Matendo 6:1-15, Matendo 7:1-19 NEN

Matendo 6:1-15

Mateso Na Kuenea Kwa Injili

(6:1–9:31)

Saba Wachaguliwa Kuhudumu

6:1 Mdo 2:21; 4:35; 9:29, 39-41; 1Tim 5:3Basi ikawa katika siku hizo, wakati idadi ya wanafunzi ilipokuwa ikiongezeka sana, palitokea manungʼuniko kati ya Wayahudi wa Kiyunani, dhidi ya Waebrania kwa sababu wajane wao walisahaulika katika mgawanyo wa chakula wa kila siku. 6:2 Mdo 11:26; Ebr 4:12; Kut 18:17Wale mitume kumi na wawili wakakusanya wanafunzi wote pamoja wakasema, “Haitakuwa vyema sisi kuacha huduma ya neno la Mungu ili kuhudumu mezani. 6:3 Mdo 1:14-16; Lk 1:15; Kut 18:21; Neh 13:13; 1Tim 3:7, 8Kwa hiyo ndugu, chagueni watu saba miongoni mwenu, watu wenye sifa njema, waliojawa na Roho Mtakatifu na hekima, ambao tunaweza kuwakabidhi kazi hii, 6:4 Mdo 2:42nasi tutatumia muda wetu kuomba na huduma ya neno.”

6:5 Mdo 11:19; 22:20; 8:5-40; 21:8; Lk 1:15Yale waliyosema yakawapendeza watu wote, nao wakamchagua Stefano (mtu aliyejawa na imani na Roho Mtakatifu) pamoja na Filipo, Prokoro, Nikanori, Timoni, Parmena na Nikolao, mwongofu kutoka Antiokia. 6:6 Mdo 13:3; 2Tim 1:6; Hes 27; 18; Mk 5:23Wakawaleta watu hawa mbele ya mitume, nao wakawaombea na kuwawekea mikono juu yao.

6:7 Mdo 12:24; 19:20Neno la Mungu likazidi kuenea. Idadi ya wanafunzi ikazidi kuongezeka sana katika Yerusalemu hata makuhani wengi wakaitii ile imani.

Kukamatwa Kwa Stefano

6:8 Yn 4:48Stefano, akiwa amejaa neema na nguvu za Mungu, alifanya ishara na miujiza mikubwa miongoni mwa watu. 6:9 Mt 27:32; 22:3; 23:34; 2:9Hata hivyo, ukainuka upinzani wa watu wa Sinagogi la Watu Huru (kama lilivyokuwa linaitwa), la Wayahudi wa Kirene na wa Iskanderia, na wengine kutoka Kilikia na Asia. Watu hawa wakaanza kupingana na Stefano. 6:10 Lk 21:15; Mdo 5:39Lakini hawakuweza kushindana na hekima yake wala huyo Roho ambaye alisema kwake.

6:11 2Fal 21:10; Mt 26:59-61Ndipo kwa siri wakawashawishi watu fulani waseme, “Tumemsikia Stefano akisema maneno ya kufuru dhidi ya Mose na dhidi ya Mungu.”

Stefano Afikishwa Mbele Ya Baraza

6:12 Mt 5:22Wakawachochea watu, wazee na walimu wa Sheria, nao wakamkamata Stefano wakamfikisha mbele ya baraza. 6:13 Mt 24:15; Mdo 7:48Wakaweka mashahidi wa uongo ambao walishuhudia wakisema, “Mtu huyu kamwe haachi kusema dhidi ya mahali hapa patakatifu na dhidi ya Sheria. 6:14 Mdo 26:3; 28:17Kwa maana tumemsikia akisema kwamba Yesu wa Nazareti atapaharibu mahali patakatifu na kubadili desturi zote tulizopewa na Mose.”

6:15 Mt 5:22Watu wote waliokuwa wameketi katika baraza wakimkazia macho Stefano, wakaona uso wake unangʼaa kama uso wa malaika.

Read More of Matendo 6

Matendo 7:1-19

Hotuba Ya Stefano

Ndipo kuhani mkuu akamuuliza Stefano, “Je, mashtaka haya ni ya kweli?”

7:2 Za 29:3; Mwa 11:31; 15:7; Mdo 22:1Stefano akajibu, “Ndugu zangu na baba zangu, nisikilizeni! Mungu wa utukufu alimtokea baba yetu Abrahamu, alipokuwa bado yuko Mesopotamia, kabla hajaishi Harani, 7:3 Mwa 12:1-5; 48:4akamwambia, ‘Ondoka kutoka nchi yako na kutoka kwa jamii yako, uende hadi nchi nitakayokuonyesha.’

7:4 Mwa 12:5; Ebr 11:13“Hivyo aliondoka katika nchi ya Wakaldayo akaenda kukaa Harani. Baada ya kifo cha baba yake, Mungu akamtoa huko akamleta katika nchi hii ambayo mnaishi sasa. 7:5 Mwa 17:8; 26:3; 12:7; Ebr 11:13Mungu hakumpa urithi wowote katika nchi hii, hakumpa hata mahali pa kuweka wayo mmoja. Bali Mungu alimwahidi kuwa yeye na uzao wake baada yake wangeirithi hii nchi, ingawa wakati huo Abrahamu hakuwa na mtoto. 7:6 Kut 1:8-11; 12:40Mungu akasema naye hivi: ‘Wazao wako watakuwa wageni kwenye nchi ambayo si yao, nao watafanywa watumwa na kuteswa kwa miaka mia nne.’ 7:7 Mwa 15:13-14; Kut 3:12Mungu akasema, ‘Lakini mimi nitaliadhibu taifa watakalolitumikia kama watumwa, na baadaye watatoka katika nchi hiyo na wataniabudu mahali hapa.’ 7:8 Mwa 17:9-14; 21:2-4; 29:31-35; 35:16-18, 22-26Ndipo akampa Abrahamu Agano la tohara. Naye Abrahamu akamzaa Isaki na kumtahiri siku ya nane. Baadaye Isaki akamzaa Yakobo, naye Yakobo akawazaa wale wazee wetu kumi na wawili.

7:9 Mwa 37:4-11; 37:28; 39:2, 21-23; Hag 2:4“Kwa sababu wazee wetu walimwonea wivu Yosefu ndugu yao, walimuuza kama mtumwa huko Misri. Lakini Mungu alikuwa pamoja naye. 7:10 Mwa 41:37-41; Za 105:20-22Akamwokoa kutoka mateso yote yaliyompata, tena akampa kibali na hekima aliposimama mbele ya Farao, mfalme wa Misri, ambaye alimweka kuwa mtawala juu ya Misri na juu ya jumba lote la kifalme.

7:11 Mwa 41:54; 42:5“Basi kukawa na njaa katika nchi yote ya Misri na Kanaani, ikasababisha dhiki kubwa, nao baba zetu wakawa hawana chakula. 7:12 Mwa 42:12Lakini Yakobo aliposikia kwamba kuna nafaka huko Misri, aliwatuma baba zetu, wakaenda huko kwa mara yao ya kwanza. 7:13 Mwa 45:1-4Walipokwenda mara ya pili, Yosefu alijitambulisha kwa ndugu zake, nao ndugu zake Yosefu wakajulishwa kwa Farao. 7:14 Mwa 45:9-10; Kut 1:5; Kum 10:22Ndipo Yosefu akawatuma kumleta Yakobo baba yake pamoja na jamaa yake yote, jumla yao walikuwa watu sabini na watano. 7:15 Mwa 49:33Hivyo Yakobo akaenda Misri ambako yeye na baba zetu walifia. 7:16 Mwa 50:13; Yos 24:32Miili yao ilirudishwa Shekemu na kuzikwa katika kaburi ambalo Abrahamu alinunua kutoka kwa wana wa Hamori kwa kiasi fulani cha fedha.

7:17 Kut 1:6-7; Za 105:24“Lakini wakati ulipokuwa unakaribia wa kutimizwa kwa ile ahadi ambayo Mungu alikuwa amempa Abrahamu, watu wetu walizidi kuongezeka sana huko Misri. 7:18 Kut 1:8Ndipo mfalme mwingine ambaye hakujua lolote kuhusu Yosefu akatawala Misri. 7:19 Kut 1:8-22Huyu mfalme akawatendea watu wetu hila na kuwatesa baba zetu kwa kuwalazimisha wawatupe watoto wao wachanga ili wafe.

Read More of Matendo 7