Matendo 15:1-21 NEN

Matendo 15:1-21

Baraza La Yerusalemu

15:1 Gal 2:12; 5:2, 3; Mdo 6:14Baadhi ya watu wakashuka Antiokia kutoka Uyahudi, nao wakawa wanawafundisha wandugu: “Msipotahiriwa kufuatana na desturi aliyofundisha Mose, hamwezi kuokoka.” 15:2 Gal 2:2; Mdo 11:30Baada ya Paulo na Barnaba kutokubaliana nao kukawa na mabishano makali, Paulo na Barnaba na baadhi ya wengine miongoni mwao wakachaguliwa kwenda Yerusalemu ili kujadiliana jambo hili na mitume na wazee. 15:3 Mdo 14:27Hivyo wakasafirishwa na kanisa, wakiwa njiani wakapitia nchi ya Foinike na Samaria, wakawaeleza jinsi watu wa Mataifa walivyookoka. Habari hizi zikaleta furaha kubwa kwa ndugu wote. 15:4 Mdo 21:19Walipofika Yerusalemu, walipokelewa na kanisa na mitume pamoja na wazee, ndipo Paulo na Barnaba wakawaarifu kila kitu Mungu alichokuwa amefanya kupitia kwao.

15:5 Mdo 5:17; Mt 3:7; Mdo 15:1Ndipo baadhi ya walioamini wa madhehebu ya Mafarisayo wakasimama na kusema, “Hao watu wa Mataifa lazima watahiriwe na waagizwe kutii sheria ya Mose.”

Mitume na wazee wakakutana pamoja ili kufikiri jambo hili. 15:7 Mdo 10:20; 11:12; 10:1-48Baada ya majadiliano mengi, Petro akasimama na kusema, “Ndugu zangu, mnajua kwamba siku za kwanza Mungu alinichagua ili kwa midomo yangu watu wa Mataifa wapate kusikia ujumbe wa Injili na kuamini. 15:8 Mdo 1:24; Ufu 2:23; Mdo 10:44, 47Mungu, yeye ajuaye mioyo, alionyesha kwamba anawakubali kwa kuwapa Roho Mtakatifu kama vile alivyotupa sisi. 15:9 Mdo 10:28, 34; 11:12; 10:43Mungu hakutofautisha kati yetu na wao, bali alitakasa mioyo yao kwa imani. 15:10 Mt 23:4; Gal 5:1Sasa basi, mbona mnataka kumjaribu Mungu kwa kuweka kongwa shingoni mwa wanafunzi ambalo baba zetu wala sisi hatukuweza kulibeba? 15:11 Gal 2:16; Efe 2:5-8Lakini sisi tunaamini ya kuwa tunaokolewa kwa neema ya Bwana Yesu Kristo, kama wao wanavyookolewa.”

15:12 Yn 4:48; Mdo 14:27; 21:19Kusanyiko lote likakaa kimya, wakawasikiliza Paulo na Barnaba wakieleza jinsi Mungu alivyowatumia kutenda ishara na maajabu kwa watu wa Mataifa. 15:13 1Kor 15:7; Gal 1:19Walipomaliza kunena, Yakobo akasema, “Ndugu zangu, nisikilizeni. 15:14 2Pet 1:1; Mdo 15:7; Lk 1:68Simoni amekwisha kutueleza jinsi Mungu, kwa mara ya kwanza alivyoonyesha kuhusika kwa kujichagulia watu kutoka watu wa Mataifa kwa ajili ya Jina lake. 15:15 Amo 9:11-12Maneno ya manabii yanakubaliana na jambo hili, kama ilivyoandikwa:

15:16 Amo 9:11-12“ ‘Baada ya mambo haya nitarudi,

nami nitajenga upya

nyumba ya Daudi iliyoanguka.

Nitajenga tena magofu yake

na kuisimamisha,

15:17 Amo 9:11, 12ili wanadamu wengine wote

wapate kumtafuta Bwana,

hata wale watu wa Mataifa wote

ambao wanaitwa kwa Jina langu,

asema Bwana, afanyaye mambo haya’

15:18 Isa 45:21ambayo yamejulikana tangu zamani.

15:19 Mdo 15:28; 1The 1:9“Kwa hivyo uamuzi wangu ni kwamba, tusiwataabishe watu wa Mataifa wanaomgeukia Mungu. 15:20 1Kor 8:7-13; Ufu 2:14, 20; 1Kor 10:7-8; Ufu 2:14; 20; Mwa 9:4; Law 7:26Badala yake, tuwaandikie kwamba wajiepushe na vyakula vilivyonajisiwa kwa kutolewa sanamu, wajiepushe na uasherati, au kula mnyama aliyenyongwa, na damu. 15:21 Mdo 13:15; 2Kor 3:14-15Kwa maana katika kila mji kwa vizazi vilivyopita, Mose amekuwa na wale wanaotangaza sheria yake kwa kuwa imekuwa ikisomwa kwa sauti kubwa katika masinagogi kila Sabato.”

Read More of Matendo 15