Danieli 11:36-45, Danieli 12:1-13 NEN

Danieli 11:36-45

Mfalme Ajikwezaye Mwenyewe

11:36 1The 2:4; Ufu 13:5-6; Kum 10:17; Isa 26:20; Yud 16; Dan 7:25; Isa 10:25“Mfalme atafanya apendavyo. Atajikweza na kujitukuza juu ya kila mungu, naye atasema mambo ambayo hayajasikiwa dhidi ya Mungu wa miungu. Atafanikiwa hadi wakati wa ghadhabu utimie, kwa maana kile kilichokusudiwa lazima kitokee. Hataonyesha heshima kwa miungu ya baba zake au kwa yule aliyetamaniwa na wanawake, wala hatajali mungu yeyote, bali atajikweza mwenyewe juu yao wote. Badala ya kuwajali miungu, ataheshimu mungu wa ngome; mungu ambaye hakujulikana na baba zake ndiye atamheshimu kwa dhahabu na fedha, kwa vito vya thamani na zawadi za thamani kubwa. Atashambulia ngome zenye nguvu mno kwa msaada wa mungu wa kigeni naye atawaheshimu sana wale watakaomkubali yeye. Atawafanya watawala juu ya watu wengi, na atagawa nchi kwa gharama.

11:40 Isa 21:1; 5:28; Eze 38:4; Isa 8:7“Katika wakati wa mwisho, mfalme wa Kusini atapigana naye vita, naye mfalme wa Kaskazini atamshambulia kwa magari ya vita, askari wapanda farasi, na idadi kubwa ya meli. Atavamia nchi nyingi na kuzikumba nchi hizo kama mafuriko. 11:41 Isa 11:14; Yer 48:47; Mal 3:12; Eze 20:6Pia ataivamia Nchi ya Kupendeza. Nchi nyingi zitapinduliwa, bali Edomu, Moabu na viongozi wa Amoni wataokolewa kutoka mkono wake. Atapanua mamlaka yake juu ya nchi nyingi; hata Misri haitaepuka. 11:43 Eze 30:4; 2Nya 12:3; Nah 3:9Atamiliki hazina za dhahabu, fedha na utajiri wote wa Misri, pamoja na Walibia na Wakushi kwa kujisalimisha. Lakini taarifa kutoka mashariki na kaskazini zitamshtua, naye ataondoka kwa ghadhabu nyingi ili kuangamiza na kuharibu kabisa wengi. 11:45 Isa 2:2-4; Dan 8:9Atasimika hema zake za ufalme kati ya bahari na mlima mtakatifu wa kupendeza. Hata hivyo, atafikia mwisho wake, wala hakuna yeyote atakayemsaidia.

Read More of Danieli 11

Danieli 12:1-13

Nyakati Za Mwisho

12:1 Dan 10:13; Yud 9; Dan 9:12; Lk 10:20; Yer 17:13; Mt 24:21; Mk 13:19; Yer 30:7; Za 56:8; Kut 32:32“Katika wakati huo Mikaeli, mtawala mkuu ambaye huwalinda watu wako, atainuka. Kutakuwako wakati wa taabu ambao haujatokea tangu mwanzo wa mataifa hadi wakati huo. Lakini wakati huo, watu wako, kila mmoja ambaye jina lake litakutwa limeandikwa kwenye kitabu, ataokolewa. 12:2 Isa 26:19; Yn 5:28-29; Mt 25:46; Yn 11:24Wengi ambao wamelala kwenye mavumbi wataamka, baadhi yao kwa uzima wa milele, wengine kwa aibu na kudharauliwa milele. 12:3 Dan 11:33; Yn 5:35; Flp 2:15; Mit 4:18; 1Kor 15:42; Mt 13:43Wale wenye hekima watangʼaa kama mwanga wa mbingu, nao wale ambao huwaongoza wengi kutenda haki, watangʼaa kama nyota milele na milele. 12:4 Isa 8:16; Ufu 22:10; Yer 5:1Lakini wewe Danieli, yafunge na kuyatia muhuri maneno ya kitabu hiki mpaka wakati wa mwisho. Wengi watakwenda huku na huko, na maarifa yataongezeka.”

12:5 Dan 10:4Ndipo mimi Danieli nikaangalia, nako mbele yangu walisimama wengine wawili, mmoja katika ukingo huu wa mto, na mwingine ukingo wa pili wa mto. 12:6 Eze 9:2; Dan 8:13; Za 74:9Mmoja wao akasema na yule mtu aliyevaa nguo za kitani, aliyekuwa juu ya maji ya mto, “Je, itachukua muda gani kabla mambo haya ya kushangaza hayajatimizwa?”

12:7 Dan 6:26; Ufu 10:5-7; Lk 21:24; Dan 8:24; 8:24; Ufu 11:2; Mwa 14:22Kisha mtu yule aliyevaa nguo za kitani, aliyekuwa juu ya maji ya mto, akainua mkono wake wa kuume na mkono wake wa kushoto kuelekea mbinguni, nami nikamsikia akiapa kwa jina lake yeye aishiye milele, akisema, “Itakuwa wakati, nyakati mbili, na nusu wakati.12:7 Wakati, nyakati mbili na nusu wakati maana yake mwaka mmoja, miaka miwili, na nusu mwaka, yaani miaka mitatu na nusu. Nguvu za watu watakatifu zitakapokuwa zimevunjwa kabisa, ndipo mambo haya yote yatakapotimizwa.”

Nilisikia, lakini sikuelewa. Kwa hiyo nikauliza, “Bwana wangu, matokeo ya haya yote yatakuwa nini?”

12:9 Isa 29:11Akajibu, “Danieli, enenda zako, kwa sababu maneno haya yamefungwa na kutiwa muhuri mpaka wakati wa mwisho. 12:10 Isa 1:25; Zek 13:9; Hos 14:9; Isa 32:7; Ufu 22:11; Dan 11:35Wengi watatakaswa, na kuondolewa mawaa na kufanywa safi, lakini waovu wataendelea kuwa waovu. Hakuna mmoja wa waovu atakayefahamu, lakini wale wenye hekima watafahamu.

12:11 Mk 13:14; Dan 8:11; 9:27; Mt 24:15; Kut 29:38; Ufu 11:2“Tangu wakati ule wa kukomeshwa dhabihu ya kila siku na kusimamishwa kwa chukizo la uharibifu, kutakuwako siku 1,290. 12:12 Isa 30:18; Eze 4:5-6; Dan 8:14Amebarikiwa mtu yule atakayevumilia hadi kufikia mwisho wa hizo siku 1,335.

12:13 Isa 57:2“Lakini wewe, enenda zako mpaka mwisho. Utapumzika, nawe ndipo mwisho wa hizo siku utafufuka ili kuupokea urithi uliowekewa.”

Read More of Danieli 12