Matendo 9:32-43, Matendo 10:1-23 NEN

Matendo 9:32-43

Matendo Ya Petro

(9:32–12:25)

Kuponywa Kwa Ainea

9:32 Mdo 9:13; 8:14Petro alipokuwa akisafiri sehemu mbalimbali, alikwenda kuwatembelea watakatifu walioishi huko Lida. Huko alimkuta mtu mmoja aitwaye Ainea, ambaye alikuwa amepooza na kwa muda wa miaka minane alikuwa hajaondoka kitandani. 9:34 Mdo 3:6, 16; 4:10Petro akamwambia, “Ainea, Yesu Kristo anakuponya, inuka utandike kitanda chako.” Mara Ainea akainuka. 9:35 Wim 2:1; Isa 65:10; Mdo 2:41; 11:21Watu wote wa Lida na Sharoni walipomwona Ainea akitembea wakamgeukia Bwana.

Petro Amfufua Dorkasi

9:36 Yn 1:3; Mdo 10:5; 1Tim 2:10; Tit 3:8Huko Yafa palikuwa na mwanafunzi jina lake Tabitha (ambalo kwa Kiyunani ni Dorkasi9:36 Tabitha kwa Kiaramu na Dorkasi kwa Kiaramu yote yamaanisha Paa.). Huyu alikuwa mkarimu sana, akitenda mema na kuwasaidia maskini. 9:37 Mdo 1:13; 20:8Wakati huo akaugua, akafa na wakiisha kuuosha mwili wake wakauweka katika chumba cha ghorofani. 9:38 Mdo 11:26Kwa kuwa Yafa hapakuwa mbali sana na Lida, wanafunzi waliposikia kwamba Petro yuko huko waliwatuma watu wawili kwake ili kumwomba, “Tafadhali njoo huku pasipo kukawia.”

9:39 Mdo 6:1; 1Tim 5:3Kwa hiyo Petro akainuka akaenda nao, naye alipowasili, wakampeleka hadi kwenye chumba cha ghorofani alipokuwa amelazwa. Wajane wengi walisimama karibu naye wakilia na kuonyesha majoho na nguo nyingine ambazo Dorkasi alikuwa amewashonea alipokuwa pamoja nao.

9:40 Mt 9:25; Lk 22:41; Mdo 7:60; Lk 7:14Petro akawatoa wote nje ya kile chumba, kisha akapiga magoti akaomba, akaugeukia ule mwili akasema, “Tabitha, inuka.” Akafumbua macho yake na alipomwona Petro, akaketi. 9:41 Mdo 9:32Petro akamshika mkono akamwinua, ndipo akawaita wale watakatifu na wajane akamkabidhi kwao akiwa hai. 9:42 Yn 11:45; 12:11Habari hizi zikajulikana sehemu zote za Yafa na watu wengi wakamwamini Bwana. 9:43 Mdo 10:6Petro akakaa Yafa kwa siku nyingi akiishi na Simoni mtengenezaji ngozi.

Read More of Matendo 9

Matendo 10:1-23

Kornelio Amwita Petro

10:1 Mdo 8:40Katika mji wa Kaisaria palikuwa na mtu jina lake Kornelio, ambaye alikuwa jemadari wa kile kilichojulikana kama kikosi cha Kiitalia. 10:2 Mdo 13:16-26Yeye alikuwa mcha Mungu pamoja na wote wa nyumbani mwake. Aliwapa watu sadaka nyingi na kumwomba Mungu daima. 10:3 Mdo 3:1; 9:10; 5:19Siku moja alasiri, yapata saa tisa, aliona maono waziwazi, malaika wa Mungu akimjia na kumwambia, “Kornelio!”

10:4 Za 20:3; Mt 10:42; Ufu 8:4Kornelio akamkazia macho kwa hofu akasema, “Kuna nini, Bwana?”

Malaika akamwambia, “Sala zako na sadaka zako kwa maskini zimefika juu na kuwa ukumbusho mbele za Mungu. 10:5 Mdo 9:36Sasa tuma watu waende Yafa wakamwite mtu mmoja jina lake Simoni aitwaye Petro. 10:6 Mdo 9:43Yeye anaishi na Simoni mtengenezaji ngozi ambaye nyumba yake iko kando ya bahari.”

Yule malaika aliyekuwa akizungumza naye alipoondoka, Kornelio akawaita watumishi wake wawili pamoja na askari mmoja mcha Mungu aliyekuwa miongoni mwa wale waliomtumikia. 10:8 Mdo 9:36Akawaambia mambo yote yaliyotukia, kisha akawatuma waende Yafa.

Maono Ya Petro

10:9 Mt 24:17; Mdo 11:5Siku ya pili yake, walipokuwa wameukaribia mji, wakati wa adhuhuri, Petro alipanda juu ya nyumba kuomba. 10:10 Mdo 22:17Alipokuwa akiomba akahisi njaa, akatamani kupata chakula. Lakini wakati walikuwa wakiandaa chakula, akalala usingizi mzito sana. 10:11 Mdo 11:5-17; Mt 3:16; Ufu 19:11Akaona mbingu zimefunguka na kitu kama nguo kubwa kikishushwa duniani kwa ncha zake nne. Ndani yake walikuwepo aina zote za wanyama wenye miguu minne, nao watambaao nchini, na ndege wa angani. Ndipo sauti ikamwambia “Petro, ondoka, uchinje na ule.”

10:14 Mdo 9:5; Kum 14:3-20; Eze 4:14Petro akajibu, “La hasha Bwana! Sijawahi kamwe kula kitu chochote kilicho najisi.”

10:15 Mwa 9:3; Tit 1:15Ile sauti ikasema naye mara ya pili, “Usikiite najisi kitu chochote Mungu alichokitakasa.”

Jambo hili lilitokea mara tatu na ghafula ile nguo ikarudishwa mbinguni.

10:17 Mdo 9:10; 10:7, 8Wakati Petro akiwa bado anajiuliza kuhusu maana ya maono haya, wale watu waliokuwa wametumwa na Kornelio wakaipata nyumba ya Simoni mtengenezaji wa ngozi wakawa wamesimama mbele ya lango. Wakabisha hodi na kuuliza kama Simoni aliyeitwa Petro alikuwa anaishi hapo.

10:19 Mdo 8:29; 13:2; 15:28Wakati Petro akiwa anafikiria juu ya yale maono, Roho Mtakatifu akamwambia, “Simoni, wako watu watatu wanaokutafuta. 10:20 Mdo 15:7-9Inuka na ushuke, usisite kwenda nao kwa kuwa mimi nimewatuma.”

Petro akashuka na kuwaambia wale watu waliokuwa wametumwa kutoka kwa Kornelio, “Mimi ndiye mnayenitafuta. Mmekuja kwa sababu gani?”

10:22 Mdo 11:14Wale watu wakamjibu, “Tumetumwa na Kornelio yule jemadari. Yeye ni mtu mwema anayemcha Mungu, na anaheshimiwa na Wayahudi wote. Yeye ameagizwa na malaika mtakatifu akukaribishe nyumbani kwake, ili asikilize maneno utakayomwambia.” 10:23 Mdo 1:16Basi Petro akawakaribisha wakafuatana naye ndani, akawapa pa kulala. Kesho yake akaondoka pamoja nao, na baadhi ya ndugu kutoka Yafa wakafuatana naye.

Read More of Matendo 10