2 Timotheo 1:1-18 NEN

2 Timotheo 1:1-18

1:1 1Tim 6:19; Tit 1:2; 1Kor 1:1; Efe 3:6; Ebr 9:15Paulo mtume wa Kristo Yesu kwa mapenzi ya Mungu, kulingana na ile ahadi ya uzima uliomo ndani ya Kristo Yesu.

1:2 Mdo 16:1; 1Tim 1:2Kwa Timotheo, mwanangu mpendwa:

Neema, rehema na amani itokayo kwa Mungu Baba, na kwa Kristo Yesu Bwana wetu.

Shukrani Na Kutiwa Moyo

1:3 Rum 1:10; Efe 1:16; Mdo 22:3; 23:1; 24:14; 27:23; Gal 1:14Ninamshukuru Mungu, ninayemtumikia kwa dhamiri safi, kama walivyofanya baba zangu, ninapokukumbuka usiku na mchana katika maombi yangu. 1:4 Mdo 20:37; 2Tim 4:9; 4:21Nikiyakumbuka machozi yako, ninatamani sana kukuona ili nipate kujawa na furaha. 1:5 1Tim 1:5; 2Tim 3:15Nimekuwa nikiikumbuka imani yako ya kweli, waliokuwa nayo bibi yako Loisi na mama yako Eunike na ambayo mimi ninasadiki sasa wewe pia unayo. 1:6 Mdo 6:6; 1The 5:19; 1Tim 4:14Kwa sababu hii nakukumbusha uchochee ile karama ya Mungu, iliyowekwa ndani yako nilipokuwekea mikono yangu. 1:7 Yer 42:11; Rum 8:15; Lk 24:49; Mdo 1:8Maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali roho ya nguvu, ya upendo na ya moyo wa kiasi.

1:8 Rum 1:16; Efe 3:1; 2Tim 2:3-9; 4:5Kwa hiyo usione haya kushuhudia kuhusu Bwana wetu, wala usinionee haya mimi niliye mfungwa kwa ajili yake. Bali uishiriki pamoja nami taabu ya Injili, kwa kadiri ya nguvu ya Mungu, 1:9 Rum 8:28; 1Tim 1:1; Tit 3:4; 1The 4:7; Ebr 3:1; Rum 3:20; 9:11; Tit 3:5ambaye alituokoa na kutuita katika mwito mtakatifu: si kwa kadiri ya matendo yetu mema bali kwa sababu ya kusudi lake mwenyewe na neema yake. Neema hii tulipewa katika Kristo Yesu tangu milele. 1:10 Efe 1:9; 1Kor 15:26, 54; Rum 16:26; Kol 1:26; Tit 1:3; 1Pet 1:20; Ebr 2:14Lakini sasa imefunuliwa kwa kudhihirishwa kwake Mwokozi wetu, Kristo Yesu, ambaye amebatilisha mauti na kuleta uzima na kutokufa kwa njia ya Injili. 1:11 1Tim 2:7; Mdo 9:15; Efe 3:7, 8; 2Tim 4:17Nami nimewekwa kuwa mhubiri, mtume na mwalimu wa Injili hii. 1:12 1Tim 6:20; 1Kor 1:8; Efe 3:1; 2Tim 2:9; 1Pet 4:19; 1Tim 6:20; 2Tim 4:8Hii ndiyo sababu ninateseka namna hii, lakini sioni haya kwa maana ninamjua yeye niliyemwamini, na kusadiki ya kuwa anaweza kukilinda kile nilichokiweka amana kwake hadi siku ile.

1:13 Tit 1:9; 1Tim 1:14Shika kwa uthabiti kielelezo cha mafundisho yenye uzima yale uliyoyasikia kwangu, pamoja na imani na upendo katika Kristo Yesu. 1:14 Rum 8:9; 1Tim 6:20; Rum 8:11Ilinde ile amana uliyokabidhiwa kwa Roho Mtakatifu akaaye ndani yetu.

1:15 2Tim 4:10-16, 19; Mdo 19:10Unajua ya kuwa watu wote katika Asia wameniacha, miongoni mwao wamo Filego na Hermogene.

1:16 Mt 5:7; 2Tim 4:19; Flm 7; Mdo 28:20Bwana akawahurumie watu wa nyumbani mwa Onesiforo, kwa sababu aliniburudisha mara kwa mara wala hakuionea aibu minyororo yangu. Badala yake, alipokuwa Rumi, alinitafuta kwa bidii mpaka akanipata. 1:18 Ebr 6:10; Mt 25:34-40; 2The 1:10; 1Tim 1:18Bwana na amjalie kupata rehema zake siku ile! Nawe unajua vyema jinsi alivyonisaidia huko Efeso.

Read More of 2 Timotheo 1