Kumbukumbu 19:1-21, Kumbukumbu 20:1-20 NEN

Kumbukumbu 19:1-21

Miji Ya Makimbilio

(Hesabu 35:9-34; Yoshua 20:1-9)

19:1 Kum 6:10-11; 12:29Wakati Bwana Mungu wenu atakapokuwa amewaangamiza mataifa ambayo nchi yao anawapa ninyi, wakati mtakapokuwa mmewafukuza na kuishi katika miji yao na nyumba zao, 19:2 Yos 20:2ndipo mtenge miji mitatu iliyopo katikati ya nchi kwa ajili yenu, katika nchi ambayo Bwana Mungu wenu anawapa kuimiliki. Jengeni barabara katika miji hiyo na kuigawa mara tatu, nchi anayowapa Bwana Mungu wenu kama urithi, ili kwamba yeyote amuuaye mtu aweze kukimbilia humo.

Hii ndiyo kanuni kuhusu mtu amuuaye mwingine na kukimbilia humo kuokoa maisha yake, yaani, yeye amuuaye jirani yake bila kukusudia, wala hakumchukia kabla ya hapo. Kwa mfano, mtu aweza kwenda msituni na jirani yake kukata miti, naye anapozungusha shoka kuangusha mti, shoka linaweza kuchomoka kutoka kwenye mpini na kumpiga jirani yake na kumuua. Yule mtu anaweza kukimbilia katika mmojawapo ya miji hii na kuokoa maisha yake. 19:6 Hes 35:12Kama sivyo, mlipiza kisasi cha damu anaweza kumfuatilia kwa hasira kali, naye akamkamata na kumuua kama umbali ni mrefu sana hata ingawa hastahili kifo, kwa sababu amemuua jirani yake bila kukusudia. Hii ndiyo sababu nimewaagiza ninyi kutenga miji mitatu ya makimbilio kwa ajili yenu.

19:8 Kut 34:24; Mwa 15:18; Kum 11:24Kama Bwana Mungu wenu akipanua nchi yenu, kama alivyoahidi kwa kiapo kwa baba zenu na kuwapa nchi yote aliyowaahidi, 19:9 Kum 6:5; Yos 20:7-8kwa sababu mmefuata kwa uangalifu sheria zote ninazowaamuru leo, kumpenda Bwana Mungu wenu na kuenenda siku zote katika njia zake, ndipo mtenge miji mingine, mitatu zaidi. 19:10 Mit 6:17; Yer 7:6; 26:15; Kum 21:1-9; Hes 35:33Fanyeni hivi ili damu isiyo na hatia isimwagwe katika nchi yenu, ambayo Bwana Mungu wenu anawapa kama urithi wenu, ili kwamba msije mkawa na hatia ya kumwaga damu.

19:11 Kut 21:12; Hes 35:16; 1Yn 3:15; Mit 28:17; 29:10Lakini kama mtu anamchukia ndugu yake, akamvizia, akamshambulia na kumuua, kisha akakimbilia katika mmojawapo ya miji hii, wazee wa mji wake watatuma ujumbe kwake, kumleta kutoka mji ule na kumkabidhi mlipiza kisasi cha damu kumuua. 19:13 Kum 7:2; 21:9; 1Fal 2:31Msimwonee huruma. Lazima mwondoe katika Israeli hatia ya umwagaji damu isiyo na hatia ili kwamba mpate kufanikiwa.

19:14 Kum 27:17; Ay 24:2; Za 16:6; Mit 15:25; 22:28; 23:10; Isa 1:23; Hos 5:10Usisogeze jiwe la mpaka wa jirani yako ambao uliwekwa na wale waliokutangulia katika urithi upokeao katika nchi Bwana Mungu wako anayowapa kuimiliki.

Mashahidi

19:15 Kum 17:6; Mt 18:16; 26:60; 2Kor 3:1; Yn 8:17; 1Tim 5:19; Ebr 10:28Shahidi mmoja hatoshi kumtia hatiani mtu kwa uhalifu au kosa lolote ambalo anaweza kuwa amelitenda. Lazima shauri lolote lithibitishwe kwa ushuhuda wa mashahidi wawili au watatu.

19:16 Kut 23:1; Mit 6:19; Za 27:12; 1Fal 21:13Kama shahidi mwenye nia ya kumdhuru mwingine akisimama kumshtaki mtu kwa uhalifu, 19:17 Kut 21:6; Kum 17:6watu wawili wanaohusika katika mabishano lazima wasimame mbele za Bwana na mbele ya makuhani na waamuzi ambao wako kazini wakati huo. 19:18 Kut 23:7Waamuzi lazima wafanye uchunguzi kwa makini na shahidi akionekana kuwa ni mwongo, akitoa ushuhuda wa uongo dhidi ya ndugu yake, 19:19 Mit 19:5-10; 1Kor 5:13; Dan 6:24basi mtende kama alivyotaka kumtendea ndugu yake. Ni lazima mwondoe uovu miongoni mwenu. 19:20 Kum 13:11; 17:13; 13:13; 21:21Watu watakaosalia watasikia hili na kuogopa, uovu kama huo kamwe hautatendeka tena miongoni mwenu. 19:21 Kut 21:24; Mt 5:38Msionyeshe huruma, uhai kwa uhai, jicho kwa jicho, jino kwa jino, mkono kwa mkono, mguu kwa mguu.

Read More of Kumbukumbu 19

Kumbukumbu 20:1-20

Kwenda Vitani

20:1 Za 20:7; Isa 31:1; Hes 14:9; Kum 3:22; 1Sam 17:45; Isa 41:10; 2Nya 32:7-8; Hes 23:21; Kum 31:6, 8; 2Nya 13:12; 32:7, 8Mtakapokwenda vitani kupigana na adui zenu na mkaona farasi na magari ya vita na jeshi kubwa kuliko lenu, msiwaogope, kwa sababu Bwana Mungu wenu aliyewatoa kutoka Misri, atakuwa pamoja nanyi. Wakati mtakapokaribia kwenda vitani, kuhani atakuja mbele na kuhutubia jeshi. 20:3 1Sam 17:32; Ay 23:16; Za 22:14; Isa 7:4; 35:4; Yer 51:46Atasema: “Sikia, ee Israeli, leo unakwenda vitani kupigana na adui zako. Usife moyo wala usiogope, usitishwe wala usitiwe hofu mbele yao. 20:4 2Nya 20:14-22; Kut 14:14; 1Nya 5:22; Neh 4:20; Amu 12:3; 15:18; Za 44:7; 144:10; Kum 1:30Kwa kuwa Bwana Mungu wenu ndiye huenda pamoja nanyi kuwapigania dhidi ya adui zenu na kuwapatia ushindi.”

20:5 Neh 12:27Maafisa wataliambia jeshi: “Je, kuna yeyote aliyejenga nyumba mpya ambayo haijawekwa wakfu? Yeye na arudi nyumbani, ama sivyo anaweza kufa vitani na mtu mwingine akaiweka wakfu. 20:6 Yer 31:5; Eze 28:26; Mik 1:6; 1Kor 9:7Je, kuna yeyote aliyepanda shamba la mizabibu na hajaanza kulifurahia? Yeye na arudi nyumbani, au sivyo anaweza kufa vitani na mtu mwingine akalifurahia. 20:7 Kum 24:5; Mit 5:18Je, kuna yeyote aliyeposa mwanamke na hajamwoa? Yeye na arudi nyumbani, ama sivyo anaweza kufa vitani na mtu mwingine akamwoa.” 20:8 Amu 7:3Kisha maafisa wataongeza haya, “Je, kuna mtu anayeogopa ama kufa moyo? Yeye na arudi nyumbani ili ndugu zake nao wasije wakafa moyo pia.” Wakati maafisa watakapomaliza kuzungumza na jeshi, watawateua wakuu wa vikosi.

20:10 Kum 2:26; Lk 14:31-32; 2Sam 20:18-20Wakati mtakapokwenda kushambulia mji, wapeni watu wake masharti ya amani. 20:11 2Fal 6:22; 1Fal 9:21; 1Nya 22:2; Isa 31:7Wakikubali na kuwafungulia malango yao, watu wake wote watawatumikia kwa kufanya kazi ngumu na watawatumikia. Ikiwa watakataa kufanya mapatano ya amani na wakiwaingiza katika vita, basi mtauzunguka mji huo kwa vita. 20:13 Hes 31:7Wakati Bwana Mungu wenu atakapouweka mji huo mkononi mwenu, waueni kwa upanga wanaume wote waliomo ndani yake. 20:14 Yos 8:2; 22:8; Hes 31:11; 31:53Kwa upande wa wanawake, watoto, mifugo na kila kitu kingine chochote ndani ya huo mji, mnaweza kuvichukua kama nyara kwa ajili yenu. Nanyi mnaweza kuzitumia hizo nyara ambazo Bwana Mungu wenu amewapa kutoka kwa adui zenu. 20:15 Yos 9:9Hivi ndivyo mtakavyofanya kwa miji yote ambayo iko mbali nanyi, ambayo haimilikiwi na mataifa ya karibu.

20:16 Kut 23:31-33; Hes 21:2-3; Kum 7:2; Yos 6:21; 10:1; 11:14Hata hivyo, katika miji ya mataifa ambayo Bwana Mungu wenu anawapa kama urithi, msiache kitu chochote hai kinachopumua. Waangamizeni kabisa Wahiti, Waamori, Wakanaani, Waperizi, Wahivi na Wayebusi, kama Bwana Mungu wenu alivyowaamuru. 20:18 Kut 34:16; 10:7; 23:33; Kum 12:30-31; Yos 23:12-13; 1Kor 15:33; 2Fal 21:3, 15; Za 106:34-41; Hos 8:11La sivyo, watawafundisha kufuata mambo yote ya machukizo wanayofanya wakiabudu miungu yao, nanyi mtatenda dhambi dhidi ya Bwana Mungu wenu.

Wakati mtakapouzunguka mji kwa vita kwa muda mrefu, mkipigana dhidi yake ili kuuteka, msiharibu miti yake kwa kuikata kwa shoka, kwa sababu mtaweza kula matunda yake. Hivyo msiikate. Je, miti hiyo ya mashambani ni watu, hata muizingire? Hata hivyo, mnaweza kuikata miti ambayo sio miti ya matunda na kuitumia kujenga ngome, mpaka mji ulio katika vita na ninyi utakapoanguka.

Read More of Kumbukumbu 20