2 Samweli 23:8-39, 2 Samweli 24:1-25 NEN

2 Samweli 23:8-39

Mashujaa Wa Daudi

(1 Nyakati 11:10-41)

23:8 2Sam 17:10; 1Nya 27:2Haya ndiyo majina ya mashujaa wa Daudi:

Yosheb-Bashebethi,23:8 Yosheb-Bashebethi au Yashobeamu (1Nya 11:11). Mtahkemoni, alikuwa kiongozi wa wale Watatu; yeye aliinua mkuki wake dhidi ya watu 800, ambao aliwaua katika pambano moja.

23:9 1Nya 27:4; 8:4; 11:12Wa pili wake alikuwa Eleazari mwana wa Dodai,23:9 Dodai tafsiri nyingine zinamwita Dodo. Mwahohi. Akiwa mmojawapo wa wale mashujaa watatu, alikuwa pamoja na Daudi wakati waliwadhihaki Wafilisti waliokuwa wamekusanyika huko Pas-Damimu kwa ajili ya vita. Kisha watu wa Israeli wakarudi nyuma, lakini yeye alisimama imara akawaua Wafilisti hadi mkono wake ukachoka na ukagandamana na upanga. Bwana akawapa ushindi mkubwa siku ile. Vikosi vikarudi kwa Eleazari, kuteka tu nyara za waliokufa.

Aliyefuata alikuwa Shama mwana wa Agee, Mharari. Wafilisti walipokusanyika pamoja mahali palipokuwa shamba lililojaa dengu, vikosi vya Israeli viliwakimbia. Lakini Shama akasimama imara katikati ya lile shamba. Akalitetea na kuwaua Wafilisti, naye Bwana akawapa ushindi mkubwa.

23:13 Mwa 38:1; Yos 12:15; 17:18; 1Sam 22:1; 2Sam 5:18; 1Nya 11:15; 14:9; Kum 33:29; 1Nya 29:11; 2Nya 11:14; 25:8; Za 3:8; 46:1; Rum 8:31; Isa 17:5Wakati wa mavuno, viongozi watatu kati ya viongozi thelathini walishuka, wakamwendea Daudi katika pango la Adulamu, wakati kikundi cha Wafilisti kilikuwa kimepiga kambi katika Bonde la Warefai. 23:14 1Sam 22:4-5; 2Sam 5:17; Rut 1:19; 1Nya 12:16Wakati huo Daudi alikuwa katika ngome, na kambi ya Wafilisti ilikuwa huko Bethlehemu. Daudi akatamani maji, akasema, “Laiti mtu angenipatia maji ya kunywa kutoka kisima kilicho karibu na lango la Bethlehemu!” 23:16 Mwa 35:14Basi mashujaa hao watatu wakapenya katikati ya Wafilisti, wakaenda kuchota maji kutoka kwa kisima kilicho karibu na lango la Bethlehemu, wakamletea Daudi. Lakini Daudi akakataa kuyanywa. Badala yake, aliyamimina mbele za Bwana. 23:17 Law 17:10-1223:17 Law 17:10Akasema, “Iwe mbali nami, Ee Bwana, kufanya kitu hiki. Je, hii si damu ya watu ambao walikwenda kwa kuhatarisha maisha yao?” Naye Daudi hakuyanywa.

Haya yalifanywa na hao mashujaa watatu.

23:18 1Sam 26:6; 1Nya 11:20; 2Sam 2:18Abishai ndugu yake Yoabu mwana wa Seruya ndiye alikuwa kiongozi wa hao Watatu. Aliinua mkuki wake dhidi ya watu 300 ambao aliwaua, kwa hiyo naye akawa na sifa kama hao Watatu. Je, hakupata heshima kubwa zaidi kuliko hao Watatu? Alikuwa jemadari wao, ingawa hakuhesabiwa miongoni mwao.

23:20 2Sam 8:18; 1Nya 27:5; Yos 15:21; Kut 15:15Benaya mwana wa Yehoyada alikuwa mpiganaji hodari kutoka Kabseeli ambaye alifanya mambo makubwa ya ujasiri. Aliwaua mashujaa wawili waliokuwa hodari kuliko wote wa Moabu. Pia alishuka shimoni kulipokuwa na theluji na kumuua simba. 23:21 1Nya 11:23Pia alimuua Mmisri mrefu mkubwa. Ingawa Mmisri alikuwa na mkuki mkononi mwake, Benaya alimwendea akiwa na rungu. Alipokonya mkuki kutoka mkononi mwa Mmisri na kumuua kwa mkuki wake mwenyewe. Haya yalikuwa mambo ya ushujaa ya Benaya mwana wa Yehoyada; naye pia alikuwa maarufu kama wale mashujaa watatu. 23:23 2Sam 8:18Yeye aliheshimiwa zaidi ya wale Thelathini, lakini hakujumuishwa miongoni mwa wale Watatu. Daudi akamweka kuwa kiongozi wa walinzi wake.

23:24 2Sam 2:18Miongoni mwa wale Thelathini walikuwepo:

Asaheli ndugu wa Yoabu;

Elhanani mwana wa Dodo kutoka Bethlehemu;

23:25 Amu 7:1; 1Nya 11:27Shama, Mharodi;

Elika, Mharodi;

23:26 1Nya 27:9-10Helesi, Mpalti;

Ira mwana wa Ikeshi kutoka Tekoa;

Abiezeri kutoka Anathothi;

Mebunai, Mhushathi;

23:28 1Nya 27:13; 2Fal 25:23; Ezr 2:22; Neh 7:26; Yer 40:8Salmoni, Mwahohi;

Maharai, Mnetofathi;

23:29 1Nya 27:15; Yos 15:57Heledi mwana wa Baana, Mnetofathi;

Itai mwana wa Ribai kutoka Gibea ya Benyamini;

23:30 Amu 12:13; Yos 24:30; Amu 2:9Benaya Mpirathoni;

Hidai kutoka mabonde ya Gaashi;

23:31 2Sam 3:16Abi-Alboni, Mwaribathi;

Azmawethi, Mbarhumi;

Eliaba, Mshaalboni;

wana wa Yasheni;

Yonathani mwana wa Shama, Mharari;

Ahiamu mwana wa Sharari, Mharari;

23:34 Kum 3:14; 2Sam 11:3; 15:12Elifeleti mwana wa Ahasbai, Mmaakathi;

Eliamu mwana wa Ahithofeli, Mgiloni;

23:35 Yos 12:22Hezro, Mkarmeli;

Paarai, Mwarbi;

23:36 1Sam 14:47Igali mwana wa Nathani kutoka Soba;

Bani, Mgadi;

23:37 Yos 9:17Seleki, Mwamoni;

Naharai, Mbeerothi, aliyekuwa mbeba silaha za Yoabu mwana wa Seruya;

23:38 1Nya 2:53; 2Sam 20:26; Yos 15:48Ira, Mwithiri;

Garebu, Mwithiri;

23:39 2Sam 11:3na Uria, Mhiti.

Jumla yao wote walikuwa watu thelathini na saba.

Read More of 2 Samweli 23

2 Samweli 24:1-25

Daudi Ahesabu Wapiganaji

(1 Nyakati 21:1-27)

24:1 Yos 9:15; Ay 1:6; Zek 3:1; Kut 30:12; 1Nya 27:23; 2Sam 16:10; 21:11; 1Fal 22:22; 1Nya 21:1; Yak 1:13Hasira ya Bwana ikawaka tena dhidi ya Israeli, naye akamchochea Daudi dhidi yao, akisema, “Nenda ukawahesabu Israeli na Yuda.”

24:2 2Sam 20:23; 3:10; 2Nya 2:17; 17:14; 25:5; Amu 20:1; Mwa 26:4; Kum 8:13-14; 2Nya 32:25-26; Mit 18:12; 29:23; Yer 17:5Kwa hiyo mfalme akamwambia Yoabu, pamoja na majemadari wa jeshi aliokuwa nao, “Nendeni kwa makabila yote ya Israeli kuanzia Dani hadi Beer-Sheba na mwandikishe watu wapiganaji, ili niweze kujua idadi yao.”

24:3 2Sam 2:18; Kum 1:11Lakini Yoabu akamjibu mfalme, “Bwana Mungu wako na azidishe jeshi mara mia, nayo macho ya bwana wangu mfalme na yaone hili. Lakini kwa nini bwana wangu mfalme anataka kufanya kitu cha namna hii?”

24:4 1Nya 21:4; Mhu 8:4; Mdo 5:29Hata hivyo, neno la mfalme likawa na nguvu juu ya Yoabu pamoja na majemadari wa jeshi, kwa hiyo wakaondoka mbele ya mfalme kuandikisha wapiganaji wa Israeli.

24:5 Yos 13:9; Hes 21:32; Kum 2:36Baada ya kuvuka Yordani, walipiga kambi karibu na Aroeri, kusini ya mji ulioko kwenye bonde jembamba, ndipo wakipitia Gadi, wakaenda hadi Yazeri. 24:6 Mwa 10:19; Amu 1:31; Yos 19:28; Amu 18:28-29Walikwenda hadi Gileadi na pia eneo la Tahtimu-Hodshi, wakaendelea hadi Dani-Yaani na kuzunguka kuelekea Sidoni. 24:7 Yos 19:29; Kut 3:8; Kum 1:31; Yos 11:3; Mwa 21:21-33Kisha wakaenda kuelekea ngome ya Tiro pamoja na miji yote ya Wahivi na ya Wakanaani. Mwishoni, walikwenda mpaka Beer-Sheba katika Negebu ya Yuda.

Baada ya kupita katika nchi nzima, walirudi Yerusalemu baada ya miezi tisa na siku ishirini.

24:9 Hes 1:44-46; 1Nya 21:5Yoabu akatoa hesabu ya wapiganaji kwa mfalme: Katika Israeli kulikuwako watu 800,000 wenye uwezo wa kupigana, na katika Yuda watu 500,000.

24:10 1Sam 24:5; Hes 22:34; 12:11; 2Sam 12:13; 1Sam 13:13; Mit 18:4; 1Yn 3:20; 1Nya 21:8; Ay 33:27-28; Za 25:11Dhamiri ya Daudi ilishtuka baada ya kuwahesabu wapiganaji, naye akamwambia Bwana, “Nimefanya dhambi kubwa kwa kufanya jambo hili. Ee Bwana, sasa ninakusihi, ondoa hatia ya mtumishi wako. Nimefanya jambo la kipumbavu sana.”

24:11 1Sam 22:5; 9:9; 1Nya 29:29Kabla Daudi hajaamka kesho yake asubuhi, neno la Bwana lilikuwa limemjia Gadi nabii, aliyekuwa mwonaji wa Daudi, kusema: “Nenda ukamwambie Daudi, ‘Hivi ndivyo asemavyo Bwana: Ninakupa wewe uchaguzi wa mambo matatu. Nichagulie mojawapo nitakalotenda dhidi yako.’ ”

24:13 Kum 28:28-48; 32:24; Eze 14:21; Kut 5:3; 30:12; Law 26:25; Kum 28:21-28, 35; 1Nya 21:12Basi Gadi akaenda kwa Daudi na kumwambia, “Je, ije njaa ya miaka mitatu katika nchi yako? Au miezi mitatu ya kukimbia adui zako wakikufuatia? Au siku tatu za tauni katika nchi yako? Basi sasa, fikiri juu ya hilo na uamue jinsi nitakavyomjibu huyo aliyenituma.”

24:14 Neh 9:28; Za 4:1; 51:1; 103:8-13; Isa 54:7; 55:7; Yer 33:8; 42:12; Dan 9:9; Isa 47:6; Zek 1:15Daudi akamjibu Gadi, “Nitataabika sana. Afadhali tuangukie mikononi mwa Bwana, kwa maana rehema zake ni kuu, lakini usiniache nianguke mikononi mwa wanadamu.”

24:15 1Nya 24:24; 21:14; 27:24Basi Bwana akatuma tauni katika Israeli kuanzia asubuhi mpaka mwisho wa muda ulioamriwa, wakafa watu 70,000 kuanzia Dani hadi Beer-Sheba. 24:16 Mwa 6:6; 16:7; 19:13; Kut 12:23; Mdo 12:23; 1Nya 21:15; Za 104:4; 1Sam 15:11; Za 78:38; Yer 18:5-10; Yoe 2:13; Yon 3:10Malaika aliponyoosha mkono wake ili kuangamiza Yerusalemu, Bwana akahuzunika kwa sababu ya maafa, akamwambia yule malaika aliyekuwa anawadhuru watu, “Yatosha! Rudisha mkono wako.” Wakati huo malaika wa Bwana alikuwa kwenye sakafu ya kupuria ya Arauna,24:16 Pia anaitwa Ornani kwa Kiebrania. Myebusi.

24:17 Za 74:1; 100:3; Yer 49:20; Mwa 18:23; Yon 1:12; 1Nya 21:17Ikawa Daudi alipomwona huyo malaika aliyekuwa akiwaua watu, akamwambia Bwana, “Mimi ndiye niliyetenda dhambi na kukosa. Hawa ni kondoo tu. Wamefanya nini? Mkono wako uwe juu yangu na nyumba yangu.”

Daudi Ajenga Madhabahu

24:18 Mwa 22:2; 2Nya 3:1Siku hiyo Gadi akamwendea Daudi na kumwambia, “Panda ukamjengee Bwana madhabahu kwenye sakafu ya kupuria ya Arauna Myebusi.” Kwa hiyo Daudi akakwea kama vile Bwana alivyokuwa ameamuru kwa kinywa cha Gadi. Arauna alipotazama na kumwona mfalme na watu wake wakija kumwelekea, alitoka nje na kusujudu mbele ya mfalme kifudifudi, akiuinamisha uso wake ardhini.

24:21 Hes 16:44-50; Mwa 23:8Arauna akasema, “Mbona bwana wangu mfalme amekuja kwa mtumishi wake?”

Daudi akajibu, “Kununua sakafu yako ya kupuria, ili niweze kumjengea Bwana madhabahu, ili tauni iliyo katika watu iondolewe.”

24:22 1Sam 6:14; 1Fal 19:21Arauna akamwambia Daudi, “Bwana wangu mfalme na achukue chochote kinachompendeza na akitoe sadaka. Hapa kuna maksai kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, pia kuna miti ya kupuria na nira za ngʼombe kwa ajili ya kuni. 24:23 Mwa 23:11; Eze 20:40-41; Za 20:3; 119:108; 1Pet 2:5Ee mfalme, Arauna anatoa vyote hivi kwa mfalme.” Pia Arauna akamwambia mfalme, “Bwana Mungu wako na akukubali.”

24:24 Mal 1:13-14; Mwa 23:16Lakini mfalme akamjibu Arauna, “La hasha, nasisitiza kuvilipia. Sitatoa sadaka ya kuteketezwa kwa Bwana Mungu wangu isiyonigharimu chochote.”

Kwa hiyo Daudi akanunua ile sakafu ya kupuria nafaka na maksai, akazilipia shekeli hamsini za fedha.24:24 Shekeli 50 za fedha ni sawa na gramu 600. 24:25 1Sam 7:17; 2Sam 21:14; 1Nya 21:28; 22:1; 2Sam 21:14; 2Nya 33:13Kisha Daudi akamjengea Bwana madhabahu mahali hapo, na kutoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani. Kisha Bwana akajibu kwa ajili ya nchi, nayo tauni ikakoma katika Israeli.

Read More of 2 Samweli 24