Wakolosai 1:1-23 NEN

Wakolosai 1:1-23

Salamu

1:1 1Kor 1:1; 2Kor 1:1; Mdo 16:1Paulo, mtume wa Kristo Yesu, kwa mapenzi ya Mungu, na Timotheo ndugu yetu:

1:2 Kol 4:18; Rum 1:7Kwa ndugu watakatifu na waaminifu katika Kristo, waishio Kolosai:

Neema na amani zitokazo kwa Mungu Baba yetu ziwe nanyi.

Shukrani Na Maombi

1:3 Rum 1:8Siku zote tunamshukuru Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, tunapowaombea ninyi, 1:4 Gal 5:6; Mdo 9:13; Efe 1:15; Flm 5kwa sababu tumesikia kuhusu imani yenu katika Kristo Yesu, na upendo wenu mlio nao kwa watakatifu wote: 1:5 Kol 1:23; 1The 5:8; Tit 1:2; 1Pet 1:4; 2Tim 2:15imani na upendo ule utokao katika tumaini mlilowekewa akiba mbinguni, na ambalo mmesikia habari zake katika neno la kweli, yaani, ile Injili 1:6 Kol 1:23; Rum 10:18; Yn 15:16iliyowafikia ninyi. Duniani kote Injili hii inazaa matunda na kuenea kama ilivyokuwa kwenu tangu siku ile mlipoisikia na kuielewa neema ya Mungu katika kweli yote. 1:7 Kol 4:12; Flm 23; Kol 4:7Mlijifunza habari zake kutoka kwa Epafra, mtumishi mwenzetu mpendwa, yeye aliye mhudumu mwaminifu wa Kristo kwa ajili yenu, 1:8 Rum 15:30ambaye pia ametuambia kuhusu upendo wenu katika Roho.

1:9 Kol 1:4; Efe 1:15; Rum 1:10; Efe 5:17Kwa sababu hii, tangu siku ile tuliposikia habari zenu, hatujakoma kuomba kwa ajili yenu na kumsihi Mungu awajaze ninyi maarifa ya mapenzi yake katika hekima yote ya kiroho na ufahamu. 1:10 Efe 4:1; 2Kor 5:9; Kol 1:6Nasi tunaomba haya ili mpate kuishi maisha yanayostahili mbele za Bwana, na mpate kumpendeza kwa kila namna: mkizaa matunda kwa kila kazi njema, mkikua katika kumjua Mungu, 1:11 Flp 4:13; Efe 4:2mkiwa mmetiwa nguvu kwa uwezo wote kwa kadiri ya nguvu yake yenye utukufu, ili mpate kuwa na wingi wa saburi na uvumilivu. Nanyi kwa furaha 1:12 Efe 5:20; Mdo 20:32; 26:18mkimshukuru Baba, ambaye amewastahilisha kushiriki katika urithi wa watakatifu katika ufalme wa nuru. 1:13 Mdo 26:13; 2Pet 1:11; Mt 3:17Kwa maana ametuokoa kutoka ufalme wa giza na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wake mpendwa, 1:14 Rum 3:24; Efe 1:7ambaye katika yeye tunao ukombozi, yaani msamaha wa dhambi.

Ukuu Wa Kristo

1:15 Yn 14:9; 1:18; 1Tim 1:17; Ebr 11:27; Kol 1:18Yeye ni mfano wa Mungu asiyeonekana, mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote. 1:16 Yn 1:3; Efe 1:20, 21; Rum 11:36Kwake yeye vitu vyote vilivyoko mbinguni na juu ya nchi viliumbwa: vitu vinavyoonekana na visivyoonekana, viwe ni viti vya enzi au falme, au wenye mamlaka au watawala; vitu vyote viliumbwa na yeye na kwa ajili yake. 1:17 Yn 1:2Yeye alikuwepo kabla ya vitu vyote, na katika yeye vitu vyote vinashikamana pamoja. 1:18 Efe 1:22; Kol 1:24; 1Kor 12:27; Za 89:27; Rum 8:29Yeye ndiye kichwa cha mwili, yaani kanisa, naye ndiye mwanzo na mzaliwa wa kwanza kutoka kwa wafu, ili yeye awe mkuu katika vitu vyote. 1:19 Efe 1:15; Yn 1:16Kwa kuwa ilimpendeza Mungu kwamba utimilifu wake wote ukae ndani yake, 1:20 Rum 5:10; Efe 1:10; Lk 2:14; Efe 2:13na kwa njia yake aweze kuvipatanisha vitu vyote na yeye mwenyewe, viwe ni vitu vilivyo duniani au vilivyo mbinguni, kwa kufanya amani kwa damu yake, iliyomwagika msalabani.

1:21 Rum 5:10; Efe 2:3Hapo kwanza mlikuwa mmetengana na Mungu, na mlikuwa adui zake katika nia zenu kwa sababu ya mienendo yenu mibaya. 1:22 Kol 1:20; Rum 5:10; 7:4; 2Kor 4:14; Efe 1:4; 5:27Lakini sasa Mungu amewapatanisha ninyi kwa njia ya mwili wa Kristo kupitia mauti, ili awalete mbele zake mkiwa watakatifu, bila dosari wala lawama, ikiwa mnaendelea katika imani yenu mkiwa imara na thabiti, pasipo kuliacha tumaini lililoahidiwa katika Injili. Hii ndiyo ile Injili mliyoisikia, ambayo imehubiriwa kwa kila kiumbe chini ya mbingu, na ambayo mimi Paulo nimekuwa mtumwa wake.

Read More of Wakolosai 1