Mhubiri 1:1-18, Mhubiri 2:1-26, Mhubiri 3:1-22 NEN

Mhubiri 1:1-18

Kila Kitu Ni Ubatili Mtupu

1:1 Mhu 7:27; 12:10Maneno ya Mhubiri, mwana wa Daudi, mfalme huko Yerusalemu:

1:2 Za 39:5-6; 62:9; Rum 8:20-21; Mhu 4:4-6; 12:8“Ubatili mtupu! Ubatili mtupu!”

Mhubiri anasema.

“Ubatili mtupu!

Kila kitu ni ubatili.”

1:3 Mhu 3:9; 5:15-16; 2:11-22Mwanadamu anafaidi nini kutokana na kazi yake yote

anayotaabikia chini ya jua?

1:4 2Pet 3:10; Za 104:5; Ay 8:19Vizazi huja na vizazi hupita,

lakini dunia inadumu milele.

1:5 Za 19:5-6Jua huchomoza na jua huzama,

nalo huharakisha kurudi mawioni.

Upepo huvuma kuelekea kusini

na kugeukia kaskazini,

hurudia mzunguko huo huo,

daima ukirudia njia yake.

1:7 Ay 36:28; 38:10Mito yote hutiririka baharini,

hata hivyo bahari kamwe haijai.

Mahali mito inapotoka,

huko hurudi tena.

1:8 Mhu 3:1; Mit 27:20Vitu vyote vinachosha,

zaidi kuliko mtu anavyoweza kusema.

Jicho kamwe halitosheki kutazama,

wala sikio halishibi kusikia.

1:9 Mwa 8:22; Mhu 3:15; 2:12Kile kilichokuwepo kitakuwepo tena,

kile kilichofanyika kitafanyika tena,

hakuna kilicho kipya chini ya jua.

Kuna kitu chochote ambacho mtu anaweza kusema,

“Tazama! Kitu hiki ni kipya”?

Kilikuwepo tangu zamani za kale,

kilikuwepo kabla ya wakati wetu.

1:11 Mhu 8:10; 9:5, 15; 2:16; Za 88:12; Mwa 40:23Hakuna kumbukumbu ya watu wa zamani,

hata na wale ambao hawajaja bado

hawatakumbukwa

na wale watakaofuata baadaye.

Hekima Ni Ubatili

Mimi, Mhubiri, nilikuwa mfalme wa Israeli katika Yerusalemu. 1:13 Mwa 3:17-19; Mhu 3:10; Ay 28:3Nilitumia muda wangu wote kujifunza na kuvumbua kwa hekima yote yanayofanyika chini ya mbingu. Jinsi gani Mungu ameweka mzigo mzito juu ya wanadamu! 1:14 Mhu 2:11; 4:4; 6:9Nimeshaona mambo yote yanayotendeka chini ya jua, hayo yote ni ubatili, hii ni kukimbiza upepo.

1:15 Mhu 7:13Kilichopindika hakiwezi kunyooshwa,

kile ambacho hakipo haiwezekani kukihesabu.

1:16 1Fal 3:12; 4:30; Mhu 2:9Niliwaza mwenyewe, “Tazama, nimekua na kuongezeka katika hekima kuliko yeyote aliyewahi kutawala Yerusalemu kabla yangu. Nimekuwa na uzoefu mkubwa wa hekima na maarifa.” 1:17 1The 5:21; Mhu 7:23, 25; 2:3, 12; 8:16Ndipo nilipojitahidi kufahamu kutofautisha hekima, wazimu na upumbavu, lakini nikatambua hata hili nalo ni kukimbiza upepo.

1:18 Mhu 2:23; 12:12; 7:16; Ay 28:28; Yer 45:3Kwa kuwa hekima nyingi huleta huzuni kubwa;

maarifa yanapoongezeka, masikitiko yanaongezeka.

Read More of Mhubiri 1

Mhubiri 2:1-26

Anasa Ni Ubatili

2:1 Za 10:6; Lk 12:19; Mhu 7:4; 8:15Nikafikiri moyoni mwangu, “Haya basi, nitakujaribu kwa anasa nione ni lipi lililo jema.” Lakini hilo nalo likaonekana ni ubatili. 2:2 Mit 14:13; Isa 22:12-13; Mhu 7:6Nikasema, “Kicheko nacho ni upumbavu. Nayo matokeo ya anasa ni nini?” 2:3 Amu 9:13; Rut 3:3; Amo 6:3-6; Mhu 3:12-13; 5:18; 8:15Nikajaribu kujifurahisha kwa mvinyo na kukumbatia upumbavu, huku bado akili yangu inaniongoza kwa hekima. Nilitaka kuona ni lipi bora watu wafanye kwa siku chache wanazoishi chini ya mbingu.

2:4 1Fal 7:1-12; Wim 8:11; 2Nya 2:1Nikafanya miradi mikubwa: Nikajijengea majumba na kulima mashamba ya mizabibu. Nikatengeneza bustani na viwanja vya starehe nikaotesha huko kila aina ya miti ya matunda. Nikajenga mabwawa ya kukusanya maji ya kunyweshea hii miti iliyokuwa inastawi vizuri. Nikanunua watumwa wa kiume na wa kike na watumwa wengine walizaliwa nyumbani mwangu. Pia nilikuwa na makundi ya ngʼombe, kondoo na mbuzi kuliko mtu yeyote aliyewahi kuishi Yerusalemu kabla yangu. 2:8 1Fal 9:28; 10:10-21; 2Sam 19:35; Amu 3:15Nikajikusanyia fedha na dhahabu, hazina za wafalme na za majimbo. Nikajipatia waimbaji wanaume na wanawake, nazo nyumba za masuria: vitu ambavyo moyo wa mwanadamu hufurahia. 2:9 1Nya 29:25; Mhu 1:12-16Nikawa maarufu sana kuliko mtu mwingine yeyote aliyepata kuishi Yerusalemu kabla yangu. Katika haya yote bado nikawa nina hekima.

Sikujinyima kitu chochote ambacho macho yangu yalikitamani,

hakuna anasa ambayo niliunyima moyo wangu.

Moyo wangu ulifurahia kazi zangu zote,

hii ilikuwa thawabu ya kazi zangu zote.

Hata hivyo nilipokuja kuangalia yote ambayo

mikono yangu ilikuwa imefanya

na yale niliyotaabika kukamilisha,

kila kitu kilikuwa ni ubatili, ni kukimbiza upepo;

hapakuwa na faida yoyote chini ya jua.

Hekima Na Upumbavu Ni Ubatili

Kisha nikageuza mawazo yangu kufikiria hekima,

wazimu na upumbavu.

Ni nini zaidi mtu anayetawala baada ya mfalme

anachoweza kufanya ambacho hakijafanywa?

2:13 Mhu 7:11-12, 19; 9:18Nikaona kuwa hekima ni bora kuliko upumbavu,

kama vile nuru ilivyo bora kuliko giza.

2:14 Za 49:10; Mit 17:24; Mhu 8:1; 3:19; 7:2; 9:3, 11-12Mtu mwenye hekima ana macho katika kichwa chake,

lakini mpumbavu anatembea gizani;

lakini nikaja kuona kwamba

wote wawili hatima yao inafanana.

2:15 Mhu 6:8Kisha nikafikiri moyoni mwangu,

“Hatima ya mpumbavu itanipata mimi pia.

Nitafaidi nini basi kwa kuwa na hekima?”

Nikasema moyoni mwangu,

“Hili nalo ni ubatili.”

2:16 Za 49:10; 112:6; Mhu 1:11Kwa maana kwa mtu mwenye hekima,

kama ilivyo kwa mpumbavu,

hatakumbukwa kwa muda mrefu,

katika siku zijazo wote watasahaulika.

Kama vile ilivyo kwa mpumbavu,

mtu mwenye hekima pia lazima atakufa!

Kutaabika Ni Ubatili

Kwa hiyo nikachukia maisha, kwa sababu kazi inayofanyika chini ya jua ilikuwa masikitiko kwangu. Yote hayo ni ubatili, ni kukimbiza upepo. 2:18 Za 39:6; 49:10; 1Fal 12:13Nikachukia kila kitu nilichokuwa nimetaabikia chini ya jua, kwa sababu ni lazima nimwachie yule ajaye baada yangu. Nani ajuaye kama atakuwa ni mtu mwenye hekima au mpumbavu? Lakini hata hivyo yeye ndiye atakayetawala kazi zote ambazo nimemiminia juhudi na ustadi chini ya jua. Hili nalo ni ubatili. Kwa hiyo moyo wangu ukaanza kukata tamaa juu ya kazi yangu yote niliyoifanya kwa taabu chini ya jua. Kwa kuwa mtu anaweza kufanya kazi yake kwa hekima, maarifa na ustadi, kisha analazimika kuacha vyote alivyo navyo kwa mtu mwingine ambaye hajavifanyia kazi. Hili nalo pia ni ubatili tena ni balaa kubwa. 2:22 Mhu 3:9; 1:3Mtu atapata nini kwa taabu yote na kuhangaika kwa bidii katika kazi anayotaabikia chini ya jua? 2:23 Ay 5:7; 7:2; 14:1; Mhu 1:18; Mwa 3:17Siku zake zote kazi yake ni maumivu na masikitiko, hata usiku akili yake haipati mapumziko. Hili nalo pia ni ubatili.

2:24 1Kor 15:32; Mhu 3:12-13, 22; 7:7-10; 8:15; 5:17-19; 9:7-10; 11:7-10; Ay 2:10Hakuna kitu bora anachoweza kufanya mtu zaidi ya kula na kunywa na kuridhika katika kazi yake. Hili nalo pia, ninaona, latokana na mkono wa Mungu, kwa sababu pasipo yeye, ni nani awezaye kula na kufurahi? 2:26 Ay 27:17; 9:4; Mit 13:22Kwa yule mtu anayempendeza Mungu, Mungu humpa hekima, maarifa na furaha, bali kwa mwenye dhambi Mungu humpa kazi ya kukusanya na kuhifadhi utajiri ili Mungu ampe yule anayempenda. Hili nalo pia ni ubatili, ni kukimbiza upepo.

Read More of Mhubiri 2

Mhubiri 3:1-22

Kila Jambo Lina Wakati Wake

3:1 Mhu 8:6Kuna wakati kwa ajili ya kila jambo,

nayo majira kwa kila tendo chini ya mbingu:

3:2 Mwa 47:29; Isa 28:24; 38:1wakati wa kuzaliwa na wakati wa kufa,

wakati wa kupanda na wakati wa kungʼoa yaliyopandwa,

3:3 Kum 5:17wakati wa kuua na wakati wa kuponya,

wakati wa kubomoa,

na wakati wa kujenga,

3:4 Kut 15:20; 2Sam 6:16wakati wa kulia na wakati wa kucheka,

wakati wa kuomboleza na wakati wa kucheza,

wakati wa kutawanya mawe na wakati wa kukusanya mawe,

wakati wa kukumbatia na wakati wa kutokumbatia,

wakati wa kutafuta na wakati wa kupoteza,

wakati wa kuweka na wakati wa kutupa,

3:7 Amo 5:13; Es 4:14wakati wa kurarua na wakati wa kushona,

wakati wa kunyamaza na wakati wa kuzungumza,

wakati wa kupenda na wakati wa kuchukia,

wakati wa vita na wakati wa amani.

Mfanyakazi anapata faida gani kutokana na taabu yake? 3:10 Mhu 1:13Nimeona mzigo Mungu alioweka juu ya wanadamu. 3:11 Kum 32:4; Mhu 8:17; Ay 11:7; 28:23; Rum 11:33Amefanya kila kitu kiwe kizuri kwa wakati wake. Pia ameiweka hiyo milele katika mioyo ya wanadamu, wala hawawezi kutambua kwa kina yale ambayo Mungu amefanya tangu mwanzo hadi mwisho. Ninajua kwamba hakuna kitu bora kwa wanadamu kuliko kuwa na furaha na kutenda mema wakati wanapoishi. 3:13 Za 34:12; Kum 12:7, 18; Mhu 2:3, 24; 5:19Tena ni karama ya Mungu kila mtu apate kula na kunywa na kujiburudisha kwa mema katika kazi yake yote. 3:14 Ay 23:15; Yak 1:17; Mhu 5:7; 7:18; 8:12-13Ninajua kwamba kila kitu anachokifanya Mungu kitadumu milele, hakuna kinachoweza kuongezwa au kupunguzwa. Mungu hufanya hivyo ili watu wamche yeye.

3:15 Mhu 6:10; 1:9Chochote kilichopo kilishakuwepo,

na kitakachokuwepo kimekwishakuwepo kabla;

naye Mungu huyaita yale yaliyopita yarudi tena.

Pia nikaona kitu kingine tena chini ya jua:

Mahali pa kutolea hukumu,

uovu ulikuwepo,

mahali pa kupatia haki,

uovu ulikuwepo.

3:17 Ay 34:11; 19:29; Mt 16:27; Mhu 11:9; 12:14Nikafikiri moyoni mwangu,

“Mungu atawaleta hukumuni

wote wawili wenye haki na waovu,

kwa maana kutakuwako na wakati kwa ajili ya kila jambo,

wakati kwa ajili ya kila tendo.”

3:18 Za 73:22Pia nikafikiri, “Kuhusu wanadamu, Mungu huwajaribu ili wajione kwamba wao ni kama wanyama. 3:19 Mhu 2:14; Za 49:12Hatima ya mwanadamu ni kama ile ya wanyama; wote wana mwisho unaofanana: Jinsi anavyokufa mnyama, ndivyo anavyokufa mwanadamu. Wote wana pumzi inayofanana; mwanadamu hana cha zaidi kuliko mnyama. Kila kitu ni ubatili. 3:20 Mwa 2:7; 3:19-20; Ay 34:10Wote huenda mahali panapofanana; wote hutoka mavumbini, mavumbini wote hurudi. 3:21 Mhu 12:7Ni nani ajuaye kama roho ya mtu huenda juu na roho ya mnyama hushuka chini ardhini?”

3:22 Mhu 2:10, 24; 5:18; Ay 31:2Kwa hiyo nikaona kwamba hakuna kitu kilicho bora zaidi kwa mwanadamu kuliko kuifurahia kazi yake, kwa sababu hilo ndilo fungu lake. Kwa maana ni nani awezaye kumrudisha ili aje kuona kile kitakachotendeka baada yake?

Read More of Mhubiri 3