Matendo 11:19-30, Matendo 12:1-19 NEN

Matendo 11:19-30

Kanisa La Antiokia

11:19 Mdo 8:1-4; 14:26; Gal 2:11Basi wale waliotawanyika kwa ajili ya mateso yaliyotokana na kifo cha Stefano, wakasafiri hadi Foinike na Kipro na Antiokia. Nao hawakuhubiri lile Neno kwa mtu yeyote isipokuwa Wayahudi. 11:20 Mdo 4:36; Mt 27:32; Mdo 4:36; Mt 27:32Lakini baadhi yao walikuwepo watu wa Kipro na Kirene, ambao walipokuja Antiokia walinena na Wayunani pia wakiwahubiria habari njema za Bwana Yesu. 11:21 Lk 1:66; Mdo 2:41-47Mkono wa Bwana ulikuwa pamoja nao, nayo idadi kubwa ya watu wakaamini na kumgeukia Bwana.

11:22 Mdo 4:36Habari hizi zilipofika masikioni mwa kanisa huko Yerusalemu, wakamtuma Barnaba aende Antiokia. 11:23 Mdo 15:40; 20:24; 14:22Alipofika na kuona madhihirisho ya neema ya Mungu, akafurahi na kuwatia moyo waendelee kuwa waaminifu kwa Bwana kwa mioyo yao yote. 11:24 Mdo 2:41; 5:14Barnaba alikuwa mtu mwema, aliyejaa Roho Mtakatifu, mwenye imani, nayo idadi kubwa ya watu wakaongezeka kwa Bwana.

11:25 Mdo 9:11Kisha Barnaba akaenda Tarso kumtafuta Sauli, 11:26 Mdo 6:1-2; 9:19-26; 26:28; 1Pet 4:16naye alipompata akamleta Antiokia. Hivyo kwa mwaka mzima Barnaba na Sauli wakakutana na kanisa na kufundisha idadi kubwa ya watu. Ilikuwa ni katika kanisa la Antiokia kwa mara ya kwanza wanafunzi waliitwa Wakristo.

11:27 1Kor 11:4; Efe 4:11Wakati huo manabii walishuka toka Yerusalemu hadi Antiokia. 11:28 Mdo 21:10; Mt 24:14; Mdo 18:2Mmoja wao, jina lake Agabo, akasimama akatabiri kwa uweza wa Roho Mtakatifu kwamba njaa kubwa itaenea ulimwengu mzima. Njaa hiyo ilitokea wakati wa utawala wa Klaudio. 11:29 Rum 15:26; 2Kor 8:1-4; Mdo 1:16Mitume wakaamua kwamba kila mtu, kulingana na uwezo alio nao, atoe msaada kwa ajili ya ndugu wanaoishi Uyahudi. 11:30 Mdo 14:23; 15:2; 22; 20:17; 1Tim 5:17; Tit 1:5; Yak 5:14; 1Pet 5:1; Mdo 4:36; 12:25Wakafanya hivyo, misaada yao ikapelekwa kwa wazee kwa mikono ya Barnaba na Sauli.

Read More of Matendo 11

Matendo 12:1-19

Yakobo Auawa, Petro Atiwa Gerezani

12:1 Mt 14:1Wakati huo huo Mfalme Herode Agripa aliwakamata baadhi ya watu wa kanisa. 12:2 Mt 4:21; Mk 10:39Akaamuru Yakobo, ndugu yake Yohana, auawe kwa upanga. 12:3 Mdo 24:27; 25:9; Kut 12:15; 23:15; Mdo 20:6Alipoona jambo hilo limewapendeza Wayahudi, akaendelea, akamkamata pia Petro. Hii ilitokea wakati wa Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu. 12:4 Yn 11:15Baada ya kumkamata alimtia gerezani, chini ya ulinzi wa vikundi vinne vya askari, vyenye askari wanne kila kimoja. Herode alikuwa amekusudia kumtoa na kumfanyia mashtaka mbele ya watu baada ya Pasaka.

12:5 Mdo 1:14; Efe 6:18Kwa hiyo Petro akawekwa gerezani, lakini kanisa lilikuwa likimwombea kwa Mungu kwa bidii.

12:6 Mdo 21:33Usiku ule kabla ya siku ambayo Herode Agripa alikuwa amekusudia kumtoa na kumfanyia mashtaka, Petro alikuwa amelala kati ya askari wawili, akiwa amefungwa kwa minyororo miwili. Nao walinzi wa zamu walikuwa wakilinda penye lango la gereza. 12:7 Mdo 5:19; Za 107:14; Mdo 16:26Ghafula malaika wa Bwana akatokea na nuru ikamulika mle ndani ya gereza. Yule malaika akampiga Petro ubavuni na kumwamsha, akisema, “Ondoka upesi!” Mara ile minyororo ikaanguka kutoka mikononi mwa Petro.

Yule malaika akamwambia, “Vaa nguo zako na viatu vyako.” Petro akafanya hivyo. Kisha akamwambia, “Jifunge vazi lako na unifuate.” 12:9 Mdo 9:10Petro akatoka mle gerezani akiwa amefuatana na yule malaika. Hakujua wakati huo kuwa yaliyokuwa yakitukia yalikuwa kweli. Alidhani kuwa anaona maono. 12:10 Mdo 5:19; 16:26Wakapita lindo la kwanza na la pili, ndipo wakafika kwenye lango la chuma linaloelekea mjini. Lango likawafungukia lenyewe, nao wakapita hapo wakatoka nje. Baada ya kutembea umbali wa mtaa mmoja, ghafula yule malaika akamwacha Petro.

12:11 Lk 15:17; Za 34:7; Dan 3:28; 6:22; 2Kor 11:10; 2Pet 2:9Ndipo Petro akarudiwa na fahamu, akasema, “Sasa ninajua bila shaka yoyote kuwa Bwana amemtuma malaika wake na kuniokoa kutoka makucha ya Herode Agripa na kutoka matazamio yote ya Wayahudi.”

12:12 Mdo 12:25; 15:37; Kol 4:10; 2Tim 4:11; 1Pet 5:13Mara Petro alipotambua hili alikwenda nyumbani kwa Maria, mama yake Yohana aliyeitwa pia Marko, ambako watu wengi walikuwa wamekutana kwa maombi. 12:13 Yn 18:16Petro alipobisha hodi kwenye lango la nje, mtumishi wa kike jina lake Roda, akaja kumfungulia. 12:14 Lk 24:41Alipoitambua sauti ya Petro, alifurahi mno akarudi bila kufungua na kuwaeleza kwamba, “Petro yuko langoni!”

12:15 Mt 18:10Wakamwambia yule mtumishi wa kike, “Umerukwa na akili.” Alipozidi kusisitiza kuwa ni kweli, wakasema, “Lazima awe ni malaika wake.”

Lakini Petro aliendelea kugonga langoni, nao walipofungua lango na kumwona Petro, walistaajabu sana. 12:17 Mdo 19:33; 21:40Yeye akawaashiria kwa mkono wake wanyamaze kimya, akawaeleza jinsi Bwana alivyomtoa gerezani. Naye akaongeza kusema, “Waelezeni Yakobo na ndugu wengine habari hizi.” Kisha akaondoka akaenda sehemu nyingine.

12:18 Mdo 5:21, 22Kulipokucha kukawa na fadhaa kubwa miongoni mwa wale askari kuhusu yaliyomtukia Petro. 12:19 Mdo 8:1-4; 16:27; 8:40Baada ya Herode kuamuru atafutwe kila mahali na bila kumpata, aliwahoji wale askari walinzi kisha akatoa amri wauawe. Basi Herode Agripa akatoka Uyahudi akaenda Kaisaria, akakaa huko kwa muda.

Read More of Matendo 12