Kumbukumbu 23:1-25, Kumbukumbu 24:1-22, Kumbukumbu 25:1-19 NEN

Kumbukumbu 23:1-25

Kutengwa Na Mkutano

23:1 Law 21:20Asiingie mtu yeyote aliyehasiwa kwa kupondwa makende au kwa kukatwa uume wake katika kusanyiko la Bwana.

Mtu yeyote ambaye amezaliwa kwenye ndoa isiyo halali au wazao wake wasiingie kwenye kusanyiko la Bwana, hata mpaka kizazi cha kumi.

23:3 Mwa 19:38; Neh 13:2; Rut 4:5; Neh 4:3-7Hapatakuwa na Mwamoni au Mmoabu au yeyote wa wazao wao atakayeruhusiwa kuingia katika kusanyiko la Bwana, hata mpaka kizazi cha kumi. 23:4 Kum 2:28; Hes 23:7; 2Pet 2:15; Mwa 24:10; 14:18; Kum 2:29; 1Sam 25:11; 1Fal 18:4; Isa 63:9Kwa kuwa hawakuja kuwalaki wakiwa na mkate na maji mlipokuwa njiani mlipotoka Misri, tena walimwajiri Balaamu mwana wa Beori kutoka Pethori iliyoko Aramu-Naharaimu23:4 Yaani Mesopotamia ya Kaskazini-Magharibi. ili kuwalaani ninyi. 23:5 Hes 24:10; Yos 24:10; Mit 26:2; Kum 4:37Hata hivyo, Bwana Mungu wenu hakumsikiliza Balaamu bali aligeuza laana kuwa baraka kwenu kwa sababu Bwana Mungu wenu anawapenda. 23:6 Hes 24:17; Isa 15:1; 25:10; Yer 25:21; 27:3; 48:1; Eze 25:8; Sef 2:9; Ezr 9:12; Mt 5:43Msitafute mapatano ya urafiki nao maisha yenu yote.

23:7 Mwa 25:30; 25:26; Law 19:34; Kut 23:9; Oba 1:11-12; Law 15:1-33; Kum 10:19; Law 19:34Usimchukie Mwedomu, kwa kuwa yeye ni ndugu yako. Usimchukie Mmisri, kwa sababu uliishi kama mgeni katika nchi yake. Kizazi cha tatu cha watoto watakaozaliwa nao wanaweza kuingia katika kusanyiko la Bwana.

Unajisi Katika Kambi

Unapokuwa umepiga kambi dhidi ya adui zako, jitenge na kitu chochote kisicho safi. 23:10 Law 15:16Ikiwa mtu amechafuka kwa sababu ya kutokwa na shahawa usiku, inampasa atoke nje ya kambi na kukaa huko. 23:11 Law 15:16; 1Sam 21:5Lakini jioni ikikaribia ataoga, na baada ya jua kuzama ataingia tena kambini.

Tengeni mahali nje ya kambi ambapo mnaweza kwenda kujisaidia. Kama sehemu ya vifaa vyenu kuweni na kitu cha kulimia, nanyi mnapojisaidia, chimba shimo na kisha funika kile kikutokacho. 23:14 Mwa 3:8; Kut 3:4-5; Law 26:12; Yer 32:40; 2Kor 6:16Kwa kuwa Bwana Mungu wenu hutembea katika kambi yenu ili kuwalinda na kuwaweka adui zenu mikononi mwenu. Kambi yenu ni lazima iwe takatifu, ili asione kitu chochote miongoni mwenu kilicho kichafu akageuka na kuwaacha.

Sheria Mbalimbali

23:15 2Sam 22:3; Za 2:12; 71:1; 1Sam 30:15Ikiwa mtumwa amekimbilia kwako, usimrudishe kwa bwana wake. 23:16 Kut 22:21; 23:6; Mt 22:22; Yer 7:6; Zek 7:10; Yak 2:6Mwache aishi miongoni mwenu mahali popote anapopapenda na katika mji wowote anaochagua. Usimwonee.

23:17 1Fal 14:24; 15:12; 22:46; 2Fal 23:7; Ay 36:14; Mwa 38:21; Law 19:29; Mit 2:16; Mwa 19:5Asiwepo Mwisraeli mwanamke kahaba au mwanaume hanithi wa mahali pa kuabudia miungu. 23:18 Mwa 19:5; Law 20:13; Ufu 22:15Kamwe usilete mapato ya ukahaba ikiwa ni ya mwanamke au ni ya mwanaume katika nyumba ya Bwana Mungu wako kwa ajili ya nadhiri yoyote, kwa sababu Bwana Mungu wako anachukizwa na yote mawili.

23:19 Law 25:35-37; Neh 5:2-7; Kut 22:25; Za 15:5; Lk 6:34Usimtoze ndugu yako riba, iwe ni fedha ama chakula ama kitu kingine chochote ambacho waweza kupata riba juu yake. 23:20 Hes 6:21; Amu 11:35; Za 15:4; Hes 30:1-2; Ay 22:27; Za 61:8; 65:1; 76:11; Mhu 5:4-5; Isa 19:21; Mt 5:33; Mdo 5:3; Kum 25:10; 28:12; Law 19:34Unaweza kumtoza mgeni riba, lakini siyo nduguyo Mwisraeli, ili kwamba Bwana Mungu wako akubariki katika kila kitu unachoweka mkono katika nchi unayoingia kuimiliki.

23:21 Ay 22:27; Za 61:8; Mhu 5:4-5Ukiweka nadhiri kwa Bwana Mungu wako, usichelewe kuitimiza, kwa kuwa Bwana Mungu wako atakudai, nawe utakuwa na hatia ya dhambi. 23:22 Mdo 5:4Lakini ukijizuia kuweka nadhiri, hutakuwa na hatia. 23:23 Za 66:13Chochote kitakachotamkwa kwa midomo yako ni lazima uhakikishe umekifanya, kwa sababu uliweka nadhiri yako kwa hiari mbele za Bwana Mungu wako kwa kinywa chako mwenyewe.

23:24 Mt 12:1; Lk 12:15; 1Kor 6:10; Kol 3:5Kama ukiingia katika shamba la mizabibu la jirani yako, unaweza kula zabibu kadiri utakavyo, lakini usiweke chochote kwenye kikapu chako. 23:25 Mt 12:1; Mk 2:23; Lk 6:1Kama ukiingia katika shamba la nafaka la jirani yako, unaweza kukwanyua kwa mikono yako, lakini usikate kwa mundu nafaka iliyosimama.

Read More of Kumbukumbu 23

Kumbukumbu 24:1-22

Sheria Kuhusu Ndoa Na Talaka

24:1 Kum 22:13; 2Fal 17:6; Isa 50:1; Yer 3:8; Mt 1:19; 5:31; 19:7-9; Mk 10:4-5; Mal 2:16Ikiwa mtu atamwoa mke na akamchukia kwa sababu ya kukosa adabu, naye akamwandikia hati ya talaka, akampa na kumfukuza kutoka nyumbani kwake, ikiwa baada ya kuondoka nyumbani kwake atakuwa mke wa mtu mwingine, ikiwa mume wake wa pili atachukizwa naye akamwandikia hati ya talaka, akampa na kumfukuza kutoka nyumbani kwake, au kama akifa, 24:4 Yer 3:1basi yule mume wake wa kwanza, ambaye alimpa talaka, haruhusiwi kumwoa tena baada ya mwanamke huyo kuwa najisi. Hayo yatakuwa machukizo machoni pa Bwana. Usilete dhambi juu ya nchi ambayo Bwana Mungu wako anakupa kama urithi.

24:5 Kum 20:7; Mit 5:18Kama mtu ameoa karibuni, kamwe asipelekwe vitani au kupewa wajibu mwingine wowote. Kwa mwaka mmoja atakuwa huru kubaki nyumbani ili amfurahishe mke aliyemwoa.

24:6 Kut 22:22; Isa 47:2Usitoe jozi ya mawe ya kusagia, hata ikiwa lile la juu, kuweka rehani kwa ajili ya deni, kwa sababu itakuwa ni kuweka uhai wa mtu kama dhamana.

24:7 Yer 11:2; Ebr 9:15; 10:15-17; Mwa 17:9; Kut 3:1; Kum 4:2324:7 Kut 21:16; 1Kor 5:13Kama mtu akikamatwa akiiba yeyote miongoni mwa ndugu zake wa Waisraeli na kumtenda kama mtumwa au akimuuza, mwizi huyo ni lazima auawe. Nawe utaondoa uovu kutoka miongoni mwenu.

24:8 Law 13:1-46; Kum 17:9; Law 14:2; Mt 8:4; Lk 5:14; 7:14Pakitokea magonjwa ya ngozi ya kuambukiza, mwe waangalifu sana kufanya sawasawa na maagizo ya makuhani, ambao ni Walawi. Ni lazima mfuate kwa uangalifu yale niliyowaamuru. 24:9 Hes 12:10; Lk 17:32; 1Kor 10:6Kumbukeni kile Bwana Mungu wenu alichomfanyia Miriamu njiani baada ya ninyi kutoka Misri.

24:10 Kut 22:25-27Unapomkopesha jirani yako chochote, usiingie nyumbani kwake kutwaa kile anachokitoa kama rehani. Ukae nje na umwache huyo mtu uliyemkopesha akuletee hiyo rehani. 24:12 Kut 22:26Ikiwa mtu huyo ni maskini, usiende kulala ukiwa na hiyo rehani yake katika milki yako. 24:13 Kut 22:26-27; Kum 6:25; Za 106:31; Dan 4:27; Ay 24:7, 8; 31:16-20; Eze 18:7, 12, 16; 33:15; Amo 2:8; Ay 29:11; 2Kor 9:13; 2Tim 1:18Rudisha vazi lake kabla ya machweo ya jua ili apate kulilalia. Kisha atakushukuru na kitaonekana kama kitendo cha haki mbele za Bwana Mungu wako.

24:14 Law 19:13; 25:35-43; Kum 15:12-18; Ay 24:4; Mit 14:31; 19:17; 1Tim 5:18; Amo 4:1; Mal 3:5Usimwonee mtu maskini na mhitaji ambaye umemwajiri, akiwa ni nduguyo Mwisraeli au mgeni anayeishi katika mojawapo ya miji yenu. 24:15 Law 25:35; 19:13; Mt 20:8; Kut 22:23; Ay 12:19; Yak 5:4; Yer 22:13Mlipe ujira wake kila siku kabla ya jua kutua, kwa sababu yeye ni maskini na anautegemea ujira huo. La sivyo, anaweza kumlilia Bwana dhidi yako, nawe ukapata hatia ya dhambi.

24:16 Hes 26:11; Yer 31:29-30; Eze 18:20; 2Fal 14:6Baba wasiuawe kwa ajili ya watoto wao, wala watoto wasiuawe kwa ajili ya baba zao; kila mmoja atakufa kwa ajili ya dhambi yake mwenyewe.

24:17 Kut 22:22; Ay 6:27; 24:9; 29:12; Za 10:17-18; 82:3; Mit 23:10; Eze 22:7; Kut 22:21; 23:2; Kum 10:18Usipotoshe hukumu ya mgeni au yatima, au kuchukua vazi la mjane kama rehani. Kumbukeni kwamba mlikuwa watumwa huko Misri, naye Bwana Mungu wenu akawakomboa kutoka huko. Hii ndiyo sababu ninawaamuru kutenda hili.

24:19 Law 19:9; Kum 10:19; 27:19; Eze 47:22; Zek 7:10; Mal 3:5; Kum 14:29; Law 23:22; Mit 19:17; 28:27; Mhu 11:1Unapovuna shamba lako na ukasahau mganda, usirudi kuuchukua. Acha kwa ajili ya mgeni, yatima na mjane, ili Bwana Mungu wako aweze kukubariki wewe katika kazi zote za mikono yako. 24:20 Law 19:10Unapovuna zeituni kutoka miti yako, usirudie matawi mara ya pili. Acha kilichobaki kwa ajili ya mgeni, yatima na mjane. Unapochuma zabibu katika shamba lako la mizabibu usirudie tena. Acha zinazobaki kwa ajili ya mgeni, yatima na mjane. Kumbuka kwamba mlikuwa watumwa katika nchi ya Misri. Ndiyo sababu ninawaamuru kufanya hili.

Read More of Kumbukumbu 24

Kumbukumbu 25:1-19

25:1 Kut 21:6; Kum 17:8-13; 19:17; Mdo 23:3; 1Fal 8:32; Kut 23:7; Kum 1:16-17Watu wanapokuwa na ugomvi, wapeleke mahakamani na waamuzi wataamua shauri hilo; watawaachia wasio na kosa na kuwahukumu wenye hatia. 25:2 Mit 10:13; 19:29; Lk 12:48-49Kama mtu mwenye hatia anastahili kuchapwa, mwamuzi atamwamuru alale chini ili achapwe mbele yake idadi ya viboko kulingana na kosa lake, 25:3 Mt 27:26; Yn 19:1; 2Kor 11:24; Ay 18:3; Yer 20:2lakini kamwe asichapwe zaidi ya viboko arobaini. Ikiwa atachapwa zaidi ya viboko arobaini, nduguyo atadhalilika machoni pako.

25:4 Hes 22:29; 1Kor 9:9; 1Tim 5:18Usimfunge maksai kinywa anapopura nafaka.

25:5 Rut 4:10-13; Mt 22:24; Mk 12:19; Lk 20:28Ikiwa ndugu wanaishi pamoja na mmoja wao akafa bila kuacha mwana, kamwe mjane wake asiolewe nje ya jamaa hiyo. Ndugu wa mumewe atamchukua, amwoe na kutimiza wajibu wa shemeji kwake. 25:6 Mwa 38:9; Rut 4:5, 10Mwana wa kwanza atakayemzaa atapewa jina la ndugu aliyekufa ili jina lake lisifutike katika Israeli.

25:7 Rut 1:15; 4:2-6; Mwa 23:10Hata hivyo, ikiwa ndugu huyo wa mume hataki kuoa huyo mke wa nduguye, mjane atawaendea wazee kwenye lango la mji na kusema, “Ndugu wa mume wangu anakataa kuendeleza jina la nduguye katika Israeli. Hataki kutimiza wajibu wa shemeji kwangu.” Ndipo wazee wa mji wake watamwita na kuzungumza naye. Kama atashikilia kukataa akisema, “Sitaki kumwoa,” 25:9 Yos 24:22; Rut 4:7-11; Hes 12:14; Ay 17:6; 30:10; Isa 50:6mjane wa nduguye atamwendea mbele ya wazee, atamvua kiatu kimoja na kumtemea mate usoni, na kusema, “Hivi ndivyo ambavyo hufanywa kwa mtu ambaye atakataa kuendeleza jamaa ya ndugu yake.” 25:10 Mit 6:33; 1Tim 3:7Jamaa ya mtu huyo itafahamika katika Israeli kama Jamaa ya Aliyevuliwa Kiatu.

Ikiwa watu wawili wanapigana na mke wa mmoja wao akaja kumwokoa mumewe na yule anayemshambulia, naye mke huyo akifika na kumkamata sehemu za siri, 25:12 Kum 7:2; 19:13huyo mwanamke utamkata mkono wake. Usimhurumie.

25:13 Mit 11:1; 20:23; Eze 45:10; Mik 6:11; Amo 8:5Usiwe na mawe ya kupimia ya aina mbili katika mkoba wako, moja zito na jingine jepesi. 25:14 Law 7:20; Hos 9:4Usiwe na vipimo viwili tofauti katika nyumba yako, kimoja kikubwa, kingine kidogo. 25:15 Kut 20:12Ni lazima uwe na uzito na vipimo sahihi na vya haki, ili upate kuishi maisha marefu katika nchi anayokupa Bwana Mungu wako. 25:16 Mit 11:1; 20:23; Amo 8:9-11; Ufu 21:27; 1Tim 4:6; 1Kor 8:9-11Kwa maana Bwana Mungu wako humchukia yeyote ambaye hufanya mambo kama haya, yeyote anayetenda kwa udanganyifu.

25:17 Mwa 36:12; Kut 17:8Kumbuka kile Waamaleki walichowatendea mlipokuwa njiani mkitoka Misri. 25:18 Za 36:1; Rum 3:18; Mit 16:6Wakati mlipokuwa mmechoka na kuishiwa nguvu kwa safari yenu, wakawapiga wale wote waliokuja nyuma. Waamaleki hawakumwogopa Mungu. 25:19 Kut 33:14; Ebr 3:18-19; Es 9:16; Mwa 36:12; 1Sam 15:2-3Bwana Mungu wako atakapokupa pumziko mbali na adui zako wote wanaokuzunguka katika nchi akupayo kuimiliki kuwa urithi, utafutilia mbali kumbukumbu lote la Waamaleki chini ya mbingu. Usisahau!

Read More of Kumbukumbu 25