Wakolosai 1:24-29, Wakolosai 2:1-5 NEN

Wakolosai 1:24-29

Taabu Ya Paulo Kwa Ajili Ya Kanisa

1:24 2Kor 6:10; 1:5; 1Kor 12:27Sasa nafurahia kule kuteseka kwangu kwa ajili yenu, na katika mwili wangu ninatimiliza yale yaliyopungua katika mateso ya Kristo kwa ajili ya mwili wake, ambao ni kanisa. 1:25 Kol 1:23; 1Kor 3:5; Efe 3:2; Ebr 4:12Mimi nimekuwa mtumishi wa kanisa kwa wajibu alionipa Mungu ili kuwaletea ninyi Neno la Mungu kwa ukamilifu: 1:26 Rum 16:25Hii ni siri iliyokuwa imefichika tangu zamani na kwa vizazi vingi, lakini sasa imefunuliwa kwa watakatifu. 1:27 Mt 13:11; Rum 2:11, 24; 8:10Kwao, Mungu amechagua kujulisha miongoni mwa watu wa Mataifa utukufu wa utajiri wa siri hii, ambayo ni Kristo ndani yenu, tumaini la utukufu.

1:28 Kol 3:16; 1Kor 2:6, 7; Mt 5:48; Efe 5:27Yeye ndiye tunayemtangaza, tukimwonya kila mtu na kumfundisha kila mtu kwa hekima yote ili tuweze kumleta kila mmoja akiwa amekamilika katika Kristo. 1:29 1Kor 15:10; 2Kor 11:23; Kol 2:1; Efe 1:19; 3:7Kwa ajili ya jambo hili, ninajitaabisha, nikijitahidi kwa kadiri ya nguvu zake ambazo hutenda kazi ndani yangu kwa uweza mwingi.

Read More of Wakolosai 1

Wakolosai 2:1-5

2:1 Kol 1:29; 4:12; 4:13, 15, 16; Ufu 1:11Nataka mjue jinsi ninavyojitaabisha kwa ajili yenu na kwa ajili ya wale walioko Laodikia, na pia kwa ajili ya wote ambao hawajapata kuniona mimi binafsi. 2:2 Efe 6:22; Kol 4:8; Rum 16:25Kusudi langu ni watiwe moyo na kuunganishwa katika upendo, ili wapate ule utajiri wa ufahamu mkamilifu, ili waijue siri ya Mungu, yaani, Kristo mwenyewe, 2:3 Isa 11:2; Yer 23:5; Rum 11:33; 1Kor 1:24, 30ambaye ndani yake kumefichwa hazina zote za hekima na maarifa. 2:4 Rum 16:18Nawaambia mambo haya ili mtu yeyote asiwadanganye kwa maneno ya kuwashawishi. 2:5 1Kor 5:4; 1The 2:17Kwa kuwa ingawa mimi siko pamoja nanyi kimwili, lakini niko pamoja nanyi kiroho, nami nafurahi kuuona utaratibu wenu na jinsi uthabiti wa imani yenu katika Kristo ulivyo.

Read More of Wakolosai 2