Matendo 7:44-60, Matendo 8:1-3 NEN

Matendo 7:44-60

7:44 Kut 38:21; Hes 17:7; Kut 25:8“Baba zetu walikuwa na lile Hema la Ushuhuda huko jangwani. Lilikuwa limetengenezwa kama Mungu alivyokuwa amemwelekeza Mose, kulingana na kielelezo alichoona. 7:45 Yos 23:9; Za 132:1-5Baba zetu wakiisha kulipokea hema kwa kupokezana wakiongozwa na Yoshua katika milki ya nchi kutoka kwa yale mataifa ambayo Mungu aliyafukuza mbele yao, nalo likadumu katika nchi mpaka wakati wa Daudi, 7:46 1Fal 8:17; Za 44:2ambaye alipata kibali kwa Mungu, naye akaomba kwamba ampatie Mungu wa Yakobo maskani. 7:47 1Fal 6:1-38; 1Nya 17:12; 2Nya 3:1Lakini alikuwa Solomoni ndiye alimjengea Mungu nyumba.

7:48 1Fal 8:27; 2Nya 2:6“Hata hivyo, Yeye Aliye Juu Sana hakai kwenye nyumba zilizojengwa kwa mikono ya wanadamu. Kama nabii alivyosema:

7:49 Mt 5:32-35; Isa 66:1, 2; Mt 23:22“ ‘Mbingu ni kiti changu cha enzi,

nayo dunia ni mahali pa kuweka miguu yangu.

Mtanijengea nyumba ya namna gani?

asema Bwana.

Au mahali pangu pa kupumzikia patakuwa wapi?

7:50 Isa 66:1-2; Lk 23:34Je, mkono wangu haukufanya vitu hivi vyote?’

7:51 Kut 32:9; 33:3-5; Law 26:41; Yer 9:26“Enyi watu wenye shingo ngumu, msiotahiriwa mioyo wala masikio, daima hamwachi kumpinga Roho Mtakatifu, kama walivyofanya baba zenu. 7:52 2Nya 36:16; Mt 5:12; Mdo 3:14; 1The 2:15Je, kuna nabii gani ambaye baba zenu hawakumtesa? Waliwaua wale waliotabiri habari za kuja kwake yule Mwenye Haki. Nanyi sasa mmekuwa wasaliti wake na wauaji. 7:53 Gal 3:19; Ebr 2:2Ninyi ndio mlipokea sheria zilizoletwa kwenu na malaika, lakini hamkuzitii.”

Stefano Apigwa Mawe

7:54 Mt 5:33; Mdo 5:33Waliposikia haya wakaghadhibika, wakamsagia meno. 7:55 Mk 16:19; Mdo 6:5; Lk 22:69Lakini yeye Stefano, akiwa amejaa Roho Mtakatifu, alikaza macho mbinguni, akaona utukufu wa Mungu, na Yesu akiwa amesimama mkono wa kuume wa Mungu. 7:56 Mt 3:16; 8:20; Eze 1:1; Mdo 10:11; Dan 7:13Akasema, “Tazameni! Naona mbingu zimefunguka, na Mwana wa Adamu amesimama upande wa kuume wa Mungu.”

Lakini wao wakapiga kelele kwa sauti kubwa, wakaziba masikio yao, wakamrukia kwa nia moja. 7:58 Lk 4:29; Law 24:14-16; Kum 13; 9; Mdo 22:20; 8:1Wakamtupa nje ya mji, wakampiga kwa mawe. Nao mashahidi wakaweka mavazi yao miguuni mwa kijana mmoja ambaye jina lake aliitwa Sauli.

7:59 Za 31:5; Lk 23:46Walipokuwa wakimpiga mawe, Stefano aliomba, “Bwana Yesu, pokea roho yangu.” 7:60 Lk 22:41; Mdo 9:40; Mt 5:44Kisha akapiga magoti, akalia kwa sauti kubwa akasema, “Bwana usiwahesabie dhambi hii.” Baada ya kusema hayo, akalala.

Read More of Matendo 7

Matendo 8:1-3

8:1 Mdo 7:58; 11:19; 9:31Naye Sauli alikuwepo pale, akiridhia kuuawa kwa Stefano.

Kanisa Lateswa Na Kutawanyika

Siku ile kukatukia mateso makuu dhidi ya kanisa huko Yerusalemu, waumini wote isipokuwa mitume wakatawanyika, wakakimbilia Uyahudi na Samaria. 8:2 Mwa 23:2; 50:10; 2Sam 3:31; Mdo 14:12Watu wacha Mungu wakamzika Stefano na kumwombolezea sana. 8:3 Flp 3:6; 1Tim 1:13Lakini kwa habari ya Sauli alikuwa analiharibu kanisa, akiingia nyumba kwa nyumba, akiwaburuta wanawake na wanaume na kuwatupa gerezani.

Read More of Matendo 8