Amosi 1:1-15, Amosi 2:1-16 NEN

Amosi 1:1-15

1:1 2Sam 14:2; Zek 14:5; 2Fal 14:21-23; Hos 1:1; 2Nya 11:6; Za 78:70; 2Nya 26:23Maneno ya Amosi, mmoja wa wachunga wanyama wa Tekoa: yale aliyoyaona kuhusu Israeli miaka miwili kabla ya tetemeko la ardhi, wakati Uzia alikuwa mfalme wa Yuda, na Yeroboamu mwana wa Yehoashi alikuwa mfalme wa Israeli.

1:2 Isa 42:13; Yoe 3:16; Amo 9:3; Yer 12:4; Za 29:3Alisema:

Bwana ananguruma toka Sayuni,

pia ananguruma kutoka Yerusalemu;

malisho ya wachunga wanyama yanakauka,

kilele cha Karmeli kinanyauka.”

Hukumu Juu Ya Majirani Wa Israeli

1:3 Isa 8:4; 7:9; 17:1-3; 8:4; 2Fal 10:33; Amo 2:6Hili ndilo asemalo Bwana:

“Kwa dhambi tatu za Dameski,

hata kwa dhambi nne, sitaizuia ghadhabu yangu.

Kwa sababu aliipura Gileadi

kwa vyombo vya chuma vyenye meno.

1:4 Eze 30:8; Yer 17:27; 49:23-27; 1Fal 20:1; 19:17; 2Fal 6:24Nitatuma moto juu ya nyumba ya Hazaeli

ambao utateketeza ngome za Ben-Hadadi.

1:5 Yer 51:30; 49:27; Isa 7:1, 16; 22:6; Zek 9:1; 2Fal 16:9Nitalivunja lango la Dameski;

nitamwangamiza mfalme aliyeko katika Bonde la Aveni,1:5 Bonde la Aveni maana yake Bonde la Uovu.

na yeye ambaye anaishika fimbo ya utawala katika Beth-Edeni.

Watu wote wa Aramu watakwenda uhamishoni huko Kiri,”

asema Bwana.

1:6 2Nya 28:18; 1Sam 6:17; Mwa 10:19; 14:6; Oba 1:11; Sef 2:4Hili ndilo asemalo Bwana:

“Kwa dhambi tatu za Gaza,

hata kwa dhambi nne, sitaizuia ghadhabu yangu.

Kwa sababu walichukua mateka jumuiya nzima

na kuwauza kwa Edomu,

1:7 2Fal 18:8nitatuma moto juu ya kuta za Gaza

ambao utateketeza ngome zake.

1:8 2Nya 26:6; Za 81:14; Eze 25:16; Isa 14:28-32; 34:8; Sef 2:4-7Nitamwangamiza mfalme wa Ashdodi

na yeye aishikaye fimbo ya utawala katika Ashkeloni.

Nitaugeuza mkono wangu dhidi ya Ekroni,

hadi Mfilisti wa mwisho atakapokufa,”

asema Bwana Mwenyezi.

1:9 Isa 23:1-18; 1Fal 5:12; 9:11-14; Yer 25:22; Yoe 3:4Hili ndilo asemalo Bwana:

“Kwa dhambi tatu za Tiro,

hata kwa dhambi nne, sitaizuia ghadhabu yangu.

Kwa sababu ameuza jumuiya nzima ya mateka kwa Edomu,

na kutokujali mapatano ya undugu,

1:10 Yer 47:6; Eze 26:2-4; Isa 23:1-18; 34:8; Zek 9:1-4Nitatuma moto kwenye kuta za Tiro

ambao utateketeza ngome zake.”

1:11 Yer 49:7-22; Eze 25:12-14; Zek 1:15; Mal 1:4; Za 83:6; Hes 20:14-21; 2Nya 28:17Hili ndilo Bwana asemalo:

“Kwa dhambi tatu za Edomu,

hata kwa dhambi nne, sitaizuia ghadhabu yangu.

Kwa sababu alimfuatia ndugu yake kwa upanga,

alikataa kuonyesha huruma yoyote,

kwa sababu hasira yake kali iliendelea kupanda wakati wote

na ghadhabu iliwaka bila kuzuiliwa.

1:12 Mwa 36:11-15; Mao 1:9-10; Isa 34:5; 63:1-6; Eze 25:12-14; Mal 1:2-5Nitatuma moto juu ya Temani

ambao utateketeza ngome za Bosra.”

1:13 Mwa 19:38; 34:29; Yer 49:1-6; 2Fal 8:12; Hos 13:16; Eze 21:28Hili ndilo asemalo Bwana:

“Kwa dhambi tatu za Amoni,

hata kwa dhambi nne, sitaizuia ghadhabu yangu.

Kwa sababu aliwatumbua wanawake wajawazito wa Gileadi

ili kuongeza mipaka yake.

1:14 Kum 3:11; Ay 39:25; Eze 25:5; Amo 2:2; Isa 30:30; Yer 23:19Nitatuma moto kwenye kuta za Raba

ambao utateketeza ngome zake

katikati ya vilio vya vita katika siku ya mapigano,

katikati ya upepo mkali katika siku ya dhoruba.

1:15 Yer 25:21; 49:1-3; Eze 21:28-32; 25:2-7; 1Nya 20:1Mfalme wake atakwenda uhamishoni,

yeye pamoja na maafisa wake,”

asema Bwana.

Read More of Amosi 1

Amosi 2:1-16

2:1 Eze 25:8; Sef 2:8; 2Fal 3:27; Isa 16:6; 33:2Hili ndilo asemalo Bwana:

“Kwa dhambi tatu za Moabu,

hata kwa dhambi nne, sitaizuia ghadhabu yangu.

Kwa sababu alichoma mifupa ya mfalme wa Edomu,

ikawa kama chokaa.

2:2 Yer 48:7, 24; Ay 39:25; Yos 6:20Nitatuma moto juu ya Moabu

ambao utateketeza ngome za Keriothi.

Moabu ataanguka kwa ghasia kubwa

katikati ya vilio vya vita na mlio wa tarumbeta.

2:3 Hes 24:17; Za 2:10; Isa 40:23; Eze 25:8-11; Sef 2:8-9Nitamwangamiza mtawala wake

na kuwaua maafisa wake wote pamoja naye,”

asema Bwana.

2:4 Law 26:14; 2Sam 12:9, 10; 2Nya 36:14-17; Neh 1:7; Hos 12:2; Eze 9:11; Dan 9:11; 2Fal 17:19; Yer 6:19; 16:12; Isa 5:24; 9:16; 28:15; Kut 34:15Hili ndilo asemalo Bwana:

“Kwa dhambi tatu za Yuda,

hata kwa dhambi nne, sitaizuia ghadhabu yangu.

Kwa sababu wameikataa sheria ya Bwana

na hawakuzishika amri zake,

kwa sababu wamepotoshwa na miungu ya uongo,

miungu ambayo babu zao waliifuata.

2:5 Yer 17:27; Hos 8:14; 2Fal 25:9; Amo 3:11; 2Nya 36:19Nitatuma moto juu ya Yuda

ambao utateketeza ngome za Yerusalemu.”

Hukumu Juu Ya Israeli

2:6 Isa 29:21; Yoe 3:3; Amo 5:11, 12; 8:6Hili ndilo asemalo Bwana:

“Kwa dhambi tatu za Israeli,

hata kwa dhambi nne, sitaizuia ghadhabu yangu.

Wanawauza wenye haki kwa fedha,

na maskini kwa jozi ya viatu.

2:7 Eze 36:20; 22:11; Law 18:21; 20:3; Amo 8:4; 5:11-12; Rum 2:24; Isa 10:2Wanakanyaga juu ya vichwa vya maskini,

kama vile juu ya mavumbi ya nchi,

na kukataa haki kwa walioonewa.

Baba na mwanawe hushiriki msichana mmoja,

kwa hivyo hulinajisi Jina langu takatifu.

2:8 Kut 22:26; Hos 7:14; 1Kor 10:21; Hab 2:6; Amo 6:6; Kum 24:12-14Watu hulala kando ya kila madhabahu

juu ya nguo zilizowekwa rehani.

Katika nyumba ya mungu wao hunywa mvinyo

ulionunuliwa kwa fedha walizotozwa watu.

2:9 Hes 13:32; 21:23-26; Yos 10:12; Ay 18:16; Mal 4:1; Isa 10:33; Za 29:9“Nilimwangamiza Mwamori mbele yao,

ingawa alikuwa mrefu kama mierezi,

na mwenye nguvu kama mialoni.

Niliyaangamiza matunda yake juu

na mizizi yake chini.

2:10 Kut 6:6; 20:2; Hes 21:23; Yos 13:4; Amo 9:7; Kum 8:2; 2:7“Niliwapandisha toka Misri,

na nikawaongoza miaka arobaini jangwani

niwape nchi ya Waamori.

2:11 Kut 18:18; Yer 7:25; Hes 6:2-3; Amu 13:5Pia niliinua manabii kutoka miongoni mwa wana wenu

na Wanadhiri kutoka miongoni mwa vijana wenu.

Je, hii si kweli, enyi watu wa Israeli?”

asema Bwana.

2:12 Mdo 4:18; Isa 30:10; Yer 11:21; Amo 7:12-13; Mik 2:6“Lakini mliwafanya Wanadhiri kunywa mvinyo

na kuwaamuru manabii wasitoe unabii.

“Sasa basi, nitawaponda

kama gari lipondavyo wakati limejazwa nafaka.

2:14 1Fal 20:11; Yer 9:23; Za 33:16; Ay 11:20; Isa 30:16-17Mkimbiaji hodari hatanusurika,

wenye nguvu wataishiwa nguvu zao,

na shujaa hataweza kuokoa maisha yake.

2:15 Eze 39:3; Kut 15:21; Zek 10:5; Mhu 9:11Mpiga upinde atakimbia,

askari wapiga mbio hawataweza kutoroka,

na mpanda farasi hataokoa maisha yake.

2:16 Yer 48:41Hata askari walio mashujaa sana

siku hiyo watakimbia uchi,”

asema Bwana.

Read More of Amosi 2