Amosi 8:1-14, Amosi 9:1-15 NEN

Amosi 8:1-14

Maono Ya Nne: Kikapu Cha Matunda Yaliyoiva

Hili ndilo alilonionyesha Bwana Mwenyezi katika maono: kikapu cha matunda yaliyoiva. 8:2 Mao 4:18; Yer 1:2, 13; 24:3; Eze 7:2-9; Amo 7:8; Mwa 40:16Akaniuliza, “Amosi, unaona nini?”

Nikajibu, “Kikapu chenye matunda yaliyoiva.”

Ndipo Bwana akaniambia, “Wakati umewadia kwa watu wangu Israeli; sitawahurumia zaidi.”

8:3 Amo 5:16-23; 6:10Bwana Mwenyezi asema, “Katika siku ile, nyimbo katika Hekalu zitageuka kuwa maombolezo. Miili mingi, mingi sana: itatupwa kila mahali! Kimya!”

8:4 Mit 30:14; Ay 20:19; Zek 14:4; Amo 2:7Lisikieni hili, ninyi ambao mnawagandamiza wahitaji,

na kuwaonea maskini wa nchi,

8:5 Kum 25:15; 2Fal 4:23; Neh 13:15-16; Hes 10:10; Isa 58:13; Mik 6:10; Mwa 31:7; Hos 12:7mkisema,

“Ni lini Mwezi Mwandamo utakapopita

ili tupate kuuza nafaka,

na Sabato itakwisha lini

ili tuweze kuuza ngano?”

Mkipunguza vipimo,

na kuongeza bei,

na kudanganya kwa mizani zisizo sawa,

8:6 Amo 2:6; 4:1; 5:11mkiwanunua maskini kwa fedha,

na wahitaji kwa jozi ya viatu,

na mkiuza hata takataka za ngano

pamoja na ngano.

8:7 Hos 8:13; Amo 6:8; Za 47:4; 68:34; Ay 35:15Bwana ameapa kwake mwenyewe, aliye Kiburi cha Yakobo: “Kamwe sitasahau chochote ambacho wamefanya.

8:8 Ay 9:6; Hos 4:3; Yer 46:8; 51:29; Za 18:7; Amo 9:5“Je, nchi haitatetemeka kwa ajili ya hili,

nao wote waishio ndani mwake hawataomboleza?

Nchi yote itainuka kama Naili;

itapanda na kushuka kama mto wa Misri.

8:9 Ay 5:14; Mk 15:33; Eze 32:7; Amo 4:13; 5:8; Isa 13:10; 59:9-10; Yer 15:9; Mik 3:6; 1The 5:2, 3; Mt 27:45“Katika siku ile,” asema Bwana Mwenyezi,

“Nitalifanya jua litue alasiri na kuifanya dunia

iwe giza wakati wa mchana mwangavu.

8:10 Yoe 1:8; Zek 12:10; Mwa 21:16; Hos 2:11; Lk 7:12, 13; Yer 6:26; 48:37; 2:19; Eze 7:18; Law 26:31; 13:40; Mao 5:15; Isa 3:17Nitageuza sikukuu zenu za kidini kuwa maombolezo,

na kuimba kwenu kote kuwe kilio.

Nitawafanya ninyi nyote mvae nguo ya gunia

na kunyoa nywele zenu.

Nitaufanya wakati ule uwe kama wa kuombolezea mwana wa pekee,

na mwisho wake kama siku ya uchungu.

8:11 1Sam 3:1; 28:6; Eze 7:26; Za 74:9; Mik 3:6; 2Nya 15:3; Yer 30:3; 31:27“Siku zinakuja,” asema Bwana Mwenyezi,

“wakati nitakapotuma njaa katika nchi yote:

si njaa ya chakula wala kiu ya maji,

lakini njaa ya kusikia maneno ya Bwana.

8:12 Eze 20:31Wanaume watayumbayumba kutoka bahari hadi bahari

na kutangatanga kutoka kaskazini mpaka mashariki,

wakitafuta neno la Bwana,

lakini hawatalipata.

8:13 Isa 41:17; 9:17; Hos 2:3; 8:14; Kum 9:21; 1Fal 12:29, 30; Hos 8:5, 6; 10:5; Mik 1:5; Za 46:2; Amo 5:2-5“Katika siku ile

“wasichana wazuri na vijana wanaume wenye nguvu

watazimia kwa sababu ya kiu.

Wale waapao kwa aibu ya Samaria,

au kusema, ‘Hakika kama miungu yenu iishivyo, ee Dani,’

au ‘Hakika kama mungu wa Beer-Sheba aishivyo’:

wataanguka, wala hawatasimama tena.”

Read More of Amosi 8

Amosi 9:1-15

Israeli Kuangamizwa

9:1 Za 68:21; Yer 11:11Nilimwona Bwana akiwa amesimama kando ya madhabahu, naye akasema:

“Piga vichwa vya nguzo

ili vizingiti vitikisike.

Viangushe juu ya vichwa vya watu wote;

na wale watakaosalia nitawaua kwa upanga.

Hakuna awaye yote atakayekimbia,

hakuna atakayetoroka.

9:2 Za 139:8-10; Ay 20:6; 7:9; Yer 51:33; Oba 1:4; Eze 26:20Wajapojichimbia chini mpaka kwenye vina vya kuzimu,

kutoka huko mkono wangu utawatoa.

Wajapopanda juu hadi kwenye mbingu,

kutoka huko nitawashusha.

9:3 Yer 23:24; 6:16-17; Za 139:8-10; 68:22; Mwa 49:17; Ay 11:20Wajapojificha juu ya kilele cha Karmeli,

huko nitawawinda na kuwakamata.

Wajapojificha kutoka kwenye uso wangu

katika vilindi vya bahari,

huko nako nitaamuru joka kuwauma.

9:4 Law 26:33; 17:10; Eze 5:12; 15:7; Kum 28:65; Yer 39:16; 21:10; 44:11Wajapopelekwa uhamishoni na adui zao,

huko nako nitaamuru upanga uwaue.

Nitawakazia macho yangu kwa mabaya

wala si kwa mazuri.”

9:5 Za 46:2; Amo 8:8; Mik 1:4Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote,

yeye agusaye dunia nayo ikayeyuka,

na wote wakaao ndani mwake wakaomboleza:

nayo nchi yote huinuka kama Naili,

kisha hushuka kama mto wa Misri;

9:6 Za 104:1-3, 5-13; Amo 5:8; Yer 43:9yeye ambaye hujenga jumba lake la kifalme katika mbingu

na kuisimika misingi yake juu ya dunia,

yeye aitaye maji ya bahari

na kuyamwaga juu ya uso wa nchi:

Bwana ndilo jina lake.

9:7 2Nya 12:3; Kum 2:23; Isa 43:3; 22:6; 2Fal 16:9; Yer 47:4; Amo 1:5; Mwa 10:14“Je, Waisraeli,

ninyi si sawa kwangu kama Wakushi?”

asema Bwana.

“Je, sikuleta Israeli kutoka Misri,

Wafilisti kutoka Kaftori,9:7 Yaani Krete.

na Washamu kutoka Kiri?

9:8 Yer 30:11; 44:27; Za 11:4“Hakika macho ya Bwana Mwenyezi

yako juu ya ufalme wenye dhambi.

Nami nitauangamiza

kutoka kwenye uso wa dunia:

hata hivyo sitaiangamiza kabisa

nyumba ya Yakobo,”

asema Bwana.

9:9 Lk 22:31; Isa 30:28; Yer 31:36; Dan 9:7“Kwa kuwa nitatoa amri,

na nitaipepeta nyumba ya Israeli

miongoni mwa mataifa yote,

kama vile nafaka ipepetwavyo katika ungo,

na hakuna hata punje moja itakayoanguka chini.

9:10 Yer 5:12; 23:17; 49:37; Eze 20:38; Amo 6:3Watenda dhambi wote miongoni mwa watu wangu

watauawa kwa upanga,

wale wote wasemao,

‘Maafa hayatatupata wala kutukuta.’

Kurejezwa Kwa Israeli

9:11 Mdo 15:16; Mik 7:8-11; Zek 12:7; Isa 7:2; 49:8; Mwa 26:22; Eze 17:24“Katika siku ile nitaisimamisha

hema ya Daudi iliyoanguka.

Nitakarabati mahali palipobomoka

na kujenga upya magofu yake,

na kuijenga kama ilivyokuwa awali,

9:12 Hes 24:18; Isa 43:7; Oba 1:19; Yer 25:29; Mdo 15:16-17ili wapate kuyamiliki mabaki ya Edomu,

na mataifa yote yale yanayobeba Jina langu,”

asema Bwana ambaye atafanya mambo haya.

9:13 Law 26:5; Amu 9:27; Yoe 3:18; 2:24; Yer 31:38; 33:14; Rut 2:3“Siku zinakuja,” asema Bwana,

“wakati mvunaji atatanguliwa na mkulima,

naye mpanzi atatanguliwa na yeye akamuaye zabibu.

Divai mpya itadondoka kutoka milimani,

na kutiririka kutoka vilima vyote.

9:14 Isa 32:18; 49:8; 62:9; 61:4; Eze 34:13-14; Yer 29:14; 33:7; 30:18Nitawarejesha tena watu wangu Israeli waliohamishwa;

wataijenga tena miji iliyoachwa magofu,

nao wataishi ndani mwake.

Watapanda mizabibu na kunywa divai yake;

watalima bustani na kula matunda yake.

9:15 Kut 15:17; Isa 60:21; 65:9; Yer 18:9; 23:8; 3:18; 24:6; 32:15; Eze 28:26; 34:28; Yoe 3:20Nitaipanda Israeli katika nchi yao wenyewe,

hawatangʼolewa tena

kutoka nchi ambayo nimewapa,”

asema Bwana Mungu wenu.

Read More of Amosi 9