2 Wafalme 19:14-37, 2 Wafalme 20:1-21 NEN

2 Wafalme 19:14-37

Maombi Ya Hezekia

19:14 2Fal 5:7Hezekia akapokea barua kutoka kwa wale wajumbe, naye akaisoma. Kisha akapanda katika Hekalu la Bwana, akaikunjua mbele za Bwana. 19:15 Mwa 3:24; Kut 25:22Naye Hezekia akamwomba Bwana akisema: “Ee Bwana, Mungu wa Israeli, uketiye juu ya kiti cha enzi kati ya makerubi, wewe peke yako ndiwe Mungu juu ya falme zote za dunia. Wewe umeumba mbingu na nchi. 19:16 Za 31:2; Kut 3:16Tega sikio, Ee Bwana, usikie; fungua macho yako, Ee Bwana, uone; sikiliza maneno ambayo Senakeribu ametuma kumtukana Mungu aliye hai.

“Ni kweli, Ee Bwana, kwamba wafalme wa Ashuru wameyaangamiza mataifa haya na nchi zao. 19:18 Yer 10:3-10; Mdo 17:29Wameitupa miungu yao kwenye moto na kuiangamiza, kwa kuwa haikuwa miungu, bali miti na mawe tu iliyotengenezwa kwa mikono ya wanadamu. 19:19 1Sam 12:10; Yos 4:24Sasa basi, Ee Bwana Mungu wetu, tuokoe kutoka mkononi mwake, ili falme zote duniani zipate kujua kwamba wewe peke yako, Ee Bwana, ndiwe Mungu.”

Isaya Anatoa Unabii Wa Kuanguka Kwa Senakeribu

(Isaya 37:21-38)

19:20 1Fal 9:3Kisha Isaya mwana wa Amozi akapeleka ujumbe kwa Hezekia, akasema: “Hili ndilo asemalo Bwana, Mungu wa Israeli: Nimesikia maombi yako kuhusu Senakeribu mfalme wa Ashuru. 19:21 Isa 47:1; Mao 2:13; Ay 16:4Hili ndilo neno ambalo Bwana amelisema dhidi yake:

“ ‘Bikira Binti Sayuni anakudharau na kukudhihaki.

Binti Yerusalemu anatikisa kichwa chake unapokimbia.

19:22 Law 19:2; Hos 11:9Ni nani uliyemtukana na kumkufuru?

Ni nani uliyeinua sauti yako dhidi yake,

na kumwinulia macho yako kwa kiburi?

Ni dhidi ya yule Aliye Mtakatifu wa Israeli!

19:23 Za 20:7; Eze 31:3Kupitia kwa wajumbe wako

umelundika matukano juu ya Bwana.

Nawe umesema,

“Kwa magari yangu mengi ya vita,

nimepanda juu ya vilele vya milima,

vilele vya juu sana katika Lebanoni.

Nami nimeiangusha mierezi yake mirefu,

misunobari yake iliyo bora sana.

Nimefikia sehemu zake zilizo mbali sana,

misitu yake iliyo mizuri sana.

Nimechimba visima katika nchi za kigeni

na kunywa maji yake.

Kwa nyayo za miguu yangu

nimekausha vijito vyote vya Misri.”

19:25 Isa 22:11; Mik 1:6“ ‘Je, hujasikia?

Zamani sana niliamuru hili.

Siku za kale nilipanga hili;

sasa nimelifanya litokee,

kwamba umegeuza miji yenye ngome

kuwa malundo ya mawe.

19:26 Eze 7:17; Ay 8:12Watu wa miji hiyo wameishiwa nguvu,

wanavunjika mioyo na kuaibishwa.

Wao ni kama mimea katika shamba,

kama machipukizi mororo ya kijani,

kama majani yachipuayo juu ya paa la nyumba,

ambayo hukauka kabla ya kukua.

19:27 Za 139:1-4“ ‘Lakini ninajua mahali ukaapo,

kutoka kwako na kuingia kwako,

na jinsi unavyoghadhibika dhidi yangu.

19:28 2Nya 33:11; Eze 29:4Kwa sababu unaghadhibika dhidi yangu,

na ufidhuli wako umefika masikioni mwangu,

nitaweka ndoana yangu puani mwako

na hatamu yangu kinywani mwako,

nami nitakufanya urudi kwa njia ile uliyoijia.’

19:29 Lk 2:12; Za 107:37“Hii ndiyo itakuwa ishara kwako, ee Hezekia:

“Mwaka huu utakula kile kiotacho chenyewe,

na mwaka wa pili utakula kutoka machipukizi yake.

Lakini katika mwaka wa tatu, panda na uvune,

panda mashamba ya mizabibu na ule matunda yake.

19:30 Mwa 45:7; Amo 9:14Mara nyingine tena mabaki ya nyumba ya Yuda

wataeneza mizizi chini na kuzaa matunda juu.

19:31 Mwa 45:7; Isa 9:7Kwa kuwa kutoka Yerusalemu watakuja mabaki,

na kutoka Mlima Sayuni kundi la walionusurika.

Wivu wa Bwana Mwenye Nguvu Zote ndio utatimiza jambo hili.

“Kwa hiyo hili ndilo asemalo Bwana kuhusu mfalme wa Ashuru:

“Hataingia katika mji huu

wala hatapiga mshale hapa.

Hatakuja mbele yake akiwa na ngao,

wala kupanga majeshi kuuzingira.

Kwa njia ile aliyoijia, ndiyo atakayorudi;

hataingia katika mji huu,

asema Bwana.

19:34 2Fal 20:6; 2Sam 7:15Nitaulinda mji huu na kuuokoa,

kwa ajili yangu mwenyewe,

na kwa ajili ya Daudi mtumishi wangu.”

19:35 Ay 24:24Usiku ule, malaika wa Bwana akaenda, akawaua wanajeshi 185,000 katika kambi ya Waashuru. Wenzao walipoamka asubuhi yake, walikuta maiti kila mahali! 19:36 Mwa 10:11Basi Senakeribu mfalme wa Ashuru akavunja kambi na kuondoka. Akarudi Ninawi na kukaa huko.

19:37 2Fal 17:31; Mwa 8:4Siku moja, alipokuwa akiabudu katika hekalu la mungu wake Nisroki, wanawe Adrameleki na Shareza wakamuua kwa upanga, nao wakakimbilia nchi ya Ararati. Naye Esar-Hadoni mwanawe akawa mfalme badala yake.

Read More of 2 Wafalme 19

2 Wafalme 20:1-21

Ugonjwa Wa Hezekia

(2 Nyakati 32:24-26; Isaya 38:1-8, 21-22)

Katika siku hizo, Hezekia akaugua, naye akawa karibu kufa. Nabii Isaya mwana wa Amozi akaenda kwake na kumwambia, “Hili ndilo asemalo Bwana: Tengeneza mambo ya nyumba yako, kwa sababu utakufa, hutapona.”

Hezekia akaelekeza uso wake ukutani, akamwomba Bwana: 20:3 Mwa 8:1; 2Nya 31:20“Ee Bwana, kumbuka jinsi nilivyoenenda mbele zako kwa uaminifu na kujitoa kwa moyo wangu wote, na kufanya yaliyo mema machoni pako.” Naye Hezekia akalia kwa uchungu.

Kabla Isaya hajaondoka katika ua wa kati, neno la Bwana likamjia, akaambiwa: 20:5 1Fal 9:3; Za 39:12“Rudi ukamwambie Hezekia, kiongozi wa watu wangu, ‘Hili ndilo asemalo Bwana, Mungu wa baba yako Daudi: Nimeyasikia maombi yako na nimeona machozi yako; nitakuponya. Siku ya tatu kuanzia sasa utapanda kwenda Hekalu la Bwana. 20:6 2Fal 19:34; 1Nya 17:19Nitakuongezea miaka kumi na mitano katika maisha yako. Nami nitakuokoa wewe pamoja na mji huu mkononi mwa mfalme wa Ashuru. Nitaulinda mji huu kwa ajili yangu, na kwa ajili ya mtumishi wangu Daudi!’ ”

Kisha Isaya akasema, “Tengenezeni dawa ya kubandika ya tini.” Wakafanya hivyo na kuiweka kwenye jipu, naye akapona.

Hezekia alikuwa amemuuliza Isaya, “Kutakuwa na ishara gani kwamba Bwana ataniponya mimi, na kwamba nitapanda kwenda Hekalu la Bwana siku ya tatu tangu leo?”

20:9 Kum 13:2; Yer 44:29Isaya akajibu, “Hii ndiyo ishara ya Bwana kwako kwamba Bwana atafanya kile alichoahidi: Je, kivuli kiende hatua kumi mbele, au kivuli kirudi nyuma hatua kumi?”

20:10 2Fal 3:18Hezekia akasema, “Ni jambo rahisi kwa kivuli kutangulia mbele hatua kumi, kuliko kukifanya kirudi nyuma hatua kumi.”

20:11 Yos 10:13; 2Nya 32:31Ndipo nabii Isaya akamwita Bwana, naye Bwana akakifanya kivuli kurudi nyuma hatua kumi ambazo kilikuwa kimeshuka kwenye ngazi ya Ahazi.

Wajumbe Kutoka Babeli

(Isaya 39:1-8)

Wakati huo Merodaki-Baladani, mwana wa Baladani mfalme wa Babeli, akamtumia Hezekia barua na zawadi, kwa sababu alikuwa amesikia habari za kuugua kwa Hezekia. Hezekia akawapokea wale wajumbe na kuwaonyesha vitu vyote vile vilivyokuwa katika ghala zake: yaani fedha, dhahabu, vikolezo na mafuta safi, ghala la silaha na kila kitu kilichokuwa katika hazina zake. Hapakuwa na kitu chochote katika jumba lake la kifalme au katika ufalme wake wote ambacho Hezekia hakuwaonyesha.

Ndipo nabii Isaya akaenda kwa Mfalme Hezekia na kumuuliza, “Watu hao walisema nini, na wametoka wapi?”

Hezekia akamjibu, “Wametoka nchi ya mbali. Walikuja kutoka Babeli.”

Nabii akauliza, “Waliona nini katika jumba lako la kifalme?”

Hezekia akajibu, “Waliona kila kitu katika jumba langu la kifalme. Hakuna kitu chochote katika hazina yangu ambacho sikuwaonyesha.”

Ndipo Isaya akamwambia Hezekia, “Sikia neno la Bwana: 20:17 2Fal 24:13; Yer 52:17-23Hakika wakati unakuja ambapo vitu vyote katika jumba lako la kifalme, na vyote ambavyo baba zako waliweka akiba mpaka siku hii, vitachukuliwa kwenda Babeli. Hakuna chochote kitakachosalia, asema Bwana. 20:18 2Fal 24:15; Mik 4:10Nao baadhi ya wazao wako, nyama yako na damu yako mwenyewe watakaozaliwa kwako, watachukuliwa mbali, nao watakuwa matowashi katika jumba la mfalme wa Babeli.”

Hezekia akamjibu Isaya, “Neno la Bwana ulilosema ni jema.” Kwa kuwa alifikiri, “Lakini si patakuwa na amani na usalama wakati wa uhai wangu?”

Matukio mengine ya utawala wa Hezekia, mafanikio yake yote, na jinsi alivyotengeneza bwawa na mfereji ambao ulileta maji katika mji, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Yuda? Hezekia akafa, akazikwa pamoja na baba zake. Naye Manase mwanawe akawa mfalme baada yake.

Read More of 2 Wafalme 20