Matendo 13:42-52, Matendo 14:1-7 NEN

Matendo 13:42-52

13:42 Mdo 13:14Paulo na Barnaba walipokuwa wakitoka nje ya sinagogi, watu wakawaomba wazungumze tena mambo hayo Sabato iliyofuata. 13:43 Mdo 11:23; 14:22; Rum 3:24Baada ya kusanyiko la Sinagogi kutawanyika, wengi wa Wayahudi na waongofu wa dini ya Kiyahudi wakawafuata Paulo na Barnaba, wakazungumza nao na kuwahimiza wadumu katika neema ya Mungu.

Sabato iliyofuata, karibu watu wote wa mji walikuja kusikiliza neno la Bwana. 13:45 Mdo 18:6; 1Pet 4:4; 1The 2:16Lakini Wayahudi walipoona ule umati mkubwa wa watu walijawa na wivu, wakayakanusha maneno Paulo aliyokuwa akisema.

13:46 Mdo 13:26; 3:26; 18:6; 22:21; 26:20; 28:28; Rum 11:11; Mt 21:41Ndipo Paulo na Barnaba wakawajibu kwa ujasiri, wakisema, “Ilitupasa kunena nanyi neno la Mungu kwanza. Lakini kwa kuwa mmelikataa, mkajihukumu wenyewe kuwa hamstahili uzima wa milele, sasa tunawageukia watu wa Mataifa. 13:47 Lk 2:32; Isa 49:6Kwa maana hili ndilo Bwana alilotuamuru:

“ ‘Nimewafanya ninyi kuwa nuru kwa watu wa Mataifa,

ili mpate kuuleta wokovu hadi miisho ya dunia.’ ”

13:48 Mdo 13:49; 8:25; Rum 8:29Watu wa Mataifa waliposikia haya wakafurahi na kulitukuza neno la Bwana; nao wote waliokuwa wamekusudiwa uzima wa milele wakaamini.

13:49 Mdo 13:48Neno la Bwana likaenea katika eneo lile lote. 13:50 1The 2:16Lakini Wayahudi wakawachochea wanawake wenye kumcha Mungu, wenye vyeo pamoja na watu maarufu katika mji, wakachochea mateso dhidi ya Paulo na Barnaba na kuwafukuza kutoka eneo hilo. 13:51 Mt 10:14; Mdo 14:1; 19:21; 2Tim 3:11Hivyo Paulo na Barnaba wakakungʼuta mavumbi ya miguu yao ili kuwapinga, nao wakaenda Ikonio. 13:52 Mdo 11:26; Lk 1:5Wanafunzi wakajawa na furaha na Roho Mtakatifu.

Read More of Matendo 13

Matendo 14:1-7

Paulo Na Barnaba Huko Ikonio

14:1 Mdo 13:51; 9:20; 2:41Huko Ikonio Paulo na Barnaba waliingia pamoja katika sinagogi la Wayahudi kama ilivyokuwa desturi yao. Huko wakahubiri kwa uwezo mkubwa kiasi kwamba Wayahudi pamoja na watu wa Mataifa wakaamini. 14:2 Mdo 4:29; Yn 4:48; Ebr 2:4Lakini wale Wayahudi waliokataa kuamini, wakawachochea watu wa Mataifa, wakatia chuki ndani ya mioyo yao dhidi ya wale walioamini. 14:3 Mt 10:23Hivyo Paulo na Barnaba wakakaa huko kwa muda wa kutosha wakihubiri kwa ujasiri juu ya Bwana, ambaye alithibitisha ujumbe wa neema yake kwa kuwawezesha kufanya ishara na miujiza. 14:4 Mdo 16:10; 13:32Lakini watu wa mji ule waligawanyika, wengine wakakubaliana na Wayahudi na wengine na mitume. 14:5 Mdo 20:3; 14:19; 2Tim 3:11Watu wa Mataifa na Wayahudi wakajiunga na baadhi ya viongozi, wakafanya mpango wa kuwatendea mitume mabaya na kuwapiga mawe. 14:6 Mt 10:23Lakini mitume walipopata habari hizi wakakimbilia Listra na Derbe, miji ya Likaonia na sehemu zilizopakana nayo. 14:7 Mdo 16:10; 13:32Huko wakaendelea kuhubiri habari njema.

Read More of Matendo 14