Mhubiri 9:13-18, Mhubiri 10:1-20, Mhubiri 11:1-10, Mhubiri 12:1-14 NEN

Mhubiri 9:13-18

Hekima Ni Bora Kuliko Upumbavu

9:13 2Sam 20:16-22Pia niliona chini ya jua mfano huu wa hekima ambao ulinivutia sana: Palikuwa na mji mdogo uliokuwa na watu wachache ndani yake. Mfalme mwenye nguvu akainuka dhidi yake, akauzunguka akaweka jeshi kubwa dhidi yake. 9:15 Mwa 40:14; Mhu 1:11; 2:16Katika mji huo kulikuwepo mtu mmoja maskini lakini mwenye hekima, naye akauokoa ule mji kwa hekima yake. Lakini hakuna aliyemkumbuka yule maskini. 9:16 Mhu 7:19; Mit 21:22; Es 6:3Kwa hiyo, nikasema, “Hekima ni bora kuliko nguvu.” Lakini hekima ya maskini imedharauliwa, wala hakuna anayesikiliza maneno yake.

9:17 2Sam 20:17; Dan 5:10Maneno ya utulivu ya mwenye hekima

husikiwa kuliko makelele ya mtawala wa wapumbavu.

9:18 Mhu 2:13; Rum 6:12, 16-23Hekima ni bora kuliko silaha za vita,

lakini mwenye dhambi mmoja

huharibu mema mengi.

Read More of Mhubiri 9

Mhubiri 10:1-20

10:1 Mit 13:16; 18:2Kama vile nzi waliokufa huacha harufu mbaya kwenye manukato,

ndivyo upumbavu kidogo huzidi nguvu hekima na heshima.

Moyo wa mwenye hekima huelekea kuume,

lakini moyo wa mpumbavu huelekea kushoto.

Hata anapotembea barabarani,

mpumbavu hukosa ufahamu

na kudhihirisha kwa kila mmoja

jinsi alivyo mpumbavu.

10:4 Mit 16:14; 25:15; Mhu 8:3Kama hasira ya mtawala ikiwaka dhidi yako,

usiache mahali pako,

utulivu huweza kuzuia makosa mengi.

Kuna ubaya niliouona chini ya jua,

aina ya kosa litokalo kwa mtawala:

10:6 Mit 29:2Wapumbavu kuwekwa kwenye nafasi nyingi za juu,

wakati matajiri hushika nafasi za chini.

10:7 Mit 19:10Mimi nimeona watumwa wamepanda farasi,

wakati wakuu wakitembea

kwa miguu kama watumwa.

10:8 Es 2:23; Amo 5:19; Mit 26:27; Za 57:6; 9:16Yeye achimbaye shimo

aweza kutumbukia ndani yake,

yeyote abomoaye ukuta

anaweza kuumwa na nyoka.

10:9 Mit 26:27Yeyote apasuaye mawe

inawezekana yakamuumiza,

yeyote apasuaye magogo

inawezekana yakamuumiza.

Kama shoka ni butu

na halikunolewa,

nguvu nyingi zinahitajika,

lakini ustadi utaleta mafanikio.

10:11 Yer 8:17; Za 58:5; Isa 3:3Kama nyoka akiuma kabla ya kufanyiwa uaguzi,

mwaguzi hatahitajika tena.

10:12 Mit 10:14, 32; 14:3; 15:2; 18:7Maneno yatokayo kinywani mwa mtu mwenye hekima

yana neema,

bali mpumbavu huangamizwa

na midomo yake mwenyewe.

Mwanzoni maneno yake ni upumbavu,

mwishoni ni wazimu mbaya,

10:14 Yak 4:14; Mit 15:2; Mhu 8:7; 5:3; 9:1naye mpumbavu huzidisha maneno.

Hakuna yeyote ajuaye linalokuja,

ni nani awezaye kueleza ni jambo gani

litakalotokea baada yake?

Kazi ya mpumbavu humchosha mwenyewe,

hajui njia iendayo mjini.

10:16 Isa 3:4-12Ole wako, ee nchi ambayo mfalme wako alikuwa mtumwa

na ambayo wakuu wako hufanya karamu asubuhi.

10:17 Mit 31:4; Kum 14:26; 1Sam 25:36Heri wewe, ee nchi ambayo mfalme wako ni wa uzao wenye kuheshimika

na ambayo wakuu wako hula chakula kwa wakati unaofaa:

ili kupata nguvu na si kwa ajili ya ulevi.

10:18 Mit 20:4; 24:30-34Kama mtu ni mvivu paa la nyumba huinama,

kutokana na mikono milegevu, nyumba huvuja.

10:19 Mwa 14:18; Amu 9:13Karamu hufanywa kwa ajili ya kicheko,

nao mvinyo hufurahisha maisha,

lakini fedha ni jawabu la mambo yote.

10:20 Kut 22:28Usimshutumu mfalme hata ikiwa ni katika mawazo yako,

au kumlaani tajiri katika chumba chako cha kulala,

kwa sababu ndege wa angani wanaweza kuchukua maneno yako,

naye ndege anayeruka anaweza kutoa taarifa ya yale uliyosema.

Read More of Mhubiri 10

Mhubiri 11:1-10

Mkate Juu Ya Maji

11:1 Kum 15:10; 24:19; Hos 10:12; Mt 10:42; Isa 32:20; Mit 19:17Tupa mkate wako juu ya maji,

kwa maana baada ya siku nyingi

utaupata tena.

11:2 Mik 5:5; Efe 5:16; Za 112:9Wape sehemu watu saba, naam hata wanane,

kwa maana hujui ni baa gani

litakalokuwa juu ya nchi.

Kama mawingu yamejaa maji,

hunyesha mvua juu ya nchi.

Kama mti ukianguka kuelekea kusini

au kuelekea kaskazini,

mahali ulipoangukia,

hapo ndipo utakapolala.

Yeyote atazamaye upepo hatapanda,

yeyote aangaliaye mawingu hatavuna.

11:5 Za 139:14-16; Yn 3:8-10Kama vile usivyofahamu njia ya upepo,

au jinsi mwili uumbwavyo

ndani ya tumbo la mama,

vivyo hivyo huwezi kufahamu kazi ya Mungu,

Muumba wa vitu vyote.

11:6 Mhu 9:10Panda mbegu yako asubuhi,

nako jioni usiruhusu mikono yako ilegee,

kwa maana hujui ni ipi itakayofanikiwa,

kwamba ni hii au ni ile,

au kwamba zote zitafanikiwa sawasawa.

Mkumbuke Muumba Wako Ukiwa Bado Kijana

11:7 Mhu 7:11Nuru ni tamu,

tena inafurahisha macho kuona jua.

Hata kama mtu ataishi miaka mingi kiasi gani,

na aifurahie yote.

Lakini na akumbuke siku za giza,

kwa maana zitakuwa nyingi.

Kila kitu kitakachokuja ni ubatili.

11:9 Ay 19:29; Kum 29:19; Mdo 14:16; Rum 14:10; Mhu 2:24; 3:17Furahi ewe kijana, wakati ungali kijana,

moyo wako na ukupe furaha

katika siku za ujana wako.

Fuata njia za moyo wako

na chochote macho yako yaonayo,

lakini ujue kwamba kwa ajili ya haya yote

Mungu atakuleta hukumuni.

11:10 2Kor 7:1; Za 94:19; Mhu 2:24Kwa hiyo basi, ondoa wasiwasi moyoni mwako

na utupilie mbali masumbufu ya mwili wako,

kwa kuwa ujana na nguvu ni ubatili.

Read More of Mhubiri 11

Mhubiri 12:1-14

12:1 2Sam 19:35; Mhu 11:8Mkumbuke Muumba wako

siku za ujana wako,

kabla hazijaja siku za taabu,

wala haijakaribia miaka utakaposema,

“Mimi sifurahii hiyo”:

kabla jua na nuru,

nao mwezi na nyota havijatiwa giza,

kabla ya kurudi mawingu baada ya mvua;

12:3 Mwa 27:1; Zek 8:4; Za 71:9siku ile walinzi wa nyumba watakapotetemeka,

nao watu wenye nguvu watakapojiinamisha,

wakati wasagao watakapokoma kwa sababu ya uchache,

nao wachunguliao madirishani kutiwa giza;

12:4 Yer 25:10; Mik 7:1wakati milango ya kuingia barabarani itakapofungwa

na sauti ya kusaga kufifia;

wakati watu wataamshwa kwa sauti ya ndege,

lakini nyimbo zao zote zikififia;

12:5 Ay 10:21; 17:13; Yer 9:17; Amo 5:16wakati watu watakapoogopa kilichoinuka juu

na hatari zitakazokuwepo barabarani;

wakati mlozi utakapochanua maua

na panzi kujikokota

nawe usiwe na shauku ya kitu chochote.

Ndipo mwanadamu aiendea nyumba yake ya milele

nao waombolezaji wakizunguka barabarani.

Mkumbuke Muumba wako: kabla haijakatika kamba ya fedha,

au bakuli la dhahabu halijavunjika;

kabla mtungi kuvunjika kwenye chemchemi,

au gurudumu kuvunjika kisimani,

12:7 Mwa 2:7; Ay 20:8; 34:15; Mhu 3:21; Za 146:4nayo mavumbi kurudi ardhini yalikotoka,

na roho kurudi kwa Mungu aliyeitoa.

Mhubiri asema, “Ubatili! Ubatili!

Kila kitu ni ubatili!”

Hitimisho La Mambo

12:9 1Fal 4:32Mhubiri hakuwa tu na hekima, bali aliwagawia watu maarifa pia. Alitafakari na kutafiti na akaweka katika utaratibu mithali nyingi. 12:10 Mit 22:20-21Mhubiri alitafiti ili kupata maneno sahihi na kila alichoandika kilikuwa sawa na kweli.

12:11 Ezr 9:8; Ay 6:25Maneno ya wenye hekima ni kama mchokoro, mithali zao zilizokusanywa pamoja ni kama misumari iliyogongomewa ikawa imara, yaliyotolewa na Mchungaji mmoja. Tena zaidi ya hayo, mwanangu, kubali maonyo, hakuna mwisho wa kutunga vitabu vingi, nako kusoma sana huuchosha mwili.

12:13 Mik 6:8; Kum 4:2-6; 10:12; Kut 20:20; 1Sam 12:24; Ay 23:15; Za 19:9Hii ndiyo jumla ya maneno;

yote yamekwisha sikiwa:

Mche Mungu, nawe uzishike amri zake,

maana kwa jumla ndiyo impasayo mtu.

12:14 Mt 10:26; Ay 19:26; 34:21; Mhu 3:17; Za 19:12; Yer 16:17Kwa maana Mungu ataleta hukumuni kila kazi,

pamoja na kila neno la siri,

likiwa jema au baya.

Read More of Mhubiri 12