Kumbukumbu 16:21-22, Kumbukumbu 17:1-20, Kumbukumbu 18:1-22 NEN

Kumbukumbu 16:21-22

Kuabudu Miungu Mingine

16:21 Kum 7:5; Kut 34:13; 1Fal 14:15; 2Fal 17:16; 21:3; 2Nya 33:3; Kut 34:13; Amu 3:7Msisimamishe nguzo yoyote ya Ashera kando ya madhabahu mliyomjengea Bwana Mungu wenu, 16:22 Kut 23:24; Law 26:1wala msisimamishe jiwe la kuabudu, kwa maana Bwana Mungu wenu anavichukia vitu hivi.

Read More of Kumbukumbu 16

Kumbukumbu 17:1-20

17:1 Kut 12:5; Law 22:20; Kum 7:25; 15:21; Mal 1:8, 13Msimtolee Bwana Mungu wenu dhabihu ya maksai au kondoo ambaye ana dosari yoyote au hitilafu ndani yake, kwa kuwa hilo litakuwa chukizo kwake.

17:2 Kum 13:6-11Ikiwa mwanaume au mwanamke anayeishi kati ya mojawapo ya miji akupayo Bwana, anakutwa anafanya uovu mbele za Bwana Mungu wenu, kwa kuvunja Agano lake, 17:3 Yer 7:31; Kut 22:20; Mwa 1:16; 2:1; 37:9; Ay 31:26naye amekwenda kinyume na agizo langu kuabudu miungu mingine na kuisujudia, kama vile jua, mwezi au nyota za angani, 17:4 Kum 22:20; 13:12-14hili likiwa limeletwa mbele yenu, ni lazima kulichunguza kikamilifu. Ikiwa ni kweli na kuwa limehakikishwa kwamba hili ni chukizo lililofanyika katika Israeli, 17:5 Law 24:14mchukueni huyo mwanaume au mwanamke ambaye amelifanya tendo hili ovu kwenye lango la mji wenu na kumpiga mawe mtu huyo mpaka afe. 17:6 Hes 35:30; Kum 19:15; Mt 18:16; Yos 7:25; Yn 8:1717:6 Hes 35:30; Mt 18:16; Yn 8:17; 2Kor 13:1; 1Tim 5:19; Ebr 10:28Kwa ushuhuda wa mashahidi wawili au watatu mtu huyo atauawa, bali hakuna mtu atakayeuawa kwa ushuhuda wa shahidi mmoja tu. 17:7 Yn 8:7; Law 24:14; Mdo 7:58; Kum 13:5, 9; 1Kor 15:13Ni lazima kwanza mikono ya mashahidi itangulie kumuua huyo mtu, kisha mikono ya watu wote. Ni lazima mwondoe uovu miongoni mwenu.

Mahakama Za Sheria

17:8 Kut 21:6, 13; 2Nya 19:10; Kum 12:5; Za 122:3-5; Hag 2:11; Mal 2:7; Hes 35:11; Kum 19:17Kama mashauri yanaletwa katika mahakama zenu ambayo ni magumu zaidi kwenu kuyaamua, ikiwa ni umwagaji wa damu, madai au mashambulio, yapelekeni mahali ambapo Bwana Mungu wenu atapachagua. 17:9 Kum 24:8; 27:9; Kut 21:6; Mwa 25:22; Kum 19:17; Eze 44:24; Hag 2:11; Amu 4:5; 1Fal 3:16Nendeni kwa makuhani, ambao ni Walawi, na kwa mwamuzi ambaye atakuwa kazini wakati huo. Ulizeni kwao nao watawapa maamuzi. Ni lazima mtende sawasawa na maamuzi watakayowapa mahali Bwana atakapopachagua. Kuweni waangalifu kufanya kila kitu watakachowaongoza kufanya. 17:11 Law 10:11; Kum 5:32; 25:1Fanyeni sawasawa na sheria wanayowafundisha na maamuzi wanayowapa. Msigeuke mkono wa kuume au kushoto kuacha kufanya yale wanayowaambia. 17:12 Hes 15:30; 16:9-13; Mwa 17:14; Kum 13:11; 18:20; 19:20; 1Fal 18:40; Yer 14:14; Hos 4:4; Zek 13:3; Kum 13:5Mwanaume atakayeonyesha dharau kwa mwamuzi au kwa kuhani ambaye amewekwa kumtumikia Bwana Mungu wenu lazima auawe. Lazima mwondoe uovu katika Israeli. 17:13 Kum 13:11Watu wote watasikia na kuogopa, nao hawatakuwa wenye kudharau tena.

Mfalme

17:14 Hes 33:53; Yos 21:43; 1Sam 8:5-9; 19:20; 10:19Wakati utakapoingia katika nchi anayowapa Bwana Mungu wenu kuimiliki na kukaa humo, nanyi mkasema, “Na tumweke mfalme juu yetu kama mataifa yanayotuzunguka,” 17:15 1Sam 16:3; 2Sam 5:3; Yer 30:21kuweni na uhakika wa kumweka mfalme juu yenu ambaye Bwana Mungu wenu atamchagua. Ni lazima atoke miongoni mwa ndugu zenu wenyewe. Msimweke mgeni juu yenu ambaye si ndugu wa Kiisraeli. 17:16 Isa 2:7; 30:16; 1Sam 8:11; 1Fal 4:26; 9:19; 10:26; 2Nya 1:14; Za 20:7; Isa 31:1; Yer 42:14; 1Fal 10:28-29; Eze 17:15; Kut 13:17Hata hivyo, kamwe mfalme asijipatie hesabu kubwa ya farasi kwa ajili yake mwenyewe, au kuwafanya watu warudi Misri ili kupata farasi zaidi, kwa maana Bwana amekuambia, “Hamtairudia njia ile tena.” 17:17 Kut 34:16; 2Sam 5:13; 12:11; 1Fal 11:3; 2Nya 11:21; Za 31:3Kamwe asioe wake wengi, la sivyo moyo wake utapotoka. Kamwe asijilimbikizie kiasi kikubwa cha fedha na dhahabu.

17:18 2Fal 11:12; Kum 31:9; 2Fal 22:8Atakapokuwa amekalia kiti cha ufalme wake, ajiandikie kwenye kitabu nakala ya sheria kwa ajili yake mwenyewe kutoka zile sheria za makuhani ambao ni Walawi. 17:19 Yos 8; Za 119:97Atakuwa na nakala hiyo, naye ataisoma siku zote za maisha yake ili kwamba ajifunze kumheshimu Bwana Mungu wake na kufuata kwa uangalifu maneno yote ya sheria hii na amri hizi, 17:20 Kum 5:32naye asijifikirie kuwa ni bora kuliko ndugu zake na kuipotosha sheria. Ndipo yeye na wazao wake watatawala katika ufalme wake kwa muda mrefu katika Israeli.

Read More of Kumbukumbu 17

Kumbukumbu 18:1-22

Sadaka Kwa Makuhani Na Walawi

18:1 Yer 33:21; Hes 18:8, 20; 1Kor 9:13Makuhani ambao ni Walawi, yaani kabila lote la Lawi, hawatakuwa na mgawo wala urithi pamoja na Israeli. Wataishi kwa sadaka zitolewazo kwa ajili ya Bwana za kuteketezwa kwa moto, kwa maana huo ndio urithi wao. 18:2 Hes 18:20; Yos 13:14Hawatakuwa na urithi miongoni mwa ndugu zao; Bwana ndiye urithi wao, kama alivyowaahidi.

18:3 Kut 29:27; Law 1:5; 7:28-34; Hes 18:12Hili ndilo fungu la makuhani kutoka kwa watu watakaotoa dhabihu ya fahali au kondoo: mguu wa mbele, mataya na matumbo. 18:4 Kut 22:29; Hes 18:12Mtawapa malimbuko ya nafaka zenu, divai mpya, mafuta na sufu ya kwanza kutoka manyoya ya kondoo zenu, 18:5 Kut 28:1; 29:9; Kum 10:8; Kut 29:9kwa kuwa Bwana Mungu wenu amewachagua pamoja na wazao wao kutoka makabila yenu kusimama na kuhudumu katika jina la Bwana siku zote.

18:6 Hes 35:2-3; Kum 12:5Ikiwa Mlawi atahama kutoka mmojawapo ya miji yenu popote katika Israeli ambapo anaishi, akaja kwa moyo wote mahali ambapo Bwana atapachagua, 18:7 1Fal 18:32; 22:16; Za 118:26anaweza akahudumu katika jina la Bwana Mungu wake kama Walawi wenzake wote wanaohudumu hapo mbele za Bwana. 18:8 Hes 18:24; 2Nya 31:4; Neh 12:44, 47; 13:12Atashiriki sawa katika mafao yao, hata kama amepokea fedha kutoka mauzo ya mali ya jamaa yake.

Matendo Ya Machukizo

18:9 Kum 9:5; 12:29-31; Law 18:3; 2Fal 21:2; 2Nya 28:3; 33:2; 34:33; Ezr 6:21; 9:11; Yer 44:4Wakati mtakapoingia katika nchi ambayo Bwana Mungu wenu anawapa, msijifunze kuiga njia za machukizo za mataifa ya huko. 18:10 Law 18:21; 1Sam 15:23; Kut 7:11; Law 19:31; Kum 12:31Asionekane mtu yeyote miongoni mwenu ampitishaye mwanawe au binti yake katika moto, atakayefanya uaguzi, ulozi, anayetabiri nyakati, anayejishughulisha na uchawi, 18:11 Isa 47:9; Kut 22:18; 1Sam 28:13wala arogaye kwa kupiga mafundo, wala mwaguzi au anayeabudu mizimu, wala awaombaye wafu. 18:12 Law 18:24; Kum 9:4Mtu yeyote afanyaye mambo haya ni chukizo kwa Bwana, tena ni kwa sababu ya matendo haya ya kuchukiza wayafanyayo ndiyo maana Bwana Mungu wenu atayafukuza mataifa hayo mbele yenu. 18:13 Mwa 6:9; 17:1; Za 119:1; Mt 5:48Kamwe msilaumiwe mbele za Bwana Mungu wenu.

Nabii

18:14 2Fal 21:6Mataifa mtakayowafukuza husikiliza wale wafanyao ulozi na uaguzi. Lakini kwenu ninyi, Bwana Mungu wenu hajawaruhusu kufanya hivyo. 18:15 Mt 21:11; Lk 2:25-35; Yn 1:21; Mdo 3:22; 7:37; Hes 24:17; Isa 11:1; 61:1; Mt 11:3; 21:11; Lk 2:25-34; 4:16-22; 7:16; 24:19; Yn 4:19-26; 6:14; 7:40Bwana Mungu wenu atawainulia nabii kama mimi kutoka miongoni mwa ndugu zenu wenyewe. Msikilizeni yeye. 18:16 Kut 20:19; Kum 5:23-27Kwa kuwa hivi ndivyo mlivyomwomba Bwana Mungu wenu kule Horebu siku ile ya kusanyiko, wakati mliposema, “Na tusiisikie sauti ya Bwana Mungu wetu, wala kuuona moto huu mkubwa tena, ama sivyo tutakufa.”

Bwana akaniambia: “Wanachosema ni vyema. 18:18 Mwa 20:7; Isa 2:3; 26:8; 51:4; Mik 4:2; Kut 4:12; Yn 4:25-26; 14:24; Mdo 3:22; Yn 17:8; 4:25; 8:28; 12:49, 50Nitawainulia nabii kama wewe kutoka miongoni mwa ndugu zao; nitaweka maneno yangu kinywani mwake, naye atawaambia kila kitu nitakachomwamuru. 18:19 Kut 23:21; Law 19:12; 2Fal 2:24; Yos 22:23; Mdo 3:23; Ebr 12:25Kama mtu yeyote hatasikiliza maneno yangu ambayo huyo nabii atayasema kwa Jina langu, mimi mwenyewe nitamwajibisha. 18:20 Kut 23:13; Kum 13:1-5; 17:12; Yer 14:14; 2:8; Zek 13:3Lakini nabii ambaye atathubutu kusema kwa Jina langu kitu chochote ambacho sikumwamuru akiseme, au nabii ambaye husema kwa jina la miungu mingine ni lazima auawe.”

Mnaweza kuulizana wenyewe, “Tutawezaje kujua wakati ujumbe haukusemwa na Bwana?” 18:22 Kum 13:2; 1Sam 3:20; 1Fal 22:28; Yer 28:9Ikiwa kile nabii anachotangaza kwa jina la Bwana hakikutokea au kutimia, huo ni ujumbe ambao Bwana hakusema. Nabii huyo amesema kwa ujuaji. Msimwogope huyo.

Read More of Kumbukumbu 18