Waefeso 6:1-24 NEN

Waefeso 6:1-24

Mafundisho Kuhusu Watoto Na Wazazi

6:1 Kol 3:20; Mt 6:20Enyi watoto, watiini wazazi wenu katika Bwana, kwa kuwa hili ni jema. 6:2 Kut 20:12; Kum 5:16; 27:16; Yer 35:18; Eze 22:7; Mal 1:6; Mt 15:4; Mk 7:10“Waheshimu baba yako na mama yako,” hii ndio amri ya kwanza yenye ahadi, 6:3 Kut 20; 12; Kum 5:16“upate baraka na uishi siku nyingi duniani.”

6:4 Kol 3:21; Mit 13:24; 22:6Ninyi akina baba, msiwachokoze watoto wenu, bali waleeni kwa nidhamu na mafundisho ya Bwana.

Mafundisho Kuhusu Watumwa Na Mabwana

6:5 Tit 2:9; Kol 3:22; Efe 5:22Ninyi watumwa, watiini hao walio mabwana zenu hapa duniani kwa heshima na kwa kutetemeka na kwa moyo mmoja, kama vile mnavyomtii Kristo. 6:6 Rum 6:22; Kol 3:22, 23Watiini, si tu wakati wakiwaona ili mpate upendeleo wao, bali mtumike kama watumwa wa Kristo, mkifanya mapenzi ya Mungu kwa moyo. 6:7 Kol 3:23Tumikeni kwa moyo wote, kama vile mnamtumikia Bwana na si wanadamu. 6:8 Kol 3:24Mkijua kwamba Bwana atampa kila mtu thawabu kwa lolote jema alilotenda, kama yeye ni mtumwa au ni mtu huru.

6:9 Ay 31:13, 14Nanyi mabwana, watendeeni watumwa wenu kwa jinsi iyo hiyo. Msiwatishe, kwa kuwa mnajua ya kwamba yeye aliye Bwana wenu na Bwana wao yuko mbinguni, naye hana upendeleo.

Silaha Za Mungu

6:10 Hag 2:4; Efe 1:19Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake. 6:11 Rum 13:12Vaeni silaha zote za Mungu ili kwamba mweze kuzipinga hila za ibilisi. 6:12 Efe 1:21; Rum 8:38; Efe 1:3Kwa maana kushindana kwetu si juu ya nyama na damu, bali dhidi ya falme, mamlaka, dhidi ya wakuu wa giza na majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. 6:13 Efe 6:11; 2Kor 6:7; 10:4, 11; Efe 5:16Kwa hiyo vaeni silaha zote za Mungu ili mweze kushindana siku ya uovu itakapokuja nanyi mkiisha kufanya yote, simameni imara. 6:14 Isa 1:5; Za 132:9Kwa hiyo simameni imara mkiwa mmejifunga kweli kiunoni na kuvaa dirii ya haki kifuani, 6:15 Isa 52:7; Rum 10:15nayo miguu yenu ifungiwe utayari tuupatao kwa Injili ya amani. 6:16 1Yn 5:4; Mt 5:37Zaidi ya haya yote, twaeni ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu. 6:17 Isa 59:17; Ebr 4:12Vaeni chapeo ya wokovu na mchukue upanga wa Roho, ambao ni Neno la Mungu. 6:18 Lk 18:1; Mt 26:41; Flp 4:6Mkiomba kwa Roho siku zote katika sala zote na maombi, mkikesha kila wakati mkiwaombea watakatifu wote.

6:19 1The 5:25; Mdo 4:29; 2Kor 3:12Niombeeni na mimi pia, ili kila nifunguapo kinywa changu, nipewe maneno ya kusema, niweze kutangaza siri ya Injili kwa ujasiri, 6:20 2Kor 5:20; Mdo 21:23ambayo mimi ni balozi wake katika vifungo. Ombeni ili nipate kuhubiri kwa ujasiri kama inipasavyo.

Salamu Za Mwisho

6:21 Mdo 20:4Tikiko, aliye ndugu mpendwa na mtumishi mwaminifu katika Bwana, atawaambia kila kitu, ili pia mpate kujua hali yangu na kile ninachofanya sasa. 6:22 Kol 4:7-9Ninamtuma kwenu kwa ajili ya kusudi hili hasa, ili mpate kujua hali yetu, na awatie moyo.

6:23 Gal 6:16; 1Pet 5:14Amani iwe kwa ndugu, na pendo pamoja na imani kutoka kwa Mungu Baba na Bwana Yesu Kristo. 6:24 Tit 2:7; 1Pet 1:8Neema iwe na wote wampendao Bwana wetu Yesu Kristo kwa upendo wa dhati. Amen.

Read More of Waefeso 6