2 Samweli 15:13-37, 2 Samweli 16:1-14 NEN

2 Samweli 15:13-37

Kukimbia Kwa Daudi

15:13 Amu 9:3Mjumbe akaja na kumwambia Daudi, “Mioyo ya watu wa Israeli inaambatana na Absalomu.”

15:14 1Fal 2:26; Za 132:1; 3; 2Sam 16:9Ndipo Daudi akawaambia maafisa wake wote waliokuwa pamoja naye huko Yerusalemu, “Njooni! Ni lazima tukimbie, la sivyo hakuna hata mmoja wetu atakayeokoka kutoka mkononi mwa Absalomu. Ni lazima tuondoke kwa haraka, la sivyo atakuja mbio na kutupata, atatuangamiza na kuupiga mji kwa upanga.”

Maafisa wa mfalme wakamjibu, “Watumishi wako tu tayari kufanya lolote mfalme bwana wetu analochagua.”

15:16 2Sam 16:21-22; 20:3; 12:11Mfalme akatoka, pamoja na watu wa nyumbani mwake wakimfuata; lakini akawaacha masuria kumi ili kuangalia jumba la kifalme. Hivyo mfalme akaondoka, pamoja na watu wote wakimfuata, wakatua mahali mbali kiasi. 15:18 1Sam 30:14; 2Sam 20:7, 23; 1Fal 1:34, 44; 1Nya 18:17; 2Sam 8:18Watu wake wote wakatembea, wakampita wakiwa wamefuatana na Wakerethi na Wapelethi wote; pia Wagiti wote mia sita waliokuwa wamefuatana naye kutoka Gathi wakapita mbele ya mfalme.

15:19 2Sam 18:2; Mwa 31:15Mfalme akamwambia Itai, Mgiti, “Kwa nini ufuatane na sisi? Rudi ukakae pamoja na Mfalme Absalomu. Wewe ni mgeni, mkimbizi kutoka nchini mwako. 15:20 1Sam 22:2; 2:6; 23:13Ulikuja jana tu. Nami leo nikufanye utangetange pamoja nasi, wakati sijui niendako? Rudi, nawe ukawachukue watu wa kwenu. Wema na uaminifu na viwe pamoja nawe.”

15:21 Rut 1:16-17; Mit 17:17; 1Sam 20:3; 2Fal 2:2-6Lakini Itai akamjibu mfalme, “Hakika kama Bwana aishivyo na kama mfalme bwana wangu aishivyo, popote mfalme bwana wangu atakapokuwa, ikiwa ni kuishi au kufa, hapo ndipo mtumishi wako atakapokuwa.”

Daudi akamwambia Itai, “Songa mbele, endelea.” Kwa hiyo Itai, Mgiti, akaendelea pamoja na watu wake wote, pia jamaa zote waliokuwa pamoja naye.

15:23 1Sam 11:4; Ay 2:12; 1Fal 2:37; 2Fal 23:12; 2Nya 15:16; 29:16; 30:14; Yer 31:40; Yn 18:1; 2Sam 16:2; Mt 3:1-3Watu wote wa nje ya mji wakalia kwa sauti wakati watu wote walipokuwa wakipita. Mfalme naye akavuka Bonde la Kidroni, nao watu wote wakaelekea jangwani.

15:24 2Sam 8:17; 19:11; Hes 4:18; 10:33; 1Fal 2:26; 1Sam 22:20Sadoki pia alikuwako, kadhalika Walawi wote waliokuwa pamoja naye walikuwa wamechukua Sanduku la Agano la Mungu. Wakaweka chini Sanduku la Mungu, naye Abiathari akatoa dhabihu mpaka watu wote walipokuwa wameondoka mjini.

15:25 Kut 15:13; Law 15:31; Za 43:3; 46:4; 84:1; 132:7; 2Sam 6:17Kisha mfalme akamwambia Sadoki, “Rudisha Sanduku la Mungu mjini. Ikiwa nitapata kibali mbele za Bwana, atanirudisha, nami nitaliona Sanduku hili tena pamoja na Maskani yake. 15:26 Amu 10:15; 2Sam 22:20; 1Fal 10:9; Hes 14:8; 2Nya 9:8; Isa 62:4; 1Sam 3:18Lakini kama yeye atasema, ‘Mimi sipendezwi nawe,’ basi mimi niko tayari; yeye na anifanye chochote aonacho chema kwake.”

15:27 1Sam 9:9; 2Sam 17:17; 1Fal 1:42; 2Sam 24:11Pia mfalme alimwambia kuhani Sadoki, “Je, wewe si mwonaji? Rudi mjini kwa amani pamoja na mwanao Ahimaasi na Yonathani mwana wa Abiathari. Wewe na Abiathari wachukueni wana wenu wawili. 15:28 2Sam 17:16Nitasubiri kwenye vivuko katika jangwa mpaka neno litakapotoka kwenu kuniarifu.” Kwa hiyo Sadoki na Abiathari wakarudisha Sanduku la Mungu mpaka Yerusalemu na kukaa huko.

15:30 Hes 25:6; Za 30:5; Es 6:12; Isa 20:2-4; Zek 14:4; Mt 21:1; Lk 19:20; Mdo 1:12; Yer 14:3; Za 126:6; Mt 5:4; Rum 12:15Bali Daudi akaendelea, akapanda Mlima wa Mizeituni, akaenda huku analia, akiwa amefunika kichwa chake na bila viatu miguuni. Watu wote waliokuwa pamoja naye nao wakafunika vichwa vyao, wakawa wanapanda mlima huku wanalia. 15:31 2Sam 16:23; 17:14, 23; Za 3:1; 55:12Basi Daudi alikuwa ameambiwa, “Ahithofeli alikuwa miongoni mwa washiriki wa shauri baya la Absalomu.” Ndipo Daudi akaomba, akisema, “Ee Bwana, geuza shauri la Ahithofeli kuwa ujinga.”

15:32 2Sam 16:16; 17:5; 1Fal 4:16; Yos 16:2; 7:6; 2Sam 1:2Daudi alipofika kwenye kilele cha mlima, mahali ambapo watu walikuwa wamezoea kumwabudu Mungu, Hushai, Mwariki, alikuwako huko kumlaki, joho lake likiwa limeraruka na mavumbi kichwani mwake. 15:33 2Sam 19:35Daudi akamwambia, “Kama ukienda pamoja nami, utakuwa mzigo kwangu. 15:34 2Sam 16:19; 17:14; Mit 11:14Lakini ikiwa utarudi mjini na kumwambia Absalomu, ‘Nitakuwa mtumishi wako, ee mfalme; nilikuwa mtumishi wa baba yako wakati uliopita, lakini sasa nitakuwa mtumishi wako,’ basi utaweza kunisaidia kwa kupinga shauri la Ahithofeli. 15:35 2Sam 17:15-16Je, makuhani Sadoki na Abiathari hawatakuwa pamoja nawe? Waambie lolote utakalosikia katika jumba la mfalme. 15:36 2Sam 18:19; 17:17; 1Fal 1:42Wana wao wawili, Ahimaasi mwana wa Sadoki na Yonathani mwana wa Abiathari, wako pamoja nao huko. Watume kwangu na lolote utakalosikia.”

15:37 1Nya 27:33; 2Sam 16:15-17; Mit 17:17Kwa hiyo Hushai, rafiki wa Daudi, akafika Yerusalemu wakati Absalomu alipokuwa anaingia mjini.

Read More of 2 Samweli 15

2 Samweli 16:1-14

Daudi Na Siba

16:1 2Sam 9:1-3; 1Sam 25:18; 1Nya 12:40; 2Sam 15:30Daudi alipokuwa amekwenda umbali mfupi kupita kilele cha mlima, akamkuta huko Siba, msimamizi wa shughuli za Mefiboshethi, akingojea kumlaki Daudi. Alikuwa na punda wawili wakiwa wametandikwa na kupakiwa mikate mia mbili, maandazi mia ya zabibu kavu, maandazi mia ya tini na kiriba cha divai.

16:2 2Sam 17:27-29; Amu 5:10; 10:4; 1Sam 25:27; 2Sam 15:23; Mit 15:23; 31:6; Za 104:15; 1Tim 5:23Mfalme Daudi akamuuliza Siba, “Kwa nini umeleta vitu hivi?”

Siba akamjibu, “Punda ni kwa ajili ya watu wa nyumba ya mfalme kupanda, mikate na matunda ni kwa ajili ya watu kula, nayo divai ni kwa kuwaburudisha watakaochoka jangwani.”

16:3 2Sam 9:9-10; 19:26-27Kisha mfalme akauliza, “Yuko wapi mwana wa bwana wako?”

Siba akamwambia, “Anakawia Yerusalemu, kwa sababu anafikiri, ‘Leo nyumba ya Israeli itanirudishia utawala wa baba yangu.’ ”

16:4 2Sam 4:4; 14:10-11; Mit 18:13Ndipo mfalme akamwambia Siba, “Yote yaliyokuwa mali ya Mefiboshethi sasa ni mali yako.”

Siba akasema, “Nasujudu kwa unyenyekevu. Naomba nipate kibali mbele yako, bwana wangu mfalme.”

Shimei Amlaani Daudi

16:5 2Sam 3:16; 19:16-23; 1Fal 2:8, 36, 44; Kut 22:28; 2Sam 19:16Mfalme Daudi alipokuwa anakaribia Bahurimu, mtu mmoja kutoka ukoo huo huo kama jamaa ya Sauli, akatoka humo, ambaye jina lake ni Shimei mwana wa Gera; akawa analaani alipokuwa akitoka. Akamtupia Daudi na maafisa wote wa mfalme mawe, ingawa vikosi vyote na walinzi maalum walikuwa kulia na kushoto mwa Daudi. Shimei alivyokuwa akilaani, akasema, “Toka hapa, toka hapa, wewe mtu wa damu, wewe mtu mbaya kabisa! 16:8 2Sam 19:28; 21:9; 19:19; Za 55:3; Amu 9:24; 1Fal 2:32-33; Ufu 16:6Bwana amekulipiza kwa ajili ya damu yote uliyomwaga ya watu wa nyumba ya Sauli, ambaye nafasi yake umeimiliki wewe. Bwana amekabidhi ufalme mkononi mwa mwanao Absalomu. Maangamizi yamekupata kwa sababu wewe ni mtu wa damu!”

16:9 1Sam 26:6; 2Sam 3:8, 39; Lk 9:54; Kut 22:28Ndipo Abishai mwana wa Seruya akamwambia mfalme, “Kwa nini huyu mbwa mfu amlaani bwana wangu mfalme? Niruhusu nivuke nikatilie mbali kichwa chake.”

16:10 2Sam 2:18; 19:22; Rum 9:20; 2Sam 3:39; 1Pet 2:23; 1Fal 18:25; Mao 3:38Lakini mfalme akamwambia, “Mna nini nami, enyi wana wa Seruya? Ikiwa analaani kwa sababu Bwana amemwambia, ‘Mlaani Daudi,’ nani awezaye kuuliza, ‘Kwa nini unafanya hivi?’ ”

16:11 2Sam 12:11; Mwa 45:5; 1Sam 26:17Ndipo Daudi akamwambia Abishai na maafisa wake wote, “Mwanangu, yeye ambaye ametoka viunoni mwangu mwenyewe, anajaribu kuuondoa uhai wangu. Je, si zaidi sana kwa huyu Mbenyamini! Mwacheni, acha alaani, kwa maana Bwana amemwambia afanye hivyo. 16:12 Za 4:1; 25:18; Kum 23:5; Rum 8:28; Mwa 29:32; Za 37:7; Yer 24:5-7; Mao 3:22-26; Mt 5:11-12; 2Kor 4:17Inawezekana kwamba Bwana ataona dhiki yangu na kunilipa mema kwa ajili ya laana ninayopokea leo.”

Kwa hiyo Daudi na watu wake wakaendelea na safari yao barabarani, huku Shimei akiwa anatembea pembezoni mwa kilima sambamba na Daudi, huku akimlaani na kumtupia Daudi mawe na kumrushia mavumbi. 16:14 Za 109:28; 2Sam 17:2Mfalme na watu wote aliokuwa pamoja nao wakafika kwenye kituo chao wakiwa wamechoka. Mfalme akajiburudisha hapo.

Read More of 2 Samweli 16