Kumbukumbu 4:15-49, Kumbukumbu 5:1-33 NEN

Kumbukumbu 4:15-49

Kuabudu Sanamu Kwakatazwa

4:15 Isa 40:18; 41:22-24; Kut 3:1; Yos 23:11; Mal 2:15; Mit 4:23, 27; Yer 17:21; Mdo 17:24-29Hamkuona umbo la aina yoyote siku ambayo Bwana alizungumza nanyi kule Horebu kutoka kwenye moto. Kwa hiyo mjihadhari kwa uangalifu sana, 4:16 Mwa 6:11-12; Kum 9:12; 31:29; 32:5; Amu 2:19; Kut 20:4-5; 32:7; Rum 1:23ili msije mkajichafua na kujitengenezea sanamu au kinyago chenye umbo lolote kama la mwanaume au mwanamke, 4:17 Rum 1:23au kama mnyama aliye juu ya nchi au ndege yeyote arukaye angani, au kama kiumbe kitambaacho juu ya ardhi au samaki yeyote aliye ndani ya maji. 4:19 2Fal 23:11; Kum 17:3; Ay 31:26; Yer 8:2; 43:13; Eze 8:16; Mwa 1:16; 2:1; 37:9; Rum 1:25; Kum 13:5; Hes 25:3Na utazamapo juu angani na ukaliona jua, mwezi na nyota na vyote vinavyoipamba mbingu, usije ukashawishiwa kuviinamia na kuviabudu vile ambavyo Bwana Mungu wenu alivyogawia mataifa yote chini ya mbingu. 4:20 Kut 1:13; 3:10; Mwa 17:7; Kut 8:22; 34:9; Tit 2:14; Kut 19:5Lakini kwenu ninyi, Bwana amewatoa kutoka kwenye tanuru ya kuyeyushia chuma, katika Misri kuwa watu wa urithi wake kama mlivyo sasa.

4:21 Hes 20:12; Kum 1:37Bwana alinikasirikia kwa sababu yenu na akaapa kwamba sitavuka Yordani kuingia katika nchi nzuri Bwana Mungu wenu anayowapa kuwa urithi wenu. 4:22 Hes 27:13-14; Kum 3:25Nitakufa katika nchi hii; sitavuka Yordani, lakini ninyi ni karibu mvuke mkaimiliki ile nchi nzuri. 4:23 Kut 20:4Jihadharini msilisahau Agano la Bwana Mungu wenu lile alilofanya nanyi; msijitengenezee sanamu katika umbo la kitu chochote ambacho Bwana Mungu wenu amewakataza. 4:24 Kut 15:7; 19:18; Ebr 12:29; Kut 20:5Kwa kuwa Bwana Mungu wenu ni moto ulao, Mungu mwenye wivu.

4:25 1Fal 11:6; 15:26; 16:25-30; 2Fal 17:2; 17:21Baada ya kuwa na watoto na wajukuu na kuishi katika nchi hiyo siku nyingi, tena kama mkijichafua na kutengeneza sanamu ya aina yoyote, mkifanya maovu machoni pa Bwana Mungu wenu na kumfanya awe na hasira, 4:26 Mwa 31:50; Mit 14:5; Kum 30:18-19; 31:28; 32:1; Za 50:4; Isa 1:2; 34:1; Yer 6:19; Mik 6:2; Kum 6:15; 7:4ninaziita mbingu na nchi kama mashahidi dhidi yenu siku hii kwamba mtaangamia mara moja kutoka nchi ile ambayo mnavuka Yordani kuimiliki. Hamtaishi kule kwa muda mrefu bali kwa hakika mtaangamizwa. 4:27 Law 26:23; Kum 28:36-64; 29:28; 1Fal 8:46; 2Fal 17:16; Za 44:11; 106:27; Yer 3:8; Mik 1:16; Isa 17:6; 21:17; Oba 1:5; Neh 1:8Bwana atawatawanya miongoni mwa mataifa, na ni wachache wenu tu watakaosalia miongoni mwa mataifa hayo ambayo Bwana atawafukuzia. 4:28 Kum 13:2; 28:36-64; 1Sam 26:19; Yer 5:19; 16:13; Mdo 19:26; Kum 29:17; Za 115:4-8; 135:15-18; Isa 8:19; 26:14; 44:17-20; Ufu 9:20Huko mtaabudu miungu ya miti na mawe iliyotengenezwa na watu, ambayo haiwezi kuona au kusikia wala kula au kunusa. 4:29 1Sam 13:12; 2Fal 13:4; 2Nya 7:14; 15:4; 33:12; Za 78:34; 119:58; Isa 45:19, 22; 55:6; Yer 26:19; Dan 9:13; Hos 3:5; Amo 5:4; 1Sam 7:3; 1Fal 8:48; Yer 29:13; Kum 6:5; 30:1-3, 10Lakini kama mtamtafuta Bwana Mungu wenu, mtampata; kama mtamtafuta kwa moyo wenu wote na kwa roho yote. 4:30 Hos 3:5; Law 26:41; Kum 31:17-21; Za 4:1; 18:6; 48:1; 59:16; 107:6; Kum 31:29; Yer 23:20; 3:1-12, 22; 4:1; 18:11; Ebr 1:2; Kum 30:2; 1Fal 8:48; Neh 1:9; Yoe 2:12Wakati mnapokuwa katika dhiki, nayo mambo haya yote yamewatokea siku hizo, ndipo mtamrudia Bwana Mungu wenu na kumtii. 4:31 Kut 34:6; Neh 9:31; Za 111:9; Kum 31:6-8; Yoe 1:5; 1Fal 8:57; 1Nya 28:9-20; Za 9:10; 27:9; 71:9; Isa 42:16; Ebr 13:5; Law 26:44-45; Yon 4:2Kwa maana Bwana Mungu wenu ni Mungu mwenye huruma, hatawaacha au kuwaangamiza wala kusahau Agano alilofanya na baba zenu, alilowathibitishia kwa kiapo.

Bwana Ndiye Mungu

4:32 Kum 32:7; Mwa 1:27; Isa 45:12; Kum 28:64; 30:1; Yer 9:16; Mt 24:31; 2Sam 7:23; Ay 8:8Sasa uliza kuhusu siku za zamani, zamani kabla ya wakati wako, tangu siku ile Mungu alipomuumba mtu juu ya nchi, uliza kutoka mwisho mmoja wa mbingu mpaka mwisho mwingine wa mbingu. Je, kumepata kutokea jambo jingine lililo kubwa kama hili, au kuna jambo jingine kama hilo limepata kusikiwa? 4:33 Kut 20:22; Kum 5:24-26Je, kuna watu wengine wowote waliosikia sauti ya Mungu ikizungumza kwenye moto, kama mlivyosikia, nao wakaishi? 4:34 Kut 14:30; Isa 7:12; Kut 4:17; Kum 7:19; 26:8; 29:3; 1Nya 16:12; Za 9:1; 40:5; Yer 32:20; Kut 32:20; 3:20; Kum 5:15; 6:21; 15:15; Kut 15:1; Kum 34:12; Za 45:4; 65:5Je, kuna mungu yeyote amepata kujaribu mwenyewe kuchukua taifa moja kutoka taifa lingine, kwa mapigo, kwa ishara za miujiza na maajabu, kwa vita, kwa mkono wenye nguvu na mkono ulionyooshwa au kwa matendo makuu ya kutisha, kama yale ambayo Bwana Mungu wenu aliyofanya kwa ajili yenu huko Misri mbele ya macho yenu?

4:35 Kum 4:39; 7:9; 32:4-12; Kut 8:10; 1Sam 2:2; 1Fal 8:60; 2Fal 19:19; Isa 3:10; Mk 12:32Mlionyeshwa mambo haya ili mpate kujua kuwa Bwana ndiye Mungu; hakuna mwingine ila yeye. 4:36 Kut 19:19; Kum 8:5; Kut 19:20; 18:22; 24:16; 1Nya 29:1; 2Nya 20:6; Ebr 12:18, 25Kutoka mbinguni amewasikizisha sauti yake ili kuwaadilisha. Hapa duniani aliwaonyesha moto wake mkubwa, nanyi mlisikia maneno yake kutoka kwenye ule moto. 4:37 Kum 7:8; 10:15; 23:5; 33:3; Za 44:3; Yer 31:3; Hos 11:1; Mal 1:2; 2:11; Kut 3:20; 13:3, 9-14Kwa sababu aliwapenda baba zenu na alichagua wazao wao baada yao, aliwatoa katika nchi ya Misri kwa Uwepo wake na kwa uwezo wake mkuu, 4:38 Hes 34:14-15; Kum 7:1; 9:5aliwafukuza mbele yenu mataifa makubwa na yenye nguvu kuliko ninyi na kuwaleta ninyi katika nchi yao na akawapa ninyi kuwa urithi wenu, kama ilivyo leo.

4:39 Kum 8:10; Kut 15:11; Yos 2:11; Isa 42:8; Dan 4:35Kubalini na mweke moyoni leo kuwa Bwana ndiye Mungu mbinguni juu na duniani chini. Hakuna mwingine. 4:40 Law 22:31; Mwa 26:5; Kum 5:29; 11:1; Za 105:45; Isa 48:18; Kum 5:16; 12:25; Isa 3:10; Kut 23:26; Efe 6:2-3Mshike amri na maagizo yake ninayowapa leo, ili mpate kufanikiwa ninyi na watoto wenu baada yenu, na mpate kuishi maisha marefu katika nchi awapayo Bwana Mungu wenu siku zote.

Miji Ya Makimbilio

4:41 Hes 35:6Kisha Mose akatenga miji mitatu mashariki ya Yordani, 4:42 Kut 21:13ambayo mtu yeyote aliyemuua mtu angeweza kukimbilia ikiwa amemuua jirani yake bila kukusudia na bila kuwa na chuki naye siku zilizopita. Angeweza kukimbilia katika mmojawapo ya miji hii na kuokoa maisha yake. 4:43 Yos 21:38; 1Fal 22:3; 2Fal 8:28; 9:14Miji hiyo ilikuwa: Bezeri katika tambarare ya jangwa kwa ajili ya Wareubeni; Ramothi katika nchi ya Gileadi kwa ajili ya Wagadi; nao mji wa Golani katika nchi ya Bashani kwa ajili ya Wamanase.

Utangulizi Wa Sheria

Hii ndiyo sheria Mose aliyoweka mbele ya Waisraeli. Haya ndiyo masharti, amri na sheria Mose aliyowapa wana wa Israeli wakati walitoka Misri, 4:46 Hes 21:26; Kum 3:29nao walikuwa katika bonde karibu na Beth-Peori mashariki ya Yordani, katika nchi ya Sihoni mfalme wa Waamori, ambaye alitawala Heshboni, naye alishindwa na Mose na Waisraeli walipokuja toka Misri. 4:47 Hes 21:25; Kum 3:3, 4Waliimiliki nchi yake na nchi ya Ogu mfalme wa Bashani, wafalme wawili Waamori waliotawala mashariki ya Yordani. 4:48 Kum 2:36; 3:8-9; Za 133:3Nchi hii ilienea kutoka Aroeri ukingoni mwa Bonde la Arnoni mpaka Mlima Sioni (yaani Hermoni), pamoja na eneo lote la Araba mashariki ya Yordani, na kuenea mpaka Bahari ya Araba kwenye miteremko ya Pisga.

Read More of Kumbukumbu 4

Kumbukumbu 5:1-33

Amri Kumi

(Kutoka 20:1-17)

5:1 Kut 18:20Mose akawaita Israeli wote, akawaambia:

Ee Israeli, sikilizeni amri na sheria ninazowatangazia leo. Jifunzeni, na mwe na hakika kuzifuata. 5:2 Kut 19:5Bwana Mungu wetu alifanya Agano nasi katika mlima wa Horebu. 5:3 Kum 11:2-7; Hes 26:63-65; Ebr 8:9; Mt 13:17Si kwamba Bwana alifanya Agano na baba zetu, bali alifanya nasi, nasi sote ambao tuko hai hapa leo. 5:4 Kut 19:9, 18-19; 20:22; Kum 4:33, 36; 34:10; Hes 14:4Bwana alisema nanyi uso kwa uso kutoka moto juu ya mlima. 5:5 Gal 3:19; Mwa 3:10; Ebr 12:18-21; Kut 20:18-21; 20:18-21; Hes 16:48; Za 106:23; Yer 30:21(Wakati huo nilisimama kati ya Bwana na ninyi kuwatangazia neno la Bwana, kwa sababu mliogopa ule moto, nanyi hamkupanda mlimani.) Naye Mungu alisema:

5:6 Kut 13:3; 29:46; Law 26:1; Kum 6:4; Za 81:10“Mimi ndimi Bwana Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, kutoka nchi ya utumwa.

5:7 Kut 20:3“Usiwe na miungu mingine ila mimi.

5:8 Law 26:1; Kum 4:15-16; Za 78:58; 97:7; Kut 20:4; Mdo 17:29Usijitengenezee sanamu katika umbo la kitu chochote kilicho juu mbinguni au duniani chini au ndani ya maji. 5:9 Hes 26:11; Kut 34:7; Hes 10:35; 14:18; Kut 34:7Usivisujudie wala kuviabudu; kwa kuwa Mimi, Bwana Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu, ninayewaadhibu watoto kwa ajili ya dhambi za baba zao hadi kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao, 5:10 Kut 34:2; Hes 14:18; Kum 7:9; Neh 1:5; Yer 32:18; Dan 9:4lakini ninaonyesha upendo kwa maelfu ya vizazi vya wale wanipendao na kuzishika amri zangu.

5:11 Za 139:20; Law 19:12; Kum 10:20; Mt 5:33-37Usilitaje bure jina la Bwana Mungu wako, kwa kuwa Bwana hataacha kumhesabia hatia yeye alitajaye jina lake bure.

5:12 Kut 16:23-30; 31:13; Mk 2:27-28; Kut 20:8Adhimisha siku ya Sabato na kuiweka takatifu, kama Bwana Mungu wako alivyokuagiza. Kwa siku sita utafanya kazi na kutenda shughuli zako zote. 5:14 Mwa 2:2; Mt 12:2; Mk 2:17; Ebr 4:4; Ay 31:13; Yer 34:9-11; 17:21-24Lakini siku ya Saba ni Sabato kwa Bwana, Mungu wako. Siku hiyo hutafanya kazi yoyote, wewe, wala mwanao au binti yako, wala mtumishi wa kiume au mtumishi wa kike, wala ngʼombe wako, punda wako au mnyama wako yeyote, wala mgeni aliyeko malangoni mwako, ili kwamba mtumishi wako wa kiume na wa kike wapate kupumzika kama wewe. 5:15 Mwa 15:13; Kut 6:1; Za 108:6; Yer 32:21; Kum 4:34Kumbuka mlikuwa watumwa huko Misri, na Bwana Mungu wenu aliwatoa huko kwa mkono wenye nguvu na kwa mkono ulionyooshwa. Kwa hiyo Bwana Mungu wako amekuagiza kuiadhimisha siku ya Sabato.

5:16 Mal 1:6; Kut 21:17; Law 19:3; Eze 22:7; Mt 15:4; 19:19; Mk 7:10; 10:19; Lk 18:20; Efe 6:2-3; Kum 4:40; 11:9; Mit 3:1-2Waheshimu baba yako na mama yako, kama Bwana Mungu wako alivyokuagiza, ili siku zako zipate kuwa nyingi na kufanikiwa katika nchi Bwana Mungu wako anayokupa.

5:17 Mwa 9:6; Law 24:17; Mhu 3:3; Yer 40:15; 41:3; Mt 5:21-22; 19:19; Mk 10:19; Lk 18:20; Rum 13:9; Yak 2:11Usiue.

5:18 Law 20:10; Mt 5:27-30; 19:18; Mk 10:19; Lk 18:20; Rum 13:9; Yak 2:11Usizini.

5:19 Law 19:11; Mt 19:19; Mk 10:19; Lk 18:20; Rum 13:9Usiibe.

5:20 Kut 23:1; Mt 19:18; Mk 10:19; Lk 18:20Usimshuhudie jirani yako uongo.

5:21 Rum 7:7; 13:9Usitamani mke wa jirani yako. Usitamani nyumba ya jirani yako au shamba lake, mtumishi wake wa kiume au wa kike, ngʼombe au punda wake, wala kitu chochote cha jirani yako.”

5:22 Kut 20:21; 24:12; 31:18; Kum 4:13Hizi ndizo amri alizozitangaza Bwana kwa sauti kubwa kwa kusanyiko lenu lote huko mlimani kutoka kwenye moto, wingu na giza nene, wala hakuongeza chochote zaidi. Kisha akaziandika juu ya vibao viwili vya mawe, naye akanipa mimi.

Woga Wa Watu Mlimani

(Kutoka 20:18-21)

5:23 Kut 3:16Mliposikia sauti kutoka kwenye giza, mlima ulipokuwa ukiwaka moto, viongozi wenu wote wa makabila yenu na wazee wenu walinijia mimi. 5:24 Kum 4:34; 8:5; 11:2; Isa 53:4; Kum 3:24; Kut 19:19Nanyi mkasema, “Bwana Mungu wetu ametuonyesha utukufu na enzi yake, nasi tumesikia sauti yake kutoka kwenye moto. Leo tumeona kwamba mwanadamu anaweza kuishi hata kama Mungu akizungumza naye. 5:25 Kut 20:18-19; Kum 18:16; Ebr 12:19Lakini sasa, kwa nini tufe? Moto huu mkubwa utatuteketeza sisi na tutakufa kama tukiendelea kusikia sauti ya Bwana Mungu wetu zaidi. 5:26 Kut 33:20; Kum 4:33; Amu 6:22-23; 13:22; Isa 6:5Ni mtu yupi mwenye mwili ambaye amewahi kuisikia sauti ya Mungu aliye hai akizungumza kutoka kwenye moto, kama sisi tulivyoisikia, naye akaishi? 5:27 Kut 19:8; 24:7Sogea karibu usikie yale yote asemayo Bwana Mungu wetu. Kisha utuambie chochote kile ambacho Bwana Mungu wetu anakuambia. Tutasikiliza na kutii.”

5:28 Kum 18:17Bwana aliwasikia wakati mlipozungumza nami, na Bwana akaniambia, “Nimesikia kile hawa watu walichokuambia. Kila kitu walichokisema ni kizuri. 5:29 Za 81:8, 13; Yos 22:5; Za 78:7; Kum 4:1-40; 12:25; 22:7; Isa 48:18; Kum 12:25; Yer 44:4; Mt 23:37; Lk 19:42; 2Kor 5:20; 6:1; 7:1; Ebr 12:25; Yn 15:14; Ufu 22:14Laiti kama mioyo yao ingekuwa na mwelekeo wa kuniogopa na kuzishika amri zangu zote daima, ili kwamba wafanikiwe wao pamoja na watoto wao milele!

5:30 Mal 4:4; Gal 3:19“Nenda uwaambie warudi kwenye mahema yao. 5:31 Kut 24:12Lakini wewe baki hapa pamoja nami ili niweze kukupa maagizo yote, amri na sheria ambazo utawafundisha wazifuate katika nchi ninayokwenda kuwapa waimiliki.”

5:32 Kum 4:29; 10:12; 17:11, 20; 28:14; Yos 1:7; 1Fal 15:5; 2Fal 22:2; Mit 4:27; Kum 10:12; Za 119:6; Mhu 8:12; 1Tim 4:8; Efe 6:3Hivyo kuweni waangalifu kuyafanya yale Bwana Mungu wenu aliyowaagiza; msigeuke upande wa kuume wala wa kushoto. 5:33 Isa 3:10; Yer 7:23; 38:20; Lk 1:6; Kum 4:40Fuateni yale yote ambayo Bwana Mungu wenu aliwaagiza, ili mpate kuishi, kustawi na kuziongeza siku zenu katika nchi mtakayoimiliki.

Read More of Kumbukumbu 5