Kumbukumbu 6:1-25, Kumbukumbu 7:1-26, Kumbukumbu 8:1-20 NEN

Kumbukumbu 6:1-25

Mpende Bwana Mungu Wako

Haya ndiyo maagizo, amri na sheria ambazo Bwana Mungu wenu aliniagiza niwafundishe ninyi ili mpate kuyashika katika nchi ambayo ninyi mnavuka Yordani kuimiliki, 6:2 Kut 20:20; 1Sam 12:24; Kum 4:9; Mwa 26:5; Kut 20:12ili kwamba ninyi, watoto wenu na watoto wao baada yao wamche Bwana Mungu wenu siku zote kwa kushika amri na maagizo yake yote ninayowapa, ili mweze kuyafurahia maisha marefu. 6:3 Mwa 15:5; Kum 5:33; 32:13-14; Kut 3:8; 13:5; 19:5Sikia, ee Israeli, nawe uwe mwangalifu kutii ili upate kufanikiwa na kuongezeka sana katika nchi itiririkayo maziwa na asali, kama Bwana, Mungu wa baba zenu, alivyowaahidi ninyi.

6:4 Zek 14:9; Kum 4:35-39; Neh 9:6; Za 86:10; Isa 44:6; Mk 12:29; Yn 10:30; 1Kor 8:4; Efe 4:6; Yak 2:19Sikia, ee Israeli: Bwana Mungu wako, Bwana ni mmoja. 6:5 Kum 11:1, 22; Mt 22:37; Mk 12:30; Lk 10:27; 1Sam 12:24; Kum 4:29; 10:12; Yos 22:5Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote. 6:6 Kum 11:18; 30:14; 32:46; Za 26:2; 37:31; 40:8; 119:11; Mit 3:3; Isa 51:7; Yer 17:1; 31:33; Eze 40:4Amri hizi ninazokupa leo zitakuwa katika moyo wako. 6:7 Kum 4:9; 11:19; Mit 22:6; Efe 6:4Wafundishe watoto wako kwa bidii. Nena kuhusu amri hizi uketipo nyumbani na wakati utembeapo njiani, ulalapo na uamkapo. 6:8 Kut 13:9; Mt 23:5; Mit 3:3; 7:3; 6:21Zifunge kama alama juu ya mkono wako, na uzifunge juu ya paji la uso wako. 6:9 Kum 11:20; Isa 50:8; 57:8Ziandike kwenye miimo ya milango ya nyumba yako na juu ya malango yako.

6:10 Mwa 11:4; Kum 12:29; 19:1; Yos 24:13Wakati Bwana Mungu wako atakapokuleta katika nchi aliyowaapia baba zako, Abrahamu, Isaki na Yakobo, kukupa wewe, nchi kubwa, ina miji inayopendeza ambayo hukuijenga, 6:11 Yer 22:13; Law 26:5; Kum 8:10; 11:29; 31:20nyumba zilizojaa vitu vizuri vya aina nyingi ambavyo hukuvijaza, visima ambavyo hukuchimba, na mashamba ya mizabibu na mizeituni ambayo hukupanda wewe, basi, utakapokula na kushiba, 6:12 Kum 4:9, 23; 2Fal 17:38; Za 44:17; 78:7; 103:2jihadhari usije ukamwacha Bwana, aliyekutoa katika nchi ya Misri, kutoka nchi ya utumwa.

6:13 Za 33:8; 34:9; Kum 13:4; 1Sam 7:3; Yer 44:10; Mt 4:10; Lk 4:4, 8; 1Sam 20:3; Kut 20:7; Mt 5:33Utamcha Bwana Mungu wako, na umtumikie yeye peke yake na kuapa kwa jina lake. Usifuate miungu mingine, miungu ya mataifa yanayokuzunguka; 6:15 Kum 4:24kwa kuwa Bwana Mungu wako, ambaye yuko katikati yako, ni Mungu mwenye wivu na hasira yake itawaka dhidi yako, naye atakuangamiza kutoka uso wa nchi. 6:16 Kut 17:2; Mt 4:7; Lk 4:12Usimjaribu Bwana Mungu wako kama ulivyofanya huko Masa. 6:17 Law 26:3; Kum 11:22; Za 119:4-5, 56, 100, 134, 168Utayashika maagizo ya Bwana Mungu wako kwa bidii, na masharti na amri alizokupa. 6:18 2Fal 18:6; Isa 36:7; 38:3; Kum 4:40Fanya lililo haki na jema mbele za Bwana, ili upate kufanikiwa, uweze kuingia na kuimiliki nchi nzuri ambayo Bwana aliahidi kwa kiapo kwa baba zako, 6:19 Kut 23:27; Yos 21:44; Za 78:53; 107:2; 136:24kuwafukuza kwa nguvu adui zako mbele yako kama Bwana alivyosema.

6:20 Kut 10:2; 13:14Siku zijazo, mtoto wako atakapokuuliza, “Ni nini maana ya masharti haya, amri na sheria hizi ambazo Bwana Mungu wako alikuagiza wewe?” 6:21 Kum 4:34Mwambie: “Tulikuwa watumwa wa Farao huko Misri, lakini Bwana alitutoa sisi kutoka Misri kwa mkono wenye nguvu. Bwana akapeleka mbele yetu ishara za miujiza na maajabu makubwa na ya kutisha mno juu ya Misri na Farao pamoja na nyumba yake yote. Lakini Mungu akatutoa huko, akatuleta na kutupa nchi hii ambayo aliwaahidi baba zetu kwa kiapo. 6:24 Kum 10:12; 30:6; Za 86:11; Yer 32:39; Za 27:12; 41:2; Rum 10:5Bwana akatuagiza tutii amri hizi zote na kumcha Bwana Mungu wetu, ili tupate kustawi na kuendelea kuwa hai kama ilivyo leo. 6:25 Za 103:18; 119:34, 55; Kum 24:13; Rum 9:31Kama tukizitii kwa bidii amri hizi zote mbele za Bwana Mungu wetu, kama alivyotuamuru sisi, hiyo itakuwa haki yetu.”

Read More of Kumbukumbu 6

Kumbukumbu 7:1-26

Kuyafukuza Mataifa

(Kutoka 34:11-16)

7:1 Law 14:34; Kum 4:38; 20:16-18; 31:3; Mwa 15:20; 10:16; 13:7; 10:17; Yos 3:10; Mdo 13:19Bwana Mungu wako akuletapo katika nchi unayoingia kuimiliki, na awafukuzapo mbele yako mataifa mengi, yaani Wahiti, Wagirgashi, Waamori, Wakanaani, Waperizi, Wahivi na Wayebusi, mataifa saba makubwa tena yenye nguvu kuliko wewe, 7:2 Kum 2:33-34; Hes 31:17; Kum 33:27; Yos 11:11; Kut 23:32; Kum 13:8; 19:13; 25:12pia Bwana Mungu wako atakapowatia mkononi mwako na ukawashinda, basi ni lazima uwaangamize wote kabisa. Usifanye agano nao, wala usiwahurumie. 7:3 Kut 34:15-16; Yos 22:16; Dan 9:7; Ezr 9:2Usioane nao. Usimtoe binti yako kuolewa na mwanawe, au kumchukua binti yake aolewe na mwanao. 7:4 Amu 3:6; Kum 4:26; 6:15; Isa 9:6; Mk 12:29; Yn 1:1; 10:30; 17:3; 1Kor 8:4; Efe 4:6; Flp 2:5, 6Kwa maana watamgeuza mwanao aache kunifuata, ili aitumikia miungu mingine, nayo hasira ya Bwana itawaka dhidi yako, naye atakuangamiza ghafula. 7:5 Kut 23:24; 24:13; Kum 12:2-3; 16:21; 30:6; Mt 22:37; Mk 12:30-32Hili ndilo utakalowafanyia: Vunja madhabahu yao, vunja mawe yao ya kuabudia, katakata nguzo zao za Ashera na kuchoma sanamu zao kwa moto. 7:6 Kut 19:6; Law 27:30; Kum 26:19; Za 30:4; 37:28; 50:5; 52:9; Kum 14:2; 1Fal 3:8; Isa 41:9; Eze 20:5; Mwa 17:7; Kut 8:22; 34:9; Isa 43:1; Rum 9:4; Tit 2:14; 1Pet 2:9; Yer 2:3Kwa kuwa wewe ni taifa takatifu kwa Bwana Mungu wako. Bwana Mungu wako amekuchagua wewe kutoka mataifa yote juu ya uso wa dunia kuwa watu wake, hazina yake ya thamani.

7:7 Mwa 22:17; 34:30; Kum 4:37; 10:22Bwana hakuweka upendo wake juu yenu na kuwachagua kwa sababu mlikuwa wengi mno kuliko watu wengine, kwa maana ninyi ndio mliokuwa wachache sana kuliko mataifa yote. 7:8 Kum 4:37; 1Fal 10:9; 2Nya 2:11; Za 44:3; Kut 32:13; Hes 14:8; Rum 11:28; Kut 3:20; 6:6; 13:14Lakini ni kwa sababu Bwana aliwapenda ninyi na kutunza kiapo alichowaapia babu zenu kwamba atawatoa ninyi kwa mkono wenye nguvu na kuwakomboa kutoka nchi ya utumwa, kutoka nguvu za Farao mfalme wa Misri. 7:9 Kum 4:35; Za 18:25; 33:4; 108:4; 145:13; 146:6; Isa 49:7; Yer 42:5; Hes 11:12; 1Kor 1:9; 1Fal 8:23; 2Nya 6:14; Neh 1:5; 9:32; Kut 20:6; Kum 5:10; Dan 9:4; 2Tim 2:13Basi ujue kwamba Bwana Mungu wako ndiye Mungu; ni Mungu mwaminifu, anayetunza Agano la upendo kwa maelfu ya vizazi vya wale wanaompenda na kuzishika amri zake. 7:10 Law 26:28; Hes 10:35; Neh 1:2Lakini

kwa wale wanaomchukia

atawalipiza kwenye nyuso zao

kwa maangamizi;

hatachelewa kuwalipiza kwenye nyuso zao

wale wamchukiao.

Kwa hiyo, kuweni waangalifu kufuata maagizo, amri na sheria ninazowapa leo.

Baraka Za Utiifu

(Kumbukumbu 28:1-14)

7:12 Law 26:3-13; Kum 28:1-14; Za 105:8-9; Mik 7:20Kama mkizingatia sheria hizi na kuzifuata kwa uangalifu, basi Bwana Mungu wenu atatunza Agano lake la upendo nanyi, kama alivyowaapia baba zenu. 7:13 Za 11:5; 146:8; Mit 15:9; Isa 51:1; Yn 14:21; Mwa 17:6; Kut 1:7; Kum 1:10; 13:17; 30:5; Za 107:38; Mwa 49:25; 27:28; Hes 18:12; Kum 28:4Atawapenda ninyi na kuwabariki na kuongeza idadi yenu. Atabariki uzao wa tumbo lenu, mazao ya nchi yenu, nafaka, divai mpya na mafuta, ndama za ngʼombe wa makundi yenu, na kondoo za makundi yenu katika nchi ile aliyoapa kuwapa baba zenu. 7:14 Kut 23:26Mtabarikiwa kuliko mataifa mengine yote, hakuna wanaume wala wanawake kwenu watakaokosa watoto, wala mifugo yenu haitakuwa tasa. Bwana atawakinga na kila ugonjwa. Mungu hatatia juu yenu ugonjwa wowote mbaya mlioufahamu huko Misri, lakini atatia ugonjwa juu ya wale wote wanaokuchukia. 7:16 Yos 6:2; 10:26; Amu 3:6; Ezr 9:1; Za 106:36; Kut 10:7; Amu 8:27Ni lazima mwangamize watu wote ambao Bwana Mungu wenu atawatia mikononi mwenu. Msiwatazame kwa kuwahurumia na msiitumikie miungu yao, kwa kuwa itakuwa mtego kwenu.

7:17 Hes 33:53Mnaweza kujiuliza wenyewe “Mataifa haya ni yenye nguvu kuliko sisi. Tutawezaje kuwafukuza?” 7:18 Hes 14:9; Kum 1:21; 29; Za 105:5; 119:52Lakini msiwaogope. Kumbukeni vyema jinsi Bwana Mungu wenu alivyofanya kwa Farao na kwa wote huko Misri. 7:19 Za 136:12; Kum 4:34Mliona kwa macho yenu wenyewe majaribu makubwa, ishara za miujiza na maajabu, mkono wenye nguvu na ulionyooshwa, ambao kwa huo Bwana Mungu wenu aliwatoa mtoke Misri. Bwana Mungu wenu atawafanyia hivyo watu wote ambao mnawaogopa sasa. 7:20 Kut 23:28; Yos 24:12Zaidi ya hayo, Bwana Mungu wenu atatuma manyigu miongoni mwao hadi yale mabaki watakaojificha waangamie. 7:21 Mwa 17:7; Yos 3:10; Kum 10:17; Neh 1:5; 9:32; Za 47:2; 66:3; 68:35; Isa 9:6; Dan 9:4Msiingiwe na hofu kwa sababu yao, kwa kuwa Bwana Mungu wenu, ambaye yupo miongoni mwenu ni mkuu naye ni Mungu wa kutisha. 7:22 Kut 23:30Bwana Mungu wenu atawafukuza mataifa hayo mbele yenu kidogo kidogo. Hamtaruhusiwa kuwaondoa wote kwa mara moja, la sivyo wanyama mwitu wataongezeka na kuwa karibu nanyi. 7:23 Kut 23:27; Yos 10:11Lakini Bwana Mungu wenu atawatia watu hao mikononi mwenu, akiwatia katika kuchanganyikiwa kukubwa mpaka wawe wameangamizwa. 7:24 Yos 10:24; 1:5; 10:8; 23:9; 21:44; Za 110:5; Kut 23:31; Kum 11:25; Ay 35:7, 8; Yer 32:39; Za 41:2; Lk 10:23Atawatia wafalme wao mikononi mwenu, nanyi mtayafuta majina yao chini ya mbingu. Hakuna hata mmoja atakayeweza kusimama dhidi yenu bali mtawaangamiza. 7:25 Kut 4:14; 32:20; 20:17; Yos 7:21; Amu 8:27; 1Nya 14:12; Kum 17:1; Rum 10:3Vinyago vya miungu yao mtavichoma moto. Msitamani fedha wala dhahabu iliyo juu yao, wala msizichukue kwa ajili yenu, la sivyo mtakuwa mmetekwa navyo. Kwa kuwa ni chukizo kwa Bwana Mungu wenu. 7:26 Law 27:28-29Msilete vitu vya machukizo katika nyumba zenu kwani ninyi, mtatengwa kama vitu hivyo kwa maangamizo. Ukichukie kabisa kitu hicho kwa kuwa kimetengwa kwa maangamizo.

Read More of Kumbukumbu 7

Kumbukumbu 8:1-20

Usimsahau Bwana

8:1 Kum 4:1; Kut 19:5; Ay 36:11; Za 16; 11; Eze 20:19Uwe mwangalifu kufuata kila agizo ninalokupa wewe leo, ili mweze kuishi, kuongezeka na mweze kuingia mkamiliki nchi ambayo Bwana aliahidi kwa kiapo kwa baba zenu. 8:2 Kum 29:5; Za 136:16; Amo 2:10; Mwa 22:1; Yos 6:17; 11:11; Kut 23:32; Amu 1:24; 2:2Kumbuka jinsi Bwana Mungu wenu alivyowaongoza katika njia yote katika jangwa kwa miaka hii arobaini, kukunyenyekeza na kukujaribu ili ajue lililoko moyoni mwako, kwamba utayashika maagizo yake au la. 8:3 Isa 2:11; Yer 44:10; Kut 16:14; 1Fal 8:36; Za 25:5; 94:12; 119:171; Mwa 3:19; Ay 23:12; Za 104:15; Mit 28:21; Isa 51:14; Yer 42:14; Ay 22:22; Za 119:13; 138:4; Kut 16:2-3; Mt 4:4; Lk 4:4Alikudhili na kukufanya uone njaa kisha akulishe kwa mana, ambayo wewe wala baba zako hamkuijua, awafundishe kuwa mwanadamu hataishi kwa mkate tu bali kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Bwana. 8:4 Kum 29:5; Neh 9:21Nguo zenu hazikuchakaa wala miguu yenu haikuvimba kwa miaka hii arobaini. 8:5 Kum 4:36; 2Sam 7:14; Ay 5:17; 33:19; Mit 3:11-12; Ebr 12:5-11; Ufu 3:19Mjue basi ndani ya mioyo yenu kama mtu anavyomwadibisha mwanawe, ndivyo Bwana Mungu wako atawaadibisha ninyi.

8:6 Kut 33:13; 1Fal 3:14; Za 81:13; 95:10; Kum 5:33Shikeni maagizo ya Bwana Mungu wenu mtembee katika njia zake na kumheshimu. 8:7 Za 106:24; Yer 3:19; Eze 20:6; Kum 11:9-12; Yer 2:7Kwa kuwa Bwana Mungu wenu anawaleta katika nchi nzuri, nchi yenye vijito na mabwawa ya maji, yenye chemchemi zinazotiririka mabondeni na katika vilima; 8:8 Kut 9:31; Mwa 49:11; Hes 13:23; 1Fal 4:25; Kum 32:13; Za 81:16nchi yenye ngano na shayiri, mizabibu na mitini, mikomamanga, mafuta ya zeituni na asali; 8:9 Amu 18:10; Ay 28:2nchi ambayo chakula hakitapungua na hamtakosa chochote; nchi ambayo miamba yake ni chuma na mnaweza kuchimba shaba kutoka kwenye vilima.

8:10 Kum 6:10-12Wakati mtakapokwisha kula na kushiba, msifuni Bwana Mungu wenu kwa ajili ya nchi nzuri aliyowapa. 8:11 Kum 4:9Jihadharini msimsahau Bwana Mungu wenu, mkashindwa kushika maagizo yake, sheria na amri zake ambazo ninawapa leo. 8:12 Mit 30:9; Hos 13:6Angalia wakati mtakapokuwa mmekula na kushiba, mkajenga nyumba nzuri na kukaa humo, na wakati makundi yenu ya ngʼombe na mbuzi na kondoo yatakapoongezeka na fedha na dhahabu yenu itakapoongezeka na vyote mlivyo navyo vitakapozidishwa, 8:14 Za 78:7; 106:21basi mioyo yenu isiwe na kiburi mkamsahau Bwana Mungu wenu aliyewatoa katika nchi ya Misri, kutoka nchi ya utumwa. 8:15 Kum 1:19; 32:13; 32:10; Hes 21:6; Isa 14:29; 30:6; Kut 17:6; Ay 28:9; Za 78:15; 114:8Aliwaongoza kupitia jangwa lile kubwa na la kutisha, nchi ile ya kiu isiyo na maji, yenye nyoka wa sumu na nge. Aliwatolea maji kutoka kwenye mwamba mgumu. 8:16 Kut 16:14; 16:15; Mwa 22:1; Rum 8:28; 2Kor 4:17; Ebr 12:11; Yak 1:12; 1Pet 1:7Aliwapa mana ya kula jangwani, kitu ambacho baba zenu hawakukijua, ili kuwanyenyekesha na kuwajaribu ninyi ili mwishoni apate kuwatendea mema. 8:17 Kum 9:4, 24; 31:27; Amu 7:2; Za 44:3; Isa 10:13Mnaweza kusema, “Uwezo wangu na nguvu za mikono yangu ndizo zilizonipatia utajiri huu.” 8:18 Mwa 26:13; Kum 26:10; 28:4; 1Sam 2:7; Za 25:13; 112:3; Mit 8:18; 10:22; Mhu 9:11; Hos 2:8Lakini kumbukeni Bwana Mungu wenu, ndiye ambaye huwapa uwezo wa kupata utajiri, na hivyo kulithibitisha Agano lake, ambalo aliwaapia baba zenu, kama ilivyo leo.

8:19 Kum 6:14; 4:26; 30:18; Za 16:4; Yer 7:6; 13:10; 25:6Ikiwa mtamsahau Bwana Mungu wenu, mkaifuata miungu mingine, mkaiabudu na kuisujudia, ninashuhudia dhidi yenu leo kwamba hakika mtaangamizwa. 8:20 2Fal 21:2; Za 10:16; Eze 5:5-17; Mao 1:1-22; 2:17; Dan 9:12; Zek 1:6Kama mataifa Bwana aliyoyaangamiza mbele yenu, ndivyo ninyi mtakavyoangamizwa kwa kutokumtii Bwana Mungu wenu.

Read More of Kumbukumbu 8