Kumbukumbu 9:1-29, Kumbukumbu 10:1-22 NEN

Kumbukumbu 9:1-29

Si Kwa Sababu Ya Haki Ya Waisraeli

(Kutoka 32:1-35)

9:1 Hes 35:10; Kum 1:28; 4:38; 11:23, 31; Hes 13:28; Mwa 11:4Sikiliza, ee Israeli. Sasa mnakaribia kuvuka Yordani mwingie na kuwafukuza mataifa makubwa na yenye nguvu kuliko ninyi pamoja na miji mikubwa yenye kuta zilizofika juu angani. 9:2 Hes 13:22; Yos 11:12Watu ni wenye nguvu na warefu, ni wana wa Waanaki! Mnafahamu habari zao na mmesikia inavyosemekana: “Ni nani awezaye kusimama dhidi ya Waanaki?” 9:3 Kum 7:23-24; 31:3; Yos 3:11; Kut 15:7; 19:18; 23:31; Ebr 12:29; Mik 2:13; Ufu 19:11-15; Isa 30:27; 33:14; Nah 1:5, 6; 2The 1:8; Kut 23:31Kuweni na hakika leo kwamba Bwana Mungu wenu ndiye atakayetangulia kuvuka mbele yenu kama moto uteketezao. Atawaangamiza; atawatiisha mbele yenu. Nanyi mtawafukuza na kuwaangamiza mara moja, kama Bwana alivyowaahidi.

9:4 Kum 8:17; 18:9-14; 2Fal 16:3; 17:8; 21:2; Ezr 9:11; Kut 23:24; Law 18:21-24, 30; Eze 36:32; Rum 11:6; 1Kor 4:4; Mwa 15:16Baada ya Bwana Mungu wenu kuwafukuza mbele yenu, msiseme mioyoni mwenu, “Bwana ametuleta hapa kuimiliki nchi hii kwa sababu ya haki yetu.” La, ni kwa sababu ya uovu wa mataifa haya ndiyo Bwana anawafukuza mbele yenu. 9:5 Efe 2:9; Kum 18:9; 4:38; 11:22; Law 18:25; Mwa 12:7; 13:15; 26:4; Eze 36:32; Tit 3:5; 2Tim 1:9; Lk 1:54; Mdo 13:32, 33; Rum 15:8Si kwa sababu ya haki yenu wala uadilifu wenu kwamba mtaimiliki nchi yao; lakini kwa sababu ya uovu wa mataifa haya, Bwana Mungu wenu atawafukuza mbele yenu, ili kutimiza lile alilowaapia baba zenu Abrahamu, Isaki na Yakobo. 9:6 Kut 32:9; Mdo 7:51Basi mjue, si kwa sababu ya haki yenu Bwana Mungu wenu anawapa nchi hii nzuri kuimiliki, kwa kuwa ninyi ni taifa lenye shingo ngumu.

Ndama Ya Dhahabu

9:7 Hes 11:33; Kut 23:21; 14:11Kumbukeni hili, kamwe msisahau jinsi mlivyomkasirisha Bwana Mungu wenu kwa hasira huko jangwani. Tangu siku mlipotoka Misri mpaka mlipofika hapa, mmekuwa waasi dhidi ya Bwana. 9:8 Hes 16:46; 1Sam 28:18; Ay 20:28; Za 2:12; 7:11; 69:24; 110:5; 106:19; Isa 9:19; Eze 20:13; Kut 32:12; Ezr 9:14Kule Horebu mliamsha ghadhabu ya Bwana, kwa hiyo alikasirika vya kutosha hata akataka kuwaangamiza. 9:9 Kum 9:13; Mwa 7:4; Kut 24:12-18; 34:28; Lk 4:1Nilipopanda mlimani kupokea mbao za mawe, mbao za Agano lile Bwana alilofanya nanyi, nilikaa mlimani siku arobaini usiku na mchana, sikula mkate wala sikunywa maji. 9:10 Kut 31:18; Kum 10:4; 18:16Bwana alinipa mbao mbili za mawe zilizoandikwa kwa kidole cha Mungu. Juu ya mbao hizo kulikuwepo amri zote ambazo Bwana aliwatangazia kule mlimani kwa njia ya moto, siku ya kusanyiko.

9:11 Mwa 7:4; Kut 24:12Mwisho wa siku arobaini usiku na mchana, Bwana alinipa mbao mbili za mawe, mbao za Agano. 9:12 Kum 4:16; Amu 2:17; Kut 32:7-8Kisha Bwana akaniambia, “Shuka chini mara moja, kwa sababu watu wako ambao umewatoa katika nchi ya Misri wamepotoka. Wamegeukia mbali haraka kutoka lile nililowaagiza, wamejitengenezea sanamu ya kusubu.”

9:13 Kut 32:9; Kum 10:16; 2Fal 17:14Naye Bwana akaniambia, “Nimewaona watu hawa nao ni watu wenye shingo ngumu sana! 9:14 Kut 34:10; Hes 14:12; Yer 7:16; Kum 29:20; Za 9:5; 109:13Niache, ili nipate kuwaangamiza na kufuta jina lao kutoka chini ya mbingu. Nami nitakufanya kuwa taifa lenye nguvu zaidi na kuwa wengi kuliko wao.”

9:15 Kut 19:18; 32:15Kwa hiyo niligeuka na kuteremka kutoka mlimani kwani mlima ulikuwa ukiwaka moto. Pia vibao vile viwili vya Agano vilikuwa mikononi mwangu. 9:16 Kut 32:4, 9Nilipotazama, niliona kuwa mmefanya dhambi dhidi ya Bwana Mungu wenu; mmejifanyia sanamu ya kusubu katika umbo la ndama. Mmegeuka upesi kutoka njia ile Bwana aliyowaagiza. 9:17 Za 69:9; 119:139Kwa hiyo nilichukua vibao vile viwili nikavitupa na kuvipasua vipande vipande mbele ya macho yenu.

9:18 Kut 34:28; 32:31Ndipo tena nikasujudu mbele za Bwana kwa siku arobaini usiku na mchana. Sikula mkate wala sikunywa maji, kwa sababu ya dhambi yote mliyoifanya, mkifanya lile lililo ovu mbele za Bwana na kumkasirisha. 9:19 Kut 32:14; Ebr 12:21; Kut 34:10; Hes 11:2; 1Sam 7:9; Yer 15:1; Kum 9:26; 10:10; Za 106:23; Yak 5:15; Amo 7:1-6Niliogopa hasira na ghadhabu ya Bwana, kwa kuwa aliwakasirikia vya kutosha na kutaka kuwaangamiza. Lakini Bwana alinisikiliza tena. Bali yeye alimkasirikia Aroni kiasi cha kutaka kumwangamiza, nami wakati huo nilimwombea Aroni pia. 9:21 Za 18:42; Isa 2:18; 29:5; 40:15; Kut 32:20; Mk 1:7; Hos 8:11Kisha nikachukua ile sanamu ya ndama mliyoitengeneza na kuichoma kwenye moto. Nikaiponda na kuisaga ikawa unga laini kama vumbi, nikatupa lile vumbi kwenye kijito kilichotiririka toka mlimani.

9:22 Hes 1:53; 11:3; 11:34; Kut 17:7Pia mlimkasirisha Bwana huko Tabera, Masa na Kibroth-Hataava.

9:23 Kum 1:32; Hes 14:9; Za 106:24; Hes 13:3; 14:1; Za 78:22; Ebr 3:18, 19; 4:2Vilevile wakati Bwana alipowatuma kutoka Kadesh-Barnea, alisema, “Kweeni, mkaimiliki nchi ambayo nimewapa.” Lakini mliasi dhidi ya agizo la Bwana Mungu wenu. Hamkumtegemea wala kumtii. 9:24 Kum 8:17; 31:27Mmekuwa waasi dhidi ya Bwana tangu nilipowajua ninyi.

9:25 Mwa 7:4; Kut 33:17Nilianguka kifudifudi mbele za Bwana kwa zile siku arobaini usiku na mchana kwa sababu Bwana alikuwa amesema angewaangamiza ninyi. 9:26 Kut 33:13; 34:9; 6:6; 32:11; Kum 15:15; 2Sam 7:23; Za 78:35; 1Sam 7:9; Mit 15:29; Yer 15:1Nilimwomba Bwana na kusema, “Ee Bwana Mwenyezi, usiangamize watu wako, urithi wako mwenyewe ule ulioukomboa kwa uweza wako mkuu na kuwatoa katika nchi ya Misri kwa mkono wenye nguvu. 9:27 Kut 32:9Wakumbuke watumishi wako Abrahamu, Isaki na Yakobo. Usiangalie ukaidi wa watu hawa, uovu wao wala dhambi yao. 9:28 Kum 32:27; 1:27; Kut 32:12; Yos 7:9; Hes 14:16; Mwa 41:57; 1Sam 14:25; Yos 7:7-9; Za 115:1, 2; Isa 48:9-11Watu wa nchi ile uliyotutoa sisi wasije wakasema, ‘Ni kwa sababu Bwana hakuweza kuwachukua mpaka nchi aliyokuwa amewaahidia, kwa sababu aliwachukia, akawaleta ili aje kuwaua jangwani.’ 9:29 Kut 33:13; 34:9; Kum 32:9; 4:34; Neh 1:10; Yer 27:5; 32:17; 1Fal 8:51; Neh 1:10; Za 95:7Bali wao ni watu wako, urithi wako ule ulioutoa Misri kwa uweza wako mkuu na kwa mkono wako ulionyooka.”

Read More of Kumbukumbu 9

Kumbukumbu 10:1-22

Vibao Vingine Vya Amri Kumi

(Kutoka 34:1-10)

10:1 Kut 34:2; 25:10Wakati ule Bwana aliniambia, “Chonga vibao viwili vya mawe kama vile vya kwanza uje kwangu juu mlimani. Pia utengeneze Sanduku la mbao. 10:2 Kut 25:16, 21; 2Nya 5:10; 6:11Nitaandika juu ya vibao maneno yaliyokuwa katika vile vibao vya kwanza, ambavyo ulivivunja. Kisha utaviweka ndani ya Sanduku.”

10:3 Kut 37:1-9; 34:4; 26:5Hivyo nikatengeneza Sanduku kwa mti wa mshita, nikachonga pia vibao vya mawe kama vile vya kwanza, kisha nikakwea mlimani nikiwa na vibao viwili mikononi mwangu. 10:4 Kut 24:12; 34:28; 20; 1; Kum 9:10; Yer 31:33Bwana akaandika juu ya hivi vibao kile alichokuwa amekiandika kabla, Amri Kumi alizokuwa amewatangazia juu mlimani, kutoka kwenye moto siku ile ya kusanyiko. Bwana akanikabidhi. 10:5 Kut 19:11; 25:10; 25:21; 34:29; 40:21; 1Sam 8:3; 1Fal 8:9Kisha nikashuka kutoka mlimani na kuweka vibao ndani ya Sanduku nililokuwa nimelitengeneza, kama Bwana alivyoniagiza, navyo viko huko sasa.

10:6 Hes 33:30; 27:13; 20:25-28; Kut 6:23(Waisraeli walisafiri kutoka visima vya Yaakani hadi Mosera. Huko Aroni alifariki na kuzikwa, naye Eleazari mwanawe akachukua nafasi yake kama kuhani. 10:7 Hes 33:32-34; Za 42:1; Wim 5:12; Isa 32:2Kutoka pale, walisafiri hadi Gudgoda wakaendelea mpaka Yotbatha, nchi yenye vijito vya maji. 10:8 Hes 3:6; 10:33; 16:9; Mwa 48:20; 1Nya 23:26; Kum 18:5; 21:5; Law 9:22Wakati huo Bwana aliteua kabila la Lawi kulibeba Sanduku la Agano la Bwana, kusimama mbele za Bwana ili kutoa huduma, na kutangaza baraka kwa Jina lake, kama wanavyofanya mpaka leo. 10:9 Hes 18:20; Eze 44:28Hiyo ndiyo sababu ya Walawi kutokuwa na sehemu wala urithi miongoni mwa ndugu zao; Bwana ndiye urithi wao, kama Bwana Mungu wao alivyowaambia.)

10:10 Kut 33:17; 34:28; Kum 9:18-19; 25Basi nilikaa mlimani kwa siku arobaini usiku na mchana, kama nilivyofanya mara ya kwanza, pia Bwana alinisikiliza hata wakati huu. Haikuwa nia yake kuwaangamiza. Bwana akaniambia, “Nenda, ukawaongoze watu katika njia yao ili kwamba waweze kuingia na kuimiliki nchi ile niliyowaapia baba zao kuwapa.”

Mche Bwana

10:12 Mik 6:8; Kut 20:20; 1Fal 2:3; 3:3; 4:4; Kum 5:32; 5:33; 6:13; 6:5; 11:13; 28:47; Mt 22:37; 1Tim 1:5; Za 100:2; Kum 6:5; Za 119:2; Kum 5:32Na sasa, ee Israeli, Bwana Mungu wako anataka nini kwako ila kumcha Bwana Mungu wako, kwenda katika njia zake, kumpenda na kumtumikia Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote, 10:13 Kum 4:2; 5:33; 6:25na kuyashika maagizo ya Bwana na amri zake ninazokupa leo kwa mafanikio yako mwenyewe?

10:14 Za 148:4; Isa 19:1; Hab 3:8; Neh 9:6; Ay 35:5; Za 8:3; 89:11; 104:3; Kum 33:26; Za 115:16; 1Fal 8:27; Kut 19:5; Za 24:1; Mdo 17:24Mbingu, hata mbingu za juu sana, dunia na kila kitu kilichomo ndani yake, ni mali ya Bwana Mungu wako. 10:15 Kum 4:37; Za 105:6; 135:4; Hes 14:8; Rum 11:28; 1Pet 2:9Hata hivyo Bwana alikuwa na shauku na baba zako, akawapenda na akawachagua ninyi, wazao wao, kuliko mataifa yote, kama ilivyo leo. 10:16 Mwa 17:11; Law 26:41; Kum 30:6; Yer 32:39; Kut 32:9; 9:13; Yer 4:4; Kum 9:6Kwa hiyo tahirini mioyo yenu, na msiwe na shingo ngumu tena. 10:17 Yos 22:22; Za 135:9; 136:2; Dan 2:47; 11:36; Za 136:3; 1Tim 6:15; Kum 7:21; 1:17; Mal 2:9; Kut 23:8; Law 19:16; Efe 6:9Kwa kuwa Bwana Mungu wenu ni Mungu wa miungu na Bwana wa mabwana, Mungu mkuu, mwenye uweza na wa kutisha, ambaye hana upendeleo na hapokei rushwa. 10:18 Kut 22:21, 22-24; 23:9; Law 19:33; Kum 27:19; Ay 29:13; Za 94:6; Isa 10:2; Yer 49:11; Hes 10:32Huwapigania yatima na wajane, humpenda mgeni, akimpa chakula na mavazi. 10:19 Kum 7:12; Kut 22:21; Kum 24:19; Law 19:34; Eze 47:22-23Nanyi wapendeni wageni, kwa kuwa ninyi wenyewe mlikuwa wageni huko Misri. 10:20 Mt 4:10; Kum 11:22; 13:4; 30:20; Yos 23:8; Rut 1:14; 2Fal 18:6; Za 119:31; Isa 38:3; Kut 20:7; Za 63:11Mche Bwana Mungu wako na umtumikie yeye. Shikamana naye kwa uthabiti na kuapa kwa jina lake. 10:21 Kut 15:2; 1Sam 12:24; Za 126:2; 2Sam 7:23; Yer 17:14; Za 106:21-22Yeye ni sifa yako; yeye ni Mungu wako, ambaye alikutendea yale maajabu makubwa na ya kutisha uliyoyaona kwa macho yako mwenyewe. 10:22 Mwa 34:30; 46:26; Mdo 7:14; Mwa 12:2; Hes 10:36Baba zako walioshuka kwenda Misri jumla yao walikuwa sabini, na sasa Bwana Mungu wako amekufanya wengi kama nyota za angani.

Read More of Kumbukumbu 10