Danieli 4:19-37, Danieli 5:1-16 NEN

Danieli 4:19-37

Danieli Anafasiri Ndoto

4:19 Mwa 41:15; Dan 10:16-17; 2Sam 18:32; Mwa 41:8; 40:12; Dan 7:15, 28; 8:27Ndipo Danieli (aliyeitwa pia Belteshaza) alipofadhaika sana kwa muda, nayo mawazo yake yakamtia hofu. Basi mfalme akasema, “Belteshaza, usiruhusu ndoto wala maana yake kukutia hofu.”

Belteshaza akamjibu, “Bwana wangu, laiti ndoto hii ingehusu adui zako, na maana yake iwahusu watesi wako! Mti uliouona, uliokua ukawa mkubwa na wenye nguvu, nayo ncha yake ikagusa anga na kuonekana duniani kote, 4:21 Eze 31:6ukiwa na majani ya kupendeza na matunda mengi, ukitoa chakula kwa wote, na ukiwapa hifadhi wanyama wa kondeni na kuwa mahali pa viota katika matawi yake kwa ajili ya ndege wa angani. 4:22 2Sam 12:7; Yer 27:7; Dan 2:37-38; Ay 20:5; Dan 5:18-19Ee mfalme, wewe ndiwe ule mti! Umekuwa mkubwa na mwenye nguvu, nao ukuu wako umekua mpaka kufika juu angani, nayo mamlaka yako yameenea mpaka miisho ya dunia.

4:23 Dan 8:13; 5:21; Eze 31:3-4“Ee mfalme, wewe ulimwona mlinzi, aliye mtakatifu, akishuka kutoka mbinguni na kusema, ‘Ukateni mti na kuuangamiza, lakini kiacheni kisiki kikiwa kimefungwa kwa chuma na kwa shaba, kwenye majani ya kondeni, wakati mizizi yake inabaki ardhini. Mwacheni aloweshwe na umande wa mbinguni, mwacheni aishi kama wanyama pori mpaka nyakati saba zipite juu yake.’

4:24 Ay 40:12; Yer 40:2; Ay 34:19; Isa 46:10-11; Za 107:40“Ee mfalme, hii ndiyo tafsiri, na hii ni amri ya Aliye Juu Sana aliyoitoa dhidi ya bwana wangu mfalme: 4:25 Za 83:18; Yer 27:5; Dan 2:47; Ay 24:8; Dan 5:21; Za 83:18Wewe utafukuzwa mbali na wanadamu, nawe utaishi pamoja na wanyama pori; utakula manyasi kama ngʼombe, na kuloana kwa umande wa mbinguni. Nyakati saba zitapita juu yako, mpaka utakapokubali kuwa Yeye Aliye Juu Sana ndiye anayetawala juu ya falme za wanadamu, naye humtawaza yeyote amtakaye. 4:26 Dan 2:37; Lk 15:18Amri ya kuacha kisiki pamoja na mizizi yake inamaanisha kwamba ufalme wako utarejezwa kwako utakapokubali kwamba Mbingu ndizo zitawalazo. 4:27 Isa 55:6-7; Kum 24:13; 1Fal 21:29; Mdo 8:22; Za 41:3; Mit 28:13; Yer 29:7; Eze 18:22Kwa hiyo, ee mfalme, uwe radhi kupokea shauri langu: Acha dhambi zako kwa kutenda yaliyo haki, ukaache uovu wako, na uwe na huruma kwa walioonewa. Hivyo itawezekana baada ya hayo, mafanikio yako yakaendelea.”

Ndoto Inatimia

4:28 Hes 23:19; 2Sam 22:28; Dan 5:20Haya yote yalimpata Mfalme Nebukadneza. Miezi kumi na miwili baadaye, mfalme alipokuwa akitembea juu ya paa la jumba la kifalme la Babeli, 4:30 Mit 16:18; Isa 37:24-25; Hab 1:11; Isa 13:19; 10:13; Dan 5:20alisema, “Je, huu si Babeli mji mkuu nilioujenga kama makao ya kifalme, kwa uwezo wangu mkubwa, na kwa ajili ya utukufu wa enzi yangu?”

4:31 2Sam 22:28; Dan 5:20Maneno hayo yalikuwa bado katika midomo yake wakati sauti ilipokuja kutoka mbinguni, ikisema, “Mfalme Nebukadneza, hiki ndicho kilichoamriwa kwa ajili yako: Mamlaka yako ya ufalme yameondolewa kutoka kwako. 4:32 Ay 9:12Utafukuzwa mbali na wanadamu, ukaishi pamoja na wanyama pori, na utakula manyasi kama ngʼombe. Nyakati saba zitapita juu yako, mpaka utakapokubali kuwa Yeye Aliye Juu Sana ndiye anayetawala juu ya falme za wanadamu, naye humtawaza yeyote amtakaye.”

4:33 Ay 20:5; Dan 5:20-21; Ay 24:8Papo hapo yale yaliyokuwa yamesemwa kuhusu Nebukadneza yakatimia. Alifukuzwa mbali na wanadamu, akala majani kama ngʼombe. Mwili wake uliloweshwa kwa umande wa mbinguni mpaka nywele zake zikakua kama manyoya ya tai na kucha zake kama makucha ya ndege.

4:34 Dan 12:7; Ufu 4:10; Lk 1:33; Ay 12:20; Isa 37:16; Dan 6:26; Za 145:13; Dan 2:44; 5:21Mwisho wa huo wakati, mimi Nebukadneza, niliinua macho yangu kuelekea mbinguni, nazo fahamu zangu zikanirudia. Ndipo nikamsifu Yeye Aliye Juu Sana, nikamheshimu na kumhimidi yeye aishiye milele.

Utawala wake ni utawala wa milele;

ufalme wake hudumu kutoka kizazi na kizazi.

4:35 Isa 40:17; Kum 21:8; Yon 1:14; Ay 9:4; Rum 9:20; Isa 14:24; 45:9; Za 115:3; 136:6; Kum 32:39; Dan 5:21Mataifa yote ya dunia

yanahesabiwa kuwa si kitu.

Hufanya kama atakavyo

kwa majeshi ya mbinguni,

na kwa mataifa ya dunia.

Hakuna anayeweza kuuzuia mkono wake

au kumwambia, “Umefanya nini wewe?”

4:36 Mit 22:4; Dan 5:18; Ay 42:12Wakati huo huo fahamu zangu ziliponirudia, nikarudishiwa heshima yangu na fahari yangu kwa ajili ya utukufu wa ufalme wangu. Washauri wangu na wakuu wangu walikuja kunitafuta, nami nikarudishwa kwenye kiti changu cha ufalme hata nikawa mkuu kuliko mwanzoni. 4:37 Kum 32:4; Za 33:4-5; Kut 18:11; Mt 23:12; Kut 15:2; Za 18:27; 34:3; Ay 31:4; 40:11-12; Isa 13:11; Dan 5:23; Za 119:21Basi mimi, Nebukadneza, humhimidi, na humtukuza na kumsifu Mfalme wa mbinguni, kwa sababu kila kitu afanyacho ni haki, na njia zake zote ni adili. Nao waendao kwa kiburi anaweza kuwashusha.

Read More of Danieli 4

Danieli 5:1-16

Maandishi Ukutani

5:1 1Fal 3:15; Mk 6:21; Es 3:1; Yer 50:35; Dan 7:1; 8:1Mfalme Belshaza alifanya karamu kubwa kwa ajili ya maelfu ya wakuu wake na akanywa mvinyo pamoja nao. 5:2 2Nya 36:10; Yer 52:19; Es 1:7; Mit 20:1; Isa 21:5; 2Fal 24:13; Es 2:14; Dan 1:2Wakati Belshaza alipokuwa akinywa mvinyo wake, aliamuru viletwe vile vikombe vya dhahabu na fedha ambavyo Nebukadneza baba yake alikuwa amevichukua kutoka hekaluni huko Yerusalemu, ili mfalme na wakuu wake, wake zake na masuria wake waweze kuvinywea. Kwa hiyo wakavileta vile vikombe vya dhahabu ambavyo vilikuwa vimechukuliwa kutoka Hekalu la Mungu huko Yerusalemu, naye mfalme na wakuu wake, wake zake na masuria wake wakavinywea. 5:4 Es 1:10; Ufu 9:20; Za 115:4-8; Amu 16:24; Hag 2:19; Za 135:15-18Walipokuwa wakinywa mvinyo, wakaisifu miungu ya dhahabu na fedha, ya shaba, chuma, miti na mawe.

Ghafula vidole vya mkono wa mwanadamu vilitokea na kuandika juu ya ukuta, karibu na kinara cha taa ndani ya jumba la mfalme. Mfalme akatazama kitanga kilivyokuwa kikiandika. 5:6 Dan 4:5; Za 22:14; Nah 2:10; Ay 4:15; Isa 7:2; Eze 7:17Uso wa mfalme ukageuka rangi, naye akaogopa sana, kiasi kwamba magoti yake yaligongana na miguu yake ikalegea.

5:7 Isa 44:25; 47:13; Dan 4:6-7; Mwa 41:42; Dan 2:5-6, 48; 6:2-3; Mwa 41:8; Isa 19:3; 44:25; Yer 50:35; Es 10:3Mfalme akawaita wasihiri, wanajimu na waganga waletwe, naye akawaambia hawa wenye hekima wa Babeli, “Yeyote asomaye maandishi haya na kuniambia maana yake atavikwa nguo za zambarau, na kuvikwa mkufu wa dhahabu shingoni mwake, naye atafanywa mtawala wa cheo cha tatu katika ufalme.”

5:8 Dan 2:10, 27; 4:18; Mwa 41:8; 41:8; Kut 8:18Ndipo watu wote wa mfalme wenye hekima wakaingia, lakini hawakuweza kusoma yale maandishi wala kumwambia mfalme maana yake. 5:9 Za 48:5; Isa 21:4Basi Mfalme Belshaza akazidi kujawa na hofu, na uso wake ukageuka rangi zaidi. Wakuu wake wakapigwa na bumbuazi.

5:10 Neh 2:3; Dan 3:9Malkia5:10 Au: Mama yake mfalme. aliposikia sauti za mfalme na wakuu wake, alikuja katika ukumbi wa karamu. Akasema, “Ee mfalme, uishi milele! Usishtuke! Usibadilike rangi kiasi hicho! 5:11 Mwa 41:38; Dan 4:8-9; 1:17; 2:47-48; 2:22; Mwa 41:38; Dan 2:22Yuko mtu katika ufalme wako ambaye ana roho ya miungu mitakatifu ndani yake. Wakati wa baba yako, mtu huyo alionekana kuwa na ufahamu, akili na hekima kama ile ya miungu. Mfalme Nebukadneza baba yako, yaani nasema mfalme baba yako, alimweka kuwa mkuu wa waganga, wasihiri, wanajimu na waaguzi. 5:12 Dan 1:7; 6:3; Hes 12:8; Eze 28:3Mtu huyu Danieli, ambaye mfalme alimwita Belteshaza, alionekana kuwa na akili nyepesi, maarifa na ufahamu, pia uwezo wa kufasiri ndoto, kueleza mafumbo na kutatua matatizo magumu. Mwite Danieli, naye atakuambia maana ya haya maandishi.”

5:13 Es 2:5-6; Dan 6:13Hivyo Danieli akaletwa mbele ya mfalme, naye mfalme akamuuliza, “Je, wewe ndiwe Danieli, mmoja wa watu wa uhamisho walioletwa na mfalme baba yangu kutoka Yuda? Nimesikia kwamba roho ya miungu iko ndani yako, na kwamba una ufahamu, akili na hekima ya pekee. 5:15 Dan 4:18Watu wenye hekima na wasihiri waliletwa mbele yangu ili kusoma maandishi haya na kuniambia maana yake, lakini hawakuweza kunifafanulia. 5:16 Mwa 41:15; 42; Es 5:3; Dan 2:6; Mwa 41:15, 42Basi nimesikia kwamba unaweza kutoa tafsiri na kutatua matatizo magumu. Ikiwa unaweza kusoma maandishi haya na kuniambia maana yake, utavikwa nguo za zambarau na mkufu wa dhahabu shingoni mwako, nawe utafanywa mtawala wa tatu katika ufalme.”

Read More of Danieli 5