Matendo 14:8-28 NEN

Matendo 14:8-28

Paulo Na Barnaba Huko Listra

14:8 Mdo 3:2Katika mji wa Listra, alikuwako kiwete, ambaye alikuwa amelemaa tangu kuzaliwa na hakuwa ametembea kamwe. 14:9 Mt 9:28-29; 13:58Alimsikiliza Paulo alipokuwa akihubiri. Paulo alipomtazama akaona ana imani ya kuponywa. 14:10 Mdo 3:8Paulo akapaza sauti, “Simama kwa miguu yako!” Mara yule mtu akasimama upesi akaanza kutembea!

14:11 Mdo 10:26; Yak 5:17; Mdo 13:32; 1Sam 12:2Ule umati wa watu ulipoona yaliyokuwa yamefanywa na Paulo, wakapiga kelele kwa lugha yao ya Kilikaonia wakasema, “Miungu imetushukia katika umbo la binadamu!” 14:12 Kut 7:1Wakamwita Barnaba Zeu na Paulo wakamwita Herme kwa kuwa ndiye alikuwa msemaji mkuu. 14:13 Dan 2:46Kuhani wa Zeu, ambaye hekalu lake lilikuwa nje kidogo tu ya mji, akaleta mafahali na mashada ya maua penye lango la mji kwa sababu yeye na ule umati wa watu walitaka kuwatolea dhabihu.

14:14 Mt 26:65; Mk 14:63Lakini mitume Paulo na Barnaba waliposikia haya, wakararua nguo zao, wakawaendea wale watu kwa haraka, wakawapigia kelele, wakisema, 14:15 Mdo 10:26; 13:32; 1Sam 12:21; Mt 16:16; Mwa 1:1“Enyi watu, kwa nini mnafanya mambo haya? Sisi ni wanadamu tu kama ninyi! Tunawaletea habari njema, tukiwaambia kwamba mgeuke mtoke katika mambo haya yasiyofaa, mmwelekee Mungu aliye hai, aliyeziumba mbingu na nchi na bahari na vitu vyote vilivyomo. 14:16 Mdo 17:30; Za 81:12; Mk 4:5Zamani aliwaachia mataifa waishi walivyotaka. 14:17 Mdo 17:27; Rum 1:20; Ay 5:10; Za 65:10Lakini hakuacha kuwaonyesha watu uwepo wake: Ameonyesha wema kwa kuwanyeshea mvua toka mbinguni na kuwapa mazao kwa majira yake, naye amewapa chakula tele na kuijaza mioyo yenu na furaha.” Hata kwa maneno haya yote, ilikuwa vigumu kuuzuia ule umati wa watu kuwatolea dhabihu.

14:19 Mdo 13:45; 13:51; 2Kor 11:25; 2Tim 3:11Ndipo wakaja baadhi ya Wayahudi kutoka Antiokia na Ikonio wakawashawishi wale watu, wakampiga Paulo kwa mawe, wakamburuta hadi nje ya mji, wakidhani amekufa. 14:20 Mdo 11:26Lakini baada ya wanafunzi kukusanyika akainuka na kurudi mjini. Kesho yake yeye na Barnaba wakaondoka kwenda Derbe.

Paulo Na Barnaba Warudi Antiokia Huko Syria

14:21 Mdo 13:51Wakahubiri habari njema katika mji huo na kupata wanafunzi wengi. Kisha wakarudi Listra, Ikonio na Antiokia, 14:22 Mdo 11:23; 13:43; 2Tim 3:12wakiwaimarisha wanafunzi na kuwatia moyo waendelee kudumu katika imani. Wakawaonya wakisema, “Imetupasa kuingia katika Ufalme wa Mungu kwa kupitia katika taabu nyingi.” 14:23 Mdo 11:30; Tit 1:5; Mdo 13:3; 20:32Nao baada ya kuwateua wazee katika kila kanisa, kwa kufunga na kuomba wakawakabidhi kwa Bwana waliyemwamini. 14:24 Mdo 2:10Kisha wakapitia Pisidia wakafika Pamfilia. Baada ya kuhubiri neno la Mungu huko Perga, wakateremkia Atalia.

14:26 Mdo 11:19; 11:23; 15:40; 13:13Kutoka Atalia wakasafiri baharini wakarudi Antiokia, ambako walikuwa wamesifiwa kwa ajili ya neema ya Mungu kutokana na ile huduma waliyokuwa wameikamilisha. 14:27 Mdo 15:4-12; 21:19; Kol 4:3; Ufu 3:8Walipowasili Antiokia wakaliita kanisa pamoja na kutoa taarifa ya yale yote Mungu aliyokuwa ametenda kupitia kwao na jinsi alivyokuwa amefungua mlango wa imani kwa ajili ya watu wa Mataifa. Nao wakakaa huko pamoja na wanafunzi kwa muda mrefu.

Read More of Matendo 14