Matendo 12:19-25, Matendo 13:1-12 NEN

Matendo 12:19-25

12:19 Mdo 8:1-4; 16:27; 8:40Baada ya Herode kuamuru atafutwe kila mahali na bila kumpata, aliwahoji wale askari walinzi kisha akatoa amri wauawe. Basi Herode Agripa akatoka Uyahudi akaenda Kaisaria, akakaa huko kwa muda.

Kifo Cha Herode Agripa

12:20 Mt 11:21; 1Fal 5:9, 11; Eze 27:17Basi Herode Agripa alikuwa amekasirishwa sana na watu wa Tiro na Sidoni. Hivyo watu wa miji hiyo miwili wakaungana pamoja wakatafuta kukutana naye. Wakiisha kuungwa mkono na Blasto, mtumishi maalum wa Mfalme Herode Agripa aliyeaminika, wakaomba mapatano ya amani maana nchi zao zilitegemea nchi ya huyo mfalme kwa mahitaji yao ya chakula.

Katika siku iliyochaguliwa Herode Agripa akavaa mavazi yake ya kifalme, akaketi kwenye kiti chake cha enzi na kuwahutubia watu. 12:22 Eze 28:2Watu waliokuwa wamekusanyika wakapiga kelele, wakisema, “Hii si sauti ya mwanadamu, bali ni ya Mungu.” 12:23 Mdo 5:19; 1Sam 25:38; 2Sam 24:16; 2Fal 19:35Ghafula, kwa kuwa Herode hakumpa Mungu utukufu, malaika wa Bwana akampiga, naye akaliwa na chango, akafa.

12:24 Ebr 4:12; Mdo 6:7; 19:20Lakini neno la Mungu likaendelea mbele na kuenea, nao wengi wakaambatana nalo.

12:25 Mdo 4:36; 11:30; 12:12Barnaba na Sauli walipomaliza ile huduma yao iliyowapeleka, wakarudi Yerusalemu wakiwa pamoja na Yohana aitwaye Marko.

Read More of Matendo 12

Matendo 13:1-12

Safari Ya Kwanza Ya Paulo Kueneza Injili

(13:1–14:28)

Barnaba Na Sauli Wanatumwa

13:1 Mdo 11:19, 27; Efe 4:11; Mdo 4:36; Mt 27:32; 14:1Katika kanisa huko Antiokia ya Shamu walikuwako manabii na walimu, yaani: Barnaba, Simeoni aitwaye Nigeri, Lukio Mkirene, Manaeni aliyekuwa amelelewa pamoja na Mfalme Herode Agripa, na Sauli. 13:2 Mdo 8:29; 14:26; 9:15; 22:21Walipokuwa wakimwabudu Bwana na kufunga, Roho Mtakatifu akasema, “Nitengeeni Sauli na Barnaba kwa kazi ile maalum niliyowaitia.” 13:3 Mdo 6:6; 14:26; 1Tim 4:14; 5:22Ndipo baada ya kufunga na kuomba, wakawawekea mikono yao na wakawatuma waende zao.

Barnaba Na Sauli Waenda Kipro

13:4 Mdo 13:2, 3; 4:36; 15:39Hivyo, wakiwa wametumwa na Roho Mtakatifu, wakashuka kwenda Seleukia na kutoka huko wakasafiri baharini mpaka kisiwa cha Kipro. 13:5 Ebr 4:12; 9:20; 12:12Walipowasili katika mji wa Salami, wakahubiri neno la Mungu katika sinagogi la Wayahudi. Pia walikuwa na Yohana Marko kuwa msaidizi wao.

13:6 Mdo 8:9; Mt 7:15Walipokwisha kupita katika nchi zote hizo wakafika Pafo, ambapo walikutana na Myahudi mmoja mchawi aliyekuwa nabii wa uongo, jina lake Bar-Yesu. 13:7 Mdo 13:8, 12; 18:12; 19:38Mtu huyu alikuwa pamoja na Sergio Paulo, mtu mwenye hekima aliyekuwa msaidizi wa mwakilishi wa mtawala wa kile kisiwa. Sergio Paulo akawaita Sauli na Barnaba akitaka kusikia neno la Mungu. 13:8 Mdo 8:9; Isa 30:11; Mdo 6:7; 2Tim 3:8Lakini Elima yule mchawi (hii ndiyo maana ya jina lake), aliwapinga Barnaba na Sauli na kujaribu kumpotosha yule mkuu wa kile kisiwa aiache imani. 13:9 Lk 1; 15Ndipo Sauli, ambaye pia aliitwa Paulo, akiwa amejawa na Roho Mtakatifu, akamkazia macho Elima huyo mchawi, 13:10 Mt 13:38; Yn 8:44; Hos 14:9akamwambia, “Ewe mwana wa ibilisi, wewe ni adui wa kila kilicho haki! Umejaa kila aina ya udanganyifu na ulaghai. Je, hutaacha kuzipotosha njia za Bwana zilizonyooka? 13:11 Kut 9:3; 1Sam 5:6, 7; Za 32:4; Mwa 19:10, 11Nawe sasa sikiliza, mkono wa Bwana u dhidi yako. Utakuwa kipofu, wala hutaona jua kwa muda.”

Mara ukungu na giza vikamfunika, naye akaenda huku na huko akitafuta mtu wa kumshika mkono ili amwonyeshe njia. 13:12 Mdo 13:7Yule mkuu wa kile kisiwa alipoona yaliyotukia, akaamini kwa sababu alistaajabishwa na mafundisho kuhusu Bwana.

Read More of Matendo 13