Amosi 3:1-15, Amosi 4:1-13 NEN

Amosi 3:1-15

Mashahidi Waitwa Dhidi Ya Israeli

3:1 Amo 2:10; Sef 2:5Sikilizeni neno hili alilosema Bwana dhidi yenu, enyi watu wa Israeli, dhidi ya jamaa nzima niliowapandisha toka Misri:

3:2 Kut 19:6; 1Pet 4:17; Lk 12:47; Mik 2:3; Eze 9:6; Dan 9:12; Mt 11:22; Rum 2:9; Kum 7:6; Yer 14:10“Ni ninyi tu niliowachagua

kati ya jamaa zote za dunia;

kwa hiyo nitawaadhibu

kwa ajili ya dhambi zenu zote.”

Je, watu wawili hutembea pamoja

wasipokubaliana kufanya hivyo?

3:4 Za 104:21; Hos 5:14; Isa 42:13Je, simba hunguruma katika kichaka

wakati hana mawindo?

Aweza kuvuma katika pango

wakati ambao hajakamata chochote?

Je, ndege aweza kuanguka kwenye mtego ulio ardhini

ambapo hajategewa chambo?

Je, mtego unaweza kufyatuka toka ardhini

wakati ambapo hakuna chochote cha kunasa?

3:6 Isa 14:24-27; 31:2; 45:7; Hes 10:2; Eze 33:3; Ay 39:24; Yer 4:21Je, tarumbeta inapopigwa mjini kujulisha hatari,

watu hawatetemeki?

Mji upatwapo na maafa,

je, si Bwana amesababisha?

3:7 1Sam 3:7; Mwa 6:13; 18:17; Mit 3:32; Yn 15:15; Yer 23:22; Mit 3:32; Dan 9:22-27; Ufu 1:1, 19Hakika Bwana Mwenyezi hatafanya neno lolote

bila kuwafunulia watumishi wake manabii siri yake.

3:8 1Kor 9:16; Yn 3:1-3; Mdo 4:20; Isa 31:4; 42:13; Yer 20:9Simba amenguruma:

je, ni nani ambaye hataogopa?

Bwana Mwenyezi ametamka:

je, ni nani awezaye kukosa kutoa unabii?

3:9 Yos 13:3; 2Nya 26:6Tangazeni katika ngome za Ashdodi

na katika ngome za Misri:

“Kusanyikeni juu ya milima ya Samaria;

angalieni wingi wa wasiwasi ulio ndani yake,

na uonevu ulio miongoni mwa watu wake.”

3:10 Yer 4:22; Amo 6:12; 5:7; Mik 6:10; Hab 2:8Bwana asema: “Hawajui kutenda lililo jema,

wale ambao hujilundikia nyara

na vitu vilivyotekwa katika ngome zao.”

3:11 Amo 2:5; 6:14; 2Fal 17:6Kwa hiyo hili ndilo asemalo Bwana Mwenyezi:

“Adui ataizingira nchi;

ataangusha chini ngome zenu

na kuteka nyara maboma yenu.”

3:12 1Sam 17:34; Es 1:6; Amo 6:4Hili ndilo asemalo Bwana:

“Kama vile mchungaji aokoavyo kinywani mwa simba

vipande viwili tu vya mfupa wa mguu

au kipande cha sikio,

hivyo ndivyo Waisraeli watakavyookolewa,

wale wakaao Samaria

kwenye kingo za vitanda vyao,

na katika Dameski

kwenye viti vyao vya fahari.”

“Sikia hili na ushuhudie dhidi ya nyumba ya Yakobo,” asema Bwana, Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote.

3:14 Mwa 12:8; Amo 5:5-6; Kut 27:2; Law 26:18“Siku nitakapomwadhibu Israeli kwa sababu ya dhambi zake,

nitaharibu madhabahu za Betheli;

pembe za madhabahu zitakatiliwa mbali

na kuanguka chini.

3:15 Yer 36:22; Amu 3:20; 1Fal 22:39; Hos 10:5-8; Isa 34:5; Amo 5:11; 6:11Nitabomoa nyumba ya wakati wa masika,

pamoja na nyumba ya wakati wa kiangazi;

nyumba zilizonakshiwa kwa pembe za ndovu

na majumba makubwa ya fahari yatabomolewa,”

asema Bwana.

Read More of Amosi 3

Amosi 4:1-13

Israeli Hajarudi Kwa Mungu

4:1 Za 22:12; Isa 58:6; Eze 39:18; 18:12; Amo 3:9; 2:8; 8:6; Yer 44:19Sikilizeni neno hili, ninyi ngʼombe wa Bashani

mlioko juu ya Mlima Samaria,

ninyi wanawake mnaowaonea maskini,

na kuwagandamiza wahitaji,

na kuwaambia wanaume wenu,

“Tuleteeni vinywaji!”

4:2 Amo 6:8; Isa 19:8; Yer 31:31; 2Fal 19:28; 2Nya 33:11Bwana Mwenyezi ameapa kwa utakatifu wake:

“Hakika wakati utakuja

mtakapochukuliwa na kulabu,

na wanaosalia kwa ndoana za samaki.

4:3 Eze 12:5Nanyi mtakwenda moja kwa moja

kupitia mahali palipobomolewa kwenye ukuta,

nanyi mtatupwa nje kuelekea Harmoni,”

asema Bwana.

4:4 Hos 4:15; Hes 28:3, 4; 28:3; Eze 20:39; Kum 14:28; Yos 7:2; Amo 5:21, 22“Nendeni Betheli mkatende dhambi;

nendeni Gilgali mkazidi kutenda dhambi.

Leteni dhabihu zenu kila asubuhi,

zaka zenu kila mwaka wa tatu.

Mchome mkate uliotiwa chachu kama sadaka ya shukrani,

jisifuni kuhusu sadaka zenu za hiari:

jigambeni kwa ajili ya sadaka hizo, enyi Waisraeli,

kwa kuwa hili ndilo mnalopenda kulitenda,”

asema Bwana Mwenyezi.

4:6 Isa 9:13; 1Fal 17:1; Hag 2:17; Yer 5:3; Hos 5:15“Niliwapa njaa kwenye kila mji,

na ukosefu wa chakula katika kila mji,

hata hivyo bado hamjanirudia mimi,”

asema Bwana.

4:7 Kum 11:17; Isa 5:6; Zek 14:17; Kut 9:4, 26; 2Nya 7:13“Pia niliwazuilia ninyi mvua miezi mitatu

kabla ya kufikia mavuno.

Nilinyesha mvua kwenye mji mmoja,

lakini niliizuia mvua isinyeshe mji mwingine.

Shamba moja lilipata mvua,

na lingine halikupata, nalo likakauka.

4:8 Eze 4:16-17; Ay 36:31; Yer 14:4; 2:7; Hag 1:6Watu walitangatanga mji hata mji kutafuta maji,

lakini hawakupata ya kuwatosha kunywa,

hata hivyo hamjanirudia mimi,”

asema Bwana.

4:9 Kum 28:22; Isa 9:13; Hag 2:17; Yer 3:10; Yoe 1:7; 2:25; Kut 10:13“Mara nyingi nilizipiga bustani zenu na mashamba ya mizabibu,

niliyapiga kwa kutu na ukungu.

Nzige walitafuna tini zenu na miti ya mizeituni,

hata hivyo hamjanirudia mimi,”

asema Bwana.

4:10 Kut 9:3; 11:5; Kum 28:27; Isa 9:13, 17“Niliwapelekea tauni miongoni mwenu

kama nilivyofanya kule Misri.

Niliwaua vijana wenu wa kiume kwa upanga,

niliwachukua farasi wenu.

Nilijaza pua zenu kwa uvundo kutoka kwenye kambi zenu,

hata hivyo hamjanirudia mimi,”

asema Bwana.

4:11 Mwa 19:29; Yer 23:14; Isa 7:4; 13:19; Zek 3:2; Yud 23; Ay 36:13“Niliwaangamiza baadhi yenu kama

nilivyoangamiza Sodoma na Gomora.

Mlikuwa kama kijiti kiwakacho kilichonyakuliwa motoni,

hata hivyo hamjanirudia,”

asema Bwana.

“Kwa hiyo hili ndilo nitakalowafanyia, Israeli,

na kwa sababu nitawafanyia hili,

jiandaeni kukutana na Mungu wenu, ee Israeli.”

4:13 Dan 2:28; Za 65:6; 135:7; Yn 2:25; Amo 9:6; 5:8, 27; Isa 47:4Yeye ambaye hufanya milima, anaumba upepo,

na kufunua mawazo yake kwa mwanadamu,

yeye ageuzaye asubuhi kuwa giza,

na kukanyaga mahali pa juu pa nchi:

Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote ndilo jina lake.

Read More of Amosi 4