Kumbukumbu 15:1-23, Kumbukumbu 16:1-20 NEN

Kumbukumbu 15:1-23

Mwaka Wa Kufuta Madeni

(Walawi 25:1-7)

15:1 Kum 31:10; Neh 10:31; Kut 23:10; Yer 34:14Kila mwisho wa miaka saba ni lazima mfute madeni. Hivi ndivyo itakavyofanyika: Kila mkopeshaji atafuta mkopo aliomkopesha Mwisraeli mwenzake. Hatamtaka Mwisraeli mwenzake au ndugu yake amlipe hilo deni, kwa sababu wakati wa Bwana wa kufuta madeni umetangazwa. 15:3 Mwa 31:15; Kum 23:20; 28:12; Rut 2:10Unaweza kudai malipo kwa mgeni, lakini lazima ufute kila deni ambalo unamdai ndugu yako. 15:4 Kum 28:5, 8Hata hivyo, hapatakuwepo maskini miongoni mwenu, kwa kuwa katika nchi Bwana Mungu wenu anayowapa kuimiliki kama urithi wenu, atawabariki sana, 15:5 Kut 15:26; Kum 7:12; 28:1ikiwa tutamtii Bwana Mungu wenu kikamilifu na kuwa waangalifu kuyafuata maagizo haya yote ninayowapa leo. 15:6 Kum 28:12-13, 44; Mit 22:7Kwa kuwa Bwana Mungu wenu atawabariki kama alivyoahidi, nanyi mtawakopesha mataifa mengi lakini hamtakopa kwa yeyote. Mtatawala mataifa mengi lakini hakuna taifa litakalowatawala ninyi.

15:7 Mt 26:11; 18:30; 1Yn 3:17Ikiwa kuna mtu maskini miongoni mwa ndugu zenu, katika mji wowote wa hiyo nchi ambayo Bwana Mungu wenu anawapa, msiwe na moyo mgumu wala usimfumbie mkono ndugu yako aliye maskini. 15:8 Mt 5:42; Lk 6:34; Mdo 24:17; Law 25:35; Gal 2:10Afadhali fungua mikono yako na umkopeshe kwa hiari chochote anachohitaji. 15:9 Mt 20:15; Kut 22:23; Ay 5:15; Yak 5:4; Amo 5:11; Mit 28:22; Za 140:12Jihadhari usijiwekee wazo hili ovu: “Mwaka wa saba, mwaka wa kufuta madeni umekaribia,” usije ukaonyesha nia mbaya kwa ndugu yako mhitaji na ukaacha kumpa chochote. Anaweza kumlalamikia Bwana dhidi yako nawe utakuwa umepatikana na hatia ya dhambi. 15:10 2Kor 9:5; Kum 14:29; 24:19; Mt 25:40; Mdo 20:35; Rum 12:8; 1Tim 6:18; 1Pet 4:11Mpe kwa ukarimu na ufanye hivyo bila kinyongo moyoni, ndipo kwa sababu ya hili Bwana Mungu wenu atakubariki katika kazi zako zote na kwa kila kitu utakachokiwekea mkono wako. 15:11 Mt 26:11; Mk 14:7; Yn 12:8Siku zote watakuwepo watu maskini katika nchi. Kwa hiyo ninawaamuru mwe na mikono iliyokunjuliwa kuwaelekea ndugu zenu, kuwaelekea maskini na wahitaji katika nchi yenu.

Kuwaacha Huru Watumwa

(Kutoka 21:1-18)

15:12 Yer 34:14; Kut 21:2; Law 25:39Kama Mwebrania mwenzako, mwanaume au mwanamke, akijiuza kwako na kukutumikia miaka sita, katika mwaka wa saba ni lazima umwache aende zake akiwa huru. Nawe wakati utakapomwachia usimwache aende mikono mitupu. 15:14 Hes 18:27; Mit 10:22Mpe kwa uhuru kutoka zizi lako la kondoo na mbuzi, kutoka sakafu yako ya kupuria nafaka na kutoka mashinikizo yako ya kukamulia divai. Mpe kama vile ambavyo Bwana Mungu wako alivyokubariki. 15:15 Kut 13:3; Yer 34:13; Kut 20:2; Kum 4:34; 9:26; 16:12; 24:18; Yer 16:14; 27:7Kumbukeni kuwa ninyi mlikuwa watumwa huko Misri naye Bwana Mungu wenu aliwakomboa. Ndiyo sababu nimewapa agizo hili leo.

15:16 Kum 21:5-6Lakini mtumishi wako akikuambia, “Sitaki kukuacha,” kwa sababu anakupenda wewe na jamaa yako naye anaridhika nawe, ndipo utachukua chuma kidogo utoboe sikio lake mpaka hicho chuma kiingie kwenye ubao wa mlango, naye atakuwa mtumishi wako wa maisha. Ufanye vivyo hivyo kwa mtumishi wa kike.

15:18 Isa 16:14; 21:16Usifikiri kuwa kuna ugumu kumwacha mtumishi wako huru, kwa sababu utumishi wake kwako kwa miaka hii sita umekuwa wa thamani mara mbili ya ujira wa mtumishi wa kuajiriwa. Naye Bwana Mungu wenu atakubarikia kwa kila kitu utakachofanya.

Wazaliwa Wa Kwanza Wa Wanyama

15:19 Law 27:9; Kut 13:2; Mwa 4:4; Kut 22:30Wekeni wakfu kwa Bwana Mungu wenu kila mzaliwa wa kwanza wa kiume wa makundi yenu ya ngʼombe na ya mbuzi na kondoo. Maksai walio wazaliwa wa kwanza msiwafanyize kazi, wala msinyoe manyoya ya wazaliwa wa kwanza wa kondoo. 15:20 Law 7:15-18; Kum 12:5-7; 14:23Kila mwaka ninyi na jamaa zenu mtapaswa kuwala mbele za Bwana Mungu wenu pale mahali atakapopachagua. 15:21 Kut 12:5; Law 22:19-25; Kum 17:1; Mal 1:8, 13Kama mnyama ana dosari, akiwa ni kilema au kipofu au kama ana kilema kibaya, kamwe usimtoe dhabihu kwa Bwana Mungu wenu. 15:22 Kum 12:15, 22Itawapasa kumla ninyi wenyewe katika miji yenu. Wote wasio safi na walio safi kwa desturi za kiibada mwaweza kula kama vile mnavyokula paa au kulungu. 15:23 Mwa 9:4; Kum 12:16; Eze 33:25; Law 7:26; 17:10Lakini kamwe msinywe damu; imwageni ardhini kama maji.

Read More of Kumbukumbu 15

Kumbukumbu 16:1-20

Pasaka

(Kutoka 12:1-20)

16:1 Kut 12:2; 12:11; 2Fal 23:21; Mt 26:17-29; Kut 13:4; Law 23:5; Hes 9:2-5; Yn 18:28; 1Kor 5:7, 8; Ebr 11:28; 1Kor 5:7, 8; Ebr 11:28Shikeni mwezi wa Abibu, na kuiadhimisha Pasaka ya Bwana Mungu wenu, kwa sababu katika mwezi wa Abibu, Mungu aliwatoa Misri usiku. 16:2 Kum 12:5, 26Mtatoa dhabihu ya Pasaka ya mnyama kwa Bwana Mungu wenu kutoka kundi lenu la mbuzi na kondoo au la ngʼombe, mahali pale ambapo Bwana atapachagua kama makao kwa ajili ya Jina lake. 16:3 Kut 12:15-20, 39; 34:18; 1Kor 5:8; Kut 12:11; Kum 4:9; Kut 13:3, 6-7; Hes 28:19; 2Nya 35:7; Mt 26:2Msile nyama hiyo pamoja na mikate iliyotiwa chachu, lakini kwa siku saba mtakula mikate isiyotiwa chachu, mikate ya kujitesa, kwa sababu mliondoka Misri kwa haraka, ili kwamba siku zote za maisha yenu mpate kukumbuka wakati wenu wa kuondoka Misri. 16:4 Kut 12:6; 12:8; Mk 14:12; Kut 12:10Chachu isionekane katika mali zenu katika nchi yenu yote kwa siku saba. Nyama yoyote ya dhabihu mtakayotoa jioni ya siku ya kwanza isibakizwe mpaka asubuhi.

Kamwe msitoe dhabihu ya Pasaka katika mji wowote ambao Bwana Mungu wenu amewapa, 16:6 Kut 12:42; Kum 12:5; Mt 27:46isipokuwa mahali atakapopachagua kama makao kwa ajili ya Jina lake. Hapo ndipo lazima mtoe dhabihu ya Pasaka jioni, jua litakapotua, iwe kumbukumbu yenu ya kutoka Misri. 16:7 Kut 12:8; 2Nya 35:13; 2Fal 23:23; Yn 2:13; 11:55Okeni na mle mahali pale ambapo Bwana Mungu wenu atakapopachagua, kisha asubuhi mrudi kwenye mahema yenu. 16:8 Law 23:8; Mt 26:17; Lk 2:41; 22:7; Yn 2:13; Kut 12:16Kwa siku sita mtakula mikate isiyotiwa chachu na siku ya saba fanyeni kusanyiko kwa ajili ya Bwana Mungu wenu na msifanye kazi.

Sikukuu Ya Mavuno

(Kutoka 34:22; Walawi 23:15-21)

16:9 Mdo 2:1; Kut 23:16; 34:22; Hes 28:26; Law 23:15Mhesabu majuma saba tangu wakati mnapoanza kuchukua mundu kuvuna nafaka. 16:10 Mt 10:22; Yoe 2:14; 1Kor 16:2Kisha msherehekee Sikukuu ya Majuma kwa Bwana Mungu wenu kwa kutoa sadaka ya hiari kwa kadiri ya baraka ambayo Bwana Mungu wenu amewapa. 16:11 Kum 12:7; Kut 20:24; 2Sam 7:13; Kum 12:12; 14:29; Neh 8:10; Lk 14:12Shangilieni mbele za Bwana Mungu wenu mahali atakapopachagua kama makao ya Jina lake, ninyi, wana wenu na binti zenu, watumishi wenu wa kiume na wa kike, Walawi walio katika miji yenu, na wageni, yatima na wajane waishio miongoni mwenu. 16:12 Kum 15:15Kumbukeni kwamba mlikuwa watumwa kule Misri na mfuate amri hizi kwa uangalifu.

Sikukuu Ya Vibanda

(Walawi 23:33-43)

16:13 Law 2:14; Mwa 2:14; 27:37; Kut 23:16; Law 23:34; Mwa 15:13; Kut 1:11, 14; Za 105:23, 2516:13 Kut 23:16; Law 23:34; Hes 29:12Adhimisheni sikukuu ya vibanda kwa siku saba baada ya kukusanya mazao yenu ya nafaka na kukamua zabibu. 16:14 Kum 26:11; Neh 8:9; Mhu 9:7; 1Sam 12:1-6; 25:6-8Mfurahie sikukuu yenu, ninyi, wana wenu, binti zenu, watumishi wenu wa kiume na wa kike, Walawi, wageni, yatima na wajane ambao wanaishi katika miji yenu. 16:15 Ay 38:7; Za 4:7; 28:7; 30:11; Law 23:39Kwa siku saba mtaiadhimisha sikukuu ya Bwana Mungu wenu katika mahali atakapopachagua Bwana. Kwa kuwa Bwana Mungu wenu atawabariki katika mavuno yenu na katika kazi zote za mikono yenu na furaha yenu itakamilika.

16:16 Kum 31:11; Za 84:7; Kut 12:17; 23:14, 16; Ezr 3:4; Kut 34:20Wanaume wenu wote lazima wajitokeze mara tatu kwa mwaka mbele za Bwana Mungu wenu mahali atakapopachagua: kwa ajili ya Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu, Sikukuu ya Majuma, na Sikukuu ya Vibanda. Hakuna mtu atakayejitokeza mbele za Bwana mikono mitupu: 16:17 2Kor 8:12Kila mmoja wenu ni lazima alete zawadi kulingana na jinsi ambavyo Bwana Mungu wenu alivyowabariki.

Waamuzi

16:18 Kut 18:21, 26; Mwa 31:37; Kum 1:16Wateue waamuzi na maafisa kwa kila kabila lenu katika kila mji ambao Bwana Mungu wenu anawapa, nao watawaamua watu kwa usawa. 16:19 Kut 23:2, 8; Law 19:15; Kut 18:21; 1Sam 8:3; Kum 1:17; Mhu 7:7; Ay 31:21, 22; Mit 17:23; 24:23; Isa 1:17, 23; Mdo 10:34Msipotoshe haki wala msifanye upendeleo. Msikubali rushwa kwa sababu rushwa hupofusha macho ya wenye busara na kugeuza maneno ya wenye haki. 16:20 Kum 4:1Mfuate haki na haki peke yake, ili mweze kuishi na kuimiliki nchi ambayo Bwana Mungu wenu anawapa.

Read More of Kumbukumbu 16