:18; 4:5; Kum 5:19; 29:1; 1Fal 19:12; Kum 33:16; Mk 12:26; Lk 20:37; Mdo 7:30Huko malaika wa Bwana akamtokea Mose katika mwali wa moto kutoka kichakani. Mose akaona kwamba ingawa kile kichaka kilikuwa kinawaka moto, kilikuwa hakiteketei. Ndipo Mose akawaza, “Nitageuka sasa nione kitu hiki cha ajabu, nami nione ni kwa nini kichaka hiki hakiteketei.”

3:4 Kut 19:3; 4:5; Mwa 31:11; 1Sam 3:4; Isa 6:8Bwana alipoona kuwa amegeuka ili aone, Mungu akamwita kutoka ndani ya kile kichaka, “Mose! Mose!”

Naye Mose akajibu, “Mimi hapa.”

3:5 Yer 30:21; Mwa 28:17; Mdo 7:33Mungu akamwambia, “Usikaribie zaidi. Vua viatu vyako, kwa maana mahali unaposimama ni patakatifu.” 3:6 Mwa 24:12; Kut 5:4; 24:11; 33:20; Mt 22:32; Mk 12:26; Lk 20:37; Mdo 3:13; 7:32; 1Fal 19:13; Amu 13:22; Ay 13:11; 23:16; 30:15; Isa 6:5Kisha akamwambia, “Mimi ni Mungu wa baba yako, Mungu wa Abrahamu, Mungu wa Isaki, na Mungu wa Yakobo.” Mose aliposikia hayo, akafunika uso wake kwa sababu aliogopa kumtazama Mungu.

3:7 1Sam 1:11; 9:16; Mwa 16:11; Neh 9:9; Za 106:44; Kut 2:25; Mdo 7:34Bwana akamwambia, “Hakika nimeona mateso ya watu wangu katika Misri. Nimesikia kilio chao kwa sababu ya wasimamizi wao, nami naguswa na mateso yao. 3:8 Mwa 11:5; 12:7; 15:14; Mdo 7:34; Kut 13:5; 33:3; Law 20:24; Hes 13:27; Kum 1:25; 6:3; 8:7-9; 11:9; 26:9; 27:3; Yos 5:6; 11:3; Yer 11:5; 32:22; Eze 20:6; Amu 3:3Basi nimeshuka niwaokoe kutoka mkono wa Wamisri, niwatoe na kuwapandisha kutoka nchi hiyo, niwapeleke katika nchi nzuri na kubwa, nchi itiririkayo maziwa na asali, nchi ya Wakanaani, Wahiti, Waamori, Waperizi, Wahivi na Wayebusi. 3:9 Kut 1:14; Hes 10:9Sasa kilio cha Waisraeli kimenifikia, nami nimeona jinsi Wamisri wanavyowatesa. 3:10 Kut 4:12; 6:13, 26; 12:41, 51; 20:2; Yos 24:5; Mdo 7:34; 1Sam 12:6, 8; Za 105:26; Kum 4:20; 1Fal 8:16; Mik 6:4Basi, sasa nenda. Ninakutuma kwa Farao ili kuwatoa watu wangu Waisraeli kutoka Misri.”

3:11 Kut 4:10; 6:12, 30; Yer 1:6; Amu 6:15; 1Sam 9:21; 15:17; 18:18; 2Sam 7:18; 2Nya 2:6; Isa 6:5Lakini Mose akamwambia Mungu, “Mimi ni nani hata niende kwa Farao kuwatoa Waisraeli nchini Misri?”

3:12 Mwa 26:3; Kut 14:22; Rum 8:31; Hes 26:10; Yos 2:12; Amu 6:17; Za 86:17; Isa 7:14; 8:18; 20:3; Yer 44:29; Mdo 7:7Naye Mungu akasema, “Mimi nitakuwa pamoja nawe. Hii itakuwa ishara kwako kwamba ni Mimi nimekutuma: Hapo utakapokuwa umewatoa watu Misri, mtamwabudu Mungu katika mlima huu.”

3:13 Mwa 32:29Mose akamwambia Mungu, “Ikiwa nitawaendea Waisraeli na kuwaambia, ‘Mungu wa baba zenu amenituma kwenu,’ nao wakiniuliza, ‘Jina lake ni nani?’ Nitawaambia nini?”

3:14 Kut 6:2-3; Yn 8:58; Ebr 13:8; Ufu 1:8; 4:8Mungu akamwambia Mose, “Mimi niko ambaye niko. Hivyo ndivyo utakavyowaambia Waisraeli: ‘Mimi niko amenituma kwenu.’ ”

3:15 Mwa 31:42; 24:12; Dan 2:23; Kut 6:3, 7; 15:3; 23:21; 34:5-7; Law 24:11; Kum 28:58; Za 30:4; 83:18; 96:2; 97:12; 135:13; 145:21; 45:17; 72:17; 102:12; Isa 42:8; Yer 16:21; 32:2; Hos 12:5Vilevile Mungu akamwambia Mose, “Waambie Waisraeli, ‘Bwana, Mungu wa baba zenu, Mungu wa Abrahamu, Mungu wa Isaki, na Mungu wa Yakobo amenituma kwenu.’ Hili ndilo Jina langu milele, Jina ambalo mtanikumbuka kwalo kutoka kizazi hadi kizazi.

3:16 Kut 4:29, 31; 17:5; Law 4:15; Hes 16:25; 11:16; Kum 5:23; 19:12; Amu 8:14; Rut 4:2; Mit 31:23; Eze 8:11; Mwa 24:12; 2Fal 19:16; 2Nya 6:20; Za 33:18; 66:7“Nenda, ukawakusanye wazee wa Israeli, uwaambie, ‘Bwana, Mungu wa baba zenu, Mungu wa Abrahamu, Isaki na Yakobo, alinitokea akaniambia: Nimewatazama, nami nimeona mliyofanyiwa katika Misri. 3:17 Mwa 15:16; 46:4; Kut 6:6Nami nimeahidi kuwapandisha kutoka mateso yenu katika nchi ya Misri, niwapeleke nchi ya Wakanaani, Wahiti, Waamori, Waperizi, Wahivi na Wayebusi, nchi itiririkayo maziwa na asali.’

3:18 Kut 4:1, 8; 31:6; 6:12, 30; 4:23; 5:1-3; 6:11; 7:16; 9:13; 8:20, 27; 10:9, 26; Mwa 14:13; 30:26; Hes 23:4, 16“Wazee wa Israeli watakusikiliza. Kisha wewe na wazee mtakwenda kwa mfalme wa Misri na kumwambia, ‘Bwana, Mungu wa Waebrania ametutokea. Turuhusu twende safari ya siku tatu huko jangwani kutoa dhabihu kwa Bwana Mungu wetu.’ 3:19 Kut 4:21; 6:6; 7:3; 10:1; 11:9; Kum 4:34; 2Nya 6:32Lakini nafahamu kwamba mfalme wa Misri hatawaruhusu kwenda, mpaka mkono wenye nguvu umlazimishe. 3:20 Kut 6:16; 7:4-5; 9:15; 13:3-9, 14-16; 11:1; 12:31-33; 4:21; 15:11; Kum 4:34; 5:15; 7:8; 26:8; 3:24; 6:22; 2Fal 17:36; 2Nya 6:32; Za 118:15-16; 136:12; 71:19; 72:18; 77:14; 78:43; 86:10; 105:27; 106:22; Isa 41:10; 63:12; Yer 21:5; 51:25; 30:20; Mik 7:15; Mdo 7:36; Dan 9:15; Hes 14:11; Neh 9:10Kwa hiyo nitaunyoosha mkono wangu na kuwapiga Wamisri kwa maajabu yote nitakayofanya miongoni mwao. Baada ya hayo, atawaruhusu mwondoke.

3:21 Mwa 39:21; Kut 11:2; 2Nya 30:9; Neh 1:11; Za 105:37; 106:46; Yer 42:12“Nami nitawapa hawa watu upendeleo mbele ya Wamisri, kwa hiyo mtakapoondoka nchini hamtaondoka mikono mitupu. 3:22 Ay 27:16-17; Kut 11:2; 12:35; Ezr 1:4-6; 7:16; Mwa 15:14; Eze 39:10; 29:10; Za 105:37Kila mwanamke Mwisraeli atamwomba jirani yake Mmisri na mwanamke yeyote anayeishi nyumbani kwake ampe vyombo vya fedha, dhahabu na nguo, ambavyo mtawavika wana wenu na binti zenu. Hivyo mtawateka nyara Wamisri.”

Read More of Kutoka 3