Kumbukumbu 11:1-32, Kumbukumbu 12:1-32 NEN

Kumbukumbu 11:1-32

Mpende Na Umtii Bwana

11:1 Kum 6:5; Law 8:35; Zek 3:7Mpende Bwana Mungu wako na kushika masharti yake, amri zake, sheria zake na maagizo yake siku zote. 11:2 Kum 31:13; Za 78:6; 136:12; Kum 3:24; 5:24; 8:5; Za 11:3; Kut 7:8-21Kumbuka hivi leo kwamba sio watoto wako walioona na kujua adhabu ya Bwana Mungu wako: utukufu wake, mkono wake wenye nguvu, mkono wake ulionyooshwa; ishara alizozifanya na mambo aliyoyafanya katikati ya Misri, kwa Farao mfalme wa Misri na kwa nchi yake yote; 11:4 Kut 15:1; 14:27; Hes 21:4lile alilolifanyia jeshi la Wamisri, farasi na magari yake, jinsi alivyowafurikisha na maji ya Bahari ya Shamu walipokuwa wakiwafuatilia ninyi, na jinsi Bwana alivyowaletea angamizo la kudumu juu yao. Sio watoto wenu walioyaona yale Mungu aliyowafanyia huko jangwani mpaka mkafika mahali hapa, 11:6 Hes 16:1-35; Za 106:16-18; Isa 24:19wala lile Mungu alilowafanyia Dathani na Abiramu, wana wa Eliabu wa kabila la Reubeni, wakati ardhi ilipofungua kinywa chake katikati ya Israeli yote, ikawameza pamoja na walio nyumbani mwao, hema zao na kila kitu kilichokuwa hai ambacho kilikuwa mali yao. 11:7 Kum 5:3Bali ilikuwa ni macho yenu wenyewe ambayo yaliyaona mambo haya yote makuu Bwana aliyoyatenda.

11:8 Ezr 9:10; Kum 31:6-7, 23; Yos 1:7Kwa hiyo fuateni maagizo yote ninayowapa leo, ili mpate kuwa na nguvu za kuingia na kuiteka nchi ile ambayo mnavuka Yordani kuimiliki, 11:9 Kum 5:16; 9:5; Kut 3:8; Mit 10:27; Kum 4:40; Mit 3:1, 26ili mpate kuishi siku nyingi katika nchi ile ambayo Bwana aliapa kuwapa baba zenu na wazao wao, nchi itiririkayo maziwa na asali. 11:10 Isa 11:15; 37:25; Zek 8:7Nchi mnayoiingia kuimiliki haifanani na nchi ya Misri mlikotoka ambako mlipanda mbegu yenu na kuinywesha, kama bustani ya mboga. 11:11 Eze 36:4; Kum 8:7; Neh 9:25Lakini nchi mnayovuka Yordani kuimiliki ni nchi ya milima na mabonde inywayo mvua kutoka mbinguni. 11:12 1Fal 8:29; 9:3Ni nchi ambayo Bwana Mungu wenu anaitunza; macho ya Bwana Mungu wenu yanaitazama daima kutoka mwanzo wa mwaka hadi mwisho wa mwaka.

11:13 Kum 6:17; 10:12; 4:29; Yer 17:24; 2The 3:5Hivyo kama mkiyatii maagizo yangu ninayowapa leo kwa uaminifu, yaani kwa kumpenda Bwana Mungu wenu, na kumtumikia kwa moyo wako wote na kwa roho yenu yote, 11:14 Law 26:4; Mdo 14:17; Za 147:8; Yer 3:3; Yoe 2:23; Yak 5:7; Yer 5:24ndipo atawanyweshea mvua katika nchi yenu kwa majira yake, mvua ya masika na ya vuli, ili mpate kuvuna nafaka zenu, divai mpya na mafuta. 11:15 Za 104:14; Law 26:5; Kum 6:11; Za 104:14; Yoe 2:19Nitawapa majani kwa ajili ya ngʼombe wenu, nanyi mtakula na kushiba.

11:16 Kum 4:19; 8:19; 29:18; Ay 31:9; 27Jihadharini, la sivyo mtashawishika kugeuka na kuabudu miungu mingine na kuisujudia. 11:17 Kum 6:15; 9:19; 1Fal 17:1; 2Nya 6:26; 7:13; Law 26:20; Kum 4:26; 28:12, 24Ndipo hasira ya Bwana itawaka dhidi yenu, naye atafunga mbingu ili mvua isinyeshe nayo ardhi haitatoa mazao, nanyi mtaangamia mara katika nchi nzuri ambayo Bwana anawapa. 11:18 Kut 13:9; Kum 6:6-8Yawekeni haya maneno yangu katika mioyo yenu na akili zenu, yafungeni kama alama juu ya mikono yenu na kwenye paji za nyuso zenu. 11:19 Kut 12:26; Kum 6:7; Za 145:4; Isa 38:19; Yer 32:39; Kum 4:9-10Wafundisheni watoto wenu, yazungumzeni wakati mketipo nyumbani na wakati mtembeapo njiani, wakati mlalapo na wakati mwamkapo. 11:20 Kum 6:9; Hab 2:2Yaandikeni juu ya miimo ya nyumba zenu na juu ya malango yenu, 11:21 Ay 5:26; Mit 3:2; 4:10; 9:11; Za 72:5ili kwamba siku zenu na siku za watoto wenu zipate kuwa nyingi katika nchi ile Bwana aliyoapa kuwapa baba zenu, kama zilivyo nyingi siku za mbingu juu ya nchi.

11:22 Kum 6:17; 6:5; 10:20Kama mkishika kwa makini maagizo haya yote ninayowapa kuyafuata, ya kumpenda Bwana Mungu wenu, kuenenda katika njia zake zote na kushikamana naye kwa uthabiti, 11:23 Kum 9:5; 4:38; Kut 23:28; Kum 9:1ndipo Bwana atawafukuza mataifa haya yote mbele yako, nawe utawafukuza mataifa yaliyo makubwa na yenye nguvu kukuliko wewe. 11:24 Mwa 15:18; Kum 1:36; 12:20; 19:8; Yos 1:3; 14:9; Mwa 2:14Kila mahali mtakapoweka mguu wenu patakuwa penu: Nchi yenu itaenea kutoka jangwa la Lebanoni, na kutoka mto wa Frati hadi bahari ya magharibi11:24 Yaani Bahari ya Mediterania. 11:25 Kum 2:25; Kut 23:27; Kum 7:24Hapatakuwa na mtu atakayeweza kusimama dhidi yenu. Bwana Mungu wenu, kama alivyoahidi, ataweka juu ya nchi yote utisho na hofu kwa ajili yenu popote mwendako.

11:26 Za 24:5; Law 26:14-17; Kum 27:13-26; 30:1, 15, 19; Mao 2:17; Dan 9:11; Mal 3:9; 4:6Tazama, leo ninaweka mbele yenu baraka na laana: 11:27 Kum 28:1-14; Za 24:5baraka kama mtatii maagizo ya Bwana Mungu wenu, ambayo ninawapa leo; 11:28 2Nya 24:20; Yer 42:13; 44:16; Kum 4:28; 13:6-13; 29:26; 1Sam 26:19laana kama hamtatii maagizo ya Bwana Mungu wenu na kuacha njia ambayo ninawaamuru leo kwa kufuata miungu mingine, ambayo hamkuijua. 11:29 Mwa 9:7; Kum 27:4; Yos 8:30; Kum 27:12-13; Yos 8:33; Yn 4:20Wakati Bwana Mungu wenu atakapokuwa amewaleta katika nchi mnayoiingia kuimiliki, mtatangaza baraka kutoka Mlima Gerizimu, na kutangaza laana kutoka Mlima Ebali. 11:30 Mwa 12:6; Yos 4:19; 5:9; 9:6; 10:6; 14:6; 15:7; Amu 2:1; 2Fal 2:1; Mik 6:5; Hes 33:53; Kum 12:10; Yos 1:11; 11:23Kama mnavyofahamu, milima hii ipo ngʼambo ya Yordani, magharibi ya barabara, kuelekea machweo ya jua, karibu na miti mikubwa ya More, katika nchi ya wale Wakanaani wanaoishi Araba, jirani na Gilgali. 11:31 Kum 28:1-14; Za 24:5Karibu mvuke ngʼambo ya Yordani kuingia na kuimiliki nchi ambayo Bwana Mungu wenu anawapa. Wakati mtakapokuwa mmeichukua na mnaishi humo, hakikisheni kwamba mnatii amri na sheria zote ninazoziweka mbele yenu leo.

Read More of Kumbukumbu 11

Kumbukumbu 12:1-32

Mahali Pekee Pa Kuabudia

12:1 Za 119:5; Kum 4:9-10; 6:15; 1Fal 8:40; Eze 20:19; Gal 6:9Hizi ndizo amri na sheria ambazo ni lazima mwe waangalifu kuzifuata katika nchi ambayo Bwana, Mungu wa baba zenu, amewapa kumiliki, kwa muda wote mtakaoishi katika nchi. 12:2 Hes 21:28; 1Fal 14:23; 2Fal 17:10; Isa 57:5; Yer 2:20; 3:6-13; Kut 34:33Haribuni kabisa kila mahali pao pa kuabudia kwenye milima mirefu, vilima na chini ya kila mti mkubwa ambamo mataifa haya mnayokwenda kuchukua ardhi yao huabudia miungu yao. 12:3 2Fal 11:8; Kut 32:20; 34:13; 1Fal 14:15; Hes 33:53; Kut 23:13; Amu 2:2; Za 16:4; Zek 13:2Bomoeni madhabahu zao, vunjeni yale mawe wanayoabudu, chomeni moto nguzo zao za Ashera; katilieni mbali sanamu za miungu yao na mfute majina yao mahali hapo.

12:4 2Fal 17:15; Yer 10:2Kamwe msimwabudu Bwana Mungu wenu kama wanavyoabudu wao. 12:5 Kut 20:24; 2Sam 7:13; Kum 14:23; 15:20; 16:2, 11; 18:6; 26:2; 1Sam 2:29; 1Fal 1:5; 5; 8:16; 9:3; 2Nya 2:4; 6:6; 7:12-16; Ezr 6:12; 7:15; Za 26:8; 78:68; Zek 2:12Bali mtatafuta mahali Bwana Mungu wenu atakapopachagua katika makabila yenu yote ili aliweke jina lake huko kuwa makao yake. Mahali hapo ndipo iwapasapo kwenda; 12:6 Law 27:30; Mwa 28:20; Yos 22:27; Isa 66:20; Kum 14:22hapo ndipo mtakapoleta sadaka zenu za kuteketezwa na dhabihu, zaka zenu na changizo zenu, kile ulichoweka nadhiri kutoa, sadaka zenu za hiari na malimbuko ya makundi yenu ya ngʼombe pamoja na mbuzi na kondoo. 12:7 Kut 18:12; Mhu 3:12-13; Law 23:40; Isa 62:9Hapo, katika uwepo wa Bwana Mungu wenu, ninyi pamoja na jamaa zenu, mtakula na kufurahia kila kitu ambacho mmegusa kwa mikono yenu, kwa sababu Bwana Mungu wenu amewabariki.

12:8 Amu 17:6; 21:25Msifanye kama tunavyofanya hapa leo, kila mtu anavyopenda mwenyewe, 12:9 Kut 33:14; Kum 3:20; Za 95:11; Mik 2:10; Kum 4:21kwa kuwa bado hamjafikia mahali pa mapumziko na urithi ambao Bwana Mungu wenu anawapa. 12:10 Kum 11:31; Kut 33:14; Law 1:3; Yos 22:23Lakini mtavuka Yordani na kuishi katika nchi Bwana Mungu wenu anayowapa kama urithi, naye atawapa pumziko kutokana na adui zenu wote wanaowazunguka ili ninyi mpate kuishi kwa salama. 12:11 Kum 14:23; 15:20; 16:2; Yos 18:1; 1Fal 8:29; Za 78:68; 87:2Kisha kuhusu mahali Bwana Mungu wenu atakapopachagua kuwa mahali pa makao ya Jina lake, hapo ndipo inapowapasa kuleta kila kitu ninachowaamuru: sadaka zenu za kuteketezwa na dhabihu, zaka zenu na changizo, pamoja na vitu vyote vyenye thamani ambavyo mmeweka nadhiri kumtolea Bwana. 12:12 Kum 26:11-13; 18:20; 9:10; 10:9; 14:29Hapo furahini mbele za Bwana Mungu wenu, ninyi, wana wenu na binti zenu, watumishi wenu wa kiume na wa kike, pamoja na Walawi kutoka miji yenu ambao hawana mgawo wala urithi wao wenyewe. 12:13 Law 17:4Kuweni waangalifu, msitoe dhabihu zenu za kuteketezwa mahali popote mnapopapenda. Mtazitoa tu mahali pale ambapo Bwana atachagua katika mojawapo ya makabila yenu, nanyi hapo zingatieni kila jambo ninalowaamuru.

12:15 Kum 14:5; 15:22; Mwa 9:3Hata hivyo, mnaweza kuwachinja wanyama wenu katika miji yenu yoyote ile na kula nyama nyingi mpendavyo kama vile mmemchinja paa au kulungu, kulingana na baraka mtakazojaliwa na Bwana Mungu wenu. Watu walio najisi au walio safi wanaweza kula. 12:16 Mwa 9:4; Mdo 15:20; Mwa 35:14; 1Nya 11:18; Yer 7:18; Law 17:13; Kum 15:23; Yn 19:34; Law 7:26Lakini kamwe usinywe damu; imwage juu ya ardhi kama maji. 12:17 Law 27:30; Hes 18:12-19; Kum 14:23; 15:20Hamruhusiwi kula katika miji yenu zaka yenu ya nafaka, ya divai mpya na ya mafuta, au mzaliwa wa kwanza wa makundi yenu ya ngʼombe na makundi yenu ya mbuzi na kondoo, wala chochote ambacho mmeweka nadhiri kukitoa, au sadaka zako za hiari, wala matoleo maalum. 12:18 Kum 14:23; 15:20; 14:26; Neh 8:10; Mhu 3:12-13; 5:18-20Badala yake, mtakula vitu hivyo katika uwepo wa Bwana Mungu wenu mahali ambapo Bwana Mungu wenu atapachagua: wewe, wana wako na binti zako, watumishi wako wa kiume na wa kike, na Walawi kutoka miji yenu. Mnatakiwa mfurahi mbele za Bwana Mungu wenu kwa kula kitu mtakachoweka mikono yenu. 12:19 Kum 14:27; Neh 13:10; Mal 3:8Mwe waangalifu msiwapuuze Walawi kwa muda wote mnaoishi katika nchi yenu.

12:20 Kut 34:24; Mwa 15:8, 18; Kum 11:24; Kut 16:3Bwana Mungu wenu atakapokuwa ameongeza nchi yenu kama alivyowaahidi, nanyi mkitamani nyama na mkisema, “Ningependa nyama,” hapo unaweza kula nyingi upendavyo. 12:21 Kum 14:24; Law 17:4Kama mahali ambapo Bwana Mungu wenu atapachagua kuweka Jina lake ni mbali sana kutoka kwenu, unaweza kuchinja wanyama kutoka makundi yenu ya ngʼombe, ya mbuzi na ya kondoo ambayo Bwana amewapa, kama nilivyokuamuru, na mkiwa katika miji yenu wenyewe mnaweza kula nyingi mtakavyo. Mle kama vile mngekula paa na kulungu. Wote walio najisi kiibada na walio safi mwaweza kula. 12:23 Law 7:26; Eze 33:25; Mwa 9:4; Law 17:11, 14Lakini hakikisheni kwamba hamkunywa damu, kwa sababu damu ni uhai, kamwe msile uhai pamoja na nyama. Hamruhusiwi kamwe kunywa damu; imwageni juu ya ardhi kama maji. 12:25 Kum 4:40; Kut 15:26; Kum 13:18; 1Fal 11:38; 2Fal 12:2; Isa 3:10Msinywe damu, ili mweze kufanikiwa ninyi pamoja na watoto wenu baada yenu, kwa sababu mtakuwa mkifanya lililo haki machoni pa Bwana.

12:26 Hes 5:9-10; 18:19Lakini vichukueni vitu vyenu vilivyowekwa wakfu pamoja na vile mlivyoweka nadhiri, mwende mahali pale Bwana atakapopachagua. 12:27 Law 1:13; 3:1-17Leteni sadaka zenu za kuteketezwa juu ya madhabahu ya Bwana Mungu wenu, vyote nyama na damu. Damu ya dhabihu zenu lazima imiminwe kando ya madhabahu ya Bwana Mungu wenu, lakini nyama mnaweza kula. 12:28 Kum 4:40; Mhu 8:12; Za 25:12, 13; Mit 1:33; 3:1-4Mwe waangalifu kutii masharti haya yote ninayowapa, ili kwamba siku zote mweze kufanikiwa, ninyi pamoja na watoto wenu baada yenu, kwa sababu mtakuwa mkifanya lililo jema na sahihi mbele za macho ya Bwana Mungu wenu.

12:29 Yos 23:4; Kum 6:10; Kut 23:23; Yos 23:4; Za 78:55Bwana Mungu wenu atayakatilia mbali mbele yenu mataifa ambayo punde kidogo mtayavamia na kuyaondoa. Lakini mtakapokuwa mmeyafukuza na kuishi katika nchi yao, 12:30 Kut 10:7na baada ya kuangamizwa mbele yenu, mwe waangalifu msijiingize katika tanzi kwa kuuliza habari za miungu yao, mkisema, “Je, mataifa haya hutumikiaje miungu yao? Nasi tutafanya vivyo hivyo.” 12:31 Law 18:25; 2Fal 3:27; Kum 9:5; Yer 32:35; 2Fal 17:15; 2Nya 33:2; 36:14Kamwe msimwabudu Bwana Mungu wenu kwa njia wanayoabudu miungu yao, kwa sababu katika kuabudu miungu yao, wanafanya aina zote za machukizo anayoyachukia Bwana. Hata huwateketeza wana wao na binti zao kwa moto kama kafara kwa miungu yao.

12:32 Kum 4:2; Ufu 22:18-19; Yos 1:7; Mit 30:6Angalieni kwamba mnafanya yote niliyowaamuru; msiongeze kitu wala msipunguze kitu.

Read More of Kumbukumbu 12