Waefeso 4:17-32
Maisha Ya Zamani Na Maisha Mapya
4:17 Rum 1:21Hivyo nawaambia hivi, nami nasisitiza katika Bwana kwamba, msiishi tena kama watu wa Mataifa waishivyo, katika ubatili wa mawazo yao. 4:18 Rum 1:21; Efe 2:12; 2Kor 3:14Watu hao akili zao zimetiwa giza na wametengwa mbali na uzima wa Mungu kwa sababu ya ujinga wao kutokana na ugumu wa mioyo yao. 4:19 1Tim 4:2; Rum 1:24; Kol 3:5Wakiisha kufa ganzi, wamejitia katika mambo ya ufisadi na kupendelea kila aina ya uchafu, wakiendelea kutamani zaidi.
Lakini ninyi, hivyo sivyo mlivyojifunza Kristo. 4:21 Efe 1:13Kama hivyo ndivyo ilivyo, ninyi mmemsikia, tena mmefundishwa naye, vile kweli ilivyo katika Yesu. 4:22 1Pet 2:1; Rum 6:6Mlifundishwa kuuvua mwenendo wenu wa zamani, utu wenu wa kale, ulioharibiwa na tamaa zake za udanganyifu, 4:23 Kol 3:10ili mfanywe upya roho na nia zenu, 4:24 Rum 6:4; Efe 2:10mkajivike utu mpya, ulioumbwa sawasawa na mfano wa Mungu katika haki yote na utakatifu.
Kanuni Za Maisha Mapya
4:25 Law 19:11; Rum 12:15Kwa hiyo kila mmoja wenu avue uongo na kuambiana kweli mtu na jirani yake, kwa maana sisi sote tu viungo vya mwili mmoja. 4:26 Za 4:4; Yak 1:19, 20; Mt 5:22Mkikasirika, msitende dhambi, wala jua lisichwe mkiwa bado mmekasirika, 4:27 Yak 4:7; 1Pet 5:9wala msimpe ibilisi nafasi. 4:28 Mdo 20:35; 1The 4:11; Lk 3:11Yeye ambaye amekuwa akiiba, asiibe tena, lakini lazima ajishughulishe, afanye kitu kifaacho kwa mikono yake mwenyewe, ili awe na kitu cha kuwagawia wahitaji.
4:29 Kol 3:8; Mt 12:36; Efe 5:4; Kol 3:8; 4:6; 1The 5:11Maneno mabaya yasitoke vinywani mwenu, bali yale yafaayo kwa ajili ya kuwajenga wengine kulingana na mahitaji yao, ili yawafae wale wasikiao. 4:30 1The 5:19; Rum 8:23Wala msimhuzunishe Roho Mtakatifu wa Mungu, ambaye kwake mlitiwa muhuri kwa ajili ya siku ya ukombozi. 4:31 Kol 3:8; Tit 3:2; Yak 4:11; 1Pet 2:1; Tit 3:3Ondoeni kabisa uchungu, ghadhabu, hasira, makelele na masingizio pamoja na kila aina ya uovu. 4:32 Mt 6:14, 15Kuweni wafadhili na wenye kuhurumiana ninyi kwa ninyi, mkisameheana, kama vile naye Mungu katika Kristo alivyowasamehe ninyi.
Waefeso 5:1-7
Kuenenda Nuruni
5:1 Lk 6:36; Mt 5:45; 8; Lk 6:26; Efe 4:32Kwa hiyo, mfuateni Mungu kama watoto wapendwao, 5:2 Gal 1:4; 2Kor 6:15; Ebr 7:27mkiishi maisha ya upendo, kama vile Kristo alivyotupenda sisi akajitoa kwa ajili yetu kuwa sadaka yenye harufu nzuri na dhabihu kwa Mungu.
5:3 Kol 3:5; 1Kor 6:18; Efe 4:29Lakini uasherati, usitajwe miongoni mwenu, wala uchafu wa aina yoyote, wala tamaa, kwa sababu mambo haya hayastahili miongoni mwa watakatifu. 5:4 Mt 12:35; Efe 4:29; Rum 1:28; Kol 3:8Wala pasiwepo mazungumzo machafu ya aibu, au maneno ya upuzi au mzaha, ambayo hayafai, badala yake mshukuruni Mungu. 5:5 Kol 3:5; 1Kor 6:9Kwa habari ya mambo haya mjue hakika kwamba: Msherati, wala mtu mwovu, wala mwenye tamaa mbaya, mtu kama huyo ni mwabudu sanamu, kamwe hataurithi Ufalme wa Kristo na wa Mungu. 5:6 Rum 1:18; Kol 2:4, 8; Yer 29:8; Mt 24:4; Kol 2:4, 8, 18; 2The 2:3; Rum 1:1Mtu yeyote na asiwadanganye kwa maneno matupu, kwa kuwa hasira ya Mungu huwaka kwa sababu ya mambo kama haya juu ya wale wasiomtii. Kwa hiyo, msishirikiane nao.