Kumbukumbu 13:1-18, Kumbukumbu 14:1-29 NEN

Kumbukumbu 13:1-18

Kuabudu Miungu Mingine

13:1 Mt 24:24; Mk 13:22; 2The 2:9; Mwa 20:3; Yer 23:25; 27:9; 29:8Kama nabii, au yule anayetabiri kwa njia ya ndoto, akijitokeza miongoni mwenu na akawatangazia ishara ya miujiza na ajabu, 13:2 Kum 11:28; 18:22; 1Sam 2:34; 10:9; 2Fal 19:29; 20:9; Isa 7:11; Kum 11:28ikiwa ishara au ajabu ya aliyozungumza ikatokea, naye akasema, “Na tufuate miungu mingine” (miungu ambayo hamjaifahamu) “na tuiabudu,” 13:3 2Pet 2:1; 1Sam 28:6; Mwa 22:1; 1Fal 13:18; 22:23; Yer 29:31; 43:2; Eze 13:9; 1Kor 11:19; Kum 6:5kamwe msiyasikilize maneno ya nabii wala mwota ndoto huyo. Bwana Mungu wenu anawajaribu kuangalia kama mnampenda kwa moyo wenu wote na kwa roho yenu yote. 13:4 2Fal 23:8; 2Nya 34:31; 2Yn 6; Kum 6:13; 10:20; Za 5:7Ni Bwana Mungu wenu ambaye mnapaswa kumfuata tena ni yeye mnapaswa kumheshimu. Shikeni maagizo yake na kumtii, mtumikieni na kushikamana naye. 13:5 Kut 21:12; 22:20; Kum 4:19; 17:7-12; 19:19; 24:7; Amu 20:13; 1Kor 5:13Huyo nabii au mwota ndoto lazima auawe, kwa sababu amehubiri uasi dhidi ya Bwana Mungu wenu, ambaye aliwatoa kutoka nchi ya Misri na kuwakomboa kutoka nchi ya utumwa; amejaribu kuwageuza kutoka njia ambayo Bwana Mungu wenu aliwaagiza mfuate. Ni lazima mwondoe uovu miongoni mwenu.

13:6 Kum 17:2-7; 29:18; 11:28Kama ndugu yako hasa, au mwanao au binti yako, au mke umpendaye, au rafiki yako wa karibu sana akikushawishi kwa siri, akisema, “Na twende tukaabudu miungu mingine” (miungu ambayo ninyi wala baba zenu hamkuifahamu, miungu ya watu wanaowazunguka, ikiwa karibu au mbali, kutoka mwisho mmoja wa nchi mpaka mwingine), 13:8 Mit 1:10; Kum 7:2; Kut 20:3; Gal 1:8-9; 1Yn 5:21usikubali wala usimsikilize. Usimhurumie! Usimwache wala usimkinge. 13:9 Law 24:14; Kum 17:5-7; Mdo 7:58Hakika ni lazima auawe. Ni lazima mkono wako uwe wa kwanza katika kumuua kisha mikono ya watu wengine wote. 13:10 Kut 20:3Mpigeni kwa mawe mpaka afe, kwa sababu alijaribu kuwageuza mtoke kwa Bwana Mungu wenu ambaye aliwatoa Misri, kutoka nchi ya utumwa. 13:11 Kum 17:13; 19:20; 21:21; 1Tim 5:20Kisha Israeli wote watasikia na kuogopa, wala hakuna mmoja miongoni mwenu atakayefanya uovu tena.

13:12 Yos 22:11; Amu 20:1Kama mkisikia ikisemwa kwamba moja ya miji ambayo Bwana Mungu wenu anawapa mkae ndani yake 13:13 Amu 19:22; 20:13; 1Sam 2:12; 10:27; 25:17; 1Fal 21:10; 1Yn 2:19kuna wanaume waovu wameinuka miongoni mwenu na wamewapotosha watu wa mji, wakisema, “Twendeni tukaabudu miungu mingine” (miungu ambayo hamkuifahamu), 13:14 Amu 20:12; Kum 17:4ndipo itakubidi kuuliza, kupima na kuchunguza kwa makini. Kama ni kweli, tena ikihakikishwa kwamba jambo hili lichukizalo limefanyika miongoni mwenu, 13:15 Isa 24:6; 34:5; 43:28; 47:6; Mao 2:6; Dan 9:11; Zek 8:13; Mal 4:6; Kut 22:20kwa hakika ni lazima mwaue kwa upanga wale wote wanaoishi katika mji ule. Uharibuni kabisa, pamoja na watu wake na mifugo yake. 13:16 2Fal 25:9; Yer 39:9; 52:13; Eze 16:41; Kum 7:25-26; Yos 6:24; 8:28; Isa 7:16; 17:1; 24:10; 25:2; 27:10; 32:14-19; 37:26; Yer 49:2; Mik 1:6Kusanyeni nyara zote za mji katika uwanja wa wazi na kuuchoma mji kabisa pamoja na nyara zake zote kama sadaka ya kuteketezwa kwa Bwana Mungu wenu. Utabaki kuwa magofu milele na hautajengwa tena. 13:17 Kut 30:12; Mwa 12:2; 13:14; 26:24; 28:14; 43:14; Hes 25:4; Kum 30:3; 7:13Hakuna kimoja kati ya vitu vilivyolaaniwa kitakachokutwa mikononi mwenu, ili Bwana ageuze hasira yake kali. Atawahurumia na kuwa na rehema kwenu pia kuongeza idadi yenu, kama alivyowaahidi baba zenu, 13:18 Kum 12:25-28; 12:25-28; Mt 6:33; 7:21-24kwa sababu mnamtii Bwana Mungu wenu, mkizishika amri zake zote zile ninazowapa leo na kufanya lile lililo jema machoni pake.

Read More of Kumbukumbu 13

Kumbukumbu 14:1-29

Vyakula Vilivyo Najisi Na Vilivyo Safi

(Walawi 11:1-47)

14:1 Yn 1:12; Rum 8:14; 9:8; Yer 16:6; Mwa 6:2-4; Kut 4:22-23; Gal 3:26; 1The 4:13Ninyi ni watoto wa Bwana Mungu wenu. Msijichanje ama kujinyoa upara kwenye paji la uso kwa ajili ya aliyekufa, 14:2 Mwa 28:14; Kut 8:22; 22:31; Isa 6:13; Mt 2:15; Law 20:26; Rum 12:1; Kum 7:6; 26:18-1914:2 Kut 19:5; 2Sam 7:23, 24kwa maana ninyi ni taifa takatifu kwa Bwana Mungu wenu. Bwana amewachagua ninyi kuwa taifa la kipekee kutoka mataifa yote juu ya uso wa dunia, mwe tunu yake.

14:3 Eze 4:14; Isa 65:4; Mdo 10:13; Rum 14:14Msile kitu chochote ambacho ni machukizo. 14:4 Mdo 10:14; Law 7:23; 11:2-45Hawa ndio wanyama mtakaokula: ngʼombe, kondoo, mbuzi, 14:5 Kum 12:15; Ay 39:1; Za 104:18kulungu, paa, kongoni, paa mweupe, mbuzi-mwitu, pofu na kondoo wa mlimani. Mnaweza kumla mnyama yeyote mwenye kwato zilizogawanyika mara mbili, pia yule anayecheua. Hata hivyo, miongoni mwa wale wanaocheua au wale walio na kwato zilizogawanyika kamwe msile ngamia, sungura na pelele. Iwapo wanacheua, lakini hawana kwato zilizogawanyika; ni najisi kwenu kwa taratibu za kiibada. 14:8 Law 5:12; 11:26-27Nguruwe pia ni najisi; ingawa ana kwato zilizogawanyika, hacheui. Msile nyama yake wala kugusa mzoga wake.

Katika viumbe hai vyote viishivyo kwenye maji, mnaweza kula yeyote aliye na mapezi na magamba. Lakini chochote kisicho na mapezi na magamba msile; kwenu ni najisi.

Mnaweza kula ndege yeyote aliye safi. 14:12 Law 11:13Lakini wafuatao msiwale: tai, furukombe, kipungu, 14:13 Mwa 2:11; Isa 34:15kengewa mwekundu, kengewa mweusi, mwewe wa aina yoyote, 14:14 Mwa 8:17kunguru wa aina yoyote, mbuni, kiruka-njia, dudumizi, kipanga wa aina yoyote, bundi, mumbi, bundi mkubwa, 14:17 Za 102:6; Isa 13:21; 14:23; 34:11; Sef 2:14mwari, nderi, mnandi, korongo, koikoi wa aina yoyote, hudihudi na popo.

Wadudu wote warukao kwa makundi ni najisi kwenu, msiwale. 14:20 Law 20:25Lakini viumbe vyote vyenye mabawa vilivyo safi mwaweza kula.

14:21 Law 11:39; 14:2; 17:15; Kut 23:19; 22:31; Law 22:8; Eze 44:31Msile kitu chochote mtakachokuta kimekufa. Mnaweza kumpa mgeni yeyote anayeishi katika mojawapo ya miji yenu, naye anaweza kula au mnaweza kumuuzia mtu wa nchi nyingine. Lakini ninyi ni watu watakatifu kwa Bwana Mungu wenu.

Msitokose mwana-mbuzi katika maziwa ya mama yake.

Zaka

14:22 Mwa 14:20; Law 27:30; Hes 18:21; Neh 10:37; Kum 12:6, 17Hakikisheni mmetenga sehemu ya kumi ya mazao yote ya mashamba yenu kila mwaka. 14:23 Kum 12:5, 17, 18; Za 4:7; 1Fal 3:2; Kum 4:10; Za 22:23; 33:8; Mal 2:5; Mit 3:13; Isa 8:13; Yer 32:38-41; Ebr 12:28Mtakula zaka za nafaka yenu, divai mpya, mafuta na wazaliwa wa kwanza wa makundi yenu ya ngʼombe na ya kondoo na mbuzi mbele za Bwana Mungu wenu pale mahali atakapopachagua kama maskani kwa ajili ya Jina lake, ili kwamba mpate kujifunza kumheshimu Bwana Mungu wenu daima. 14:24 Kum 12:21Lakini ikiwa mahali pale ni mbali sana nanyi mmebarikiwa na Bwana Mungu wenu na hamwezi kubeba zaka yenu (kwa sababu mahali pale Bwana atakapopachagua kuliweka Jina lake ni mbali sana), 14:25 Mt 21:12; Yn 2:14basi badilisheni zaka yenu kuwa fedha, mkaichukue hiyo fedha mwende nayo mahali Bwana Mungu wenu atakapopachagua. 14:26 Law 10:9; 23:40; Mhu 10:16-17; Kum 12:7-8Tumieni hiyo fedha kununua chochote ukitakacho: ngʼombe, kondoo, divai au kinywaji chochote chenye chachu au chochote mnachotaka. Kisha ninyi na wa nyumbani mwenu mtaila mbele za Bwana Mungu wenu na kufurahi. 14:27 Kum 12:19; Hes 18:20; 26:62; Kum 18:1-2; Rum 13:4; 15:27; 1Kor 9:1-14Msiache kuwajali Walawi waishio katika miji yenu, kwa kuwa hao hawana shamba wala urithi wao wenyewe.

14:28 Law 27:30; Kum 26:12Mwishoni mwa kila mwaka wa tatu, leteni zaka zote za mazao ya miaka ile na uyahifadhi kwenye miji yenu, 14:29 Mwa 47:22; Hes 26:62; Kum 16:11; 24:19-21; Za 94:6; Isa 1:17; 58:6; Kum 6:11; 15:10; Za 41:1; Mit 22:9; Mt 3:10; Kum 10:18; Eze 22:7, 29; Lk 14:12; Ebr 13:2; Mal 3:10; Lk 11:41; 2Kor 9:6-11ili Walawi (ambao hawana mashamba wala urithi wao wenyewe) na wageni, yatima na wajane wanaoishi kwenye miji yenu wapate kuja kula na kushiba, ili Bwana Mungu wenu apate kuwabariki ninyi katika kazi zote za mikono yenu.

Read More of Kumbukumbu 14