Matendo 5:12-42 NEN

Matendo 5:12-42

Mitume Waponya Wengi

5:12 Yn 4:48; Mdo 2:43; 4:32; Yn 10:23Mitume wakafanya ishara nyingi na miujiza miongoni mwa watu. Walioamini wote walikuwa wakikusanyika katika ukumbi wa Solomoni. 5:13 Mdo 2:47; 4:21; Yn 9:22; 12:42; 19; 18Hakuna mtu mwingine aliyethubutu kuambatana nao ijapokuwa waliheshimiwa sana na watu. 5:14 Mdo 2:41, 47; 6; 7; 21:20Hata hivyo, waliomwamini Bwana wakazidi kuongezeka, wanaume na wanawake. 5:15 Mdo 19; 12Hata wakawa wanawaleta wagonjwa na kuwalaza kwenye magodoro na kwenye vitanda barabarani ili yamkini Petro akipita kivuli chake kiwaguse baadhi yao. 5:16 Mt 8:16; Mk 16:17Pia watu wakakusanyika kutoka miji iliyokuwa karibu na Yerusalemu, wakileta wagonjwa na watu walioteswa na pepo wachafu. Hao wote wakaponywa.

Mitume Washtakiwa

5:17 Mdo 15:5; 4:1Kisha kuhani mkuu na wenzake wote waliokuwa pamoja naye, waliokuwa wa kundi la Masadukayo, wakajawa na wivu. Wakawakamata mitume na kuwatia gerezani. 5:19 Kut 3:2; Mt 28:2; Mdo 16:26Lakini wakati wa usiku, malaika wa Bwana akaja, akafungua milango ya gereza na akawatoa nje. Akawaambia, 5:20 Yn 6:63-68; 17:3; 1Yn 5:11“Nendeni, mkasimame Hekaluni mkawaambie watu maneno yote ya uzima huu mpya.”

5:21 Mdo 4:5-6; Mt 5:22Waliposikia haya wakaenda Hekaluni alfajiri wakaendelea kufundisha watu.

Kuhani mkuu na wale waliokuwa pamoja nao walipowasili, alikusanya baraza na wazee wote wa Israeli wakatuma wale mitume waletwe kutoka gerezani. 5:22 Mdo 12:18, 19Lakini wale walinzi wa Hekalu walipokwenda gerezani hawakuwakuta mitume mle. Kwa hiyo wakarudi na kutoa habari. Wakasema, “Tumekuta milango ya gereza imefungwa sawasawa na askari wa gereza wamesimama nje ya mlango, lakini tulipofungua milango hakuwepo mtu yeyote ndani.” 5:24 Lk 22:4; Mdo 4:1Basi mkuu wa walinzi wa Hekalu na viongozi wa makuhani waliposikia haya, wakafadhaika na kushangaa sana kwa ajili yao kwamba jambo hili litakuwaje.

Ndipo mtu mmoja akaja akawaambia, “Tazameni watu mliowatia gerezani wako Hekaluni wakiwafundisha watu.” 5:26 Mdo 4:21Ndipo yule mkuu wa walinzi wa Hekalu wakaenda pamoja na askari wakawaleta wale mitume, lakini bila ghasia kwa sababu waliogopa kupigwa mawe na watu.

5:27 Mt 5:22Wakiisha kuwaleta mitume wakawaamuru kusimama mbele ya baraza ili kuhani mkuu awahoji. 5:28 Mdo 4:18; Mt 23:35; 27:25“Tuliwaonya kwa nguvu msifundishe kwa jina hili, lakini ninyi mmeijaza Yerusalemu yote mafundisho yenu na tena mmekusudia kuleta damu ya mtu huyu juu yetu.”

5:29 Kut 1:17; Mdo 4:19Petro na wale mitume wengine wakajibu, “Imetupasa kumtii Mungu kuliko wanadamu. 5:30 Mdo 3:13; 2:24; Gal 3:13; 1Pet 2:24Mungu wa baba zetu alimfufua Yesu kutoka kwa wafu, ambaye ninyi mlimuua kwa kumtundika kwenye msalaba. 5:31 Mk 16:19; Lk 2:11; Mdo 2:23Mungu alimtukuza, akamweka mkono wake wa kuume kuwa Kiongozi na Mwokozi ili awape Israeli toba na msamaha wa dhambi. 5:32 Lk 24:48; Yn 15:26Nasi tu mashahidi wa mambo haya, vivyo hivyo na Roho Mtakatifu ambaye Mungu amewapa wale wanaomtii.”

5:33 Mdo 2:37; 7:54Wale wajumbe wa baraza la wazee waliposikia haya, walijawa na ghadhabu, wakataka kuwaua mitume. 5:34 Mdo 22:3; Lk 2:46; 5:17Lakini Farisayo mmoja, jina lake Gamalieli, aliyekuwa mwalimu wa sheria, aliyeheshimiwa na watu wote, akasimama mbele ya baraza akaamuru mitume watolewe nje kwa muda. Ndipo alipowaambia wajumbe wa baraza, “Enyi watu wa Israeli, fikirini kwa uangalifu mnayotaka kuwatendea watu hawa. 5:36 Mdo 21:38Kwa maana wakati uliopita, aliinuka mtu mmoja jina lake Theuda, alijidai kuwa yeye ni mtu maarufu, akapata wafuasi wapatao 400 walioambatana naye. Lakini aliuawa, na wafuasi wake wote wakatawanyika, wakawa si kitu. 5:37 Lk 2:2Baada yake, alitokea Yuda Mgalilaya wakati wa kuorodhesha watu, naye akaongoza kundi la watu kuasi. Yeye pia aliuawa, nao wafuasi wake wakatawanyika. 5:38 Lk 15:13Kwa hiyo, kwa habari ya jambo hili nawashauri, jiepusheni na watu hawa. Waacheni waende zao! Kwa maana kama kusudi lao na shughuli yao imetokana na mwanadamu, haitafanikiwa. 5:39 2Nya 13:12; Mdo 11:17Lakini ikiwa imetoka kwa Mungu, hamtaweza kuwazuia watu hawa. Badala yake mtajikuta mnapigana na Mungu.”

5:40 Mt 10:17Wakapokea ushauri wa Gamalieli. Wakawaita mitume ndani, wakaamuru wachapwe mijeledi, kisha wakawaagiza wasinene tena kwa jina la Yesu, wakawaachia waende zao.

5:41 Mt 5:12; Mk 15:21Nao mitume wakatoka nje ya baraza, wakiwa wamejaa furaha kwa sababu wamehesabiwa kustahili kupata aibu kwa ajili ya jina la Yesu. 5:42 Mdo 2:46; 4:20, 29; 9:22; 13:32Kila siku, Hekaluni na nyumba kwa nyumba, hawakuacha kufundisha na kuhubiri habari njema kwamba Yesu ndiye Kristo.5:42 Kristo maana yake ni Masiya, yaani Aliyetiwa mafuta.

Read More of Matendo 5