Matendo 13:13-41 NEN

Matendo 13:13-41

Paulo Na Barnaba Huko Antiokia Ya Pisidia

13:13 Mdo 13:6; 2:10; 12:12Kisha Paulo na wenzake wakasafiri toka Pafo wakafika Perga huko Pamfilia. Lakini, Yohana Marko akawaacha huko, akarejea Yerusalemu. 13:14 Mdo 14:19, 21; 13:27, 42, 44; 16:13; 18:4; 9:20Kutoka Perga wakaendelea hadi Antiokia ya Pisidia. Siku ya Sabato wakaingia ndani ya sinagogi, wakaketi. 13:15 Mdo 15:21; Lk 4:16; Ebr 13:22Baada ya Sheria ya Mose na Kitabu cha Manabii kusomwa, viongozi wa sinagogi wakawatumia ujumbe wakisema, “Ndugu, kama mna neno la kuwafariji watu hawa, tafadhali lisemeni.”

13:16 Mdo 12:17; 10:35Paulo akasimama, akawapungia mkono na kusema: “Enyi wanaume wa Israeli na ninyi nyote mnaomcha Mungu. 13:17 Kut 6:6, 7; Kum 7:6-8Mungu wa watu hawa wa Israeli aliwachagua baba zetu, akawafanya kustawi walipokuwa huko Misri, kwa uwezo mwingi akawaongoza na kuwatoa katika nchi ile. 13:18 Kum 1:31; Hes 14:33; Za 95:10; Mdo 7:36Kwa muda wa miaka arobaini alivumilia matendo yao walipokuwa jangwani. 13:19 Kum 7:1; Yos 14:2; Za 78:55Naye baada ya kuyaangamiza mataifa saba waliokuwa wakiishi katika nchi ya Kanaani, akawapa Waisraeli nchi yao iwe urithi wao. 13:20 Amu 2:17; 1Sam 3:19, 20; Mdo 3:24Haya yote yalichukua kama muda wa miaka 450.

“Baada ya haya, Mungu akawapa waamuzi mpaka wakati wa nabii Samweli. 13:21 1Sam 8:5, 19; 10:1; 9:1, 2Ndipo watu wakaomba wapewe mfalme, naye Mungu akawapa Sauli mwana wa Kishi wa kabila la Benyamini, aliyetawala kwa miaka arobaini. 13:22 1Sam 15:23, 26; 16:13; Za 89:20; Yer 3:15; Isa 44:28; 1Sam 13:14Baada ya kumwondoa Sauli katika ufalme, akawainulia Daudi kuwa mfalme wao. Mungu pia alimshuhudia, akisema, ‘Nimemwona Daudi mwana wa Yese, mtu anayeupendeza moyo wangu, atakayetimiza mapenzi yangu yote.’

13:23 Mt 1:1; Lk 2:11; Mt 1:21; 2Sam 7:11; 22:51; Yer 30:9“Kutoka uzao wa mtu huyu, Mungu amewaletea Israeli Mwokozi Yesu, kama alivyoahidi. 13:24 Mk 1:4; Lk 3:3Kabla ya kuja kwa Yesu, Yohana alihubiri toba na ubatizo kwa watu wote wa Israeli. 13:25 Mdo 20:24; Yn 1:20; Mt 3:11; Yn 1:27Yohana alipokuwa anakamilisha kazi yake, alisema: ‘Ninyi mnadhani mimi ni nani? Mimi si yeye. La hasha, lakini yeye yuaja baada yangu, ambaye mimi sistahili kufungua kamba za viatu vya miguu yake.’

13:26 Mdo 22:5; Lk 3:8; Mt 4:12; Mdo 28:28; Mt 10:6“Ndugu zangu, wana wa Abrahamu, nanyi watu wa Mataifa mnaomcha Mungu, ujumbe huu wa wokovu umeletwa kwetu. 13:27 Mdo 3:17; Lk 24:27; Mt 1:22Kwa sababu wakaao Yerusalemu na viongozi wao hawakumtambua wala kuelewa maneno ya manabii yasomwayo kila Sabato, bali waliyatimiza maneno hayo kwa kumhukumu yeye. 13:28 Mt 27:20-25; Mdo 3:13Ijapokuwa hawakupata sababu yoyote ya kumhukumu kifo, walimwomba Pilato aamuru auawe. 13:29 Mt 1:22; Lk 8:31; Mdo 5:30; Lk 23:53Walipokwisha kufanya yale yote yaliyoandikwa kumhusu, walimshusha kutoka msalabani na kumzika kaburini. 13:30 Mt 16:21; 28:6; Mdo 2:24Lakini Mungu alimfufua kutoka kwa wafu. 13:31 Mt 28; 16; Lk 24:48Naye kwa siku nyingi akawatokea wale waliokuwa pamoja naye kuanzia Galilaya hadi Yerusalemu. Nao sasa wamekuwa mashahidi wake kwa watu wetu.

13:32 Isa 40:9; 52:7; Mdo 5:42; 8:35; 10:36; Rum 12; 4:13; 9:4“Nasi tunawaletea habari njema, kwamba yale Mungu aliyowaahidi baba zetu 13:33 Mdo 2:24; Za 2:7; Mt 3:17sasa ameyatimiza kwetu sisi watoto wao, kwa kumfufua Yesu, kama ilivyoandikwa katika Zaburi ya pili:

“ ‘Wewe ni Mwanangu;

leo mimi nimekuzaa.’

13:34 Isa 55:6; 55:3Kwa kuwa Mungu alimfufua kutoka kwa wafu asioze kamwe, alitamka maneno haya:

“ ‘Nitakupa wewe baraka takatifu zilizo za hakika

nilizomwahidi Daudi.’

13:35 Za 16; 10; Mdo 2:27Kama ilivyosemwa mahali pengine katika Zaburi,

“ ‘Hutamwacha Aliye Mtakatifu wako kuona uharibifu.’

13:36 Mt 9:24; 2Sam 7:12; 1Fal 2:10; 2Nya 29:28; Mdo 2:29“Kwa maana Daudi akiisha kulitumikia kusudi la Mungu katika kizazi chake, alilala; akazikwa pamoja na baba zake na mwili wake ukaoza. 13:37 Mdo 2:24Lakini yule ambaye Mungu alimfufua kutoka kwa wafu hakuona uharibifu.

13:38 Lk 24:47; Mdo 2:38“Kwa hiyo ndugu zangu, nataka ninyi mjue kwamba kwa kupitia huyu Yesu msamaha wa dhambi unatangazwa kwenu. 13:39 Yn 3:15; Rum 3:28; 10:4Kwa kupitia yeye, kila mtu amwaminiye anahesabiwa haki kwa kila kitu ambacho asingeweza kuhesabiwa haki kwa sheria ya Mose. 13:40 Hab 1:4Kwa hiyo jihadharini ili yale waliyosema manabii yasiwapate:

13:41 Hab 1:5“ ‘Angalieni, enyi wenye dhihaka,

mkastaajabu, mkaangamie,

kwa maana nitatenda jambo wakati wenu

ambalo hamtasadiki,

hata kama mtu akiwaambia.’ ”

Read More of Matendo 13