Kumbukumbu 21:1-23, Kumbukumbu 22:1-30 NEN

Kumbukumbu 21:1-23

Upatanisho Kuhusu Mauaji

21:1 Hes 25:17; Za 9:12; Mit 28:17Kama mtu akikutwa ameuawa, naye amelala kwenye shamba katika nchi ambayo Bwana Mungu wenu anawapa kuimiliki, wala haijulikani ni nani aliyemuua, wazee wenu na waamuzi watatoka na kupima umbali kutoka maiti alipolala mpaka kwenye miji ya jirani. 21:3 Hes 19:2Kisha wazee wa ule mji ulio karibu zaidi na yule maiti watamchukua mtamba ambaye hajapata kufanyishwa kazi na ambaye hajafungwa nira, na kumpeleka kwenye bonde ambalo halijapata kulimwa au kupandwa mazao na ambapo kuna chemchemi itiririkayo. Huko kwenye hilo bonde, wazee watamvunja yule mtamba shingo. 21:5 Mwa 48:20; Kut 39:43; Kum 17:8-11Makuhani, hao wana wa Lawi, watasogea mbele, kwa kuwa Bwana Mungu wenu, amewachagua kuhudumu na kutoa baraka katika jina la Bwana, na kuamua mashauri yote ya mabishano na mashambulio. 21:6 Mt 27:24; 1Nya 23:1321:6 Ay 9:30; Za 19:12; Yer 2:22; Mt 27:14; Ebr 9:10Ndipo wazee wote wa mji ulio karibu zaidi na huyo maiti watanawa mikono yao juu ya huyo mtamba ambaye shingo yake imevunjwa huko kwenye bonde, 21:7 2Sam 3:28nao watatangaza: “Mikono yetu haikumwaga damu hii, wala macho yetu hayakuona likifanyika. 21:8 Hes 35:33-34; Yer 26:15; Eze 22:3; Yn 1:14Ee Bwana, ukubali upatanisho kwa watu wako Israeli, ambao umewakomboa, wala usiwahesabie watu wako hatia ya damu ya mtu asiyekuwa na hatia.” Nayo damu iliyomwagika itakuwa imefanyiwa upatanisho. 21:9 Kum 19:13Hivyo mtakuwa mmejitakasa wenyewe kutoka hatia ya kumwaga damu isiyokuwa na hatia, kwa kuwa mmefanya lile lililo sawa mbele za macho ya Bwana.

Kuoa Mwanamke Mateka

21:10 Yos 21:44; 1Fal 8:46; 1Nya 9:1; Ezr 5:12; Yer 40:1; Eze 1:1; 17:12; Dan 2:25; Mik 4:10; 2Nya 32:8Mkienda vitani kupigana na adui zenu naye Bwana Mungu wenu akawatia adui mikononi mwenu, nanyi mkachukua mateka, 21:11 Mwa 6:2; 34:8kama ukiona miongoni mwa mateka mwanamke mzuri wa sura nawe wavutwa naye, waweza kumwoa akawa mke wako. 21:12 Law 14:9; Hes 8:7; 1Kor 11:5; Hes 6:9Mlete nyumbani mwako, anyoe nywele na kukata kucha zake, 21:13 Za 45:10avue nguo alizokuwa amevaa alipotekwa. Baada ya kuishi nyumbani mwako na kumwombolezea baba yake na mama yake kwa mwezi mzima, ndipo utakapoweza kumwendea na kuwa mume wake naye atakuwa mke wako. 21:14 Mwa 34:2; Amu 19:24Lakini kama hutaendelea kupendezwa naye, mwache aende popote anapotaka. Kamwe huwezi kumuuza au kumtendea kama mtumwa, kwa sababu utakuwa umemvunjia heshima.

Haki Ya Mzaliwa Wa Kwanza

21:15 Mwa 4:19; 29:33Kama mwanaume ana wake wawili, naye anampenda mmoja na mwingine hampendi na wote wawili wamemzalia wana wa kiume, lakini mwana mzaliwa wa kwanza ni wa yule mke asiyempenda, 21:16 1Nya 26:10; Rum 8:29wakati anapotoa wosia wa mali yake kwa wanawe, kamwe asitoe haki za mzaliwa wa kwanza kwa mwana wa mke ampendaye kwa upendeleo, badala ya mzaliwa hasa wa kwanza, ambaye ni mwana wa mke ambaye hampendi. 21:17 2Fal 2:9; Isa 40:2; 61:7; Zek 9:12; Mwa 49:3; 25:31; Lk 15:12; 1Nya 5:1Ni lazima amkubali mwana wa mke asiyempenda kama mzaliwa wa kwanza kwa kumpa sehemu ya vile vyote alivyo navyo maradufu. Mwana huyo ni ishara ya kwanza ya nguvu za baba yake. Haki ya mzaliwa wa kwanza ni yake yeye.

Mwana Mwasi

21:18 Za 78:8; Yer 5:23; Sef 3:1; Mit 30:17; Mwa 31:35; Mit 1:8; Isa 30:1; Efe 6:1-3; Kut 20:12; 21:15, 17; Law 19:3; 21:9Kama mtu ana mwana mkaidi na mwasi ambaye hamtii baba yake na mama yake, na hasikii wazazi wanapomrudi, baba yake na mama yake watamleta kwa wazee kwenye lango la mji wake. Watawaambia wazee, “Huyu mwanetu ni mkaidi na mwasi. Hatutii sisi, yeye ni mpotovu na mlevi.” 21:21 Law 20:9; Kum 19:19; 1Kor 5:13; Kum 13:11; 1Sam 26:16Kisha wanaume wote wa mjini mwake watampiga kwa mawe mpaka afe. Ndivyo imewapasa kuondoa maovu kati yenu. Israeli yote itasikia hili na kuogopa.

Sheria Mbalimbali

21:22 Kum 22:26; Mt 26:66; Mk 14:64; Mdo 23:29Kama mtu ana hatia ya kosa linalompasa kuuawa naye akauawa, mwili wake utaangikwa mtini, 21:23 Yos 8:29; 10:27; Yn 19:31; Eze 39:12; Ezr 6:11; Es 2:23; 7:9; 8:7; 9:13, 25; Isa 50:11; Gal 3:13; Law 18:25kamwe msiuache mwili wake mtini usiku kucha. Hakikisheni mnauzika mwili wake siku ile ile, kwa sababu kila mtu anayeangikwa mtini yupo chini ya laana ya Mungu. Msiinajisi nchi ambayo Bwana Mungu wenu anawapa kama urithi wenu.

Read More of Kumbukumbu 21

Kumbukumbu 22:1-30

22:1 Kut 23:4-5; Mit 27:10; Zek 7:9Kama ukimwona ngʼombe au kondoo wa ndugu yako anapotea, usipuuze, bali uhakikishe unamrudisha kwa mwenyewe. Ikiwa huyo ndugu haishi karibu nawe au kama hufahamu yeye ni nani, mchukue nyumbani kwako huyo mnyama umweke mpaka mwenyewe aje kumtafuta. Ndipo umrudishie. Fanya vivyo hivyo ukimkuta punda wa nduguyo au joho lake au chochote alichopoteza. Usipuuze jambo hilo.

22:4 Kut 23:5; 1Kor 9:9; Rum 12:10; 2Pet 1:7; 1Yn 3:15; 4:21; Zek 7:9Kama ukimwona punda wa nduguyo au ngʼombe wake ameanguka barabarani, usipuuze jambo hilo. Msaidie asimame kwa miguu yake.

22:5 1Kor 14:40Haimpasi mwanamke kuvaa nguo za kiume wala mwanaume kuvaa nguo za kike, kwa maana Bwana Mungu wenu anachukia yeyote ambaye hufanya hivi.

22:6 Law 22:28; Neh 9:6; Za 36:6; 145:9; Mt 10:29; Lk 12:6Kama ukikuta kiota cha ndege kando ya barabara, iwe juu ya mti au chini, naye ndege amelala juu ya makinda au mayai, usimchukue huyo ndege pamoja na makinda yake. 22:7 Law 22:28; Kum 5:29; 4:20Waweza kuchukua makinda, lakini uwe na hakika ya kumwacha huyo ndege, ili upate kufanikiwa na uweze kuishi maisha marefu.

22:8 Yos 2:8; 1Sam 11:2Wakati unapojenga nyumba mpya, fanya ukuta wa kuzuia kandokando ya dari ili usijiletee hatia ya kumwaga damu juu ya nyumba yako ikiwa yeyote ataanguka kutoka humo.

22:9 Law 19:9; Mt 6:24; 9:16; 2Kor 6:14-16Usipande aina mbili za mbegu katika shamba lako la mizabibu; ikiwa utafanya hivyo, si mazao utakayopanda tu yatakuwa najisi, bali nayo matunda ya shamba la mizabibu pia.

22:10 2Kor 6:14-16Usilime kwa maksai aliyefungwa nira pamoja na punda.

22:11 Law 19:9; 19:19Usivae nguo za sufu na kitani zilizofumwa pamoja.

22:12 Hes 15:37-41; Mt 23:5Fanya vishada kwenye pembe nne za joho unalovaa.

Kukiuka Taratibu Za Ndoa

22:13 Kum 24:1; Mwa 29:21; Amu 15:1; Efe 5:28-29Ikiwa mtu atamwoa mke na, baada ya kufanya naye tendo la ndoa, akamchukia, akimsingizia na kumwita jina baya, akisema, “Nilimwoa mwanamke huyu, lakini nilipomkaribia sikupata uthibitisho wa ubikira wake” 22:15 Mwa 23:10ndipo baba na mama wa msichana wataleta uthibitisho kwamba alikuwa bikira kwa wazee wa mji kwenye lango. Baba wa msichana atawaambia wazee, “Nilimwoza binti yangu kwa huyu mwanaume, lakini hampendi. Sasa amemsingizia na kusema, ‘Sikumkuta huyu binti akiwa bikira.’ Lakini hapa kuna uthibitisho wa ubikira wa binti yangu.” Kisha wazazi wake wataonyesha nguo zake kwa wazee wa mji, 22:18 Kut 18:21; Kum 1:9-18; Rum 13:3nao wazee watamchukua huyo mwanaume na kumwadhibu. Watamtoza shekeli mia moja22:19 Shekeli 100 za fedha ni sawa na kilo moja. za fedha na kupewa wazazi wa msichana, kwa sababu mwanaume huyu amempa bikira wa Kiisraeli jina baya. Ataendelea kuwa mke wake; kamwe hawezi kumpa talaka siku zote za maisha yake.

22:20 Kum 17:4Hata hivyo, kama shtaka ni la kweli na hakuna uthibitisho juu ya ubikira wa huyo msichana ulioweza kupatikana, 22:21 Mwa 34:7; 38:24; Law 19:29; Kum 23:17-18; 1Kor 5:13; 2Sam 13:12, 13huyo msichana ataletwa kwenye mlango wa nyumba ya baba yake, na hapo watu wa mji wake watampiga kwa mawe hadi afe. Amefanya kitu cha aibu katika Israeli kwa kufanya ukahaba akiwa nyumbani kwa babaye. Lazima mwondoe uovu katikati yenu.

22:22 2Sam 11:4; Mwa 38:24; Kut 21:12; Mt 5:27-28; Yn 8:5; 1Kor 6:9; Ebr 13:4; Law 20:10; Mit 6:22; Mal 3:5; Yn 8:5Ikiwa mwanaume atakutwa akizini na mke wa mtu mwingine, wote wawili, mwanaume na mwanamke aliyezini naye, lazima wauawe. Lazima mwondoe uovu katika Israeli.

22:23 Mt 1:18, 19Ikiwa mwanaume atakutana na bikira mjini ambaye ameposwa na mtu akazini naye, 22:24 1Kor 5:13; Kum 21:14; Mt 1:20, 24utawachukua wote wawili kwenye lango la mji na kuwapiga kwa mawe mpaka wafe; yule msichana kwa kuwa alikuwa mjini na hakupiga kelele kuomba msaada, na yule mwanaume kwa sababu amemtenda jeuri mke wa mtu mwingine. Lazima mwondoe uovu katikati yenu.

Lakini ikiwa itatokea mwanaume akakutana na msichana aliyeposwa huko mashambani, akambaka, mwanaume aliyefanya hivi peke yake ndiye atakayeuawa. Usimtendee msichana yule jambo lolote; hajafanya dhambi inayostahili kifo. Shauri hili ni kama lile la yeyote ambaye anamshambulia na kumuua kwa makusudi jirani yake, 22:27 Mwa 39:14kwa maana mwanaume huyo alimkuta msichana huko mashambani, na ingawa msichana aliyeposwa alipiga kelele, hapakuwa na mtu wa kumwokoa.

22:28 Kut 22:16, 17Ikiwa itatokea mwanaume akutane na bikira ambaye hajaposwa na kumbaka nao wakakutwa, mwanaume atamlipa baba wa msichana shekeli hamsini22:29 Shekeli 50 za fedha ni sawa na gramu 600. za fedha. Ni lazima amwoe huyo msichana, kwa maana amemfanyia jeuri. Kamwe hawezi kumpa talaka siku zote za maisha yake.

22:30 Mwa 29:29; Law 18:8; 20:9; Kum 27:20Mwanaume asimwoe mke wa baba yake; kamwe asidhalilishe kitanda cha baba yake.

Read More of Kumbukumbu 22