Matendo 1:23-26, Matendo 2:1-21 NEN

Matendo 1:23-26

1:23 Mdo 15:22Wakapendekeza majina ya watu wawili: Yosefu, aitwaye Barsaba (ambaye pia alijulikana kama Yusto) na Mathiya. 1:24 Mdo 13:3; 14:23; 1Sam 16:7; Ufu 2:23Kisha wakaomba, wakasema, “Bwana, wewe waujua moyo wa kila mtu. Tuonyeshe ni yupi kati ya hawa wawili uliyemchagua 1:25 Mdo 1:17ili achukue nafasi ya huduma ya utume ambayo Yuda aliiacha ili aende mahali pake mwenyewe.” 1:26 Mdo 2:14Kisha wakawapigia kura, nayo kura ikamwangukia Mathiya, naye akaongezwa kwenye wale mitume kumi na mmoja.

Read More of Matendo 1

Matendo 2:1-21

Kushuka Kwa Roho Mtakatifu

2:1 Law 23:15-16; 1Kor 16:18; Mdo 1:14Siku ya Pentekoste ilipowadia, waamini wote walikuwa mahali pamoja. 2:2 Mdo 4:31Ghafula sauti kama mvumo mkubwa wa upepo mkali uliotoka mbinguni ukaijaza nyumba yote walimokuwa wameketi. 2:3 Mt 3:11Zikatokea ndimi kama za moto zilizogawanyika na kukaa juu ya kila mmoja wao. 2:4 Mk 16:17; 1Kor 12:10Wote wakajazwa na Roho Mtakatifu, wakaanza kunena kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia.

2:5 Lk 2:25; Mdo 8:2Basi walikuwepo Yerusalemu Wayahudi wanaomcha Mungu kutoka kila taifa chini ya mbingu. Waliposikia sauti hii, umati wa watu ulikusanyika pamoja wakistaajabu, kwa sababu kila mmoja wao aliwasikia wakisema kwa lugha yake mwenyewe. 2:7 Mdo 1:11Wakiwa wameshangaa na kustaajabu wakauliza, “Je, hawa wote wanaozungumza si Wagalilaya? Imekuwaje basi kila mmoja wetu anawasikia wakinena kwa lugha yake ya kuzaliwa? 2:9 Mdo 18:2; 1Pet 1:1; 2Kor 1:8; Ufu 1:4Wapathi, Wamedi, Waelami, wakazi wa Mesopotamia, Uyahudi, Kapadokia, Ponto na Asia, 2:10 Mdo 16:6; 18:23; 14:24; Mt 27:32Frigia, Pamfilia, Misri na pande za Libya karibu na Kirene na wageni kutoka Rumi, Wayahudi na waongofu, Wakrete na Waarabu, sote tunawasikia watu hawa wakisema mambo makuu ya ajabu ya Mungu katika lugha zetu wenyewe.” Wakiwa wameshangaa na kufadhaika wakaulizana, “Ni nini maana ya mambo haya?”

2:13 1Kor 14:23; Efe 5:18Lakini wengine wakawadhihaki wakasema, “Hawa wamelewa divai!”

Petro Ahutubia Umati

Ndipo Petro akasimama pamoja na wale mitume kumi na mmoja, akainua sauti yake na kuhutubia ule umati wa watu, akasema: “Wayahudi wenzangu na ninyi nyote mkaao Yerusalemu, jueni jambo hili mkanisikilize. 2:15 1The 5:7Hakika watu hawa hawakulewa kama mnavyodhania, kwa kuwa sasa ni saa tatu asubuhi! 2:16 Yoe 2:28-32La, hili ni jambo lililotabiriwa na nabii Yoeli, akisema:

2:17 Eze 39:29; Yn 7:37-39; Mdo 21:9“ ‘Katika siku za mwisho, asema Mungu,

nitamimina Roho wangu

juu ya wote wenye mwili.

Wana wenu na binti zenu watatabiri,

vijana wenu wataona maono,

na wazee wenu wataota ndoto.

2:18 Mdo 21:9-12; 1Kor 12:10, 28; 14:1Hata juu ya watumishi wangu, wanaume kwa wanawake,

katika siku zile nitamimina Roho wangu,

nao watatabiri.

2:19 Yoe 2:30, 31; Lk 21:11Nami nitaonyesha maajabu juu mbinguni,

na ishara chini duniani:

damu, moto, na mawimbi ya moshi.

2:20 Mt 24:29Jua litakuwa giza

na mwezi utakuwa mwekundu kama damu,

kabla ya kuja siku ile kuu ya Bwana

iliyo tukufu.

2:21 Yoe 2:28-32; Rum 10:13Na kila mtu atakayeliitia

jina la Bwana, ataokolewa.’

Read More of Matendo 2