2 Wakorintho 9:6-15 NEN

2 Wakorintho 9:6-15

Kupanda Kwa Ukarimu

9:6 Mit 11:24-25; 22:9; Gal 6:7-9Kumbukeni kwamba: Yeyote apandaye kwa uchache pia atavuna kwa uchache, naye apandaye kwa ukarimu pia atavuna kwa ukarimu. 9:7 Kut 25:2; 2Kor 8:12; Kum 15:10; Rum 12:8Kila mtu atoe kama anavyokusudia moyoni mwake, si kwa uchoyo au kwa kulazimishwa, kwa maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo mkunjufu. 9:8 Efe 3:20; Flp 4:19Naye Mungu aweza kuwapa kila baraka kwa wingi, ili katika mambo yote kila wakati, mwe na kila kitu mnachohitaji, ili mweze kushiriki kwa wingi katika kila kazi njema. 9:9 Mal 3:10; Za 112:9Kama ilivyoandikwa:

“Ametawanya vipawa vyake kwa ukarimu

akawapa maskini;

haki yake hudumu milele.”

9:10 Isa 55:10; Hos 10:12Yeye ampaye mpanzi mbegu kwa ajili ya kupanda na mkate kuwa chakula, atawapa na kuzizidisha mbegu zenu za kupanda na kuongeza mavuno ya haki yenu. 9:11 1Kor 1:5; 2Kor 1:11; 4:15Mtatajirishwa kwa kila namna ili mpate kuwa wakarimu kila wakati, na kupitia kwetu, ukarimu wenu utamletea Mungu shukrani.

9:12 2Kor 8:12; 1:11Huduma hii mnayofanya si tu kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya watakatifu, bali huzidi sana kwa shukrani nyingi apewazo Mungu. Kwa sababu ya huduma ambayo mmejithibitisha wenyewe, watu watamtukuza Mungu kwa ajili ya utiifu ufuatanao na ukiri wenu wa Injili ya Kristo, na kwa ukarimu wenu wa kushiriki pamoja nao na pia wengine wote. 9:14 2Kor 8:1Nao katika maombi yao kwenu mioyo yao itawaonea shauku kwa sababu ya neema ipitayo kiasi mliyopewa na Mungu. 9:15 2Kor 2:14; Rum 5:15-16Ashukuriwe Mungu kwa karama yake isiyoelezeka.

Read More of 2 Wakorintho 9