Matendo 2:22-47 NEN

Matendo 2:22-47

2:22 Yn 4:48; Mdo 10:38; Yn 3:2“Enyi Waisraeli, sikilizeni maneno haya nisemayo: Yesu wa Nazareti alikuwa mtu aliyethibitishwa kwenu na Mungu kwa miujiza, maajabu na ishara, ambayo Mungu alitenda miongoni mwenu kupitia kwake, kama ninyi wenyewe mjuavyo. 2:23 Isa 53:10; Lk 22:22; 24:20; Mt 16:21Huyu mtu akiisha kutolewa kwa shauri la Mungu lililokusudiwa kwa kujua kwake Mungu tangu zamani, ninyi, kwa mikono ya watu wabaya, mlimuua kwa kumgongomea msalabani. 2:24 Rum 8:11; Ebr 13:20; Yn 20:9Lakini Mungu alimfufua kutoka kwa wafu akamwondolea uchungu wa mauti, kwa sababu haikuwezekana yeye kushikiliwa na nguvu za mauti. 2:25 Za 16:8Kwa maana Daudi asema kumhusu yeye:

“ ‘Nalimwona Bwana mbele yangu daima.

Kwa sababu yuko mkono wangu wa kuume,

sitatikisika.

Kwa hiyo moyo wangu unafurahia,

na ulimi wangu unashangilia;

mwili wangu nao utapumzika kwa tumaini.

2:27 Mdo 13:35Kwa maana hutaniacha kaburini,

wala hutamwacha Aliye Mtakatifu wako kuona uharibifu.

2:28 Za 16:8-11Umenionyesha njia za uzima,

utanijaza na furaha mbele zako.’

2:29 Mdo 7:8-9; 1Fal 2:10; Neh 3:16“Ndugu zangu Waisraeli, nataka niwaambie kwa uhakika kwamba baba yetu Daudi alikufa na kuzikwa, nalo kaburi lake lipo hapa mpaka leo. 2:30 2Sam 7:12; Mt 1:1; Za 132:11; Lk 1:32, 69; Rum 1:3; 2Tim 2:8Lakini alikuwa nabii na alijua ya kuwa Mungu alikuwa amemwahidi kwa kiapo kwamba angemweka mmoja wa wazao wake penye kiti chake cha enzi. 2:31 Za 16:10; Mdo 13:35Daudi, akiona mambo yaliyoko mbele, akanena juu ya kufufuka kwa Kristo,2:31 Kristo maana yake ni Masiya, yaani Aliyetiwa mafuta. kwamba hakuachwa kaburini, wala mwili wake haukuona uharibifu. 2:32 Mdo 1:8; 2:24; Lk 24:48Mungu alimfufua huyu Yesu na sisi sote ni mashahidi wa jambo hilo. 2:33 Flp 2:9; Mk 16:19; Yn 14:26; Mdo 10:45; Yn 15:26Basi ikiwa yeye ametukuzwa kwa mkono wa kuume wa Mungu, amepokea kutoka kwa Baba ahadi ya Roho Mtakatifu, naye amemimina kile mnachoona sasa na kusikia. 2:34 Za 110:1; Mt 22:44; 1Kor 15:25; Efe 1:20; Ebr 1:13Kwa kuwa Daudi hakupaa kwenda mbinguni, lakini anasema,

“ ‘Bwana alimwambia Bwana wangu:

“Keti mkono wangu wa kuume,

2:35 Za 110:1; Mt 22:44hadi nitakapowaweka adui zako

chini ya miguu yako.” ’

2:36 Lk 2:11; Mdo 5:31; Mt 28:18“Kwa hiyo Israeli wote na wajue jambo hili kwa uhakika kwamba: Mungu amemfanya huyu Yesu, ambaye ninyi mlimsulubisha, kuwa Bwana na Kristo.”

Waumini Waongezeka

2:37 Lk 3:10-14; Mdo 16:30Watu waliposikia maneno haya yakawachoma mioyo yao, wakawauliza Petro na wale mitume wengine, “Ndugu zetu tufanye nini?”

2:38 Mdo 22:16; Kol 2:12; Yer 36:3Petro akawajibu, “Tubuni, mkabatizwe kila mmoja wenu kwa jina la Yesu Kristo, ili mpate kusamehewa dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu. 2:39 Isa 44:3; 66:23; 57:19; Efe 2:13Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu na watoto wenu, na kwa wote walio mbali, na kila mtu ambaye Bwana Mungu wetu atamwita amjie.”

2:40 Kum 32:5; Flp 2:15Petro akawaonya kwa maneno mengine mengi na kuwasihi akisema, “Jiepusheni na kizazi hiki kilichopotoka.” 2:41 Mdo 2:47; 4:4; 5:14; 9:31, 35, 42; 11:21, 24; 14:1, 21Wale wote waliopokea ujumbe wa Petro kwa furaha wakabatizwa na siku ile waliongezeka watu wapatao 3,000.

Ushirika Wa Waumini

2:42 Mdo 1:14Nao wakawa wanadumu katika mafundisho ya mitume, katika ushirika, katika kumega mkate na katika kusali. 2:43 Mdo 5:12Kila mtu akaingiwa na hofu ya Mungu, nayo miujiza mingi na ishara zikafanywa na mitume. 2:44 Mdo 4:32Walioamini wote walikuwa mahali pamoja, nao walikuwa na kila kitu shirika. 2:45 Mt 19:21; Lk 12:33Waliuza mali zao na vitu walivyokuwa navyo, kila mtu akagawiwa kadiri ya mahitaji yake. 2:46 Lk 24:53; Mdo 3:1; 20:7; Mt 14:19Siku zote kwa moyo mmoja walikutana ndani ya ukumbi wa Hekalu, wakimega mkate nyumba kwa nyumba, wakila chakula chao kwa furaha na moyo mweupe, 2:47 Rum 14:18; Mdo 5:14wakimsifu Mungu na kuwapendeza watu wote. Kila siku Bwana akaliongeza kanisa wale waliokuwa wakiokolewa.

Read More of Matendo 2