Matendo 7:20-43 NEN

Matendo 7:20-43

7:20 Kut 2:2; Ebr 11:23“Wakati huo Mose alizaliwa, naye hakuwa mtoto wa kawaida. Akalelewa nyumbani kwa baba yake kwa muda wa miezi mitatu. 7:21 Kut 2:3-10Waliposhindwa kumficha zaidi, wakamweka nje mtoni na binti Farao akamchukua akamtunza kama mtoto wake mwenyewe. 7:22 1Fal 4:30; Isa 19:11Mose akafundishwa hekima yote ya Wamisri, akawa mtu hodari kwa maneno na matendo.

7:23 Kut 2:11; 2:12“Mose alipokuwa na umri wa miaka arobaini aliamua kuwatembelea ndugu zake Waisraeli. Aliona mmoja wao akidhulumiwa na Mmisri, akamtetea yule aliyeonewa, akampiga yule Mmisri akamuua kulipiza kisasi. Mose alidhani kuwa ndugu zake wangetambua kwamba Mungu anamtumia ili kuwaokoa, lakini wao hawakuelewa. 7:26 Kut 2:13Siku iliyofuata Mose aliwakuta Waisraeli wawili wakigombana, akajaribu kuwapatanisha kwa kuwaambia, ‘Enyi watu, ninyi ni ndugu, mbona mnataka kudhulumiana?’

7:27 Lk 12:14; Mdo 4:7; Mwa 19:9; Hes 16; 13; Kut 2:14“Lakini yule mtu aliyekuwa akimdhulumu mwenzake akamsukuma Mose kando, akamuuliza, ‘Ni nani aliyekufanya mtawala na mwamuzi juu yetu? Je, unataka kuniua kama ulivyomuua yule Mmisri jana?’ 7:29 Kut 2:11-15Mose aliposikia maneno haya, alikimbilia huko Midiani alikokaa kama mgeni, naye akapata watoto wawili wa kiume.

7:30 Kut 3:2; 2:15, 22; 18:3, 4“Basi baada ya miaka arobaini kupita, malaika wa Mungu akamtokea Mose jangwani karibu na Mlima Sinai katika kichaka kilichokuwa kinawaka moto. 7:31 Kut 3:1-5Alipoona mambo haya, alishangaa yale maono. Aliposogea ili aangalie kwa karibu, akaisikia sauti ya Bwana, ikisema: 7:32 Mt 22:32; Ebr 11:16; Mdo 3:13; Kut 3:6‘Mimi ndimi Mungu wa baba zako, Mungu wa Abrahamu, Isaki na Yakobo.’ Mose alitetemeka kwa hofu na hakuthubutu kutazama.

7:33 Kut 3:5-6; Yos 5:15“Ndipo Bwana akamwambia, ‘Vua viatu vyako kwa maana mahali unaposimama ni patakatifu. 7:34 Kut 3:7-10Hakika nimeona mateso ya watu wangu huko Misri. Nimesikia kilio chao cha uchungu, nami nimeshuka ili niwaokoe. Basi sasa njoo, nami nitakutuma Misri.’

7:35 Mdo 7:27; Kut 2:14“Huyu ndiye Mose yule waliyemkataa wakisema, ‘Ni nani aliyekufanya mtawala na mwamuzi juu yetu?’ Alikuwa ametumwa na Mungu mwenyewe kuwa mtawala na mkombozi wao, kwa njia ya yule malaika aliyemtokea katika kile kichaka. 7:36 Kut 12:41; 33; 1; 14:21Aliwaongoza wana wa Israeli kutoka Misri, baada ya kufanya ishara na maajabu mengi huko Misri, katika Bahari ya Shamu,7:36 Yaani Bahari ya Mafunjo. na katika jangwa kwa muda wa miaka arobaini.

7:37 Kum 18:15, 18; Mdo 3:22; Mt 15:5“Huyu ndiye yule Mose aliyewaambia Waisraeli, ‘Mungu atawainulia nabii kama mimi kutoka miongoni mwa ndugu zenu wenyewe.’ 7:38 Kut 19:17; Law 27:34; Ebr 4:12; Rum 3:2Huyu ndiye yule Mose aliyekuwa katika kusanyiko huko jangwani, ambaye malaika alisema naye pamoja na baba zetu kwenye Mlima Sinai, naye akapokea maneno yaliyo hai ili atupatie.

7:39 Hes 14:3-4“Lakini baba zetu walikataa kumtii Mose, badala yake wakamkataa na kuielekeza mioyo yao Misri tena. 7:40 Kut 32:1-23Wakamwambia Aroni, ‘Tufanyie miungu watakaotuongoza, kwa maana mtu huyu Mose aliyetutoa nchi ya Misri, hatujui yaliyompata.’ 7:41 Za 106:19-20; Ufu 9:20Huu ni ule wakati walitengeneza sanamu katika umbo la ndama, wakailetea sadaka kufanya maadhimisho kwa ajili ya kile kitu walichokitengeneza kwa mikono yao wenyewe. 7:42 Yos 24:20; Isa 63:19; Yer 19:13Ndipo Mungu akageuka, akawaacha waabudu jeshi lote la mbinguni, kama ilivyoandikwa katika Kitabu cha Manabii:

“ ‘Je, mliniletea dhabihu na sadaka

kwa miaka arobaini kule jangwani,

ee nyumba ya Israeli?

7:43 Amo 5:25-27La, ninyi mliinua madhabahu ya Moleki,

na nyota ya mungu wenu Refani,

vinyago mlivyotengeneza ili kuviabudu.

Kwa hiyo nitawapeleka mbali’ kuliko Babeli.

Read More of Matendo 7