Matendo 21:1-26 NEN

Matendo 21:1-26

Paulo Aenda Yerusalemu

21:1 Mdo 16:10Tulipokwisha kujitenga nao, tukaanza safari kwa njia ya bahari moja kwa moja mpaka Kosi. Siku ya pili yake tukafika Rodo na kutoka huko tukaenda Patara. 21:2 Mdo 11:19Hapo tukapata meli iliyokuwa inavuka kwenda Foinike tukapanda tukasafiri nayo. 21:3 Lk 2:2Tulipokiona kisiwa cha Kipro, tukakizunguka tukakiacha upande wetu wa kushoto, tukasafiri mpaka Shamu, tukatia nanga katika bandari ya Tiro ambapo meli yetu ilikuwa ipakue shehena yake. 21:4 Mdo 11:26; 20:23Baada ya kuwatafuta wanafunzi wa huko, tukakaa nao kwa siku saba. Wale wanafunzi wakiongozwa na Roho wakamwambia Paulo asiende Yerusalemu. 21:5 Mdo 20:36Lakini muda wetu ulipokwisha, tukaondoka tukaendelea na safari yetu. Wale wanafunzi pamoja na wake zao na watoto wakatusindikiza hadi nje ya mji. Wote tukapiga magoti pale pwani tukaomba. 21:6 Yn 1:11Baada ya kuagana, tukapanda melini, nao wakarudi majumbani mwao.

21:7 Mdo 12:20; 1:16Tukaendelea na safari yetu toka Tiro tukafika Tolemai, tukawasalimu ndugu wa huko, tukakaa nao kwa siku moja. 21:8 Efe 4:11; 2Tim 4:5; Mdo 6:5; 8:26, 40Siku iliyofuata tukaondoka, tukafika Kaisaria. Huko tukaenda nyumbani kwa mwinjilisti mmoja jina lake Filipo, aliyekuwa mmoja wa wale Saba, tukakaa kwake. 21:9 Yoe 2:28; Mdo 2:17; Kut 15:20Filipo alikuwa na binti wanne mabikira waliokuwa wanatoa unabii.

21:10 Mdo 11:28Baada ya kukaa kwa siku kadhaa, akateremka nabii mmoja kutoka Uyahudi jina lake Agabo. 21:11 Isa 20:2, 4Alipotufikia akachukua mshipi wa Paulo akajifunga, akautumia kufunga mikono na miguu yake mwenyewe akasema, “Roho Mtakatifu anasema: ‘Hivi ndivyo Wayahudi wa Yerusalemu watakavyomfunga mwenye mshipi huu na kumkabidhi kwa watu wa Mataifa.’ ”

Tuliposikia maneno haya sisi na ndugu wengine tukamsihi Paulo asiende Yerusalemu. 21:13 Mdo 20:24Lakini Paulo akajibu, “Kwa nini mnalia na kunivunja moyo? Mimi niko tayari si kufungwa tu, bali hata kufa huko Yerusalemu kwa ajili ya jina la Bwana Yesu.” 21:14 Mt 6:10; 26:42; Lk 11:2; 22:42; Rum 1:18Alipokuwa hashawishiki, tukaacha kumsihi, tukasema, “Mapenzi ya Bwana na yatendeke.”

21:15 Mdo 19:21Baada ya haya, tukajiandaa, tukaondoka kwenda Yerusalemu. 21:16 Mdo 8:40Baadhi ya wanafunzi kutoka Kaisaria wakafuatana nasi na kutupeleka nyumbani kwa Mnasoni, ambaye tungekaa kwake. Yeye alikuwa mtu wa Kipro, mmoja wa wanafunzi wa zamani.

Kukamatwa Kwa Paulo, Na Safari Yake Kwenda Rumi

(21:17–28:31)

Paulo Awasili Yerusalemu

21:17 Mdo 15:4Tulipofika Yerusalemu ndugu wakatukaribisha kwa furaha. 21:18 Mdo 15; 13; 11:30Kesho yake Paulo pamoja na wengine wetu tulikwenda kumwona Yakobo, na wazee wote walikuwepo. 21:19 Mdo 14:27; 1:17Baada ya kuwasalimu, Paulo akatoa taarifa kamili ya mambo yote ambayo Mungu alikuwa amefanya miongoni mwa watu wa Mataifa kupitia huduma yake.

21:20 Gal 1:14; Flp 3:6Baada ya kusikia mambo haya wakamwadhimisha Mungu. Ndipo wakamwambia Paulo, “Ndugu, unaona kulivyo na maelfu ya Wayahudi walioamini, nao wote wana juhudi kwa ajili ya sheria. 21:21 Mdo 15:19-21; 1Kor 7:18, 19; Mdo 6:14Lakini wameambiwa habari zako kwamba unafundisha Wayahudi wote waishio miongoni mwa watu wa Mataifa kumkataa Mose, na kwamba unawaambia wasiwatahiri watoto wao wala kufuata desturi zetu. Sasa tufanyeje? Bila shaka watasikia kwamba umekuja Yerusalemu. 21:23 Mdo 18:18Kwa hiyo fanya lile tunalokuambia. Tunao watu wanne hapa ambao wameweka nadhiri. 21:24 Mdo 24:18; 18:18Jiunge na watu hawa, mfanye utaratibu wa ibada ya kujitakasa pamoja nao, na ulipe gharama ili wanyoe nywele zao. Kwa njia hii kila mtu atafahamu ya kuwa mambo waliyosikia si ya kweli na kwamba wewe unaishika sheria. 21:25 Mdo 15:20-29Lakini kuhusu wale watu wa Mataifa walioamini, tumewaandikia uamuzi wetu: kwamba wajitenge na vyakula vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na damu, au kula nyama ya mnyama aliyenyongwa, na wajiepushe na uasherati.”

21:26 Hes 6:13, 20; Mdo 24:18Ndipo kesho yake Paulo akawachukua wale watu na akajitakasa pamoja nao. Akaingia ndani ya hekalu ili atoe taarifa ya tarehe ambayo siku zao za utakaso zingemalizika na sadaka ingetolewa kwa ajili ya kila mmoja wao.

Read More of Matendo 21