2 Samweli 2:8-32, 2 Samweli 3:1-21 NEN

2 Samweli 2:8-32

Vita Kati Ya Nyumba Ya Daudi Na Sauli

2:8 1Sam 14:50; 2Sam 3:27; 4:5; 1Nya 8:33; 9:36-39; Mwa 32:2; 1Sam 17:55; 2Sam 17:27Wakati huo Abneri mwana wa Neri, jemadari wa jeshi la Sauli, alikuwa amemchukua Ish-Boshethi mwana wa Sauli na kumleta hadi Mahanaimu. 2:9 Hes 32:26; Yos 19:24-31; 1Nya 12:29; Amu 1:32Akamweka awe mfalme juu ya nchi ya Gileadi, Waasheri,2:9 Waasheri hapa ni kabila moja la Israeli. Yezreeli, Efraimu, Benyamini na Israeli yote.

Ish-Boshethi2:10 Ish-Boshethi maana yake Mtu wa Aibu, pia anaitwa Esh-Baali maana yake Mtu wa Baali (1Nya 8:33; 9:39). mwana wa Sauli alikuwa na umri wa miaka arobaini alipoanza kutawala Israeli, naye akatawala miaka miwili. Hata hivyo, nyumba ya Yuda ikamfuata Daudi. 2:11 2Sam 5:5Muda ambao Daudi alikuwa mfalme juu ya nyumba ya Yuda huko Hebroni ilikuwa miaka saba na miezi sita.

2:12 Yos 9:3; 18:25; Isa 28:21Abneri mwana wa Neri, pamoja na watu wa Ish-Boshethi mwana wa Sauli, wakatoka Mahanaimu kwenda Gibeoni. 2:13 2Sam 8:16; 19:13; 1Fal 1:17; 1Nya 2:16; 22:6; 27:34; Yer 41:12Yoabu mwana wa Seruya na watu wa Daudi wakatoka na kukutana nao kwenye bwawa la Gibeoni. Kikundi kimoja kiliketi upande mmoja wa bwawa, na kikundi kingine upande wa pili.

2:14 Mit 10:23; 13:10Ndipo Abneri akamwambia Yoabu, “Tuwaweke baadhi ya vijana wasimame na wapigane ana kwa ana mbele yetu.”

Yoabu akasema, “Sawa, na wafanye hivyo.”

Kwa hiyo vijana wakasimama, wakahesabiwa: watu wa Benyamini na wa Ish-Boshethi mwana wa Sauli kumi na wawili, na upande wa Daudi kumi na wawili. 2:16 Amu 3:21Kisha kila mtu akakamatana na mpinzani wake kichwani na kuchomana kwa upanga, nao wakaanguka chini pamoja. Kwa hiyo mahali pale katika Gibeoni pakaitwa Helkath-Hasurimu.2:16 Helkath-Hasurimu maana yake Uwanja wa Mapambano.

2:17 2Sam 3:1; 1Sam 17:8; 1Fal 20:11Siku hiyo vita vilikuwa vikali sana, naye Abneri na watu wa Israeli wakashindwa na watu wa Daudi.

2:18 2Sam 3:39; 16:10; 19:22; 3:30; 10:7; 11:1; 14:1; 18:14; 20:8; 24:3; 1Fal 1:7; 2:5, 34; 1Sam 26:6; 2Sam 23:24; 2Nya 2:16; 1Nya 11:26; 27:1; 12:8; Za 6:5; Wim 2:9Wana watatu wa Seruya walikuwako huko: nao ni Yoabu, Abishai na Asaheli. Basi huyo Asaheli alikuwa na mbio kama paa. Asaheli akamfukuza Abneri, pasipo kugeuka kulia wala kushoto wakati akimfuata. Abneri akaangalia nyuma na kumuuliza, “Ni wewe, Asaheli?”

Akamjibu, “Ndiyo.”

2:21 1Sam 17:42Ndipo Abneri akamwambia, “Geuka upande wa kulia au kushoto. Mchukue mmoja wa vijana wa kiume na umvue silaha zake.” Lakini Asaheli hakuacha kumfukuza.

2:22 2Sam 3:27Abneri akamwonya tena Asaheli akimwambia, “Acha kunifukuza! Kwa nini nikuue? Je, nitawezaje kumtazama ndugu yako Yoabu usoni?”

2:23 2Sam 3:27; 4:6; 20:17Lakini Asaheli alikataa kuacha kumfuatia, kwa hiyo Abneri akamchoma Asaheli tumboni kwa ncha butu ya mkuki wake, mkuki ukamtoboa ukatokea mgongoni mwake. Akaanguka na kufa papo hapo. Ikawa kila mtu alisimama alipofika mahali pale Asaheli alipoanguka na kufa.

2:24 Yos 9:3; 10:2Lakini Yoabu na Abishai walimfuata Abneri, na jua lilipokuwa linatua, wakafika kwenye kilima cha Ama, karibu na Gia kwenye njia ya kuelekea kwenye nyika ya Gibeoni. Ndipo watu wa kabila la Benyamini wakakusanyika tena nyuma ya Abneri. Wakaunda kikosi na kujiimarisha juu ya kilima.

2:26 Kum 32:42; Yer 46:10, 14; Nah 2:13; 3:15; Ay 18:2; 19:2; Za 4:2; Mdo 7:16Abneri akamwita Yoabu, akamwambia, “Je, ni lazima upanga uendelee kuangamiza milele? Hutambui kwamba jambo hili litaishia katika uchungu? Utaacha kuwaagiza watu wako waache kuwafuatilia ndugu zao hata lini?”

2:27 Mit 17:14; 20:18; Lk 14:31-32Yoabu akajibu, “Hakika kama aishivyo Mungu, kama hukusema, hawa watu wangeendelea kuwafuatia ndugu zao mpaka asubuhi.”

2:28 2Sam 18:16; 20:23; Amu 3:27Basi Yoabu akapiga tarumbeta, nao watu wote wakasimama, hawakuwafuata Israeli tena, wala hawakuwapiga tena.

2:29 Kum 3:17; Mwa 32:2; Wim 2:17; Yos 21:38; 2Sam 17:24Usiku ule wote Abneri na watu wake wakatembea kupitia Araba. Wakavuka Mto Yordani, wakaendelea wakipitia nchi yote ya Bithroni wakafika Mahanaimu.

Basi Yoabu akarudi kutoka kumfuatia Abneri, na kuwakusanya watu wake wote. Pamoja na Asaheli, watu kumi na tisa wa Daudi walikuwa wamepotea. Lakini watu wa Daudi walikuwa wamewaua watu wa kabila la Benyamini 360 waliokuwa pamoja na Abneri. 2:32 Mwa 49:29; 47:29-30; Amu 8:32; 2Sam 17:24Wakamchukua Asaheli, wakamzika katika kaburi la baba yake huko Bethlehemu. Kisha Yoabu na watu wake wakatembea usiku kucha na kufika huko Hebroni wakati wa mapambazuko.

Read More of 2 Samweli 2

2 Samweli 3:1-21

3:1 1Fal 14:30; 2Sam 5:12; 2:17; 22:44; Es 9:4; Za 46:9; Isa 2:4; Mik 4:3; Mt 10:35-36; Gal 5:17; Efe 6:12Vita kati ya nyumba ya Sauli na nyumba ya Daudi vilidumu kwa muda mrefu. Daudi akaendelea kuwa imara zaidi na zaidi, wakati nyumba ya Sauli iliendelea kudhoofika zaidi na zaidi.

3:2 2Sam 13:1; 1Sam 25:43; 1Nya 3:1-3Wana walizaliwa kwa Daudi huko Hebroni:

Mzaliwa wake wa kwanza alikuwa Amnoni mwana wa Ahinoamu wa Yezreeli;

3:3 1Sam 25:42; 2Sam 13:1, 28, 37; 14:32; 15:8mzaliwa wake wa pili alikuwa Danieli3:3 Jina lingine lake ni Kileabu. mwana wa Abigaili, mjane wa Nabali wa Karmeli;

wa tatu, Absalomu mwana wa Maaka, binti Talmai mfalme wa Geshuri;

3:4 1Fal 1:5-11; 2:13, 22wa nne, Adoniya mwana wa Hagithi;

wa tano, Shefatia mwana wa Abitali;

wa sita, Ithreamu mwana wa Egla, mkewe Daudi.

Hawa ndio waliozaliwa kwa Daudi huko Hebroni.

Abneri Anamwendea Daudi

3:6 1Sam 14:50; 2Sam 2:8-9; 2Nya 25:8Wakati wa vita kati ya nyumba ya Sauli na nyumba ya Daudi, Abneri alikuwa anajiimarisha katika nafasi yake kwenye nyumba ya Sauli. 3:7 Mwa 22:24; 2Sam 16:21-22; 1Fal 1:3; 2Sam 21:8-11Basi Sauli alikuwa amekuwa na suria, jina lake Rispa binti wa Aiya. Naye Ish-Boshethi akamwambia Abneri, “Kwa nini umekutana kimwili na suria wa baba yangu?”

3:8 1Sam 17:43; 2Sam 9:8; 16:9; 8; 13; 1Sam 24:14; Kut 23:18Abneri akakasirika sana kwa sababu ya kile Ish-Boshethi alichosema, naye akamjibu, “Je, mimi ni kichwa cha mbwa, kwa upande wa Yuda? Siku hii ya leo mimi ni mtiifu kwa nyumba ya baba yako Sauli, kwa jamaa yake na rafiki zake. Sijakukabidhi kwa Daudi, lakini bado unanilaumu kwa kosa la kuhusika na huyu mwanamke! 3:9 1Sam 15:28; Rut 1:17; 1Fal 19:2; 1Sam 16:12; 1Nya 12:23; Za 78:70; 89:19-20; Mdo 13:22Mungu na amshughulikie Abneri, tena kwa ukali, ikiwa sitafanya kwa ajili ya Daudi kile Bwana alichomwahidi kwa kiapo, 3:10 Amu 20:1; 1Sam 25:28-31; 2Sam 24:2; 17:11; 1Fal 4:25na kuuhamisha ufalme kutoka kwenye nyumba ya Sauli na kuimarisha kiti cha ufalme cha Daudi juu ya Israeli na Yuda kuanzia Dani mpaka Beer-Sheba.” Ish-Boshethi hakuthubutu kusema neno jingine kwa Abneri, kwa sababu alimwogopa Abneri.

Ndipo Abneri akatuma wajumbe kwa niaba yake kwa Daudi, kumwambia, “Nchi hii ni ya nani? Fanya mapatano na mimi, nami nitakusaidia kuiweka Israeli yote juu yako.”

3:13 Mwa 43:5; 1Sam 18:20; Mwa 44:23-26Daudi akasema, “Vyema, nitafanya mapatano nawe. Lakini nahitaji jambo moja kwako: Usije mbele yangu mpaka umemleta Mikali binti Sauli wakati utakapokuja kuniona.” 3:14 1Sam 18:27Kisha Daudi akapeleka wajumbe kwa Ish-Boshethi mwana wa Sauli, kudai, “Nipe Mikali mke wangu, ambaye nilimposa mwenyewe kwa mahari ya magovi 100 ya Wafilisti.”

3:15 Kum 24:1-4; 1Sam 25:44Kwa hiyo Ish-Boshethi akatoa amri kwamba Mikali achukuliwe kutoka kwa Paltieli mumewe, mwana wa Laishi. 3:16 2Sam 16:5; 17:18; 19:16Hata hivyo, mumewe alikwenda pamoja naye, akilia nyuma ya mkewe njia yote hadi Bahurimu. Ndipo Abneri akamwambia Paltieli, “Rudi nyumbani!” Kwa hiyo akarudi.

3:17 Amu 11:11Abneri akafanya shauri pamoja na wazee wa Israeli, akasema, “Muda mrefu mmetaka kumfanya Daudi mfalme wenu. 3:18 1Sam 9:16; 2Sam 8:6; 1Sam 15:28Sasa fanyeni hivyo! Kwa maana Bwana alimwahidi Daudi akisema, ‘Kwa kupitia Daudi mtumishi wangu nitawaokoa watu wangu Israeli kutoka mikononi mwa Wafilisti na kutoka mikononi mwa adui zako wote.’ ”

3:19 1Nya 12:2, 16, 29; 1Sam 10:20-21Pia Abneri mwenyewe akazungumza na kabila la Benyamini. Kisha akaenda mpaka Hebroni kumwambia Daudi kila kitu ambacho Israeli na nyumba yote ya Benyamini walichotaka kufanya. 3:20 1Nya 12:29Wakati Abneri aliyekuwa na watu ishirini pamoja naye, alipokuja kwa Daudi huko Hebroni, Daudi akamwandalia karamu pamoja na watu wake. 3:21 2Sam 5:3; 1Fal 11:37; Kum 14:26; Za 20:4Ndipo Abneri akamwambia Daudi, “Niache niende mara moja nikakusanye Israeli yote kwa ajili ya mfalme bwana wangu, ili waweze kufanya mapatano na wewe, ili kwamba uweze kutawala juu ya yote yale ambayo moyo wako unaonea shauku.” Basi Daudi akamuaga Abneri, naye akaenda kwa amani.

Read More of 2 Samweli 3