Danieli 1:1-21, Danieli 2:1-23 NEN

Danieli 1:1-21

Mafunzo Ya Danieli Huko Babeli

1:1 Yer 28:4; 35:11; 46:2; 2Nya 36:6; 2Fal 24:1Katika mwaka wa tatu wa utawala wa Yehoyakimu mfalme wa Yuda, Nebukadneza mfalme wa Babeli alikuja akazingira Yerusalemu kwa jeshi. 1:2 2Nya 36:7; Yer 27:19; Zek 5:5-11; 2Fal 24:13Bwana akamtia Yehoyakimu mfalme wa Yuda mkononi mwa Nebukadneza, pamoja na baadhi ya vyombo kutoka Hekalu la Mungu. Hivi akavichukua hadi kwenye hekalu la mungu wake huko Shinari, naye akaviweka nyumbani ya hazina ya mungu wake.

1:3 2Fal 20:18; Isa 39:7; Amu 8:18; Mdo 7:20-22; Mwa 39:6; Ezr 4:7Kisha mfalme akamwagiza Ashpenazi, mkuu wa maafisa wa mfalme, kumletea baadhi ya Waisraeli kutoka jamaa ya mfalme na kutoka jamaa kuu, vijana wanaume wasio na dosari mwilini, wenye sura nzuri, wanaoonyesha kipaji katika kila aina ya elimu, wenye ufahamu mzuri, wepesi kuelewa, na waliofuzu kuhudumu katika jumba la kifalme. Alikuwa awafundishe lugha na maandiko ya Wakaldayo. 1:5 Es 2:5-6, 9Mfalme akawaagizia kiasi cha chakula na divai ya kila siku kutoka meza ya mfalme. Walikuwa wafundishwe kwa miaka mitatu, na hatimaye waingie kwenye utumishi wa mfalme.

1:6 Eze 14:14; Dan 2:17-25Baadhi ya hawa vijana walitoka Yuda: nao ni Danieli, Hanania, Mishaeli na Azaria. 1:7 Dan 5:12; 10:1; Isa 39:7; Dan 3:12; 2:49; 2:26Mkuu wa maafisa akawapa majina mapya: Danieli akamwita Belteshaza, Hanania akamwita Shadraki, Mishaeli akamwita Meshaki, na Azaria akamwita Abednego.

1:8 Mwa 39:21; Mit 16:7; 1Fal 8:50; Eze 4:13-14Lakini Danieli alikusudia kuwa hatajitia unajisi kwa chakula cha mfalme na divai, naye akamwomba mkuu wa maafisa ruhusa ili asijinajisi kwa njia hii. 1:9 Mwa 39:21; Mit 16:7; 1Fal 8:50Basi Mungu alikuwa amemfanya huyo mkuu wa maafisa kuonyesha upendeleo na huruma kwa Danieli, 1:10 Ufu 2:10lakini huyo mkuu wa maafisa akamwambia Danieli, “Ninamwogopa bwana wangu mfalme, aliyeagizia chakula na kinywaji chenu. Kwa nini aone nyuso zenu zikiwa mbaya kuliko za vijana wengine wa rika lenu? Mfalme atakata kichwa changu kwa sababu yenu.”

Ndipo Danieli akamwambia mlinzi aliyeteuliwa na huyo mkuu wa maafisa kuwasimamia Danieli, Hanania, Mishaeli na Azaria, 1:12 Ufu 2:10“Tafadhali wajaribu watumishi wako kwa siku kumi. Usitupe chochote ila nafaka na mboga za majani1:12 Nafaka na mboga za majani, yaani zeroimu kwa Kiebrania, ina maana ya aina za ngano na shayiri, na jamii ya kunde kama maharagwe, dengu, choroko, n.k. tule, na maji ya kunywa. Baadaye ulinganishe sura zetu na vijana wanaokula chakula cha mfalme, ukawatendee watumishi wako kulingana na unachoona.” 1:14 Mhu 2:26; Yak 1:5; Dan 2:19, 30; 7:1; 8:1Basi akakubali jambo hili, akawajaribu kwa siku kumi.

1:15 Kut 23:25Mwisho wa zile siku kumi, walionekana kuwa na afya na kunawiri zaidi kuliko yeyote kati ya wale vijana waliokula chakula cha mfalme. Hivyo mlinzi wao akaondoa chakula chao na divai yao waliopangiwa kula na kunywa, akawapa nafaka na mboga za majani badala yake.

1:17 1Fal 3:12; Ay 12:13; Mhu 2:26; Dan 2:23; Kol 1:9; Dan 5:11; Mdo 7:22Mungu akawapa hawa vijana wanne maarifa na ufahamu wa kila aina ya maandiko na elimu. Naye Danieli aliweza kufahamu maono na aina zote za ndoto.

Mwisho wa muda uliowekwa na mfalme kuwaingiza kwake, mkuu wa maafisa akawaleta mbele ya Mfalme Nebukadneza. 1:19 Mwa 41:46Mfalme akazungumza nao, akaona hakuna aliyelingana na Danieli, Hanania, Mishaeli na Azaria. Hivyo wakaingia katika utumishi wa mfalme. 1:20 Es 2:15; Eze 28:3; Mwa 41:8; 1Fal 4:30; Dan 4:18; 2:13; 6:3Katika kila jambo la hekima na ufahamu kuhusu kile mfalme alichowauliza, aliwaona bora mara kumi zaidi kuliko waganga na wasihiri wote katika ufalme wake wote.

1:21 Dan 6:28; 2Nya 36:22; Dan 10:1Naye Danieli akabaki huko mpaka mwaka wa kwanza wa utawala wa Mfalme Koreshi.

Read More of Danieli 1

Danieli 2:1-23

Ndoto Ya Nebukadneza

2:1 Mwa 20:3; 41:8; Ay 33:15-18; Es 6:1; Dan 6:18; 4:5Katika mwaka wa pili wa utawala wake, Nebukadneza aliota ndoto. Mawazo yake yakasumbuka na hakuweza kulala. 2:2 Mwa 41:8; Kut 7:11; Yer 27:9; Isa 9:13; 44:25; Dan 4:6Hivyo mfalme akawaita waganga, wasihiri, wachawi na wanajimu ili wamwambie ndoto yake aliyokuwa ameota. Walipoingia ndani na kusimama mbele ya mfalme, 2:3 Dan 4:5akawaambia, “Niliota ndoto inayonisumbua, nami nataka nijue maana yake.”

2:4 Ezr 4:7; Neh 2:3; Dan 5:10Ndipo wanajimu wakamjibu mfalme kwa lugha ya Kiaramu,2:4 Kutoka hapa hadi Dan 7:28, mwandishi aliandika na Kiaramu. “Ee mfalme, uishi milele! Waambie watumishi wako hiyo ndoto, nasi tutaifasiri.”

2:5 Ezr 6:11; Dan 3:29; Mwa 41:32Mfalme akawajibu wanajimu, “Nimeamua hivi kwa uthabiti: Ikiwa hamtaniambia ndoto yangu ilikuwa ipi na kuifasiri, mtakatwa vipande vipande na nyumba zenu zitafanywa kuwa vifusi. 2:6 Dan 5:7, 16Lakini mkiniambia ndoto yangu na kuielezea, mtapokea kwangu zawadi, tuzo na heshima kubwa. Basi niambieni ndoto yangu na mnifasirie.”

Wakajibu kwa mara nyingine, “Mfalme na awaambie watumishi wake ndoto yake, nasi tutaifasiri.”

Ndipo mfalme akajibu, “Nina hakika kuwa mnajaribu kupata muda zaidi, kwa sababu mnatambua kuwa nimeamua hivi kwa uthabiti: 2:9 Es 4:11; Isa 41:22-24; 2:10Ikiwa hamtaniambia ndoto yangu, ipo adhabu moja tu kwenu. Mmefanya shauri kuniambia habari za kunipotosha na mambo maovu, mkitumaini kwamba hali itabadilika. Hivyo basi, niambieni hiyo ndoto, nami nitajua kuwa mwaweza kunifasiria.”

2:10 Dan 3:8; 4:7; 5:8Wanajimu wakamjibu mfalme, “Hakuna mtu duniani ambaye anaweza kufanya analotaka mfalme! Vilevile hakuna mfalme hata awe mkuu na mwenye uweza namna gani, aliyeuliza kitu kama hicho kwa mganga au kwa msihiri, wala kwa mnajimu yeyote. 2:11 Kut 8:10; Mwa 41:38; Dan 5:11Anachouliza mfalme ni kigumu mno. Hakuna yeyote awezaye kumfunulia mfalme isipokuwa miungu, nao hawaishi miongoni mwa wanadamu.”

2:12 Dan 3:13-19; Mit 16:14; 28:15Jambo hili lilimkasirisha na kumghadhibisha mfalme mno hata kuagiza kuuawa kwa wenye hekima wote wa Babeli. 2:13 Dan 1:20; 5:19Hivyo amri ikatolewa ya kuwaua wenye hekima, nao watu wakatumwa kuwatafuta Danieli na rafiki zake ili wawaue.

Wakati Arioko, mkuu wa askari wa walinzi wa mfalme, alikuwa amekwenda kuwaua watu wenye hekima wa Babeli, Danieli akazungumza naye kwa hekima na busara. Akamuuliza huyo afisa wa mfalme, “Kwa nini mfalme ametoa amri kali hivyo?” Ndipo Arioko akamweleza Danieli jambo hilo. Aliposikia jambo hili, Danieli akamwendea mfalme, akamwomba ampe muda ili aweze kumfasiria ile ndoto.

Ndipo Danieli akarudi nyumbani kwake na kuwaeleza rafiki zake Hanania, Mishaeli na Azaria jambo hilo. 2:18 Isa 37:4; Yer 33:3; Ufu 11:13; Ezr 1:2; Neh 1:4Aliwasihi waombe rehema kutoka kwa Mungu wa mbinguni kuhusu siri hii, ili yeye na rafiki zake wasije wakauawa pamoja na wenye hekima wengine wa Babeli. 2:19 Ay 33:15; Dan 1:17; Hes 12:6; Yos 22:23Wakati wa usiku lile fumbo lilifunuliwa kwa Danieli katika maono. Ndipo Danieli akamhimidi Mungu wa mbinguni, 2:20 Za 113:2; 145:1-2; Ay 9:4; Yer 32:19; Ay 12:13na akasema:

“Lihimidiwe jina la Mungu milele na milele;

hekima na uweza ni vyake.

2:21 Dan 7:25; Ay 12:19; Rum 13:1; Yak 1:5; Yer 27:5; Za 75:6-7; 2Sam 14:17; Dan 4:17Yeye hubadili nyakati na majira;

huwaweka wafalme na kuwaondoa.

Huwapa hekima wenye hekima,

na maarifa wenye ufahamu.

2:22 Mwa 40:8; 1Kor 2:10; Ay 12:22; Ebr 4:13; Isa 45:7; Yak 1:17; Za 139:11-12; Dan 4:17Hufunua siri na mambo yaliyofichika;

anajua yale yaliyo gizani,

nayo nuru hukaa kwake.

2:23 Mwa 31:5; Kut 3:15; Dan 1:17; Eze 28:3Ninakushukuru na kukuhimidi,

Ee Mungu wa baba zangu:

Umenipa hekima na uwezo,

umenijulisha kile tulichokuomba,

umetujulisha ndoto ya mfalme.”

Read More of Danieli 2