Danieli 8:15-27, Danieli 9:1-19 NEN

Danieli 8:15-27

Tafsiri Ya Maono

8:15 Eze 2:1; Dan 10:16-18Mimi Danieli nilipokuwa ninaangalia maono na kujaribu kuelewa, mbele yangu alisimama mmoja aliyefanana na mwanadamu. 8:16 Dan 9:21; Lk 1:19; Dan 7:16Kisha nikasikia sauti ya mwanadamu kutoka Mto Ulai ikiita, “Gabrieli, mwambie mtu huyu maana ya maono haya.”

8:17 Eze 44:4; Ufu 1:17; Hab 2:3; Eze 1:28; Dan 2:46Alipokuwa akikaribia pale nilipokuwa nimesimama, niliogopa, nikaanguka kifudifudi. Akaniambia, “Mwana wa mwanadamu, fahamu kuwa maono haya yanahusu siku za mwisho.”

8:18 Dan 10:9; Eze 2:2; Zek 4:1Alipokuwa akinena nami, nilikuwa katika usingizi mzito, huku nimelala kifudifudi. Ndipo aliponigusa na kunisimamisha wima.

8:19 Isa 10:25; Za 102:13Akaniambia, “Nitakuambia yale yatakayotokea baadaye wakati wa ghadhabu, kwa sababu maono haya yanahusu wakati wa mwisho ulioamriwa. 8:20 Eze 27:10Kondoo dume mwenye pembe mbili ambaye ulimwona anawakilisha wafalme wa Umedi na Uajemi. 8:21 Dan 10:20; 11:2Yule beberu mwenye nywele nyingi ni mfalme wa Uyunani, nayo ile pembe ndefu katikati ya macho yake ni mfalme wa kwanza. Zile pembe nne zilizoota badala ya ile pembe iliyovunjika zinawakilisha falme nne ambazo zitatokea kutoka taifa lake, lakini hakuna hata mmoja utakaokuwa na nguvu kama ule uliovunjika.

“Katika sehemu ya mwisho ya utawala wao, wakati waasi watakapokuwa waovu kabisa, atainuka mfalme mwenye uso mkali, aliye stadi wa hila. 8:24 Dan 7:25; 2:34; 11:21; Ay 34:7Atakuwa na nguvu nyingi, lakini si kwa uwezo wake mwenyewe. Atasababisha uharibifu wa kutisha, na atafanikiwa kwa chochote anachofanya. Atawaangamiza watu maarufu na watu watakatifu. 8:25 Dan 11:36; 11:21; Ay 34:20Atasababisha udanganyifu ustawi, naye atajihesabu mwenyewe kuwa bora. Wakati wajisikiapo kuwa wako salama, atawaangamiza wengi, na kushindana na Mkuu wa wakuu. Lakini ataangamizwa, isipokuwa si kwa uwezo wa mwanadamu.

8:26 Isa 8:16; Ufu 10:4; Dan 10:14; Eze 12:27; Isa 29:11; Ufu 22:10“Maono kuhusu jioni na asubuhi ambayo umepewa ni kweli, lakini yatie muhuri maono haya, kwa maana yanahusu wakati mrefu ujao.”

8:27 Dan 2:47-48; Isa 21:3; Dan 7:28; 10:8; 4:19Mimi Danieli nilikuwa nimechoka sana, na nikalala nikiwa mgonjwa kwa siku kadhaa. Ndipo nikaamka, nikaenda kwenye shughuli za mfalme. Nilifadhaishwa na maono hayo, nami sikuweza kuyaelewa.

Read More of Danieli 8

Danieli 9:1-19

Maombi Ya Danieli

9:1 Dan 5:31; Ezr 4:6Katika mwaka wa kwanza wa utawala wa Dario mwana wa Ahasuero (mzaliwa wa Umedi), ambaye alifanywa mtawala juu ya ufalme wa Babeli, 9:2 Yer 29:10; Zek 7:5; Yer 25:11-12; 2Nya 36:21katika mwaka wa kwanza wa utawala wake, mimi Danieli nilielewa kutokana na Maandiko, kulingana na neno la Bwana alilopewa nabii Yeremia, kwamba ukiwa wa Yerusalemu ungetimizwa kwa miaka sabini. 9:3 2Sam 13:19; Neh 1:4; 2Nya 20:3; Yer 29:12; Dan 10:12; Yon 3:6Kwa hiyo nikamgeukia Bwana Mungu na kumsihi katika maombi na dua, katika kufunga, na kuvaa nguo ya gunia na kujipaka majivu.

9:4 Kum 7:9, 21; 1Fal 8:23, 30Nikamwomba Bwana Mungu wangu na kutubu:

“Ee Bwana, Mungu mkuu na unayetisha, anayeshika agano lake la upendo kwao wanaompenda na kutii maagizo yake, 9:5 Isa 53:6; Mao 1:20; Za 106:6; Mao 3:42; Ezr 9:6; Yer 8:14tumetenda dhambi na kufanya mabaya. Tumekuwa waovu na tumeasi; tumegeuka mbali na maagizo yako na sheria zako. 9:6 Yer 44:5; Yak 5:10; 2Fal 18:12; Ufu 10:7; 2Nya 36:16Hatukuwasikiliza watumishi wako manabii, ambao kwa jina lako walisema na wafalme wetu, wakuu wetu, baba zetu, na watu wote wa nchi.

9:7 Ezr 9:7; Za 44:15; Kum 4:27; Amo 9:9; Eze 39:23-24; Yer 24:9; Isa 42:6“Bwana, wewe ni mwenye haki, lakini siku hii ya leo tumefunikwa na aibu: tukiwa wanaume wa Yuda, na watu wa Yerusalemu, na Israeli yote, wote walio karibu na walio mbali, katika nchi zote ulikotutawanya kwa sababu ya kukosa uaminifu kwako. 9:8 Neh 9:33; Yer 14; 20; Eze 16:63Ee Bwana, sisi na wafalme wetu, wakuu wetu na baba zetu tumefunikwa na aibu kwa sababu tumefanya dhambi dhidi yako. 9:9 Kut 34:7; Hes 14:18; Neh 9:17; Yer 14:7; Za 130:4; Yer 42:12; 2Sam 24:14Bwana Mungu wetu ni mwenye rehema na anayesamehe, hata ingawa tumefanya uasi dhidi yake. 9:10 2Fal 18:12; Ufu 10:7; 2Fal 17:13-15Hatukumtii Bwana Mungu wetu wala kuzishika sheria alizotupa kupitia kwa watumishi wake manabii. 9:11 Isa 1:4-7; Yer 8:5-10; Kum 27:15-26; Yer 2:29; 2Fal 22:16; Kum 11:26; 28:15; 2Fal 17:23Israeli yote imekosea sheria yako na kugeuka mbali, nao wamekataa kukutii.

“Kwa hiyo laana na viapo vya hukumu vilivyoandikwa katika Sheria ya Mose, mtumishi wa Mungu, vimemiminwa juu yetu, kwa sababu tumefanya dhambi dhidi yako. 9:12 Isa 44:26; Yoe 2:2; Zek 1:6; 7:12; Mao 2:17; Yer 30:7; 4:23; Dan 12:1Umetimiza maneno uliyosema dhidi yetu na dhidi ya watawala wetu, kwa kuleta maafa makubwa juu yetu. Chini ya mbingu yote kamwe hapajatendeka kitu kama kile kilichotendeka kwa Yerusalemu. 9:13 Isa 9:13; Yer 2:30; Isa 31:1; Kum 4:29Kama vile ilivyoandikwa katika sheria ya Mose, misiba hii yote imekuja juu yetu, lakini hatujaomba fadhili kwa Bwana Mungu wetu kwa kugeuka kutoka dhambi zetu na kuwa wasikivu katika kweli yake. 9:14 Yer 18:8; 44:27; Neh 9:33; Yer 32:23; Mwa 18:25; 2Nya 12:6; Yer 40:3Bwana hakusita kuleta maafa juu yetu, kwa maana Bwana Mungu wetu ni mwenye haki katika kila afanyalo; lakini hata hivyo hatujamtii.

9:15 Kut 3:20; Yer 32:21; Neh 9:10“Sasa, Ee Bwana Mungu wetu, ambaye uliwatoa watu wako Misri kwa mkono wenye nguvu, na ambaye umejifanyia Jina linalodumu mpaka leo, tumetenda dhambi, tumefanya mabaya. 9:16 Amu 5:11; Kut 15:17; Zek 8:2; Za 39:8; Eze 5:14; Isa 5:25Ee Bwana, wewe kwa kadiri ya matendo yako ya haki, ondoa hasira yako na ghadhabu yako juu ya Yerusalemu, mji wako, mlima wako mtakatifu. Dhambi zetu na maovu ya baba zetu yameifanya Yerusalemu na watu wako kitu cha kudharauliwa kwa wale wote wanaotuzunguka.

9:17 Hes 6:24-26; Za 80:19“Basi Mungu wetu, sasa sikia maombi na dua ya mtumishi wako. Ee Bwana, kwa ajili yako angalia kwa huruma ukiwa wa mahali pako patakatifu. 9:18 Za 80:14; Kum 28:10; Isa 37:17; Yer 7:10-12; 25:29; Lk 18:13Ee Mungu, tega sikio na ukasikie; fumbua macho yako ukaone ukiwa wa mji ule wenye Jina lako. Hatukutolei maombi yetu kwa sababu sisi tuna haki, bali kwa sababu ya rehema zako nyingi. 9:19 Za 44:23; 1Sam 12:22Ee Bwana, sikiliza! Ee Bwana, samehe! Ee Bwana, sikia na ukatende! Kwa ajili yako, Ee Mungu wangu, usikawie, kwa sababu mji wako na watu wako wanaitwa kwa Jina lako.”

Read More of Danieli 9