2 Wakorintho 2:12-17, 2 Wakorintho 3:1-6 NEN

2 Wakorintho 2:12-17

Wasiwasi Wa Paulo Huko Troa

2:12 Rum 1:1; 2Kor 4:3-4; 8:18; 9:13; 1The 3:2; Mdo 14:21Basi nilipofika Troa kuhubiri Injili ya Kristo na kukuta kwamba Bwana alikuwa amenifungulia mlango, 2:13 2Kor 7:5; 7:6-13; 8:6-23; 12:18; Gal 2:1-3; Tit 1:4; Mdo 16:9bado nilikuwa sina utulivu akilini mwangu kwa sababu sikumkuta ndugu yangu Tito huko. Hivyo niliagana nao nikaenda Makedonia.

2:14 Rum 6:17; 7:25; 1Kor 15:57; 2Kor 9:15; Eze 20:41; Efe 5:2; Flp 4:18; 2Kor 8:7Lakini Mungu ashukuriwe, yeye ambaye siku zote hutufanya tuandamane kwa ushindi tukiwa ndani ya Kristo. Naye kupitia kwetu hueneza kila mahali harufu nzuri ya kumjua yeye. 2:15 Mwa 8:21; Kut 29:18Kwa maana sisi kwa Mungu ni harufu nzuri ya manukato ya Kristo miongoni mwa wale wanaookolewa na kwa wale wanaopotea. 2:16 Lk 2:34; Yn 3:36; 2Kor 3:5-6Kwa wale wanaopotea, sisi ni harufu ya mauti iletayo mauti; lakini kwa wale wanaookolewa, sisi ni harufu nzuri iletayo uzima. Ni nani awezaye mambo hayo? 2:17 Mdo 20:33; 2Kor 4:2; 1The 2:5; 1Kor 5:8; 2Kor 1:12; 12:19Tofauti na watu wengine wengi, sisi hatufanyi biashara na Neno la Mungu kwa ajili ya kupata faida. Kinyume chake, katika Kristo tunalisema Neno la Mungu kwa unyoofu, kama watu tuliotumwa kutoka kwa Mungu.

Read More of 2 Wakorintho 2

2 Wakorintho 3:1-6

Wahudumu Wa Agano Jipya

3:1 Rum 16:1; 2Kor 5:12; 10:12-18; 12:11; Mdo 18:17; Rum 16:1; 1Kor 3:16Je, tunaanza tena kujisifu wenyewe? Au tunahitaji kupata barua za utambulisho kwenu au kutoka kwenu, kama watu wengine? 3:2 1Kor 9:2Ninyi wenyewe ndio barua yetu iliyoandikwa katika mioyo yetu, inayojulikana na kusomwa na kila mtu. 3:3 Mt 16:16; Kut 24:12; 31:18; 32:15-16; Mit 3:3; 7:3; Yer 31:33; Eze 36:26Nanyi mwadhihirisha wazi kwamba ninyi ni barua itokayo kwa Kristo, matokeo ya huduma yetu, ambayo haikuandikwa kwa wino bali kwa Roho wa Mungu aliye hai, si katika vibao vya mawe, bali katika vibao ambavyo ni mioyo ya wanadamu.

3:4 Efe 3:12Hili ndilo tumaini tulilo nalo mbele za Mungu kwa njia ya Kristo. 3:5 2Kor 2:16; 1Kor 15:10Si kwamba sisi tunafikiri kuwa tunaweza kufanya jambo lolote wenyewe, lakini nguvu yetu inatoka kwa Mungu. 3:6 Lk 22:20; Rum 2:29; 7:6; Yn 6:63Ndiye alituwezesha sisi kuwa wahudumu wa Agano Jipya: si wa andiko, bali wa Roho; kwa kuwa andiko huua bali Roho hutia uzima.

Read More of 2 Wakorintho 3