Kumbukumbu 26:1-19, Kumbukumbu 27:1-26, Kumbukumbu 28:1-14 NEN

Kumbukumbu 26:1-19

Malimbuko Na Zaka

Mtakapokuwa mmeingia nchi ile ambayo Bwana Mungu wenu anawapa kama urithi na mtakapokuwa mmeimiliki na kukaa ndani yake, 26:2 Kut 22:29; 20:24; Kum 12:5; Hes 18:12; Mit 3:9; Rum 6:23; Yak 1:18chukueni baadhi ya mavuno ya kwanza ya yale yote mtakayozalisha kutoka udongo wa nchi ambayo Bwana Mungu wenu anawapa na mweke kwenye kapu. Kisha uende mahali ambapo Bwana Mungu wako atapachagua kuwa makao kwa ajili ya Jina lake na umwambie kuhani atakayekuwepo kwa wakati huo, “Ninatangaza leo kwa Bwana Mungu wako kwamba nimekuja katika nchi ambayo Bwana aliwaapia baba zetu kwamba atatupa.” Kuhani atapokea lile kapu mikononi mwako na kuliweka chini mbele ya madhabahu ya Bwana Mungu wako. 26:5 Mwa 26:13; 25:20; 34:30; 43:14; 12:2; Hes 12:12; Kum 10:22Kisha utatangaza mbele za Bwana Mungu wako: “Baba yangu alikuwa Mwaramu aliyekuwa anatangatanga, akaenda Misri pamoja na watu wachache, akaishi huko hadi akawa taifa kubwa, lenye nguvu na watu wengi. 26:6 Hes 20:15; Kut 1:13Lakini Wamisri walituonea na kututaabisha, wakitufanyisha kazi ngumu. 26:7 Mwa 21:17; Kut 3:9; 2Fal 13:4; 14:26; Mwa 16:11; Za 42:9; 44:24; 72:14Kisha tulimlilia Bwana, Mungu wa baba zetu, naye Bwana akasikia sauti yetu na akaona huzuni yetu, taabu yetu na mateso yetu. 26:8 Hes 20:16; Kut 3:20; Kum 4:34; 34:11-12Kwa hiyo Bwana akatutoa nchi ya Misri kwa mkono wenye nguvu na ulionyooshwa, pamoja na utisho mkuu, ishara za miujiza na maajabu. 26:9 Kut 3:8Akatuleta mahali hapa akatupa nchi hii, nchi inayotiririka maziwa na asali; 26:10 Kum 8:18nami sasa ninaleta malimbuko ya ardhi ambayo wewe, Ee Bwana, umenipa.” Weka kapu mbele za Bwana Mungu wako na usujudu mbele zake. 26:11 Mit 10:2226:11 Kum 12:7, 12, 18; Mhu 5:18-20; Isa 65:14; Mdo 2:46, 47; Flp 4:4; 1Tim 6:17; Za 63:3, 5Kisha wewe pamoja na Walawi na wageni wote walioko miongoni mwenu mtafurahi katika vitu vyote vizuri ambavyo Bwana Mungu wenu amewapa pamoja na wa nyumbani mwenu.

26:12 Mwa 14:20; Hes 18:24; Kum 14:28-29; Ebr 7:5-9; Law 27:30Wakati utakapokuwa umeshatoa zaka zote za mazao yako katika mwaka wa tatu, ambao ni mwaka wa zaka, utampa Mlawi, mgeni, yatima na mjane, ili waweze kula katika miji yenu na kushiba. 26:13 Za 119:141, 153, 176Kisha umwambie Bwana Mungu wako: “Nimeondoa katika nyumba yangu ile sehemu iliyowekwa wakfu na nimempa Mlawi, mgeni, yatima na mjane, kulingana na yote uliyoamuru. Sijazihalifu amri zako wala kusahau hata mojawapo. 26:14 Law 7:20; 21:1, 11; Hos 9:4Sijala sehemu iliyowekwa wakfu wakati nilipokuwa nikiomboleza, wala sijaondoa mojawapo wakati nilipokuwa najisi, wala sijatoa sehemu yake yoyote kwa wafu. Nimemtii Bwana Mungu wangu; nimefanya kila kitu ulichoniamuru. 26:15 Za 68:5; 80:14; 102:19; Isa 63:12; Zek 2:13; Kut 39:43; 2Nya 6:26-27; Mdo 7:49Angalia chini kutoka mbinguni, maskani yako matakatifu, uwabariki watu wako Israeli pamoja na nchi uliyotupa kama ulivyoahidi kwa kiapo kwa baba zetu, nchi inayotiririka maziwa na asali.”

Fuata Maagizo Ya Bwana

26:16 Kum 4:29Bwana Mungu wako anakuagiza leo kufuata amri hizi na sheria; zishike kwa bidii kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote. 26:17 Kut 19:8; Za 48:14Umetangaza leo kwamba Bwana ndiye Mungu wako na kwamba utafuata njia zake, kwamba utayashika maagizo yake, amri zake na sheria zake nawe utamtii. 26:18 Kut 6:7; Kum 7:6Naye Bwana ametangaza leo kwamba ninyi ni taifa lake, hazina yake ya thamani kama alivyoahidi, ili kwamba mpate kuyashika maagizo yake yote. 26:19 Isa 62:7; Sef 3:20; Kum 4:7-8; 28:1, 13, 44; 1Nya 14:2; Za 148:14; Isa 40:11; Kum 7:4; Kut 19:6; 1Pet 2:9Ametangaza kwamba atawaweka juu kuliko mataifa mengine aliyoyafanya katika sifa, kuwa fahari na heshima, na kwamba mtakuwa taifa takatifu kwa Bwana Mungu wenu, kama alivyoahidi.

Read More of Kumbukumbu 26

Kumbukumbu 27:1-26

Madhabahu Katika Mlima Ebali

27:1 Za 78:7Mose na wazee wa Israeli wakawaagiza watu: “Yashikeni maagizo haya yote ninayowaagiza leo. 27:2 Yos 4:1; Kut 24:4; Yos 24:26; 1Sam 7:12; Yos 8:31Mtakapokuwa mmevuka Mto Yordani na kuingia katika nchi awapayo Bwana Mungu wenu, msimamishe mawe makubwa na mkayatie lipu. 27:3 Kut 3:8; Kum 26:9Andikeni juu yake maneno yote ya sheria hii wakati mtakapokuwa mmevuka na kuingia katika nchi awapayo Bwana Mungu wenu, nchi itiririkayo maziwa na asali, kama vile Bwana, Mungu wa baba zenu, alivyowaahidi. 27:4 Kum 11:29; Yos 8:30Mtakapokuwa mmevuka Yordani, simamisheni mawe haya juu ya Mlima Ebali, kama ninavyowaagiza leo, mkayatie lipu. 27:5 Kut 20:24-25; Yos 8:31Huko mjengeeni Bwana Mungu wenu madhabahu, madhabahu ya mawe. Msitumie kifaa chochote cha chuma juu yake. Jengeni madhabahu ya Bwana Mungu wenu kwa mawe ya shambani, na mtoe sadaka za kuteketezwa juu yake kwa Bwana Mungu wenu. 27:7 Kut 32:6; Kum 16:11; Yos 8:31Toeni sadaka za amani juu yake, mkizila na kufurahia mbele za Bwana Mungu wenu. 27:8 Isa 8:1; 30:8; Hab 2:2; Yos 8:32Nanyi mtaandika maneno yote ya sheria hii kwa wazi sana juu ya mawe haya ambayo mmesimamisha.”

Laana Kutoka Mlima Ebali

27:9 Kum 17:9; 26:18Kisha Mose na makuhani, ambao ni Walawi, wakawaambia Israeli wote, “Nyamaza ee Israeli, sikiliza! Sasa umekuwa taifa la Bwana Mungu wako. Mtii Bwana Mungu wako, na kufuata amri zake na maagizo ninayokupa leo.”

Siku ile ile Mose akawaagiza watu:

27:12 Kum 11:29; Mwa 30:18; Yos 8:35; Amu 9:7Mtakapovuka Mto Yordani, makabila haya yatasimama juu ya Mlima Gerizimu kubariki watu: Simeoni, Lawi, Yuda, Isakari, Yosefu na Benyamini. 27:13 Kum 11:29Makabila haya yatasimama juu ya Mlima Ebali kwa kutamka laana: Reubeni, Gadi, Asheri, Zabuloni, Dani na Naftali.

27:14 Kum 33:10; Yos 8:33; Neh 8:7-8; Dan 9:11; Mal 2:7-9Nao Walawi watawasomea watu wote wa Israeli kwa sauti kubwa:

27:15 Kut 20:4; 34:17; 1Fal 11:5-7; 2Fal 23:13; Isa 44:9, 19; 66:3; Hes 5:22; 1Kor 14:6; Law 19:4; 26:1; Kum 4:16, 23; Isa 44:9; Hos 13:2; Hes 5:22; Yer 11:5“Alaaniwe mtu afanyaye sanamu ya kuchonga au mwenye kusubu sanamu, kitu ambacho ni chukizo kwa Bwana, kazi ya mikono ya fundi stadi, na kuisimamisha kwa siri.”

Kisha watu wote watasema, “Amen!”

27:16 Mwa 31:35; Kut 21:12; Kum 5:16; Law 19:3“Alaaniwe mtu amdharauye baba yake na mama yake.”

Kisha watu wote watasema, “Amen!”

27:17 Kum 19:14; Mit 22:28“Alaaniwe mtu asogezaye jiwe la mpaka wa jirani yake.”

Kisha watu wote watasema, “Amen!”

27:18 Law 19:14; Ay 29:15; Mit 28:10; Mt 15:14; Ufu 2:14“Alaaniwe mtu ampotoshaye kipofu njiani.”

Kisha watu wote watasema, “Amen!”

27:19 Kut 22:21; Kum 24:19; Kut 23:2; Kum 10:18; Mal 3:5“Alaaniwe mtu apotoshaye haki ya mgeni, yatima au mjane.”

Kisha watu wote watasema, “Amen!”

27:20 Mwa 34:5; Law 18:7; 1Kor 5:1“Alaaniwe mtu akutanaye kimwili na mke wa baba yake, kwa maana anadharau malazi ya baba yake.”

Kisha watu wote watasema, “Amen!”

27:21 Kut 22:19; Law 8:23“Alaaniwe mtu akutanaye kimwili na mnyama yeyote.”

Kisha watu wote watasema, “Amen!”

27:22 Law 18:9; 20:17; 2Sam 13:1“Alaaniwe mtu akutanaye kimwili na dada yake, binti wa baba yake au binti wa mama yake.”

Kisha watu wote watasema, “Amen!”

27:23 Law 20:14“Alaaniwe mtu akutanaye kimwili na mama mkwe wake.”

Kisha watu wote watasema, “Amen!”

27:24 Mwa 4:23; Law 24:17; Kut 21:12; Hes 35:31“Alaaniwe mtu amuuaye jirani yake kwa siri.”

Kisha watu wote watasema, “Amen!”

27:25 Kut 23:7-8; Law 19:16; Eze 22:12; Kum 10:17; 16:19; Za 15:5; Eze 22:12“Alaaniwe mtu apokeaye rushwa ili kumuua mtu asiye na hatia.”

Kisha watu wote watasema, “Amen!”

27:26 Law 26:14; Kum 28:15; Za 119:21; Yer 11:3; Gal 3:10; Yer 11:5“Alaaniwe mtu yule ambaye hatashikilia maneno ya sheria hii kwa kuyatekeleza.”

Kisha watu wote watasema, “Amen!”

Read More of Kumbukumbu 27

Kumbukumbu 28:1-14

Baraka Za Utiifu

(Walawi 26:3-13; Kumbukumbu 7:12-24)

28:1 Kum 15:5; Law 26:3; Hes 24:7; Kum 26:19; Kut 15:26; Za 106:3; 111:10; Isa 1:19; 3:10; Yer 11:4; 12:16; 1Nya 14:2; Rum 2:10Kama ukimtii Bwana Mungu wako kwa bidii na kufuata amri zake zote ninazokupa leo kwa bidii, Bwana Mungu wako atakuweka juu ya mataifa yote katika dunia. 28:2 Yer 32:24; Zek 1:6Baraka hizi zote zitakuja juu yako na kukupata, kama ukimtii Bwana Mungu wako:

28:3 Za 144:15; Mwa 39:5; Za 128:1-4Utabarikiwa mjini na utabarikiwa mashambani.

28:4 Mwa 49:25; Kum 8:18; Mit 10:22; 1Tim 4:8Utabarikiwa uzao wa tumbo lako, na mazao ya nchi yako na wanyama wako wachanga wa kufugwa, yaani ndama wa makundi yako ya ngʼombe, na wana-kondoo wa makundi yako.

Kapu lako na vyombo vyako vya kukandia vitabarikiwa.

28:6 Za 121:8Utabarikiwa uingiapo na utabarikiwa utokapo.

28:7 2Nya 6:34; Law 26:8, 17Bwana atasababisha adui wainukao dhidi yako kushindwa mbele yako. Watakujia kwa njia moja lakini watakimbia mbele yako kwa njia saba.

28:8 Kum 15:4Bwana ataagiza baraka juu ya ghala zako na juu ya kila kitu utakachogusa kwa mkono wako. Bwana Mungu wako atakubariki katika nchi anayokupa.

28:9 Kut 19:6; Law 26:3; Kum 7:6Bwana atakufanya kuwa taifa lake takatifu, kama alivyokuahidi kwa kiapo, kama ukishika maagizo ya Bwana Mungu wako na kwenda katika njia zake. 28:10 Hes 6:27; 1Fal 8:43; Yer 25:29; Dan 9:18; 2Nya 7:14Kisha mataifa yote ya dunia wataona kuwa unaitwa kwa jina la Bwana, nao watakuogopa. 28:11 Kum 30:9; Mwa 30:27; Mit 10:22Bwana atakupa kustawi kwa wingi, katika tunda la uzao wa tumbo lako, katika wanyama wachanga wa mifugo yako na katika mazao ya ardhi yako, katika nchi aliyowaapia baba zako kuwapa.

28:12 Ay 38:22; Za 135:7; Yer 10:13; 51:16; Za 65:11; 58:10; Yer 31:12; Law 26:4; 1Fal 8:35-36; 18:1; Za 104:13; Isa 5:6; 30:23; 32:20; 61:9; 65:23; Yer 32:38-41; Mal 3:12; Law 25:19; Kum 15:3-6; Eze 34:26Bwana atafungua mbingu, ghala zake za baraka, kukupa mvua kwa majira yake na kubariki kazi zako zote za mikono yako. Utakopesha mataifa mengi lakini hutakopa kwa yeyote. 28:13 Yer 11:6; Kum 26:19Bwana atakufanya kichwa, wala si mkia. Kama utazingatia maagizo ya Bwana Mungu wako ninayokupa siku hii ya leo na kuyafuata kwa bidii, daima utakuwa juu, kamwe hutakuwa chini. 28:14 Kum 5:32; Yos 1:7Usihalifu amri zangu zozote ninazokupa leo, kwa kwenda kuume au kushoto, kwa kufuata miungu mingine na kuitumikia.

Read More of Kumbukumbu 28