Amosi 6:1-14, Amosi 7:1-17 NEN

Amosi 6:1-14

Ole Kwa Wanaoridhika

6:1 Lk 6:24; Isa 32:9-11; Ay 24:23; Sef 1:12; Amo 3:9Ole wenu ninyi mnaostarehe na kuridhika katika Sayuni,

na ninyi mnaojisikia salama juu ya Mlima Samaria,

ninyi watu mashuhuri wa taifa lililoendelea kuliko mataifa mengine,

ambao watu wa Israeli wanawategemea!

6:2 2Fal 17:24; Yer 49:23; Isa 10:9; 2Fal 14:25; Hes 34:8; Mwa 10:10; 2Nya 26:6; Yos 11:22Nendeni Kalne mkaone kutoka huko;

mwende hadi Hamathi iliyo kuu,

kisha mshuke hadi Gathi ya Wafilisti.

Je, wao ni bora kuliko falme zenu mbili?

Je, nchi yao ni kubwa kuliko yenu?

6:3 Isa 47:7; 56:12; Eze 12:22, 27; Mhu 8:11; Amo 5:18; 9:10Mnaiweka mbali siku iliyo mbaya

na kuleta karibu utawala wa kuogofya.

6:4 Isa 1:11; Eze 34:2-3; Amo 3:12; Mit 3:12; 7:17; Es 1:6Ninyi mnalala juu ya vitanda vilivyofunikwa kwa pembe za ndovu,

na kujinyoosha juu ya viti vya fahari.

Mnajilisha kwa wana-kondoo wazuri

na ndama walionenepeshwa.

6:5 Isa 5:12; 14:11; Za 137:2; Amo 5:23; 1Nya 15:16Ninyi mnapiga vinubi kama Daudi,

huku mkitunga nyimbo za vinanda mbalimbali.

6:6 Isa 28:1; Amo 2:8; Eze 9:4; 16:49Mnakunywa mvinyo kwa bakuli zilizojazwa,

na mnajipaka mafuta mazuri,

lakini hamhuzuniki kwa maangamizi ya Yosefu.

Kwa hiyo mtakuwa miongoni mwa watu wa kwanza kwenda uhamishoni;

karamu zenu na kustarehe kutakoma.

Bwana Anachukia Kiburi Cha Israeli

6:8 Mwa 22:16; Ebr 6:13; Law 26:19, 30; Za 47:4; Kum 32:19; Yer 12:8; Amo 4:2Bwana Mwenyezi ameapa kwa nafsi yake mwenyewe: Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote asema:

“Nachukia kiburi cha Yakobo,

nachukia ngome zake;

nitautoa mji wao na kila kitu

kilichomo ndani mwake.”

Kama watu kumi watabaki katika nyumba moja, wao pia watakufa. 6:10 1Sam 31:12; Amo 8:3Kama jamaa ambaye atachoma miili akija ili kuitoa nje ya nyumba, na kumuuliza yeyote ambaye bado anajificha humo, “Je, yuko mtu yeyote pamoja nawe?” Naye akisema, “Hapana,” ndipo atakaposema, “Nyamaza kimya! Haturuhusiwi kutaja jina la Bwana.”

6:11 Amo 3:15; Isa 55:11; 34:5Kwa kuwa Bwana ameamuru,

naye atabomoa jumba kubwa vipande vipande

na nyumba ndogo vipande vidogo vidogo.

6:12 Hos 10:4; Isa 1:21; Amo 5:7; 3:10Je, farasi waweza kukimbia kwenye miamba mikali?

Je, aweza mtu kulima huko kwa maksai?

Lakini mmegeuza haki kuwa sumu

na matunda ya uadilifu kuwa uchungu:

6:13 Ay 13:8; 8:15; Isa 28:14-15ninyi mnaoshangilia kushindwa kwa Lo-Debari

na kusema, “Je, hatukuteka Karnaimu kwa nguvu zetu wenyewe?”

6:14 Yer 5:15; Hes 13:21; 1Fal 8:65; Amo 3:11Maana Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote asema,

“Nitainua taifa dhidi yenu, ee nyumba ya Israeli,

nalo litawatesa kuanzia Lebo-Hamathi

hadi Bonde la Araba.”

Read More of Amosi 6

Amosi 7:1-17

Maono Ya Kwanza: Nzige

7:1 Amo 8:1; Za 78:46; Yer 51:14; Yoe 1:4Hili ndilo alilonionyesha Bwana Mwenyezi katika maono: Alikuwa anaandaa makundi ya nzige baada ya kuvunwa fungu la mfalme na wakati ule tu mimea ya pili ilipokuwa ikichipua. 7:2 Kut 10:15; Eze 11:13; Isa 37:4; Amo 4:9Wakati nzige walikuwa wamekula mimea yote ya nchi, nililia kwa sauti kuu, “Bwana Mwenyezi, samehe! Je, Yakobo atawezaje kuendelea kuishi? Yeye ni mdogo sana!”

7:3 Kut 32:14; Yon 3:10; Kum 32:36; Za 106:45; 1Nya 21:15; Hos 11:8; Yoe 2:14; Yak 5:16; Yer 18:8; 26:19Kwa hiyo Bwana akaghairi.

Kisha Bwana akasema, “Hili halitatokea.”

Maono Ya Pili: Moto

7:4 Isa 66:16; Yoe 1:19; Kum 32:22Hili ndilo Bwana Mwenyezi alilonionyesha katika maono: Bwana Mwenyezi alikuwa akiita hukumu ya moto; nao ulikausha vilindi vikuu, ukateketeza nchi. 7:5 Yoe 2:17Ndipo nikalia, “Bwana Mwenyezi, nakusihi, zuia! Je, Yakobo atawezaje kuendelea kuishi? Yeye ni mdogo sana!”

7:6 Kut 32:14; Yer 18:8; 42:10; Za 102:17; Yon 3:10; Eze 9:8Kwa hiyo Bwana akaghairi.

Bwana Mwenyezi akasema, “Hili nalo halitatokea.”

Maono Ya Tatu: Timazi

Hili ndilo alilonionyesha katika maono: Bwana alikuwa amesimama karibu na ukuta ambao ulikuwa umejengwa kwa timazi, akiwa na uzi wa timazi mkononi mwake. 7:8 Isa 28:17; Mao 2:8; 2Fal 21:13; Eze 7:2-9; Yer 1:11-13; 15:6; Mik 7:18Naye Bwana akaniuliza, “Je, Amosi unaona nini?”

Nikamjibu, “Uzi wa timazi.”

Kisha Bwana akasema, “Tazama, ninaweka uzi wa timazi miongoni mwa watu wangu Israeli; sitawahurumia tena.

7:9 Law 26:31; Mwa 26:23; 2Fal 14:23; 1Fal 13:34; 2Fal 15:9-10; Isa 63:18; Hos 10:8“Mahali pa Isaki pa juu pa kuabudia miungu pataangamizwa,

na mahali patakatifu pa Israeli pa kuabudia pataharibiwa;

kwa upanga wangu nitainuka

dhidi ya nyumba ya Yeroboamu.”

Amosi Na Amazia

7:10 1Fal 12:32; Yos 7:2; 2Fal 14:23-24; Yer 38:4; 26:8-11Kisha Amazia kuhani wa Betheli akatuma ujumbe kwa Yeroboamu mfalme wa Israeli, akisema: “Amosi analeta fitina juu yako katikati ya Israeli. Nchi haiwezi kuvumilia maneno yake yote. 7:11 Amo 5:27; Yer 36:16Kwa kuwa hili ndilo Amosi analosema:

“ ‘Yeroboamu atakufa kwa upanga,

na kwa hakika Israeli watakwenda uhamishoni,

mbali na nchi yao.’ ”

7:12 Mt 8:34; 1Sam 9:9Kisha Amazia akamwambia Amosi, “Nenda zako, ewe mwonaji! Urudi katika nchi ya Yuda. Ujipatie riziki yako huko na kutoa unabii wako. 7:13 Yer 20:2; 36:5; Amo 2:12; Mdo 4:18; Yos 7:2; 1Fal 12:29Usiendelee kutoa unabii katika Betheli, kwa sababu hapa ni mahali pa mfalme pa kuabudia na Hekalu la ufalme huu.”

7:14 1Sam 10:5; Zek 13:5; 2Fal 2:5; 4:38; Isa 9:10; 1Fal 10:27Amosi akamjibu Amazia, “Mimi sikuwa nabii wala mwana wa nabii, lakini nilikuwa mchungaji wa kondoo na mtunza mikuyu. 7:15 Mwa 37:5; 2Sam 7:8; Yer 7:1-2; 26:12; Eze 2:3-4; Isa 6:9Lakini Bwana akanitoa kutoka kuchunga kondoo na kuniambia, ‘Nenda, ukawatabirie watu wangu Israeli.’ 7:16 Isa 30:10; Eze 20:46; Mik 2:6; Yer 22:2Sasa basi, sikieni neno la Bwana. Ninyi mnasema,

“ ‘Usitabiri dhidi ya Israeli,

na uache kuhubiri dhidi ya nyumba ya Isaki.’

7:17 Hos 4:13; 9:3; Eze 4:13; Yer 28:12; 29:21; Mao 5:11; Amo 5:27; 2:12-13; 2Fal 17:6“Kwa hiyo hili ndilo asemalo Bwana:

“ ‘Mke wako atakuwa kahaba mjini,

nao wana wako na binti zako watauawa kwa upanga.

Shamba lako litapimwa na kugawanywa,

na wewe mwenyewe utafia katika nchi ya kipagani.

Nayo Israeli kwa hakika itakwenda uhamishoni,

mbali na nchi yao.’ ”

Read More of Amosi 7