2 Samweli 7:1-29, 2 Samweli 8:1-18 NEN

2 Samweli 7:1-29

Ahadi Ya Mungu Kwa Daudi

(1 Nyakati 17:1-15)

7:1 1Nya 22:18; 17:1; 2Sam 6:3; Dan 4:29-30Baada ya mfalme kuingia rasmi katika jumba lake la kifalme, naye Bwana akiwa amemstarehesha pande zote mbali na adui zake, 7:2 2Sam 12:1; 1Fal 1:8, 22; 1Nya 29:29; 2Nya 9:29; 2Sam 5:11; 1Fal 3:1; 7:1-7; 9:1; 2Nya 8:1; Yer 22:14; Hag 1:4; Kut 26:1; Za 132:3; Mdo 7:45-46; Kut 40:21akamwambia nabii Nathani, “Mimi hapa, ninaishi katika jumba la kifalme la mierezi, wakati Sanduku la Mungu limebaki katika hema.”

7:3 1Sam 10:7; Za 132:1-5; 1Fal 8:17; 1Nya 22:7; 28:2Nathani akamjibu mfalme, “Lolote ulilo nalo moyoni, endelea ukalifanye, kwa maana Bwana yu pamoja nawe.”

Usiku ule neno la Bwana likamjia Nathani, kusema:

7:5 1Fal 8:19; 1Nya 22:8; 1Fal 5:3-5; 1Nya 28:3“Nenda ukamwambie mtumishi wangu Daudi, ‘Hili ndilo asemalo Bwana: Je, ewe ndiwe wa kunijengea mimi nyumba ili nikae ndani yake? 7:6 Mdo 7:45; Kut 40:18, 34; Yos 18:1; 1Fal 8:16Sijakaa ndani ya nyumba tangu siku niliyowaleta Waisraeli kutoka Misri hadi leo. Nimekuwa nikitembea kutoka mahali pamoja hadi mahali pengine ndani ya hema kama makao yangu. 7:7 Kum 23:14; 2Sam 5:2; 1Fal 8:27; Isa 66:1; Law 26:11; Za 78:72; Eze 34:2, 15, 23; Mt 2:6; Mdo 20:28; 1Pet 5:2Popote nilipotembea pamoja na Waisraeli wote, je, nimewahi kumwambia kiongozi wao yeyote niliyemwamuru kuwachunga watu wangu Israeli, “Kwa nini hujanijengea nyumba ya mierezi?” ’

7:8 1Sam 16:11; 1Nya 21:17; Za 74:1; Amo 7:15; Isa 9:16; 16:1; 2Sam 6:21; Za 78:70-72; 2Kor 6:18“Sasa basi, mwambie mtumishi wangu Daudi, ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mwenye Nguvu Zote: Nilikutoa wewe kutoka machungani na kutoka kuandama kundi la kondoo na mbuzi ili kuwaongoza watu wangu Israeli. 7:9 1Sam 18:14; 2Sam 5:10; Za 18:37-42; Kut 11:3; Mwa 12:2; 1Nya 17:8; Lk 1:52Nimekuwa pamoja nawe popote ulipokwenda, nami nimekuondolea mbali adui zako wote mbele yako. Basi nitalifanya jina lako kuwa kuu kama majina ya watu walio wakuu sana duniani. 7:10 Kut 15:17; Isa 5:1-7; 2Fal 21:8; 2Nya 33:8; Za 89:22-23; 147:14; Isa 54:14; 60:18; Za 44:2; 80:8; Yer 24:6; Amo 9:15Nami nitawapatia watu wangu Israeli mahali niwapande humo ili kwamba wawe na nyumbani kwao wenyewe wasisumbuliwe tena. Watu waovu hawatawaonea tena, kama walivyofanya mwanzoni, 7:11 Amu 2:16; 1Sam 12:9-11; 1Fal 2:24; 1Sam 25:28; Za 89:35-37; Lk 1:32-33; Mdo 13:22-23; 2Tim 2:8; Kut 1:21; Isa 7:2na kama walivyofanya tangu mwanzo wakati nilipowaweka viongozi juu ya watu wangu Israeli. Pia nitawapa raha mbele ya adui zenu wote.

“ ‘Bwana akuambia kwamba Bwana mwenyewe atakujengea nyumba. 7:12 Mwa 15:15; 1Fal 2:1; Mdo 13:36; 1Fal 8:20; Za 132:11-12; Yer 30:21; 33:15; 2Nya 23:3Siku zako zitakapokwisha nawe ulale pamoja na baba zako, nitainua mzao wako aingie mahali pako, ambaye atatoka viunoni mwako, nami nitauimarisha ufalme wake. 7:13 Kum 12:5; 1Fal 5:5; 6:12; 8:19, 29; Kum 16:11; 2Fal 21:4, 7; Mit 25:5; Dan 7:27; Mwa 9; 16; 2Sam 22:51; 1Fal 2:4, 45; 1Nya 22; 10; 28:6; 2Nya 6:16; 7:18; 13:5; 21:7; Za 89:3-4; Isa 9:7; 16:5; Yer 17:25; 33:17-21Yeye ndiye atakayejenga nyumba kwa ajili ya Jina langu, nami nitaimarisha kiti cha enzi cha ufalme wake milele. 7:14 Za 2:7; 89:26; Yer 3:19; Mt 3:17; Yn 1:49; 2Kor 6:18; Ebr 1:5; Ufu 21:7; Kum 8:5; 1Fal 11:34; 1Nya 22:10; Ebr 12:7; Za 89:30-33; Mit 13:24Nitakuwa baba yake, naye atakuwa mwanangu. Atakapokosea nitamwadhibu kwa fimbo ya wanadamu, kwa adhabu ya kupigwa na wanadamu. 7:15 1Fal 2:4; 6:12; 8:25; 9:5; 11:13; 2Fal 19:34; 2Nya 6:16; 7:18; 21:7; Za 89:34; Yer 33; 17; 1Sam 13:13; 15:28; 16:14; 7:16; Za 89:36-37; Lk 1:33; Za 9:7; 93:2; 103:19Lakini upendo wangu kamwe hautaondolewa kwake, kama nilivyouondoa kwa Sauli, niliyemwondoa atoke mbele yako. Nyumba yako na ufalme wako utadumu milele mbele zangu, kiti chako cha enzi kitafanywa imara milele.’ ”

Nathani akamwarifu Daudi maneno yote ya maono haya.

Maombi Ya Daudi

(1 Nyakati 17:16-27)

7:18 Kut 3:11; 1Sam 18:18Ndipo Mfalme Daudi akaingia ndani, akaketi mbele za Bwana, akasema:

“Ee Bwana Mwenyezi, mimi ni nani, na jamaa yangu ni nini, hata umenileta mpaka hapa nilipo? 7:19 Isa 55:8-9Naam, kana kwamba hili halitoshi machoni pako, Ee Bwana Mwenyezi, wewe umenena pia kuhusu siku zijazo za nyumba ya mtumishi wako. Je, hii ndiyo njia yako ya kawaida ya kushughulika na mwanadamu, Ee Bwana Mwenyezi?

7:20 Isa 38:15; Yn 21:17; 1Sam 16:7; Mwa 18:19; Za 139:1“Je, Daudi aweza kukuambia nini zaidi? Kwa maana unamjua mtumishi wako, Ee Bwana Mwenyezi. 7:21 Efe 4:32Kwa ajili ya neno lako na kwa mapenzi yako, umefanya jambo hili kubwa na kulifanya lijulikane na lifahamike kwa mtumishi wako.

7:22 Za 48:1; 77; 13; 86:10; Yer 10:6; Kum 3:24; Kut 9:14; 8:10; 20:4; 10:2; Amu 6:13; 1Nya 16:25; 2Nya 2:5; Kum 4:35; Isa 45:5“Tazama jinsi ulivyo mkuu, Ee Bwana Mwenyezi! Hakuna mwingine kama wewe, wala hakuna Mungu ila wewe, kama vile tulivyosikia kwa masikio yetu wenyewe, 7:23 Kum 4:32-38; 33:29; 1Sam 12:22; Hes 6:27; Kum 10:21; 7:7-8; 9:29; 15:15; Za 147:20; Neh 1:10Naye ni nani aliye kama watu wako Israeli, taifa pekee duniani ambalo Mungu alitoka kwenda kulikomboa kwa ajili yake mwenyewe, na kujifanyia jina mwenyewe, kwa kufanya maajabu makubwa na ya kutisha kwa kuwafukuza mataifa na miungu yao mbele ya watu wako, ambao uliwakomboa kutoka Misri? 7:24 Kum 26:18; Kut 6:6-7; Za 48:14Umeimarisha watu wako Israeli hasa kama watu wako mwenyewe milele, nawe, Ee Bwana, umekuwa Mungu wao.

7:25 Hes 23:19; 2Nya 1:9“Basi sasa, Bwana, ukaitimize ahadi uliyosema kuhusu mtumishi wako na nyumba yake milele. Fanya kama ulivyoahidi, 7:26 Kut 6:3; Neh 9:5; Za 72:19; 96:8; Mt 6:9; 1Sam 25:28ili kwamba jina lako litukuke milele. Ndipo watu watasema, ‘Bwana Mwenye Nguvu Zote ni Mungu juu ya Israeli!’ Nayo nyumba ya mtumishi wako Daudi itakuwa imara mbele zako.

“Ee Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, umelifunua hili kwa mtumishi wako, ukisema, ‘Nitakujengea nyumba.’ Hivyo mtumishi wako amepata ujasiri kukuletea dua hii. 7:28 Kut 34:6; Yn 17:17Ee Bwana Mwenyezi, wewe ndiwe Mungu! Maneno yako ndiyo kweli, nawe umemwahidi mtumishi wako mambo haya mazuri. 7:29 Hes 6:23-27Sasa naomba uwe radhi kuibariki nyumba ya mtumishi wako, ili idumu mbele zako milele, kwa maana wewe, Ee Bwana Mwenyezi, umesema, na kwa baraka zako nyumba ya mtumishi wako itaendelea kubarikiwa milele.”

Read More of 2 Samweli 7

2 Samweli 8:1-18

Ushindi Wa Daudi

(1 Nyakati 18:1-17)

8:1 2Sam 7:9; 21:15-22; 1Nya 18:1Baada ya muda, Daudi akawashinda Wafilisti na kuwatiisha, naye akautwaa Metheg-Amma kutoka mikononi mwa Wafilisti.

8:2 Mwa 19:37; Hes 21:29; Amu 3:15; Isa 45:14; Hes 24:17; 1Sam 14:47; Za 50:8; 72:10Pia Daudi akawashinda Wamoabu. Akawafanya walale chini kwa mstari akawapima kwa urefu wa kamba. Kila alipopima urefu wa hiyo kamba mara mbili hilo kundi waliuawa na alipopima mara ya tatu aliwaacha hai. Kwa hiyo Wamoabu wakawa chini ya Daudi nao wakamletea kodi.

8:3 2Sam 10:16; 1Fal 11:23; 1Sam 14:47; Mwa 2:14; 15:18Zaidi ya hayo, Daudi akapigana na Hadadezeri mwana wa Rehobu, mfalme wa Soba, alipokwenda kurudisha tena utawala wake kwenye eneo la Mto Frati. 8:4 Mwa 49:6; Yos 11:9Daudi akateka magari yake ya vita 1,000, askari wapanda farasi 7,000 na askari 20,000 watembeao kwa miguu. Daudi akawakata wale farasi wote wakokotao magari mishipa ya miguu, isipokuwa farasi 100 hakuwakata.

8:5 Mwa 14:15; 2Sam 10:6; 1Fal 11:24; 2Fal 8:7; 14:28Waaramu wa Dameski walipokuja kumsaidia Hadadezeri mfalme wa Soba, Daudi akawashambulia na kuwaua 22,000 miongoni mwao. 8:6 1Fal 20:34; 2Fal 10:19; 2Sam 3:18Daudi akaweka askari walinzi katika ufalme wa Waaramu huko Dameski, nao Waaramu wakawa watumwa wake na kumlipa ushuru. Bwana akampa Daudi ushindi kote alipokwenda.

8:7 1Fal 10:16; 14:26; 2Fal 11:10Daudi akazitwaa ngao za dhahabu zilizokuwa za maafisa wa Hadadezeri na kuzileta Yerusalemu. 8:8 Eze 47:16Kutoka miji ya Beta8:8 Beta ulikuwa mji wa Aramu-Soba ambao uliitwa Teba kwa Kiaramu; pia uliitwa Tibhathi (1Nya 18:8). na Berothai, iliyokuwa miji ya Hadadezeri, Mfalme Daudi akatwaa shaba nyingi sana.

8:9 1Fal 8:65; 2Fal 14:28; 2Nya 8:4; Lk 14:31-32Tou, mfalme wa Hamathi, aliposikia kwamba Daudi amelishinda jeshi lote la Hadadezeri, akamtuma mwanawe Yoramu kwa Mfalme Daudi kumsalimu na kumpongeza kwa ushindi wake katika vita dhidi ya Hadadezeri, kwa kuwa Hadadezeri alikuwa amepigana vita na Tou. Yoramu akamletea Daudi vyombo vya fedha, dhahabu na shaba.

8:11 1Fal 7:51; 15:15; 1Nya 26:26; 2Nya 5:1; 1Nya 18:11; 22:14-16; Mik 4:13; Ufu 21:24Mfalme Daudi akaviweka vifaa hivi wakfu kwa Bwana, kama vile alivyokuwa amefanya kwa fedha na dhahabu kutoka kwa mataifa yote aliyokuwa ameyashinda: 8:12 2Sam 10:14; 5:25; Hes 24:20; 1Sam 27:8yaani Edomu, Moabu, Waamoni, Wafilisti na Waamaleki. Pia akaweka wakfu nyara alizoteka kutoka kwa Hadadezeri mwana wa Rehobu, mfalme wa Soba.

8:13 2Sam 7:9; 2Fal 14:7; 1Nya 18:12; Za 60Naye Daudi akapata sifa baada ya kurudi kutoka kuwaua Waedomu 18,000 katika Bonde la Chumvi.

8:14 Hes 24:17-18; Za 108:9; Isa 34:5; 63:1; Yer 49:7; Eze 25:12; Mwa 27:29, 37-40; Za 144:10; 2Sam 22:44; Za 18:43Akaweka kambi za askari walinzi katika Edomu yote, nao Waedomu wakawa chini ya Daudi. Bwana alimpatia Daudi ushindi kila alipokwenda.

Maafisa Wa Daudi

8:15 Mwa 18:19; 1Fal 11:18; 14:8; 15:11; 22:43; 2Fal 12:2; Ay 29:14; Za 5:12; 119:121; Ebr 11:33Daudi akatawala Israeli yote, akitenda lililo haki na sawa kwa watu wake wote. 8:16 2Sam 2:13; 20:24; 1Fal 4:3; Isa 36:3, 22; 2Sam 19:13Yoabu mwana wa Seruya alikuwa jemadari wa jeshi; Yehoshafati mwana wa Ahiludi alikuwa mweka kumbukumbu; 8:17 1Sam 2:35; 15:24, 29; 2Sam 20:25; 1Fal 1:8; 4:4; 1Nya 6:8, 53; 16:39; 24:3; 27:17; 2Nya 13:10; Eze 40:46; 43:19; 44:15; 48:11; Mk 2:26; 1Fal 4:3; 2Fal 12:10; 19:2; 22:3; Isa 36:3; Yer 36:12Sadoki mwana wa Ahitubu na Ahimeleki mwana wa Abiathari walikuwa makuhani; Seraya alikuwa mwandishi; 8:18 2Sam 20:23; 23:20; 1Fal 1:8; 2:25, 35, 46; 4:4; 1Sam 30:14; 1Nya 18:17Benaya mwana wa Yehoyada alikuwa msimamizi wa Wakerethi na Wapelethi; nao wana wa Daudi walikuwa washauri wa mfalme.

Read More of 2 Samweli 8